mkuu,kwanza nikukumbushe,nia yao watu weupe ya kukufanya wewe uwaone wao ni bora kukuliko imefanikiwa kwa asilimia 100%.
wacha nikuweke sawa.
elimu na mifumo yote ya kuongeza ufahamu,wao ndio waanzilishi,hakuna namna inapoletwa kwenu itaachwa iwe katika mlengo unaowafaa wao,maana wanajua ngozi nyeusi ni bora katika upande gani(wanaogopa),hivyo mbinu ambayo hutumiwa ni kuvuruga mifumo ya elimu kupitia viongozi(matumbotumbo),na kuiondolea ubora unaotakiwa kabisa.
angalia china na japan,wao mfumo wao ni mtoto chini ya miaka 5 anafundishwa elimu ya mahusiano tu sio kusoma wala kuandika,ndipo uzalendo na siha njema mtoto anakua nao kuanzia hapa.huu ni mfumo waliuchagua wao wakauandaa uwafae wao.sisi tunabeba mitaala ya kujifunza lugha ya kiingereza badala ya kujifunza ujuzi na taaluma za kwao.sijui kiingereza kina faina gani na maendeleo yetu!!!
tabia hii ya kutothamini vya kwetu imeingia damuni,mpaka aliyefanikiwa kusoma kwao uzunguni anaona ni heri abaki huko,kuliko kuja kufanya kitu nyumbani.
nikukumbushe uwezo wa mtu mweusi.
angalia sekta za kichezo na burudani,waty weusi wametamalaki huko,hii ni kutaka kukumbusha tunaweza kufanya mambo makubwa sana nje ya elimu tulizoletewa,muhimu kujiamini tu.
hawa viongozi mawakala ndio wanasababisha africa miaka nenda rudi imesimama tu,ndio maana walipojitokeza watu kama akina jpm ikabidi lifanyike jambo kwa haraka ili mambo yasiharibike.