Mungu ametupuuza sana watu weusi

Prof P.L.O Lumumba nilimsikiliza katika speech fulani alisema "we want to build roads and we have faculty of engineers complete with PhD and Professors but we go to china to bring a diploma holders to tell us how to build roads..."
 
Sijawahi fika mkuu, ila nasema tu mbelez kuko tofauti na huku, wenzetu mawazo yao yapo mbali, wanawaza mbali sana. Sisi hata matundu ya vyoo bado.
unajua hiyo Marekani ilpata uhuru wake lini, huko ustaarabu ulianza siku nyingi sana. Mwaka 1776 unafikiri Afrika ilikuwa wapi. Tulia maendeleo ni hatua hata hapa tulipo bado ni sahihi, miaka mingine 200 ijayo we unafikiri Afrika itakuwa wapi. Km Utakuwa una uwezo wa kuona kutoka utakapokuwa utaona mwenyewe kuwa Afrika itakuwa km huko Marekani pengine na zaidi.
 

unawaza madaraja na ajira za lakini 2!!!

njaa zinafanya mnawaza vitu kwa udogo sana.
 
Kitu cha kuangalia ni je hayo mataifa yamepataje utajiri wake? Kama kuna wizi,ufisadi,uuaji,uuzaji wa watumwa,ulafi, ukandamizaji wa kila aina na kila aina ya ukiukwaji wa utu basi ujue shetani katimiza lengo ili wewe uweze kutenda dhambi kwa kumkufuru Mungu asiehusika. Shetani kakutengenezea illusion kwamba utajiri ni kuwa na mali nyingi za anasa na kakuziba akili ya kujiuiliza mambo kadhaa. Mbona Yesu aliishi kimasikini pamoja na wanafunzi wake!! Na aliwaambia nini matajiri na walafi wakubwa wa enzi zile au Mungu aliongea nini na matajiri wa enzi hizo wenye kupenda mali kuliko utu? Basi nakuomba badilisha kichwa chako cha habari na kiite kwanini shetani anawashusha waafrika? Mtu umeumbiwa mito milima mabonde maziwa misitu mizuri ardhi yenye rutuba yani umepewa nusu bustani ya Eden eti umelaaniwa duuh. Nani kakuambia utajiri ni magari ya kifahari maghorofa na majunk food? Muafrica umechagua kutamani mali ya wengine na kusahau kushukuru kwa ulichopewa ndo maana unazidi laaniwa sababu ya kukufuru Mungu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Huu ndio ukweli.
Black for slave
 
Ethiopia hali ya maisha ni duni that's why vijana wao wanakufa kwenye makontena makijaribu kwenda ng'ambo
 
Prof P.L.O Lumumba nilimsikiliza katika speech fulani alisema "we want to build roads and we have faculty of engineers complete with PhD and Professors but we go to china to bring a diploma holders to tell us how to build roads..."
Very sad indeed
 
India imepata uhuru mwaka 1947, china imepata uhuru mwaka 1949 katika hizo nchi mbili ambazo hatujapishana sana katika nyakati za kudai uhuru je, tunazifikia hizo nchi hata robo tu katika sekta yoyote.

Vietnam ambaye tulifanana Kila kitu mpaka sera za ujamaa, miaka kumi tu baada ya kupata uhuru nchi ikaingia vitani miaka ishirini anapigana vita mpaka mwaka 1976 vita vinaisha alikuwa hoi hasa kiuchumi,

Ndani ya miaka ishirini tu vietnam imebadilika Kila kitu huku sisi Bado tunaiomba serikali kujenga matundu ya vyoo. Kwa sasa huwezi kuifananisha Hanoi na Dodoma au Jiji la Hcmc na dar es salaam.

Huwezi tena kuiweka Vietnam na Tanzania kundi Moja kama ilivyokuwa miongo miwili nyuma. Race ya mwafrika kuna sehemu ilikosea inabidi tujitafakari tusiukimbie ukweli.
 
Sentensi ya mwisho umeongea ukweli sana mkuu. Yaani ni kama vile walienda kutalii na wakirudi na story za huko na kujiona wajanja kwa kuwa wamefika na kuishi ng'ambo.

Kinachobaki ni kutamba na CV mtaani na kutuibia tu. Mara utaskia ooh Prof. fulani, ooh Dr. fulani, ooh sijui Eng. fulani n. k. Yaani ni hovyo kabisa
 
Yawezekana huyu malaika aliyetumwa kwenda kukusanya udongo wa kumuumba mtu mweusi kuna kitu alisahau kuchukua
 
Hakuna alieumba chochote it just happened
 
Umeeleza vema kabisa. Weusi au weupe wa ngozi ya mtu hauna uhusiano kabisa na akili yake. Nasisitiza kuwa akili inakuwa kichwani, si kwenye ngozi!

Kuna watu weusi wamefanikiwa "against all odds" katika maisha na kuajiri hata wazungu. Wapo wazungu, wahindi, wachina nk.; nao ni watupu kabisa kichwani japo si wote.

Pia tukumbuke kuwa waafrika wamepitia madhila na mateso mengi mno pengine kuzidi watu wengine wote duniani. Hata hivyo, tusijidharau na kulemaa. Success is all about positive attitudes, creative thinking and unwavering struggle. Na Mungu hana upendeleo!
 
Safi sana, maelezo murua!
 
Ulivyosema kuwa watu weusi wamepitia madhila, ndio umezidi kusisitiza kuhusu akili ndogo ya mtu mweusi.

Ilikuwaje wakatawaliwa, na kwanini hadi sasa bado tunatawaliwa.?

Kwanini kila kukicha Waafrica wanakimbilia Ulaya na Marekani??
 
We Acha tu! Hata Wazungu walipotuletea dini zao, kielelezo cha Yesu ni picha nyeupe yenye kuvutia na kielelezo cha shetani ni picha nyeusi ya kutisha na macho ya ajabu tena mekundu. Nadiriki kusema "dini zao" kwani ni biashara na sio neno la Mungu.
 
Sasa mbona hao blacks wanaosoma mitaala sawa na hao weupe huko ulaya wanabehaves the same na sisi tulio africa
 
Wazungu wamekubrainwash sana dada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…