Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Kwa taarifa yenu wanaomuabudu Mungu wa kweli pasipo kupitia kwa hao yesu na muhamad ndiyo watakaouona Ufalme wa mbinguni.

Bila shaka kabisa.
 
Unaongea kitu baada ya kufikiri na kutafakari au unaongea tu kwa kuwa ulizaliwa na kulishwa hivyo hadi ukubwani mwako.

Huyo yesu wako aliiokoa dunia yote au Afrika tu?

Huko Uchina,India,palestina,mongolia,UAE,nk nako yesu aliwaokoa?

Kama yesu aliwaokoa wanadamu wote kwanini kuwe na dini tofauti na ya kwake?

Jiongeze siyo kila kitu ukiamini kama ulivyokikuta kuwa mdadisi.
 
Huyo Neno ni Yesu
 
Kwahiyo wasiomwabudu yesu hawataenda mbinguni kwa akili yako?

Siyo akili yangu mzee, ni maandiko
Yesu anasema
Yohana : 14 : 6 - Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Niambie wewe ni njia gani nyingine ya kufika mbinguni isipokuwa Yesu.
 
Kwa taarifa yenu wanaomuabudu Mungu wa kweli pasipo kupitia kwa hao yesu na muhamad ndiyo watakaouona Ufalme wa mbinguni.

Bila shaka kabisa.

Miungu ni wengi mzee, Mungu wa pekee wa kweli ni aliyemtuma mwanawe Yesu Kristo . Wengine wote ni wa mchongo
 
Kwa taarifa yenu wanaomuabudu Mungu wa kweli pasipo kupitia kwa hao yesu na muhamad ndiyo watakaouona Ufalme wa mbinguni.

Bila shaka kabisa.
Wewe umejuaaje Kuna Mungu wa kweli ?
 
Akili za binaadamu si kama mashine hivyo tunatofautiana kwenye uelewa wewe unaweza kuelewa hivi na mwengine vile, mfano wewe akili yako imekubaliana na hayo yote unayoyaeleza humu kuhusu mungu ila mwengine ataona unayoeleza haya make sense kabisa.
 
Miungu ni wengi mzee, Mungu wa pekee wa kweli ni aliyemtuma mwanawe Yesu Kristo . Wengine wote ni wa mchongo
Mungu aliyemtuma mwanae au ndio yeye mwenyewe alijituma? ukisema Mungu aliyemtuma mwanae ndio Mungu pekee wa kweli maana yake huyo aliiyetumwa(Yesu kristo) si Mungu wa kweli ila wa kweli ni yule tu aliyemtuma.
 
Wewe wasema
 
Mungu anaweza yote, ni mwenye nguvu kuliko kiumbe chochote, mungu hajibu popote yeye ndo mkuu. Kulikuwa na haja gani ya kusumbuka hivyo kutusamehe dhambi huku ye ndo mkubwa kwanini asinge samehe tu
 
Uhai wake ulitakiwa kutumika kulipa madeni uetu ya dhambi sasa kwanini tena alifufuka alitakiwa kufa mazima
 
Bibie Faiza umezidiwa hoja.
Ushauri
Mkiri Yesu, ubatizwe, upate uzima wa milele katika yeye.
BILA YESU MBINGUNI HUTOBOI
Siioni hoja, naona viroja. Swali nililomuuliza yeye ntakuuliza wewe.

Unamuamini Allah?

Ukiongelea kuhusu Yesu alayhi salaam, elewa kuwa hakuna kuwa Muislam kama humuamini na kufata mafundisho ya Yesu. Jiulize wewe, unamfata Yesu au unamfata mzungu aliyetundikwa msalabani kwa laana?
 
Akili za binaadamu si kama mashine hivyo tunatofautiana kwenye uelewa wewe unaweza kuelewa hivi na mwengine vile, mfano wewe akili yako imekubaliana na hayo yote unayoyaeleza humu kuhusu mungu ila mwengine ataona unayoeleza haya make sense kabisa.
Ndio ndugu. Ndio maana Nikatanguliza Neno Akili Timamu. Kila Mtu ana Akili Zake ila si Kila Mtu ana Akili Timamu
 
Mungu anaweza yote, ni mwenye nguvu kuliko kiumbe chochote, mungu hajibu popote yeye ndo mkuu. Kulikuwa na haja gani ya kusumbuka hivyo kutusamehe dhambi huku ye ndo mkubwa kwanini asinge samehe tu
Ndicho nilichouliza Ndugu yangu. Aliogopa Nini au Sisi Anatuogopa Nini Mpaka Atutolee Sadaka Ya Mwanae
 
Ndio ndugu. Ndio maana Nikatanguliza Neno Akili Timamu. Kila Mtu ana Akili Zake ila si Kila Mtu ana Akili Timamu
Kwahiyo wewe unayeamini hivyo unavyoamini ndio una akili timamu na wasioamini unavyoamini wewe hawana akili timamu?
 
Kwahiyo wewe unayeamini hivyo unavyoamini ndio una akili timamu na wasioamini unavyoamini wewe hawana akili timamu?
Sijasema ninayoamini Mm ndio ukiyaamini ndio unakuwa na Akili Timamu. Akili Timamu ni Uwezo wa Kuchambua ukweli na Uongo katika Jambo Lolote Linalokuja kwako.

Ndio maana Silazimishi mtu kuyaaamini Haya niyasemayo Ila Yeye Mwenyewe Achambue Kama Yana Ukweli au Laah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…