Kwanza Alikufa na Kufufuka kwa Ajili yangu kwanini. Kwani Mimi Nilifanya Nini mpaka Yeye aje Anifie Msalabani. Nilifanya Jambo gani mpaka Yeye aje Afe Hivyo Mie nilikuwa Afrika huku Yeye Yupo Israeli
Kuamini Kunakuja Baada ya Kuambiwa Ukweli ukisema Ukweli unaoingia Akilini watu watakuamini sana Tu.
Yaani Mtu atoke zaks Huko Uingereza au Sudani aje Aswme nimekuja Kufa Kwa Ajili yako. Si hata Ww utashangaa Utauliza kwani nimefanya Nini mpaka Uje Ufe kwa Ajili yangu
Waefeso 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
² ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
³ ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
⁴ Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda;
⁵ hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
⁶ Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
⁷ ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
⁸ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
⁹ wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
¹⁰ Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Wanadamu wote walikuwa wamekufa kiroho (kutengwa na Mungu) hapo dhambi ilipoingia kupitia kwa Adamu na wote waliozaliwa baada yake walizaliwa katika hali hiyo hiyo ya roho zao kuwa zimetengwa na Mungu.
Hakuna namna mfu anaweza kujiokoa mwenyewe au kujihuisha mwenyewe yaani kujirejesha tena katika ushirika ule wa mwanzo mwenyewe au kwa jitihada zake mwenyewe.
Hapo ilibidi Mungu mwenyewe kufanyika mwili ili kumkomboa mwanadamu aliyekufa sababu ya dhambi (kumbuka kifo alichokufa usidhani ni cha kimwil bali cha kiroho)
Mwanadamu huyu angekuwa hai tena katika roho yake kwa kuamini tu Yesu Kristo (yaani Mungu katika mwili) alikufa na kufufuka kwa ajili yake ili awe hai milele.
Hapo roho ya Mungu wakati huohuo huizaa upya na kukaa milele ndani ya roho ya mtu huyo.
Unaamini hivyo?