Mungu anaweza kutenda dhambi?

Mungu anaweza kutenda dhambi?

Yanayo ila majibu yake yatazaa maswali zaidi na majibu maswali zaidi na majibu maswali zaidi, na majibu maswali zaidi, na majibu maswali zaidi to infinity. Kwa sababu tunataka kuichunguza nguvu ambayo bado hatuielewi.
Sawa, we have time.
Anza kutoa majibu ili twende till infinity
 
Wakulungwa vipi?

Kuna swali huwa linanitatisha.

Kama tuliambiwa Mungu anaweza kila kitu.

Na mungu ana free will.

Je, Mungu anaweza kutenda dhambi?
Katu, Kamwe Mungu hawezi kutenda dhambi.

Ni MTAKATIFU mnoo
 
Sasa ushavielewa alivyokuwekea huko mwilini ukavimaliza mpaka uhamie kwenye MUNGU mwenyewe?

Embu tumia muda tu kuchunguza mfumo wa pua yako unavyotoa kamasi na kamasi zinavyotengenezwa na ni kwann zina chumvi chumvi, ukitoka hapo amia kitu kingine hivyo hivyo ukimaliza utamfikiria MUNGU kwa mtazamo tofauti.
Mbona kama unanitisha?
 
Sababu ni kwamba, hizo sheria ndio mamlaka yenyewe.

Naona huku watu wanasema ooh, kamtupa shetani duniani, iyo ndio dhambi kubwa. Huo mfano watu wanauita shetani, hauvunji sheria hata chembe.

Analogy ntakayotumia hapa, ni kwamba 'SIKU' ina 'mchana' na ina 'usiku'. Bila mchana hautojua umuhimu wa usiku, na pia bila usiku, umuhimu wa mchana hautoonekana.

Yani kila kitu kina purpose yake tayari.

Kwa hiyo usisema Mungu, ni kama umesema SIKU. Yani kwamba tegemea mwanga na giza humo humo.
Ahaaa...kwahyo tunakosea pale tunaposema Mungu anaweza kila kitu.
Kwamfano wako wa mwanga na giza, ni kuwa lazima zijitofautishe.
Na mwanga hauwezi kuwa giza maana utabadili purpose yake.
Kwahyo Mungu nayeye ana purpose yake ambayo hawezi kuikiuka.
Hivyo kuna vitu ambavyo hawezi kufanya.
Uwezo wake umeishia hapo.
Mfano Uongo, Mungu hata ajikazaje, hawezi kudaganya maana atabadili purpose yake.
Nmekuelewa vyema mkuu🤝🤝
 
Unakufuru ndugu yangu.
Heri hujui ulisemalo.
Mungu ni MWANZO na MWISHO(Alpha na Omega), wa lolote ulijualo na usilolijua.

Mungu kupitia mwanawe Yesu Kristo, ndiye MWANZO, NJIA na UZIMA.
Soma Neno la Uzima upate kukua.
Sawa mkuu, kwahyo Mungu hawezi kufanya uovu kwa kuwa ndiye njia ya uzima?
Kwahyo hana free will?
Kuna vitu HAWEZI kufanya hata ajikazaje?
Mf. Kudanganya
 
Kwanza lazima utambua kuwa Mungu aliangamiza Dunia mara moja. Kupitia Gharika kuna uzao wa malaika walioasi waliopowaingilia wanadamu wanawake na kupata watoto ambao walikuwa na tabia mchanganyiko.
Baada ya hiyo Gharika hiko kizazi kikafutika.

Kuhusu Dhambi ya Uzinzi Mungu aliangamiza Sodoma na Gomora sehem 2,

Iko kitu unacho kitaka wewe kitakuwepo na hizo Dhambi zitakoma. Pale ambao Mji Mpya utashuka.
Wakati ambao Maadui wamewekwa Chini ya Miguu.
Swali langu bado hujalitendea haki

Hao nephilim unaowazungumzia, Bible imewataja kwenye geneis 6, wakati sodoma na gomora imetajwa Genesis 19

Kwa maana hiyo ni kwamba tukio la sodoma na gomora lilitanguliwa na hao malaika waliohasi

Mungu alipokuja kuangamiza hicho kizazi kilichokuwa kina shiriki kufanya hiyo dhambi alikuwa na target ya kutokomeza kabisa na ndio maana kwa mujibu wako umesema akaamua kuua hadi vitoto vidogo ambavyo vilikuwa vimerithi kwa wazazi wao.

Sasa mbona dhambi ile bado ipo?

Imetokea wapi ikiwa Mungu aliangamiza mizizi ambayo baadaye ingeweza kuleta maafa kama ya mwanzo?

Kama dhambi hii imeweza kuwepo licha ya kuwa wale watu waliuwawa, huoni kama suluhu ya Mungu kuuwa watoto yalikuwa si maamuzi sahihi?

Dhambi hii ambayo iko sasa unafikiri nani wakumpa lawama kwa uwepo wake ikiwa Mungu alifanya kila kitu kuhakikisha haiwezi kuwepo tena?
 
Kipindi unakuja DSM uliomba Mungu akusaidie. Leo unamuona Mungu hana maana siyo?

Acha mambo ya ajabu mkuu.
Mimi wakati nakuja dar sikuomba Mungu anisaidie,
Najua Mungu hawezi kunipa msaada wowote, kwahiyo huwa sihangaiki kumuomba kwakuwa hayupo.
Mimi wakati nakuja Dar niliwaomba wanadamu wenzangu na wakanisaidia.

Maisha yangu yote nasaidiwa na wanadamu, wala siyo Mungu.

Lete ushahidi wa sehemu niliyoandika kuwa namuomba Mungu.
 
Ahaaa...kwahyo tunakosea pale tunaposema Mungu anaweza kila kitu.
Kwamfano wako wa mwanga na giza, ni kuwa lazima zijitofautishe.
Na mwanga hauwezi kuwa giza maana utabadili purpose yake.
Kwahyo Mungu nayeye ana purpose yake ambayo hawezi kuikiuka.
Hivyo kuna vitu ambavyo hawezi kufanya.
Uwezo wake umeishia hapo.
Mfano Uongo, Mungu hata ajikazaje, hawezi kudaganya maana atabadili purpose yake.
Nmekuelewa vyema mkuu🤝🤝
Ni kama unanipata,
Yaani, ukianza kutofautisha kati ya Mungu na Shetani...unapoteza 'the big picture'....
Ni kama kuona mtu ni ule mwili wake tu, wakati...vyote lazima vishabiiane.

Ukitazama kwa makini, hutojua ni saa ngapi mchana unakuwa usiku...yani unajikuta tu, imekuwa.

Sasa basi, sisi tunayo limit yetu ambayo tayari kwa kifikra, hatuna lugha picha au mfano wa kueleza ishu za baada ya hiyo limit. Ndio maana tunampersonify 'Mungu' ili tu iyo phenomenon itoshee kwenye mawasiliano yetu.

Lakini ukweli ni kwamba Mungu yuko beyond personality complex...ambayo inaeleweka, lakini hailezewi. Yani unaweza ukaelewa, na usiweze kuelezea. Ndio maana utaskia vitu kama, anaweza kuona future past na present(maana yake ni kwamba ni beyond time-ambayo sisi hapo tuma limit). Swala la time unaweza ukajionea hata hapa duniani kwamba inaweza ikawa mchana hapa, lakini saa hiyo hiyo pale marekani ni usiku.

Utasikia, Mungu yuko kila pahali(maana yake, ni beyond limit yetu ya space)...sasa hii itakuchanganya pale unaposema, 'yuko' au 'yeye' au 'ana'....maanake ukipersonify, inashindwa kueleweka maana ya kuwa beyond space.

Yani...akifanya kitu, huwa hakina mwisho, ni sawa na alifanya halafu bado anafanya. Hakuna wakati kwamba hapa ndio kinaanza kufanyika, ama hapa ndio kinaishia.

Na nikujulishe, vitabu vyetu vya dini, huwa tunaona tu aspect ama viumbe vya Mungu(ambavyo vitajiita Mungu), mkuu mwenyewe hawezi kufit kwenye historia au maneno, maana historia ina limits.

Yani ukiangalia tu kwa umakini, utanotice 'to be' ndio tunaipersonify kuwa Mungu.
 
Swali langu bado hujalitendea haki

Hao nephilim unaowazungumzia, Bible imewataja kwenye geneis 6, wakati sodoma na gomora imetajwa Genesis 19

Kwa maana hiyo ni kwamba tukio la sodoma na gomora lilitanguliwa na hao malaika waliohasi

Mungu alipokuja kuangamiza hicho kizazi kilichokuwa kina shiriki kufanya hiyo dhambi alikuwa na target ya kutokomeza kabisa na ndio maana kwa mujibu wako umesema akaamua kuua hadi vitoto vidogo ambavyo vilikuwa vimerithi kwa wazazi wao.

Sasa mbona dhambi ile bado ipo?

Imetokea wapi ikiwa Mungu aliangamiza mizizi ambayo baadaye ingeweza kuleta maafa kama ya mwanzo?

Kama dhambi hii imeweza kuwepo licha ya kuwa wale watu waliuwawa, huoni kama suluhu ya Mungu kuuwa watoto yalikuwa si maamuzi sahihi?

Dhambi hii ambayo iko sasa unafikiri nani wakumpa lawama kwa uwepo wake ikiwa Mungu alifanya kila kitu kuhakikisha haiwezi kuwepo tena?
Mbona unachanganya Habari Kuwaamgamizi watoto wachanga Mungu aliwaambia watu wa Amaleki.

Lazima ujuwe kuwa Sodoma na Gomora alivyoangamizwa kulikuwepo na Miji mingine. Watu wa Sodoma na Gomora walikuwa wanasafiri kuelekea kwenye Miji kuna mambo walikuwa wanaeneza.

Hizo Dhambi ya uzinzi inachochewa na mapepo na Shetan yeye atakapoangamizwa hivyo vitu havitakuwepo
Hiyo Dhambi lawama itaenda kwa Mwanadamu atakayevutwa na Tamaa Siyo wanadamu wote wazinzi
 
Mfano ukijiwekea sheria kwamba hautakuwa unakunywa soda. Siku ukijisahau ukanywa si utagundua umefanya makosa?
Shida sio nani katendewa, shida ni kwenda kinyume na sheria alizoziweka.
Je akiamua kuua mtu au kumtesa asiye na hatia?(mf. Alivyomfanyia Ayubu)
Hajajiwekea sheria au amri.Kawawekea binadamu.
 
Mbona unachanganya Habari Kuwaamgamizi watoto wachanga Mungu aliwaambia watu wa Amaleki.

Lazima ujuwe kuwa Sodoma na Gomora alivyoangamizwa kulikuwepo na Miji mingine. Watu wa Sodoma na Gomora walikuwa wanasafiri kuelekea kwenye Miji kuna mambo walikuwa wanaeneza.

Hizo Dhambi ya uzinzi inachochewa na mapepo na Shetan yeye atakapoangamizwa hivyo vitu havitakuwepo
Hiyo Dhambi lawama itaenda kwa Mwanadamu atakayevutwa na Tamaa Siyo wanadamu wote wazinzi
Nimeongea in general kwa maana ya kugusa stori zote mbili.

Mfano hoja kuhusu Amaleki niligusia hivi

Mungu kama aliangamiza kizazi cha Amaleki chote pamoja na watoto wachanga kwa lengo la kutokomeza dhambi, mbona bado dhambi hiyo inatendeka na watu wengine mpaka hivi sasa?

Sodoma na gomora nayo nilisema hivi

Mungu aliteketeza kile kizazi kwa moto ili kuifuta dhambi hiyo isiweze kufanyika, katika dunia hii ya kisasa still watu wanafanya hiyo dhambi. Imetoka wapi?

Jea Mungu hakuyaona haya kuwa yatajitokeza miaka ya mbele na dhana ya kufikiria kutokomeza hiyo dhambi kwa kuangamiza kizazi itakuwa ni kazi bure?
 
Back
Top Bottom