Ahaaa...kwahyo tunakosea pale tunaposema Mungu anaweza kila kitu.
Kwamfano wako wa mwanga na giza, ni kuwa lazima zijitofautishe.
Na mwanga hauwezi kuwa giza maana utabadili purpose yake.
Kwahyo Mungu nayeye ana purpose yake ambayo hawezi kuikiuka.
Hivyo kuna vitu ambavyo hawezi kufanya.
Uwezo wake umeishia hapo.
Mfano Uongo, Mungu hata ajikazaje, hawezi kudaganya maana atabadili purpose yake.
Nmekuelewa vyema mkuu🤝🤝
Ni kama unanipata,
Yaani, ukianza kutofautisha kati ya Mungu na Shetani...unapoteza 'the big picture'....
Ni kama kuona mtu ni ule mwili wake tu, wakati...vyote lazima vishabiiane.
Ukitazama kwa makini, hutojua ni saa ngapi mchana unakuwa usiku...yani unajikuta tu, imekuwa.
Sasa basi, sisi tunayo limit yetu ambayo tayari kwa kifikra, hatuna lugha picha au mfano wa kueleza ishu za baada ya hiyo limit. Ndio maana tunampersonify 'Mungu' ili tu iyo phenomenon itoshee kwenye mawasiliano yetu.
Lakini ukweli ni kwamba Mungu yuko beyond personality complex...ambayo inaeleweka, lakini hailezewi. Yani unaweza ukaelewa, na usiweze kuelezea. Ndio maana utaskia vitu kama, anaweza kuona future past na present(maana yake ni kwamba ni beyond time-ambayo sisi hapo tuma limit). Swala la time unaweza ukajionea hata hapa duniani kwamba inaweza ikawa mchana hapa, lakini saa hiyo hiyo pale marekani ni usiku.
Utasikia, Mungu yuko kila pahali(maana yake, ni beyond limit yetu ya space)...sasa hii itakuchanganya pale unaposema, 'yuko' au 'yeye' au 'ana'....maanake ukipersonify, inashindwa kueleweka maana ya kuwa beyond space.
Yani...akifanya kitu, huwa hakina mwisho, ni sawa na alifanya halafu bado anafanya. Hakuna wakati kwamba hapa ndio kinaanza kufanyika, ama hapa ndio kinaishia.
Na nikujulishe, vitabu vyetu vya dini, huwa tunaona tu aspect ama viumbe vya Mungu(ambavyo vitajiita Mungu), mkuu mwenyewe hawezi kufit kwenye historia au maneno, maana historia ina limits.
Yani ukiangalia tu kwa umakini, utanotice 'to be' ndio tunaipersonify kuwa Mungu.