Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Katika hao wa Amaleki waliohukumiwa kufa kumbuka kuna hadi watoto wanao nyonya nao wamejumuishwa1Samwel 15:3
Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda
Kosa la Amaleki walilofanya ni ili, wakastahili kupata walichopata
Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa
Kutoka 17:8. Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.
Torati 25:17-19
Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;
jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.
Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.
Mtoto anaye nyonya anawezaje kutenda dhambi kiasi umfanyie ukatili kama huo?