Mungu anaweza kutenda dhambi?

Wakulungwa vipi?

Kuna swali huwa linanitatisha.

Kama tuliambiwa Mungu anaweza kila kitu.

Na mungu ana free will.

Je, Mungu anaweza kutenda dhambi?
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Luka 6:44

Mungu ni asili na chanzo cha wema, kamwe hawezi kuwa muovu.
 
DHAMBI NI KILE MUNGU AMEKATAZA KWAHIYO HAWEZI KUFANYA DHAMBI KWASABABU YEYE NDIO ANAAMUA IPI NI DHAMBI NA IPI SIO.
Tuseme ameamua A ni dhambi.
Nayeye ana uwezo wa kufanya kila kitu(omnipotence)
Hawezi kuifanya hiyo A?
Hawezi kufanya dhambi?
 
Swali la mwanafunzi kumuuliza mwalimu kama anaweza kufeli mbona linamake sense?

Naku'quote "Dhambi ni uasi wa sheria. Sheria zipo kwa ajili ya binadamu."
Shetani na mapepo sio binadamu.
Je kina shetani hawana dhambi?
Okey, ongezea hapo dhambi ipo kwa ajili ya binadamu na viumbe alivyoviumba MUNGU yakiwepo hayo mashetani na mapepo.
 
Jibu ni Ndiyo

Katika amri kumi alizompa Musa, Mungu aliagiza kuwa "usiue"

Lakini wote tunakubaliana kuwa Gharika, sodoma na gomola yalikuwa ni mauaji ya kikatili mno yaliyo ratibiwa na Mungu mwenyewe.
Yalikuwa matokeo ya kutenda dhambi (kujitenga na Mungu - asili ya wema).
 
Tatizo mnamjadiri Mungu kama raisi au mfalme!
Yote yanayofanywa na viumbe wake yanapimwa kwa kanuni zake.
Kwahiyo hawez kutenda dhambi kwa sabab hawajibiki popote.
Hana wa kumkosea na hakosei.
Hawezi kukosea?
Kwahyo kumbe kuna vitu Mungu muweza wa vyote hawezi?
 
Kwa mujibu wa vitabu vya dini, Mungu amewahi kuua si mara moja wala si mtu mmoja.
ameua maelfu kwa maelfu.

Na bado hajaishia hapo ameandaa moto wa Jehanamu awachome wanadamu.

Mungu ni katili sana. hatupaswi kumnyenyekea katili hata kidogo
Kwanini lawama ya matokeo ya dhambi anabebeshwa Mungu badala ya mdhambi husika?
 
Waliniambia nisifanye ngono mpaka nikioa...kwahyo wao kwasababu wameoana walifanya na sikuwaona kama wanafiki.
ila wangeniambia usile kitimoto, halafu wao wakawa wanakula, ningewaona manafiki
Na MUNGU naye ameakuambia usitende dhambi mpaka pale atakapotoa utaratibu mwingine.

Kuna amabo wanaamini huko mbinguni kuna wanawake wa kujipigia utakavyo, utaratibu ambao duniani hapa kidogo ni tofauti.
 
Na MUNGU naye ameakuambia usitende dhambi mpaka pale atakapotoa utaratibu mwingine.

Kuna amabo wanaamini huko mbinguni kuna wanawake wa kujipigia utakavyo, utaratibu ambao duniani hapa kidogo ni tofauti.
Kwahyo Mungu hana utaratibu aliojiwekea?
Mungu hana consistency?
 
Tuseme ameamua A ni dhambi.
Nayeye ana uwezo wa kufanya kila kitu(omnipotence)
Hawezi kuifanya hiyo A?
Hawezi kufanya dhambi?
Swali lako halina mantiki katika kumzungumzia Mungu unless kama unadhani yeye ni jamaa anayebadilika kulingana na mazingira
 
Yeah, that would be the perfect God.
ila unaweza kuandika hiyo Novel hujachelewa.
Mbona hizi Quran na Bible wameandika hata sio zamani sana
 
Kwahyo Mungu hana utaratibu aliojiwekea?
Mungu hana consistency?
Utaratibu wake upo kama ulivyo kutaka kuuelewa ni sawa na doli lililotengeezwa na mwanadamu kujaribu kumuelewa mwanadamu. Kabla ya kumuelewa MUNGU kwann tusielewe kwanza nguvu iliyopo ndani yetu inayosababisha uhai? Utapasuka msamba bure.
 
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Luka 6:44

Mungu ni asili na chanzo cha wema, kamwe hawezi kuwa muovu.
Kwahyo kumbe kuna vitu Mungu muweza wa vyote hawezi kufanya. Kama kutenda uovu.
Kumbe sasa sio muweza wa vyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…