Kwa hiyo unaje.ga hoja kusema Mungu hufanya mauaji kwa watu wenye dhambi tu na sio kwa watu wasio na hatia?
Vipi kuhusu Samweli 15:3
1Samwel 15:3
Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda
Kosa la Amaleki walilofanya ni ili, wakastahili kupata walichopata
Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa
Kutoka 17:8. Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.
Torati 25:17-19
Kumbuka aliyokufanya Amaleki katika njia mlipokuwa mkitoka Misri;
jinsi alivyokukuta katika njia, akapiga katika watu wako walioachwa nyuma, wote waliokuwa wanyonge nyuma yako, ulipokuwa umechoka na kuzimia; wala asimche Mungu.
Basi itakuwa, hapo atakapokwisha kukupumzisha BWANA, Mungu wako, katika adui zako wote walio kando-kando, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi uimiliki, ndipo uufute ukumbuko wa Amaleki chini ya mbingu; usisahau.