Mungu anaweza kutenda dhambi?

Mungu anaweza kutenda dhambi?

Sijakuelewa

Yani unapinga kwamba Ghatika, Sodoma na gomora sio vipindi ambavyo Mungu alikuwa akiteketeza watu au namna gani?

Au unakubali kuwa Gharika, Sodoma na Gomora yalikuwa ni maangamizi ila wewe unayatafsiri kwa namna yako kuwa Mungu kuangamiza watu hao sio jambo la kumhusisha na dhambi?
Ndiyo

Hayo yalitokea ndiyo lakini ni Consequences za mambo yaliyotokana na uharibifu huo...

Hebu rudi nyuma kidogo...

Kwani Genocide iliyotokea kwa wenzetu jirani hapo Rwanda unadhani ni Hasira ya Mungu?

Ni kiasi cha juu cha GREEDY na Ethnicity...

Hicho tu!

Lakini watu waliteketea kwa malaki!!
 
Kwa mujibu wa vitabu vya dini, Mungu amewahi kuua si mara moja wala si mtu mmoja.
ameua maelfu kwa maelfu.

Na bado hajaishia hapo ameandaa moto wa Jehanamu awachome wanadamu.

Mungu ni katili sana. hatupaswi kumnyenyekea katili hata kidogo
Kipindi unakuja DSM uliomba Mungu akusaidie. Leo unamuona Mungu hana maana siyo?
 
Dhambi ni uasi wa binadamu wa sheria za MUNGU. Na ukitaka kujua kuwa ni kwa ajili ya mwanadamu na si MUNGU zigeuze.

Usiue sisi tuue, Usizeme uongo sisi tuseme uongo, Usizini sisi wote tuzini bila mipaka, Waheshimu baba yako na mama yako we tusiwaheshimu kisha tuone tutakuwa na jamii ya aina gani.
Kwahyo Mungu hawezi kusema uongo?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Baba kamzaa mtoto akiwa amemrithisha uovu wake, hakukuwa na makubaliano kati ya baba na mtoto kuwa huu uovu nakuachia na mtoto akakubali.

Mtoto amejikuta tu amezaliwa na huo uovu, hapo kosa la mtoto hapo liko wapi?

Kama Mungu alioa kuua watoto wachanga waliorithi dhambi kutoka kwa wazazi wao ndio suluhu, kwanini bado kuna wimbi la watu wanaoendelea kutenda dhambi zile zile ambazo Mungu aliangamiza hadi watoto ili kuzifuta zisiwepo kwenye uso wa dunia?

Hizi Dhambi zimetoka wapi?
Watoto wachanga ni Taifa la Kesho . Utakapowaacha wasiuliwe shida. Matatizo ya Israel na Palestina chanzo ni hiki. Israel walipewa naelekezo ya kusafisha majirani waangamizi kabisa aliye Mkubwa mpaka Mdogo.

Unapuacha Mtoto mdogo na kuangamiza wakubwa, yule mtoto akikua atambiwa sababu ya kuwa yatima, wazazi wake waliuliwa kivyovyote vile Mtoto atakapokuwa Mtu mzima lazima alipize kisasi ndipo pale Ugomvi usioisha.

Israel na Palestina Amani kupatikana lazima Taifa 1 lifutwa kuanzia Mkubwa mpka Mtoto mchanga.
Hakutakuwa na uovu utakaopitiliza kutoka kwa kizazi 1 mpaka kingine.
Kuna aina 2 za binadamu wanaoshi, kuna binadamu ambao ni halisi na siyo halisa. Kuna Dhambi zingine zinafanywa na binadamu ambao siyo halisi ili binadamu halisi wafuate njia zao.
 
Huyohuyo aliyeniumba mimi na wewe
Sasa ushavielewa alivyokuwekea huko mwilini ukavimaliza mpaka uhamie kwenye MUNGU mwenyewe?

Embu tumia muda tu kuchunguza mfumo wa pua yako unavyotoa kamasi na kamasi zinavyotengenezwa na ni kwann zina chumvi chumvi, ukitoka hapo amia kitu kingine hivyo hivyo ukimaliza utamfikiria MUNGU kwa mtazamo tofauti.
 
Mi sina la kumfanya, sema nlitaka kujua tu kama huo uwezo wa kutenda dhambi anao
kisu kinaweza kuua ? ndio kma kisu kinaweza kuua je kisu ni kibaya jibu ni hapana , ila mtumiaji wa kisu ni mbaya , kisu kpo stationary ni vile tu mtumiaji achague kwa matumuzi yapi , Mungu ni nguvu hiyo nguvu ipo ww tu uchague uitumie vpi ( uwezo wa kuchagua mema au mabaya) mimi sio muumini wamoja kwa moja wa kila kilichopo kwenye vitabu vya din mengne nachuja kulingana na wakati uliopo.
 
Hawezi kukosea?
Kwahyo kumbe kuna vitu Mungu muweza wa vyote hawezi?
We kiboko!
nakosa lugha nzuri ya "act" na "omission" kiswahili hakijanitosha.
Lakin nijuavyo Mungu ni purity. Yan utakatifu wenyewe. Mtakatifu wa watakatifu!
Mungu ni kika aina ya jambo zuri na jema bika kinyume chake mle mle. Kama ilivyo, shetan ni kila ubaya na mabaya yote.
Mungu hana kipimo had ipatikane dhambi na kutokuwepo dhambi. Mungu ni mkamilifu. Dhambi huelezea sisi viumbe wake (watu na malaika) katika kutokamilika kwetu.
Hata hivi ni kwamba Mungu hajadiriki kwa hivi kana kwamba tunamjadiri Lugola. Huku ni kukwepa majukum ya msingi dhidi yetu na jamii zetu.
 
Watoto wachanga ni Taifa la Kesho . Utakapowaacha wasiuliwe shida. Matatizo ya Israel na Palestina chanzo ni hiki. Israel walipewa naelekezo ya kusafisha majirani waangamizi kabisa aliye Mkubwa mpaka Mdogo.

Unapuacha Mtoto mdogo na kuangamiza wakubwa, yule mtoto akikua atambiwa sababu ya kuwa yatima, wazazi wake waliuliwa kivyovyote vile Mtoto atakapokuwa Mtu mzima lazima alipize kisasi ndipo pale Ugomvi usioisha.

Israel na Palestina Amani kupatikana lazima Taifa 1 lifutwa kuanzia Mkubwa mpka Mtoto mchanga.
Hakutakuwa na uovu utakaopitiliza kutoka kwa kizazi 1 mpaka kingine.
Kuna aina 2 za binadamu wanaoshi, kuna binadamu ambao ni halisi na siyo halisa. Kuna Dhambi zingine zinafanywa na binadamu ambao siyo halisi ili binadamu halisi wafuate njia zao.
Hujaelewa hoja yangu, ngoja niiweke hapa vizuri

Mungu kaona watu wanafanya dhambi ya uzinzi

Mungu akakasirishwa na dhambi hizo na sasa anaamua kudili na watu hao kuhakikisha anakomesha dhambi hiyo.

Katika namna ya kuondoa hizo dhambi akaona njia sahihi ni kuangamiza kizazi chote ambacho kinahusika na dhambi hiyo.

Kizazi chenye mchanganyiko wa wakubwa na watoto, anafanya hivyo kuwajumuisha na watoto wachanga kwa lengo la kuzuia uwezekano wa kuwepo wazinzi hapo baadaye kutokana na kwamba hao watoto wamerithi ile roho ya dhambi hizo.

Mungu akaangiza hao watu wazima pamoja na watoto wachanga ambao wana link kwenye dhambi hiyo.

Lakini baada ya muda katika ulimwengu huo huo aliofanya maangamizi, tunakuja kuona dhambi ya uzinzi bado ipo, licha ya kuwa huko nyuma alikwisha safisha kila kitu.

Maswali ya kujiuliza

Kwanini tena kuwe na muendelezo wa dhambi hii wakati wale waliokuwa na roho ya kufanya dhambi hii walikwisha kuteketezwa na waliobaki walikuwa ni watu wema?

Kama Mungu aliamua kuangamiza watoto wachanga wasiojua jema wala baya kwa lenho la kuzuia dhambi ya uzinzi halafu tunakuja tena kuona uzizi upo, huoni kuwa hao watoto waliuwawa kwa kuonewa?

Au siku ambayo Mungu alikuwa anataka kutekeleza mauaji kwa watoto wachanga, vision yake haikufika angle ya umbali huu kujua kuwa hata nikiwaua hawa watoto bado ni kazi bure kwasababu huko mbeleni nimeona hii dhambi bado ikifanyika?
 
Kwahyo tukubaliane sasa, mungu sio muweza wa vyote?
kwann unataka kutumia ubaya wa uchafu kuthibitisha uzuri wa usafi?

Mfano: ww huwezi shika mimba sababu huna mfuko wa uzazi, hata ukipewa mbengu ndoo nzima zoezi haliwezekani sababu mfumo wako hauruhusu, je hujakamilika sababu huwezi kushika mimba?

MUNGU ni mkamilifu katika usafi sio katika dhambi au uchafu. Huwezi sema MUNGU hawezi yote sababu hadanganyi. Uongo si sehemu ya kipimo cha uwezo wake kama ambavyo haiwezekani kupima ukamilifu wa mwanaume kwa kubeba ujauzito.
 
Sodoma na gomola haikuwa gharika bali ilikuwa ni vita vya high tech, nyuklia.
 
Sababu ni kwamba, hizo sheria ndio mamlaka yenyewe.

Naona huku watu wanasema ooh, kamtupa shetani duniani, iyo ndio dhambi kubwa. Huo mfano watu wanauita shetani, hauvunji sheria hata chembe.

Analogy ntakayotumia hapa, ni kwamba 'SIKU' ina 'mchana' na ina 'usiku'. Bila mchana hautojua umuhimu wa usiku, na pia bila usiku, umuhimu wa mchana hautoonekana.

Yani kila kitu kina purpose yake tayari.

Kwa hiyo usisema Mungu, ni kama umesema SIKU. Yani kwamba tegemea mwanga na giza humo humo.
 
Hujaelewa hoja yangu, ngoja niiweke hapa vizuri

Mungu kaona watu wanafanya dhambi ya uzinzi

Mungu akakasirishwa na dhambi hizo na sasa anaamua kudili na watu hao kuhakikisha anakomesha dhambi hiyo.

Katika namna ya kuondoa hizo dhambi akaona njia sahihi ni kuangamiza kizazi chote ambacho kinahusika na dhambi hiyo.

Kizazi chenye mchanganyiko wa wakubwa na watoto, anafanya hivyo kuwajumuisha na watoto wachanga kwa lengo la kuzuia uwezekano wa kuwepo wazinzi hapo baadaye kutokana na kwamba hao watoto wamerithi ile roho ya dhambi hizo.

Mungu akaangiza hao watu wazima pamoja na watoto wachanga ambao wana link kwenye dhambi hiyo.

Lakini baada ya muda katika ulimwengu huo huo aliofanya maangamizi, tunakuja kuona dhambi ya uzinzi bado ipo, licha ya kuwa huko nyuma alikwisha safisha kila kitu.

Maswali ya kujiuliza

Kwanini tena kuwe na muendelezo wa dhambi hii wakati wale waliokuwa na roho ya kufanya dhambi hii walikwisha kuteketezwa na waliobaki walikuwa ni watu wema?

Kama Mungu aliamua kuangamiza watoto wachanga wasiojua jema wala baya kwa lenho la kuzuia dhambi ya uzinzi halafu tunakuja tena kuona uzizi upo, huoni kuwa hao watoto waliuwawa kwa kuonewa?

Au siku ambayo Mungu alikuwa anataka kutekeleza mauaji kwa watoto wachanga, vision yake haikufika angle ya umbali huu kujua kuwa hata nikiwaua hawa watoto bado ni kazi bure kwasababu huko mbeleni nimeona hii dhambi bado ikifanyika?
Kwanza lazima utambua kuwa Mungu aliangamiza Dunia mara moja. Kupitia Gharika kuna uzao wa malaika walioasi waliopowaingilia wanadamu wanawake na kupata watoto ambao walikuwa na tabia mchanganyiko.
Baada ya hiyo Gharika hiko kizazi kikafutika.

Kuhusu Dhambi ya Uzinzi Mungu aliangamiza Sodoma na Gomora sehem 2,

Iko kitu unacho kitaka wewe kitakuwepo na hizo Dhambi zitakoma. Pale ambao Mji Mpya utashuka.
Wakati ambao Maadui wamewekwa Chini ya Miguu.
 
Wakulungwa vipi?

Kuna swali huwa linanitatisha.

Kama tuliambiwa Mungu anaweza kila kitu.

Na mungu ana free will.

Je, Mungu anaweza kutenda dhambi?
Unakufuru ndugu yangu.
Heri hujui ulisemalo.
Mungu ni MWANZO na MWISHO(Alpha na Omega), wa lolote ulijualo na usilolijua.

Mungu kupitia mwanawe Yesu Kristo, ndiye MWANZO, NJIA na UZIMA.
Soma Neno la Uzima upate kukua.
 
Kwahyo hayana majibu?
Yanayo ila majibu yake yatazaa maswali zaidi na majibu maswali zaidi na majibu maswali zaidi, na majibu maswali zaidi, na majibu maswali zaidi to infinity. Kwa sababu tunataka kuichunguza nguvu ambayo bado hatuielewi.
 
Back
Top Bottom