Mungu hatetewi mnanishangaza mnaosema Mungu ni muweza wa yote alafu bado mnasimama kumtetea

Mungu hatetewi mnanishangaza mnaosema Mungu ni muweza wa yote alafu bado mnasimama kumtetea

Asante sana mkuu, sehemu kama hizi unapaswa kujifunza sio kushindana ushindani usio na msingi
Mkuu subir me nilikuwa nakupima tu me haya mambo ya Mungu sio vitu vyangu naamini kama yupo inatosha

Ila swali langu la kwanza nilikuuliza unaamini Mungu yupo maana sikuelewa mada yako unasimamia wapi ila ulinijibu unaamini halafu unalazimisha wengine wasiamini kama yupo shida ndiyo ilipoanzia
 
Mkuu sio kweli sijakulazimisha usiamini naona kuna kitu hakipo sawa
 
Na baada ya kumuasi na kumsaliti shida hizo zipi zipo kwa mungu au zipo kwa shetani na kwetu ?
Hana shida
Shida ni kwetu
Ila kuna vitu vinamuumiza sana
anaumia au anasikitika kuona watu wakifanya uasi

Mwanzo 6:5-6 (Biblia Takatifu):
“Bwana akaona ya kuwa uovu wa mwanadamu ni mwingi duniani, na kwamba kila kusudi la mawazo ya moyo wake ni maovu tu siku zote. Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyoni mwake.”
 
Nani kukwambia watu wanamtetea MUNGU? Kinachofanyika ni kuwakumbusha watu kuhusu MUNGU. Hao unaosema wanamtetea MUNGU ndio actually wanakutetea wewe. Siku wakiacha nakwambia ndani ya muda mfupi mabalaa yatatutokomeza wote na MUNGU atatufutilia mbali.
 
Mungu hatetewi mnanishangaza mnaosema mungu ni muweza wa yote alafu bado mnasimama kumtetea.

Kuna hawa sijui wanatetea uislam, sijui wanamtetea allah, kuna hawa sijui wanatetea ukristo sijui wanamtetea yesu. alafu hapo hapo wanakwambia mungu wetu sisi ni muweza wa yote.

Mungu hayupo hivyo nyinyi na hatetewi na mtu yoyote, kuweni na uhalisia kwa jinsi mnavyo tamka kuwa ni muweza wa yote basi na iwe hivyo sio mnaanza kumtetea tena wakati ni mwenye nguvu asiyeshindwa jambo lolote.

watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
YESU NI MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI. NA NDIYE ATAKAYE YAHUKUMU MATAIFA YOTE NA VIUMBE VYOTE. GEUKA UTUBU MAPEMA KWANI SIKU ZI KARIBU HAKUNA MUDA. BIBLIA INASEMA BAADA YA KIFO NI HUKUMU. YAANI BINADAMU AKIFA HAPOHAPO ROHO YAKE KUNA MAHALI INAKWENDA KWAAJILI YA KUSUBIRI SIKU YA HUKUMU.
 
Mkuu sio kweli sijakulazimisha usiamini naona kuna kitu hakipo sawa
Labda sikukuelewa mkuu acha nirudi kwenye nafasi yangu ya kufatilia mdahalo ila Cha muhimu uniambie we unaamini nini Mungu yupo na kama yupo ana muweza wa wote au hana nguvu za kuondoka shida....hii itanisaidia kuelewa point zako kwenye huu mdahalo
 
Nani kukwambia watu wanamtetea MUNGU? Kinachofanyika ni kuwakumbusha watu kuhusu MUNGU. Hao unaosema wanamtetea MUNGU ndio actually wanakutetea wewe. Siku wakiacha nakwambia ndani ya muda mfupi mabalaa yatatutokomeza wote na MUNGU atatufutilia mbali.
Kabisa
 
Hoja yako dhaifu sana Mungu muweza wa yote Kwanini asitumie uweza wake wa yote kuwakumbusha walio msahau Au kuwafahamisha Uwepo wake wale wasio mtambua ,

Yaani inakuwaje awe na uweza wa yote halafu Asubiri binaadamu ndio wamsaidie kuwa kumbusha watu wengine kuhusu Uwepo wake , kama mungu huyo alitumiwa uweza wake wa yote kuumba Dunia na Kila kilichopo bila kuhitahu msaada wa binaadamu Ina kuwaje tena yeye binafsi anashindwa kufanya jambo dogo kama Hilo la kuwakumbusha watu kuhusu Uwepo wake mpaka Asubiri kutetewa na binaadamu

Hivi inaingia akilini kweli !?

Mungu wenu ni wamchongo na Jamaa mtoa thread ana Hoja asikilizwe
 
Swali la kipumbavu mno ...kwani ni lazima ufanye yote unayo weza ?wewe mbona ipo hai mbona ukujiua na uwezo huo unao ? Je wewe mbona ukutembea uchi mitaani na uwezo huo wa kutembea uchi unap ..je mbona wewe leo ukutupa fedha mtaani na usezo huo unao ...kuweza na kutaka ni vitu viwili tofauti.
Nonsense huyo hajawahi kusema kuwa yeye anauweza wa yote , ndio maana amezaliwa ktk Dunia ambayo ndani yake amekuta Kuna Sheria zimetungwa na watu na analazimika kuzifuata by force (ndio maana hatembei uchi)

Angekuwa na huo uweza wa yote asinge diriki kuzifuata hizo Sheria angezivunja tu hadharani kweupe na hakuna ambaye angemfanya kitu maana yeye ni muweza wa yote

Halafu kuanza kumfananisha mungu mnaye mbrand kuwa ni muweza wa yote na binaadamu ambaye Hana huo uweza wa yote ni kuonyesha kwamba mungu wenu ni wamchongo tena sana , Ina kuwaje mungu muweza wa yote Afanane kimatendo na binaadamu!?
 
Vita
Ukiangalia Dunia na vilivyomo ndani yake lazma ujue kama Kuna muweza wa yote siyo lazma mpaka uambiwe kwenye vitabu vya dini
Vita zinazotokea huyo muweza wa Yote kwanini hazizuii

Wapalestina pale Ghaza eneo lao limegeuzwa kuwa gereza mbona huyo muweza wa Yote hajawatetea.

Vipi ajali za kutisha? Huyo muweza wa Yote ni muweza kwenye nini?
 
Nani kukwambia watu wanamtetea MUNGU? Kinachofanyika ni kuwakumbusha watu kuhusu MUNGU. Hao unaosema wanamtetea MUNGU ndio actually wanakutetea wewe. Siku wakiacha nakwambia ndani ya muda mfupi mabalaa yatatutokomeza wote na MUNGU atatufutilia mbali.
Mungu anaejua kesho yangu kabla hajaniumba inakuaje aniumbe nikiwa na akili za kutomtukuza halafu niliacha kumtukuza anihukum.
 
Back
Top Bottom