Mungu kwenye Quran kusema kwamba Jua hutuama kwenye kisima cha matope mazito alikuwa na maana gani?

Mungu kwenye Quran kusema kwamba Jua hutuama kwenye kisima cha matope mazito alikuwa na maana gani?

Aliyeona jua linazama kwenye matope ni huyo dhul Qarnain na si MUNGU.

hapo MUNGU anamsimulia muhammad ambaye hakuwepo wakati tukio linatokezea.

Yalaumiwe macho ya DHUL QARNAIN

Mwisho wa uelewa wangu
Kwaiyo Mungu na Mudy walikua wanalishana matango pori?
 
Umeambiwa kasome tafsiri ya aya kwa ibn kathir

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mimi namsoma binadamu yake Muhammad, tena Muhammad alimsifu akasema hakuna mfasiri hodari kama ibn Abbas

18:86 Abbas - Tanwîr al-Miqbâs min Tafsîr Ibn ‘Abbâs
(Till, when he reached the setting place of the sun) where the sun sets, (he found it setting in a muddy spring) a blackened, muddy and stinking spring; it is also said that this means: a hot spring, (and found a people thereabout) these people were disbelievers: (We said: O Dhu'l-Qarnayn!) We inspired him (Either punish) either kill them until they accept to believe that there is no deity except Allah (or show them kindness) or you pardon them and let them be.
 
Mbona ukiyowema ni ya sahih international na ni translation ya juzi

Ngoma hii hapa
18:86 ,Yusuf Ali: Until, when he reached the setting of the sun, he found it set in a spring of murky water: Near it he found a People: We said: "O Zul-qarnain! (thou hast authority,) either to punish them, or to treat them with kindness."
Tupe sheikh alie sema mimi ndio mwisho wa watafsiri wa quran
Na wala sijatumia international translation hapo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Quran inasema kwamba jua hutuama kwenye kisima ama dimbwi la matope kazito na asubuhi huamka.

Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta'ala kwenye Quran kupitia Sura al-Kahf (18: 83-86), inaeleza kwamba Jua huchwea katika chemchemu ya matope meusi mazito(dark Muddy spring):

“83-Na wanakuuliza khabari za Dhul- Qarnaini. Waambie: Nitakusimulieni baadhi ya hadithi yake.84 -Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu.85 - Basi akaifuata njia. 86 - Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema.”

Nimeuliza hivyo kwa sababu Sayansi ya Dunia inatuambia kwamba Jua liko mahapa pamoja ila Dunia ndio hulizunguka hivyo halina kuzama wala kuibuka.

Je mwenyezi Mungu SWT alikua na maana gani kusema hivyo?

Ahsante.
Kwa uelewa wangu mdogo Dhul-qarnaini ni kama alitumwa na Mungu kuwaeleza wanadamu juu ya mema amabyo Mungu anawawazia binadamu lakini kwa bahati mbaya alikuta watu wenyewe wánaotakiwa kuelezewa hizo habari njema kuhusiana na SWT wameshaharibiwa kimaadili na kwamba hawawezi tena kuelewa yale ambayo Mungu amemwagiza.

Ni sawa na kusema dhul-qarnaini alikuta watu wenyewe kitumbua kimeingia mchanga ndyo maana ya jua kuza kwenye matope
 
Katika watetezi wote kuna mmoja hapo juu nimeona ana akili angalau, yeye amedai kwamba tafsili imepotosha, katika english ameakdika "as it appears to him" yani huyo mtu yeye aliona hivo kwa macho yake hivo haithibitishi kwamba mambo ni hivo
 
Tena tunaambiwa kua Allah alimshushi Mtume Mohamed moja kwa moja kwenye kichwa chake.

Tunaambiwa ni kitabu kitakatifu alichokishusha Mungu mwenyewe.

Ghafla tunaambiwa tena kuna maneno ya watu wengine.

Sasa yapi ni ya Mungu na yapi ni ya binadamu? Ya binadamu ni nani alimshushia Mtume?
Ndio maana tunakiendesha kijeshi, Kwa viapo sio tafakari.
 
Mimi namsoma binadamu yake Muhammad, tena Muhammad alimsifu akasema hakuna mfasiri hodari kama ibn Abbas

18:86 Abbas - Tanwîr al-Miqbâs min Tafsîr Ibn ‘Abbâs
(Till, when he reached the setting place of the sun) where the sun sets, (he found it setting in a muddy spring) a blackened, muddy and stinking spring; it is also said that this means: a hot spring, (and found a people thereabout) these people were disbelievers: (We said: O Dhu'l-Qarnayn!) We inspired him (Either punish) either kill them until they accept to believe that there is no deity except Allah (or show them kindness) or you pardon them and let them be.
Ni kweli Ibn Abasi alisifiwa na Mtume kwamba ni mfasiri bora wa qoran, tunaposema Messi ni mchezaji bora hatumaanishi yeye ndio kila kitu uwanjani.

Wafasiri wa qoran wapo wengi wa kwanza ni yeye Mtume mwenyewe, kuna maswahaba zake ambao wapo wengi, na tabiina.

Hii tafsiri ya qoran haikufanyika siku moja,ni mtirirko wa masimulizi na tafsiri nyingine zimefanyika wakati mtume ameshafariki lakini hao waliosimulia hizo tafsiri walikua nae wakati anapewa hizo aya.

Ibn Kathir amekusanya tafsir ya qoran yote ikihusisha tafsir kutoka kwa Mtume mwenyewe,maswahaba na tabiina,na wanazuoni wa kabla yake.
 
1. Mleta mada, mbona neno "kisima" sijaliona kwenye tafsiri uliyoleta?

2. Aya hiyo ya 86 -inasema hivi

"Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika chemchem yenye matope meusi"

Je wewe mleta mada unaweza kutueleza labda Huyo Dhurqarnain aliliona jua linazama wapi?

Maana sometimes mtu unaweza kuliona jua linazama milimani, au maporini kulingana na ulipo.

Hiyo ni perception binafsi ya mtu, na wala haimaanishi jua linazama hapo!
 
Maana sometimes mtu unaweza kuliona jua linazama milimani, au maporini kulingana na ulipo.

Hiyo ni perception binafsi ya mtu, na wala haimaanishi jua linazama hapo!
Ndipo muhammad anawaweka sawa sio perception ni halisi Jua linazama kwenye maji , tena ni chemchem inaitwa hamiyah

  • Imesimuliwa Abu Dharr:
    Nilikuwa nimekaa nyuma ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) ambaye alikuwa akipanda punda wakati jua linachomoza. Akauliza: Je! Unajua jua linazama wapi? Nilimjibu: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua bora. Alisema: linazama katika chemchemi ya maji ya joto (Hamiyah).
    Grade Sahih
 
Hebu lete source basi ya hiyo hadithi. Usije ukawa umepunguza au umeongeza kitu
 
Back
Top Bottom