Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Hiyo akili ya kuumba miungu yao wameipata wapi kama sio kwa huyo Mungu mkubwa muumba mbingu na nchi?
Ameshindwa kuumba watu wenye akili anazotaka yeye?
Ina maana hakuwa akijua kwamba binadamu anayemuumba atakuja kumsaliti baadae, haiingii akilini bana.

Unakataza mtu asinywe pombe hiyo pombe binadamu kaijuaje kama sio Mungu mwenyewe ametaka tuijue?
Na huyo kitimoto kama ni haram aliletwa duniani kwaajili gani.

Mitego kila kona.
😂😂😂🙌🙌🙌 Wee utaki kuelewa tuu hizi habari ahahahahaha
 
Siwezi mthibitishia mtu asiye mwamin Mungu, we achana naye unafikiri unampunguzia nini

We achana na Mungu sio lazima umwamini na hutakua wa kwanza kutokumuamini
Kwamba anathibitika kwa kumuamimni 🤣🤣

This is hilarious
 
Anaandika Robert Heriel,
Mtibeli.

Kuna Mungu Muumba wa mbingu na nchi halafu kuna miungu. Mungu Mkuu ambaye hajawahi kuonekana na kamwe hatokuja kuonekana Daima milele, hawezi kufanya wala kuwaza huo upuuzi wa kuchoma watu, hilo haliwezekaniki!

Miungu hii inayoabudiwa ndio inaweza kufanya hivyo, lakini yule Mungu wa miungu huo muda hana, na hawezi kufanya hivyo.

Mungu Mkuu ni Upendo, na kamwe upendo haulazimishwi. Yaani, ati Mungu aliyekuumba akulazimishe umpende (umuabudu) wakati alikuwa na uwezo wa kukuumba automatic ukawa unampenda!

Kwanza umpende (umuabudu) ili yeye apate nini? Halafu usipompende ati akuchome, wewe kosa lako lipo hapo? Yaani moyo wako haumpendi Mungu aliyekuumba, unapenda jambo jingine nini kosa lako, iko wapi haki hapo?

Mungu mwenye Upendo na muweza wa yote, anataka mtu apende anachokipenda! Kwanza yeye ndio aliyekufanya uwe hivyo ulivyo, upende unayoyapenda, achana na yale unayoyatamani na kuyachukia.

Huwezi lazimisha kupendwa bhana, na kamwe Mungu hawezi kukulazimisha umpende. Kukulazimisha haibadilishi ukweli kuwa haumpendi. Kumbuka Mungu ni Haki na Kweli.

Mchongo ukoje? Ipo hivi;

Jinsi uonavyo Ulimwengu wa nje (huu unaoonekana) ndivyo katika Ulimwengu wa ndani usioonekana, Ulimwengu wa Nafsi.

Itazame Dunia, Dunia ni moja lakini inamazingira tofauti tofauti, kuna sehemu zenye baridi kali mpaka barafu, kuna sehemu za jangwa, kuna sehemu za hali ya hewa ya kati, kuna sehemu zenye mvua nyingi, na zipo zenye mvua za Waarabu.

Kuna milimani na mabondeni, sehemu zenye maziwa, mito na bahati, sehemu yenye misitu mine, nyasi na vichaka, sehemu yenye wanyama wa aina hii sehemu nyingine hakuna.

Sasa ni uchaguzi wa mtu kutumia kile akipendacho, ukitaka kuishi kwenye baridi ni wewe, Mungu hawezi kukulazimisha uishi sehemu isiyo ya baridi wakati wewe unapenda. Haipo hiyo. Ukitaka kula chakula au wanyama fulani ni wewe mwenyewe.

Ila elewa kuwa vipo vitu ni sumu na cool vitu sio sumu. Ni wewe mwenyewe unachagua ule sumu au usile. Nasema ni wewe mwenyewe, ni kutokana na upendo wako.

Kama unavyoishi hapa Duniani kulingana na umri wako, jinsia yako, kipato na hadhi yako, mtazamo wako ndivyo nafsi yako itakavyoishi baada ya mwili wako kuondoka.

Mfano huwezi ishi Masaki, Mikocheni, Upanga wakati kipato chako na daraja lako ni kuishi kwa walalahoi huko.

Kunguru na njiwa hawawezi kaa pamoja, wanasema ndege wafananao huruka pamoja. Nenda hata wodini huko mahospitalini utaona kabisa kuwa mgonjwa wa akili hawezi lazwa wodi ya wazazi au mgonjwa aliyemahututi hawezi lazwa wodi ya wagonjwa wa meno.

Maisha ni uchaguzi wa mtu mwenyewe. Mungu kamwe hana huo muda wa kukuamulia nini chakupenda. Kuku hawezi zaa bata, kila mmoja atakaa sehemu yake. Vivyohivyo hata ukifa roho yako itaenda mahali inapopapenda, na wala hautachomwa moto.

Kama unapenda uzinzi na kuchukua wake za watu na kuua watu basi nafsi yako itaishi katika Ulimwengu wa watu wa aina yako ili mchukuliane wake na waume zenu kwa jinsi mpendavyo, ili muone utamu wa kile mnachokipenda.

Sheria siku zote sio upendo, Sheria hizi za nchi zipo kwaajili ya kudhibiti matendo ha mwili na sio nafsi. Upendo upo kwenye nafsi ya mtu wakati sheria ipo katika mwili wa mtu. Mtu anapoua akahukumiwa jela kinachoadhibiwa ni mwili wake lakini nafsi yake haiadhibiwi.

Utalipwa sawasawa na matendo ya nafsi yako, Dhamiri na utapelekwa kwenye Ulimwengu unaofanana na nafsi yako. Hiyo ndio tafsiri ya moto wa Jehanum na sio kuchomwa kama wengi walivyotafsiri au wanavyojua.

Mungu Mkuu hukupa na anatoa kitu kulingana na mtu au kiumbe husika, Ulimwengu wa wapenda haki, wapenda dhulma, wenye upendo, wenye chuki, wasema uongo na wauaji, ulimwengu wa wasema kweli na watoa uzima.

Ni wewe tuu unachagua wapi unapenda na hayo ndio yatakuwa maisha yako mpaka Mungu Mkuu atakapoona imetosha. Ukitaka kubadili vitu upendavyo ni wewe, lakini mpaka Mungu atakapoona inatosha, uende katika Ulimwengu mwingine.

Ni kama hapa Duniani, vile unavyoishi ndivyo ulivyoamua kuishi au wazazi wako walivyotaka uishi (kumbuka ulikuwa katika mwili wa wazazi wako). Hakuna kulaumiana wala hakuna wakumlaumu. Hayo ndio maisha!

Acha nipumzike sasa,
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Mimi nipo pamoja na Mungu. Nimependa jinsi alivyotupa option(uwezo na uhuru wa kuamua na kuchagua). Raha sana mtu kupata ulichokichagua iwe ni Moto wa milele au Mbingu. Muhimu usitafute wa kumlaumu kwa maamuzi uliyoyaamua na kuyachagua mwenyewe kwa utashi wako. Kila mtu ashinde mechi zake
 
Mungu Mkuu angekuwa anachukia dhambi asingeiumba. Vyote unavyoviona na usivyoviona vimeumbwa na MUNGU.

Mungu ni Upendo, ameumba Wema na Ubaya Kwa sababu ya upendo; yakuwa wapo Watu na viumbe watapenda ubaya, na wapo watakaopenda Wema. Ni MTU/kiumbe Chenye utashi kuchagua kinapenda nini.
Utakachopenda ndio yatakuwa Maisha na Ulimwengu wako. Full stop. Na huo ndio upendo

Upendo sio kumchagulia MTU Mema ikiwa kwake ubaya ndio Wema(anaoupenda).

Ndio maana Vipo viumbe ambavyo kile ukionacho ni mavi na uchafu kwao ni chakula.
Hiyo Kanuni ya upendo.

Kama Mungu angeichukia dhambi na Ubaya kama madai yenu yalivyo, basi leo Hii tusingeweza kuijua hiyo dhambi wala huo ubaya.
Yani Mungu aumbe ubaya kwa sababu ya upendo?

Huwezi kuita ubaya na dhambi kwamba ni upendo, Huo ni ukatili na unyama.

Basi huyo Mungu ni mkatili sana.
 
Kwamba anathibitika kwa kumuamimni 🤣🤣

This is hilarious
Ndo maana nikakuambia we achana naye ni ajabu unangangania na kitu ambacho umesha-conclude hakina maana kwako

Nikusaidie kwenye maisha hatuwezi fanana na usione watu hamnazo kama hawaamin mambo ambayo wewe huamini
 
Ndio ni katili achana naye kwani ni lazima umfuate
Hili ni jukwaa huru la kutoa maoni.

Mnapokuja na imani zenu za kusadikika na kuzi andika hapa JF lazima tuje na maswali ya kuhoji hizo imani zenu.

Kama hauwezi kutoa majibu na uthibitisho ya imani yako, Hupaswi kuja kuongelea hiyo imani yako hapa JF, Utegemee tukae kimya kusikiliza imaginations zako.

Kama mnataka tuachane naye msi andike nyuzi zake hapa JF, Halafu mkihojiwa hamna majibu yake.

Kama Huwezi kujenga hoja za kuthibitisha Mungu yupo kaa kimya na baki na imani yako.
 
Hili ni jukwaa huru la kutoa maoni.

Mnapokuja na imani zenu za kusadikika na kuzi andika hapa JF lazima tuje na maswali ya kuhoji hizo imani zenu.

Kama hauwezi kutoa majibu na uthibitisho ya imani yako, Hupaswi kuja kuongelea hiyo imani yako hapa JF, Utegemee tukae kimya kusikiliza imaginations zako.

Kama mnataka tuachane naye msi andike nyuzi zake hapa JF, Halafu mkihojiwa hamna majibu yake.

Kama Huwezi kujenga hoja za kuthibitisha Mungu yupo kaa kimya na baki na imani yako.
Siwezi kukuthibitia
Na kwanini unangangania uthibitishiwe kwa kitu ambacho unaamini hakipo

Swali sio jukwaa huru bali ni swala la mtu kutumia tu mantiki
 
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasioweza kutenda mabaya?

Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Uovu?

Mwanadamu aliumbwa akiwa mwema ila mabaya aliyatafuta mwenyewe
 
Akili yako haina uwezo wa kumchunguza MUNGU bro achana na habari za kumchunguza MUNGU.
Well said sisi katika dini yetu ya uislam tumefundishwa mtu anae mchunguza mungu basi hata akili zake haziko sawa (majnun) kwa maana huwezi kuchunguzu na kikujua kitu kilichokutengeneza wewe na kukupa akili kwasababu angeweza kukuumba ukawa hata mmbu lakini kakuumba binaadam na kwa ujeuri wa binaadam et unamchunguza na kumjadili mungu. BIRA USEME MUNGU YUPO KULIKO KUSEMA HAYUPO UKAKUTANA NAE NDIO UTAJUA HAUJUI.
 
Ni kwa namna gani ulitambua maarifa ya Mungu hayachunguziki?

Ulifanya uchunguzi gani uka gundua kwamba Maarifa ya Mungu haya chunguziki?

Kwani wewe kila unachokiamini umekichunguza? ingekuwa hivyo basi dunia nzima tungekuwa watafiti na wachunguzi, hakuna ambaye angeamini utafiti/uchunguzi wa mwenzake.ni imani tu inatumika
 
Unachofanya hapa ni kuingilia uhuru wa watu kuamin wanachoamin
Achana naye kwanin unateseka
Si ingilii uhuru wa mtu kuamini na wala silazimishi mtu kufuata ninacho sema.

Nachangia mada kwa kuhoji maswali ya anaye leta imani yake hapa JF.

Ni sawa kuwa na imani yako, ila unapo dai imani yako ni ya kweli lazima uthibitishe.

Na ndio maana tunahoji maswali ya uwepo wa huyo Mungu kwa vile mnaleta imani zenu hapa JF.
 
Back
Top Bottom