Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Kuna sehemu amekusikia fimbo umfuate achana naye kwanin uteseke
If you think education is expensive try ignorant

Kuna watu kibao hawana dini na wanaishi kawaida kama huamin mapokeo yake achane naye sababu huwezi mbadilisha

Kwani wapi nimesema kuwa Mungu Mkuu anashikia fimbo(analazimisha) Watu wamfuate?

Miungu inayoabudiwa kwenye Dini ndivyo inayotaka na kulazimisha Watu waifuate, na ndio inayowaambia Watu watangaze miungu Yao.

MUNGU Mkuu hawezi kutaka kutangazwa Kwa sababu vyote ni vyake,
 
MUNGU Yehova, Baba yetu wa mbinguni hamchukii mtu, Bali huichukia dhambi. Dhambi ni uasi dhidi ya MUNGU. MUNGU Huwa na uwezo wa kughadhabika kutokana na dhambi. Kuna mifano dhahiri ya madhihirisho ya ghadhabu ya MUNGU kushukia wanadamu.

Yehova YWHW Aliwahi kuiangamiza dunia yote kwa gharika ya maji. walipona watu wanane tu. Nuhu na familia yake.

Mwenyezi MUNGU, Yehova YWHW Aliwahi kuiteketeza miji miwili mikubwa ya Sodoma na Gomora kwa moto. wakaokoka watu watatu tu. Lutu na mabinti zake wawili.

hivyo endeleeni KUJIDANGANYA!

JESUS IS LORD&SAVIOR

Mungu Mkuu angekuwa anachukia dhambi asingeiumba. Vyote unavyoviona na usivyoviona vimeumbwa na MUNGU.

Mungu ni Upendo, ameumba Wema na Ubaya Kwa sababu ya upendo; yakuwa wapo Watu na viumbe watapenda ubaya, na wapo watakaopenda Wema. Ni MTU/kiumbe Chenye utashi kuchagua kinapenda nini.
Utakachopenda ndio yatakuwa Maisha na Ulimwengu wako. Full stop. Na huo ndio upendo

Upendo sio kumchagulia MTU Mema ikiwa kwake ubaya ndio Wema(anaoupenda).

Ndio maana Vipo viumbe ambavyo kile ukionacho ni mavi na uchafu kwao ni chakula.
Hiyo Kanuni ya upendo.

Kama Mungu angeichukia dhambi na Ubaya kama madai yenu yalivyo, basi leo Hii tusingeweza kuijua hiyo dhambi wala huo ubaya.
 
Ni kisema chanzo cha ulimwengu na vilivyomo ni Mungu ndy aliye viumba wew kwanini unabisha ilihali hujui chanzo chake?
Mtu akikwambia square root ya 5 ni 15 utakubali kisa hujui square root ya 5 ni ngapi?

Mtu akikwambia mama mzazi wa Rhz4567 mwenye umri wa miaka 34 Ni Mwajuma mwenye umri wa miaka 4, utakubali kisa tu humjui kwa hakika mama mzazi wa Rhz4567 ni yupi?

Nijibu
 
Hofu ya moto isiwafanye kutoamini uwepo wake.
Chamsingi ni kufanya sawa sawa na mapenzi ya MUNGU.
Kuziamini hoja za mtoa mada basi ni sawa na kusema hakuna faida ya uwepo wa MUNGU au hayupo kabisa.
Yaani iweje MUNGU awepo halafu asiweke sheria zake? Haiwezekani.
Huwezi kumjua mungu bila kutii sheria zake,Imeandikwa, 1Yohana 2:4-6 "Yeye asemaye nimemjua wala hazishiki amri zake ni mwongo wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye aliyeshika neno lake katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli katika hiyo twajua tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake imempasa kuenenda mwenyeewe vile vile kama yeye alivyoenenda."

kusudi la MUNGU kutuumba wanadamu ni tumpende na kuntumikia.
MUNGU alituumba ili tutetende mema ambayo ndiyo furaha yake na hakuna kinyume na hapo
Soma Efeso 2:10
 
Hivi wewe naomba nikuulize, iv unajua kwanini upo hai/umeletwa duniani ili iweje! ukinijibu hilo naungana nawewe kwenye imani yako
Naomba nijibu maswali yako kutokana na uelewa wangu

1. Kwanini nipo HAI
*Kwa sababu sijakumbana na sababu ya kunifanya nife, hizo sababu ni kama vile, Ajari,maradhi,msongo wa mawazo nk

ila kumbuka sio kila Ajari lazima isababishe kifo, kifo hutokea pale ambapo hiyo sababu imesababisha impact kubwa katika mwili wako

2.kwanini nimeletwa Duniani
*Nimejikuta Duniani by chances tu, nothing special, naweza kuita bahati mbaya na wakati huo huo bahati nzuri ilitokea kwa wazazi wangu kukutana kimwili katika siku za hatari

Baada ya hapo Mimba ikatungika nayo pia ikakutana na bahati ya kukutana na mazingira rafiki katika kipindi chake chote hadi kufikia siku ya Bimkubwa kujifungua

Kumbuka nasema bahati kwa sababu Mimba zingine uharibika kabla ya muda kufika, na pia watoto wengine hurafiki tu baada ya kuzaliwa

Kwahiyo kuhusu kwanini bado nipo Duniani ni kwa sababu ya kuwa miongoni mwa watu waliobahatika kutokukutana na sababu za kuweza kupekea KIFO

Na nilifika Duniani kutokana na bahati Tu mbaya au nzuri, so kila kitu unachokiaona ambacho kipo natural katika Dunia kipo by chance Tu

Kwahiyo hakuna uspecial wowote ule wa kuwepo Duniani zaidi ya kuwa umekuja kwenye balaaa Tu, ambae hajazaliwa ndio Mshindi kwa sababu hakutani na hizi Mambo za Dunia
 
Mleta mada kuna kitu haelewi kwa nini Mungu anataka waovu mwisho wa siku awachome moto

Kaweka amri .zake zile lazima tutii.Sio kuwa tumtii yeye tu la zinaleta utengamano ndani ya dunia ili tusiumize wengine.Makosa mengi tunayotaka eti.Mungu atusamehe yanaumiza wengine na Mungu hataki mtu muumiza.wengine ndio maana mwisho wa siku ni motoni.

Mfano anasema usizini unazini na kumpa ukimwi mtu mwingine wewe ni wa kuchomwa moto kabisa muuaji mkubwa unaumiza wengine

Anasema usiibe unaibia wengine kwa kupitia njia mbalimbali ziwe ujambazi nk.na kuwaachia machungu makubwa wengine kwa wizi wako mwisho wa maisha Mungu.kaweka moto jitu.kama wewe ni motoni tu

Lingine unaambiwa usiseme uongo unadanganya watu na kuwatapeli na kuwaumiza pakubwa mwisho wa siku motoni

Unaambiwa usiue wewe unaua watu kwa njia mbali za.uchawi,nk unataka Mungu akakuweke wapi ukifa.Hana sehemu bora ya kuweka mtu kama huyo ni motoni tu

Moto umewekwa mahususi kwa wote wasiotaka kuishi kwa kutii amri za Mungu za kufanya Binadamu waishi kwa utengamano

Usipotubu dhambi na kuziacha na kuokoka moto jehanamu unakusubiri
Jehanam ni sehem ambayo walikuwa wakichomea maiti zamani.
Iko nje kidogo ya mji wa Yerusalemu pale Israel ya sasa.

Inajulikana kama Gehenna.
 
Kwanza Mungu Muumba WA mbingu na nchi hajawahi kuonekana wala Sauti yake haijawahi kusikika popote pale. Huyo anayesema amri Fulani ni za Mungu Mkuu ni muongo. Sema amri za miungu kulingana na asili na tamaduni za Watu.
Kifupi wewe umekenguaka kupita maelezo naona wazi kichaa tayari kimeshakuvamia sababu ya kujaa kufuru kwa Mungu keshaanza kukushughulikia

Mene mene tekeli na peresi
 
Hofu ya moto isiwafanye kutoamini uwepo wake.
Chamsingi ni kufanya sawa sawa na mapenzi ya MUNGU.
Kuziamini hoja za mtoa mada basi ni sawa na kusema hakuna faida ya uwepo wa MUNGU au hayupo kabisa.
Yaani iweje MUNGU awepo halafu asiweke sheria zake? Haiwezekani.
Huwezi kumjua mungu bila kutii sheria zake,Imeandikwa, 1Yohana 2:4-6 "Yeye asemaye nimemjua wala hazishiki amri zake ni mwongo wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye aliyeshika neno lake katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli katika hiyo twajua tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake imempasa kuenenda mwenyeewe vile vile kama yeye alivyoenenda."

kusudi la MUNGU kutuumba wanadamu ni tumpende na kuntumikia.
MUNGU alituumba ili tutetende mema ambayo ndiyo furaha yake na hakuna kinyume na hapo
Soma Efeso 2:10
Thibitisha Mungu yupo kweli na sio hadithi za uongo tu hizo
 
Hivi wewe naomba nikuulize, iv unajua kwanini upo hai/umeletwa duniani ili iweje! ukinijibu hilo naungana nawewe kwenye imani yako
Ingawaje umeuliza swali katika msingi potofu lakini Jibu lako utalipata ukijibu swali hili

Kwanini nyani na simba wapo hai,
Wameletwa duniani ili iweje!?
 
Jehanam ni sehem ambayo walikuwa wakichomea maiti zamani.
Iko nje kidogo ya mji wa Yerusalemu pale Israel ya sasa.

Inajulikana kama Gehenna.
Na hapa ina maana gani unaelewa?

2 Petro 3:7​

Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
 
Hata kama sio moto bali ni hali tu iweje iwe ya mateso? Yaani kwanini atutese?
Yeye achukue watu wake wanaomwamini na wasiotenda dhambi, hao wengine aachane nao , iweje iwe lazima kufata anavyotaka yeye?

Hapo hapo katumwaga humu duniani tumejikuta tunatofautiana kiimani tunapigana vita wenyewe kwa wenyewe, ili iweje sasa?
Alishindwaje kufanya tuwe na imani moja anayoitaka yeye?
Anatuchanganya haeleweki
Hao wanaotenda dhambi akiwaacha watawasumbua wanaompenda Mungu

Lejea Sodima na Gomoro

quran 26:161
- Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu?

quran 26:162
- Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.

quran 26:163 -
Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.

quran 26:164 -
Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

quran 26:165 -
Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?

quran 26:166 -
Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!

quran 26:167 -
Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji!

_quran 26:168 -
Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu.

quran 26:169 -
Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.

quran 26:170 -
Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,

quran 26:171 -
Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.

_quran 26:172 -
Kisha tukawaangamiza wale wengine

2) Mungu hajawachanganya watu kuhusu dini ila watu wenyewe ndio wanachanganyana na akili aliyokupa Mungu inawezo wa kujua yapi ni kweli na yapi ni ya uongo

na ndio maana ameleta manabii zaidi ya laki Moja na vitabu 4 Yani

Taurati
Zaburi
Injili
Quran

Hivyo vitabu 4 vyote vinasema MSUJUDIE bwana Mungu wako

Alafu anatokea mtu from no where anakuambia unapomuabudu Mungu USISUJUDU

Sasa hapo Mungu anakosa gani akikupeleka Jahannam Kwa kukataa KUMSUJUDIA?
 
Na hapa ina maana gani unaelewa?

2 Petro 3:7​

Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
Sielewi.

Muktadha wangi ni kumjibu mchangiaji kuhusu habari ya Jehanam.
Nimeeleza jehanamu ni nini/wapii.

Huo mstari umeleta hauna maana yeyote kwa muktadha nlionao.
 
Hata kama sio moto bali ni hali tu iweje iwe ya mateso? Yaani kwanini atutese?
Yeye achukue watu wake wanaomwamini na wasiotenda dhambi, hao wengine aachane nao , iweje iwe lazima kufata anavyotaka yeye?

Hapo hapo katumwaga humu duniani tumejikuta tunatofautiana kiimani tunapigana vita wenyewe kwa wenyewe, ili iweje sasa?
Alishindwaje kufanya tuwe na imani moja anayoitaka yeye?
Anatuchanganya haeleweki
Duuuh ya rohoni hayo
🙌🙌🙌🤝🤝🤝🤝
Ila kama tumenyimwa uhuru hivi et
 
Huo ndiyo ukweli. Huwezi fanya dhambi miaka 70 halafu ukachomwa moto milele. Yaani miaka elfu, laki, milioni, bilioni, trilioni wewe unaungua tu. Hii ni hadithi iliyotungwa na shetani.
Ametunga mteja wako huyu....
Maaan wewe si ndo wakili wake fafanua vizuri hili swala mkuu
😂😂😂😂😂
 
Kifupi wewe umekenguaka kupita maelezo naona wazi kichaa tayari kimeshakuvamia sababu ya kujaa kufuru kwa Mungu keshaanza kukushughulikia

Mene mene tekeli na peresi

Unamaanisha mungu yupi?
Wawayahudi, Waarabu, wachina, wachaga, au wasukuma au wandendereko?

Mungu Mkuu alichokiumba hakiwezi kukengeuka ikiwa hakutaka kingengeuke,
Vile alivyoumba Muumbaji ndivyo alichotaka viwe.

Embe haliwezi kuwa Limau.
Mimi siwezi kuwa wewe kamwe.
Wewe endelea kuabudu miungu. Sio kosa Kwa sababu Mungu Mkuu ametaka iwe hivyo, wawepo watumwa wa miungu midogo
 
Kwani wapi nimesema kuwa Mungu Mkuu anashikia fimbo(analazimisha) Watu wamfuate?

Miungu inayoabudiwa kwenye Dini ndivyo inayotaka na kulazimisha Watu waifuate, na ndio inayowaambia Watu watangaze miungu Yao.

MUNGU Mkuu hawezi kutaka kutangazwa Kwa sababu vyote ni vyake,
Kama Miungu inalazamisha wewe ulishawahi kulazimishwa kuwafuata????

Mungu mkuu yupi huyo unayomsemea
 
Ungebaki kanisani/misikitini wala hata usingeona tuna argue.

Naheshimu haki za watu kuamini watakacho.
Imani haina kanuni, unaweza kuamini hata jiwe tu.

Umeleta mjadala hapa JF kunasibisha imani yako mimi nakuomba uithibitishe madai yako.

Umeleta imani yako kwenye ulingo huru, mimi nkikuuliza kuhusu imani yako hapo nakuwa sijaingilia uhuru wako.

Unaelewa hilo?

Kwanini mnatueleza masuala ambayo hamuwezi kuyatetea humu kwenye mijadala iliyo wazi kwa watu wa mitazamo yote?
Siwezi mthibitishia mtu asiye mwamin Mungu, we achana naye unafikiri unampunguzia nini

We achana na Mungu sio lazima umwamini na hutakua wa kwanza kutokumuamini
 
Unamaanisha mungu yupi?
Wawayahudi, Waarabu, wachina, wachaga, au wasukuma au wandendereko?

Mungu Mkuu alichokiumba hakiwezi kukengeuka ikiwa hakutaka kingengeuke,
Vile alivyoumba Muumbaji ndivyo alichotaka viwe.

Embe haliwezi kuwa Limau.
Mimi siwezi kuwa wewe kamwe.
Wewe endelea kuabudu miungu. Sio kosa Kwa sababu Mungu Mkuu ametaka iwe hivyo, wawepo watumwa wa miungu midogo
Mungu mkuu ndo yupi
 
Mungu mkuu ndo yupi

Aliyeumba hiyo miungu mingine mnayoiabudu.
Huyo hajulikana na hajawahi kuonekana na Hana sababu ya kujulikana na kuonekana.

Hataki lolote Kutoka kwetu Kwa sababu Sisi ni viumbe vyake, ametuumba atakavyo, na sio vile tutakavyo, kama aliamua wewe uwe mtumwa WA wengine unakuwa hivyo tuu.

Kama alivyotaka Watu wawe watumwa Kwa miungu mnayoiabudu mkidhani mnaabudu Mungu Mkuu
 
Back
Top Bottom