Muombe Mungu akusamehe kwa Uzi Huu, Kisha waombe Mods waufute Uzi Huu!!.
Ni Mungu huyuhuyu muumbaji na Upendo, aliwachoma moto sodoma na gomora sijataja zama za Nuhu, huyu Mungu alompa Samson nguvu awauwe wafilisti na maadui wa Israel, ni Mungu huyohuyo alokua anawaagiza Wana isarel wawaue maadaui zao kuanzia Watu mpaka Kuku !!.
Ni Mungu yule yule alombariki Eliya, Ayubu, Daudi,
Ni Mungu yuleyule alomponya Jenerali Naamani na wengine.
Ni Mungu alomfufua Lazaro ,na wengineo !!.
Ni Mungu yuleyule anayeturuhusu tupumue Hata Sasa tunapoandika hapaa !!!.
Kwa sisi tuonafanya kazi Ma Hosp, tunaelewa Kifo ni nini !! Na kwamba, Huchukua Sekunde Moja tu kubadili Historia ya mtu kutoka mtu kuongea, mpaka mtu kushindwa hata kufungua jicho !!.
Ni Mungu huyuhuyu aloruhusu uwe hapo ulipo.
Ni huyohuyo Mungu, aloiweka ahadi ya kutoigharikisha Dunia Kwa maji badala yake akasema, NITAICHOMA DUNIA NA WADHAMBI WOTE KATIKA ZIWA LIWAKALO MOTO.
Njia pekee ya kuukumbia Huu moto ni Kutokufanya dhambi, na tutaliweza Hilo Kwa kumuomba Mungu ili atupe Uwezo na neema zake, huku wenyewe tukichukua Jitahada binafsi.
HAKIKA, KICHWA CHA MWANADAMU KINAWAZA UPUMBAVU,,,, ILA MWANADAM ANAPOFIKIA HATUA YA KUFANYA KUFURU KWA MUNGU, NI ZAIDI YA UPUMBAVU !!.
UWEZO NA UKUU WA MWANADAMU, KAMWE HAUCHUNGUZIKI !!! NI MUNGU ATABAKI KUA MUNGU !!.