Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

To say something is real, You have to prove it. Otherwise if you cannot those are your thoughts, imaginations just an illusion.

Imani ya kumwamini Mungu haihitaji proof. Haihitaji LOGIC kama unasubiri proof uko mbali sana na kumjua Mungu maana yeye anataka watu walio tayari kumwamini pasipo maswali
 
Kwani wewe kila unachokiamini umekichunguza? ingekuwa hivyo basi dunia nzima tungekuwa watafiti na wachunguzi, hakuna ambaye angeamini utafiti/uchunguzi wa mwenzake.ni imani tu inatumika
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.
Imani haiendani na ukweli, Imani inaendana na kutokuwa na uhakika.

Ukweli una endana na uthibitisho,Ndio maana utafiti hufanyika kutafuta ukweli wa imani fulani.
 
nimeshindwa kupata muelekeo wa hii mada.

Ufu 20:14-15 SUV

Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

rahisisha injili, ongeza ladha na njonjo zote, lakini usipuuze ukweli.
 
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.
Imani haiendani na ukweli, Imani inaendana na kutokuwa na uhakika.

Ukweli una endana na uthibitisho,Ndio maana utafiti hufanyika kutafuta ukweli wa imani fulani.

Hapana,biblia inasema imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo na ni bayana(uthibitisho) ya mambo yasiyoonekana
 
Kama huwezi kuchunguza na kukijua kitu kilicho kutengeneza wewe, Ulifahamu vipi hicho kitu kili kutengeneza?

Kama hicho kitu kilicho kuumba wewe haki chunguziki, uchunguzi wa kukifahamu kwamba hakichunguziki ulifanywa na nani kujua na kuthibitisha kwamba hakichunguziki?
 

Chukua mfano rahisi tu wa roboti na mtengeneza roboti.je roboti aweza mchunguza aliyelitengeneza?
 
Hapana,biblia inasema imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo na ni bayana(uthibitisho) ya mambo yasiyoonekana
Una elewa maana ya kuwa na uhakika?

Ukisha kuwa na uhakika hiyo sio imani tena bali ni ukweli.

Mfano, mwanafunzi akifanya mtihani ana kuwa Hana uhakika wa marks ipi exactly ataipata, ila anakuwa na imani fulani ya marks atakayo ipata kwa vile Hana uhakika na imani yake. Tuseme labda mwanafunzi huyu ana imani ya kupata marks 80%.

Lakini akisha rudishiwa mtihani wake Anakuwa na uhakika na ukweli kwamba mtihani huu nimepata marks 80% na hiyo inakuwa siyo imani tena ya kwamba alipata marks 80% Bali ni ukweli wenye Uthibitisho.

Hata mtu akihitaji uthibitisho wa mwanafunzi huyu kupata marks 80% ataupata.

Ndio maana nakwambia hivi, Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.
 

Reference yangu ni biblia ndugu,sijajitungia kichwani
 
BIBLIA KTK VITABU VYA MITHALI 4:23 NA YEREMIA 17:9 INAZUNGUMZIA JUU YA MOYO, KWAMBA, TUNAPASWA KULINDA MOYO KULIKO VITU VINGINE VYOTE KWA SABABU KWENYE MOYO NDIKO KUTOKAKO CHEMICHEMI ZA UZIMA (LAKINI KUNAWEZA TOKA CHEMICHEMI ZA MAUTI PIA).LAKINI PIA, MOYO HUWA NI MDANGANYIFU.
MTU ANAUMBWA KTK MAENEO MATATU:
-ROHO, NAFSI, NA, MWILI.
BIBLIA HUREJEZEA NAFSI YA MTU KUWA NDIYO MOYO. ENEO LA NAFSI/MOYO NDIKO KUNA UTASHI, HISIA, NA, HAIBA YA MTU. WAINGEREZA WANATAMBULISHA MOYO/NAFSI KUWA NI PERSONALITY i.e. KWA KIBONGO, UTU WA MTU.
NDUGU HELIEL, LINDA SANA MOYO WAKO KULIKO VYOTE ULINDAVYO; NA, KUMBUKA MOYO HUWA MDANGANYIFU SANA. MWENYEZI MUNGU (JEHOVAH) AMBAYE ANAJITAMBULISHA KTK BIBLIA KUWA NI MUNGU WA IBRAHIMU, NA ISAKA, NA, YAKOBO (ISRAELI) HAYUKO NAMNA MOYO/NAFSI YAKO INAVYOMCHUKULIA. NI ROHO MTAKATIFU TUU NDIYE PEKEE ANAWEZA KUMFUNULIA MTU JUU YA UUNGU WA MWENYEZI MUNGU (LAKINI KWA SEHEMU).
BIBLIA NI NENO LA MUNGU. ILIANDIKWA NA WANADAMU MBALIMBALI WALIOVUVIWA MAFUNUO NA ROHO WAKE (ROHO MTAKATIFU) WAKAIANDIKA KITABU CHA MWANZO HADI UFUNUO. MANENO YAKE NI HAKIKA NA AMINI. YAMETIWA MUHURI. KWA HALI HII HELIEL, NI HATARI SANA KUJARIBU KUBADILI, KWA NAMNA YOYOTE ILE, MAUDHUI YA BIBLIA; NI DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU; DHAMBI ISIYO SAMEHEKA KTK ULIMWENGU HATA ULE UJAO. NI HATARI SANA.
NAKUSHAURI OKOKA, YAANI, INGIA AGANO (MAKUBALIANO/ MKATABA) NA BWANA YESU KRISTO KWA KUTUBU NA KUJUTIA DHAMBI ZAKO, NA, UMKIRI KUWA AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO. KWA HATUA;
- UTASAMEHEWA DHAMBI ZAKO ZOTE NA HIVYO KUTAKASWA (KUWA MTAKATIFU)
-UTAPATIWA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU ATAKAYEKUFUNDISHA JUU YA BWANA YESU KRISTO NA KUKUOMBEA KWA MUNGU PIA.
-UTAPATA KIBALI CHA KUFANYIKA MTOTO WA MUNGU.
- JINA LAKO LITAFUTWA KTK KITABU CHA HUKUMU YA KWENDA KTK ADHABU YA MILELE MOTONI JEHANAMU, NA, BADALA YAKE LITASAJILIWA KTK KITABU CHA UFALME WA MBINGUNI.
NI HIVYO NDUGU YANGU HELIEL. BWANA YESU KRISTO ANAKUPENDA. ANAKUITA.
 
Ufanye makosa hapa duniani halafu uachiwe tu?
 
Chukua mfano rahisi tu wa roboti na mtengeneza roboti.je roboti aweza mchunguza aliyelitengeneza?
Roboti Hawezi kumchunguza aliye mtengeneza, kwa vile yuko programmed kufuata matakwa na masharti ya mtengeneza roboti.

Lakini, Mtengeneza roboti ana uwezo wa kumfanya roboti amtambue yeye kama mtengenezaji wake kwaku mprogram na kum condition afanye hivyo.

Binadamu hatupo programmed ndio maana wapo wenye imani na wapo wasio na imani.

Kama aliye tutengeneza sisi binadamu angekuwepo:

Kwanza, Kusingekuwa na utata wa kujiuliza uwepo wake kwa vile tungekuwa programmed kujua yeye yupo.

Pili, Tusingekuwa na ufahamu na Akili ya kuhoji kama yeye yupo au hayupo kwa vile binadamu wote tungekuwa programmed kufuata matakwa yake ya kujua, Yeye yupo.
 

Mkuu naomba ufuate Kanuni za uandishi ndipo nisome,
Kama hujafuata Kanuni za uandishi unategemea Mimi nitaelewa kweli Mkuu!
 
Asipothibitisha utamfanyaje
 
Wanao sema hakuna Mungu naomba mniambie
Ni nini chanzo cha ulimwengu,maji,hewa ardhi na viumbe hai.

Kifo ni nini.
Mkuu kwahiyo mnaamini kwamba kwa sababu atheists wameshindwa kutoa jibu la chanzo cha ulimwengu basi automatically theists ndio wako sahihi

Hivi unafahamu kwamba haihitaji mtu kujua jibu la 1÷0 ili ajue kwamba jibu haliwezi kuwa 1, mnachofanya ninyi ni sawa na kuamua kusema kwamba 1÷0 jibu ni 1 halafu wakijitokeza watu wakabisha mnawaambia wao wawape jibu, na wakisema hawajui basi mnaconclude kuwa automatically jibu lenu ndio sahihi (hata kama halina vithibitisho) eti kwa sababu tu hao wanaowapinga wameshindwa kutoa jibu

Basi vivyo hivyo haihitaji mtu kujua jibu sahihi la chanzo cha ulimwengu ili ajue kuwa chanzo chake siyo Mungu na kwamba huyo Mungu hayupo, hao atheists kutokuwa na majibu ya chanzo cha ulimwengu haimaanishi kwamba theists ndio wako sahihi, suala siyo nani anaamini nini suala ni vithibitisho vinavyoeleweka
 
Mungu huyo unayesema ana huruma, ndiye aliyeleta gharika wakati wa Nuhu, na ndiye aliyechoma sodoma na Gomora.
 
Reference yangu ni biblia ndugu,sijajitungia kichwani
Vitabu vyote vya kidini ni stori za kusadikika, Fiction stories. Ndio maana hutofautiana maelezo kwenye kuelezea uwepo wa Mungu

Biblia ni reference kwa imani yako tu, Na si reference ya watu wote, Maana hata mwislamu atakwambia reference yake ni Quran.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…