Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Muombe Mungu akusamehe kwa Uzi Huu, Kisha waombe Mods waufute Uzi Huu!!.


Ni Mungu huyuhuyu muumbaji na Upendo, aliwachoma moto sodoma na gomora sijataja zama za Nuhu, huyu Mungu alompa Samson nguvu awauwe wafilisti na maadui wa Israel, ni Mungu huyohuyo alokua anawaagiza Wana isarel wawaue maadaui zao kuanzia Watu mpaka Kuku !!.


Ni Mungu yule yule alombariki Eliya, Ayubu, Daudi,

Ni Mungu yuleyule alomponya Jenerali Naamani na wengine.

Ni Mungu alomfufua Lazaro ,na wengineo !!.


Ni Mungu yuleyule anayeturuhusu tupumue Hata Sasa tunapoandika hapaa !!!.


Kwa sisi tuonafanya kazi Ma Hosp, tunaelewa Kifo ni nini !! Na kwamba, Huchukua Sekunde Moja tu kubadili Historia ya mtu kutoka mtu kuongea, mpaka mtu kushindwa hata kufungua jicho !!.


Ni Mungu huyuhuyu aloruhusu uwe hapo ulipo.

Ni huyohuyo Mungu, aloiweka ahadi ya kutoigharikisha Dunia Kwa maji badala yake akasema, NITAICHOMA DUNIA NA WADHAMBI WOTE KATIKA ZIWA LIWAKALO MOTO.


Njia pekee ya kuukumbia Huu moto ni Kutokufanya dhambi, na tutaliweza Hilo Kwa kumuomba Mungu ili atupe Uwezo na neema zake, huku wenyewe tukichukua Jitahada binafsi.




HAKIKA, KICHWA CHA MWANADAMU KINAWAZA UPUMBAVU,,,, ILA MWANADAM ANAPOFIKIA HATUA YA KUFANYA KUFURU KWA MUNGU, NI ZAIDI YA UPUMBAVU !!.


UWEZO NA UKUU WA MWANADAMU, KAMWE HAUCHUNGUZIKI !!! NI MUNGU ATABAKI KUA MUNGU !!.
Huyo Mungu anapaswa kuwa ICC kwa makosa hayo ya jinai, jinai no. 1 ni mauaji ya halaiki.
 
Dambi banaa, inakawaida ya Kumfanya anayetenda, kutafuta sababu za kukwepa Guilty !!

Wanadam wote hapa Duniani, wakifanya jambo lolote baya, Huwa wanakawaida ya kutafuta sababu ya kuhalalisha ubaya huo, na wengine njia pekee Huwa ni kukimbiaa .


Ulishawah jiuliza kwann , Ukifumaniwa , au ukifanya jambo baya la taharuki, Huwa watu wanaamua kuhama hiyo sehem????.

Au unadhan kwann Wenye ngoma, hupenda kuhama hama maeneo ya makazi???


Hiyo yote Huwa ni kuukwepa huo ukweli ,yaan mwanadam anahangaika kutafuta sababu za kuhalalisha Matatizo yake !!.


Mungu yupo, na yeye mwenye ni Pendo, ijapokua tunafanya dhambi, yeye ATABAKI kua Mungu, na atabaki kutupatia Rehema na muda wa kumjua na kurudi kwake.


Sasa basi, Usiache Mungu ,akurudishe yeye mwenyewe kwake , yaan usimpuuze Mungu kiasi kwamba ,yeye mwenyewe aamue kuingilia Kati !!!!!.


Habari za moto ni za Hakika, kama unaamin Titanic ilizama, Kama unaamin aliwah kuwepo Hitler, basi amini, Kuna watu waliwahi kuchomwa moto Kwa Dhambi za Ushoga na kufirana, wengine wakaangamizwa Kwa maji ya gharika !!.


Mungu ni mwema wakati wote !!.
Kwamba anachoma moto watu halafu ni wa upendo wakati wote.

Hiyo ni contradiction.
 
Hazichunguziki kwasababu hayupo.

Unawezaje kuchunguza kisichokuwepo!?
Wewe kuona kuwa Mungu kwako hayupo Haina maana wote tukufuate...

Mpumbavu asema moyoni mwake hakuna Mungu..
 
Anaandika Robert Heriel,
Mtibeli.

Kuna Mungu Muumba wa mbingu na nchi halafu kuna miungu. Mungu Mkuu ambaye hajawahi kuonekana na kamwe hatokuja kuonekana Daima milele, hawezi kufanya wala kuwaza huo upuuzi wa kuchoma watu, hilo haliwezekaniki!

Miungu hii inayoabudiwa ndio inaweza kufanya hivyo, lakini yule Mungu wa miungu huo muda hana, na hawezi kufanya hivyo.

Mungu Mkuu ni Upendo, na kamwe upendo haulazimishwi. Yaani, ati Mungu aliyekuumba akulazimishe umpende (umuabudu) wakati alikuwa na uwezo wa kukuumba automatic ukawa unampenda!

Kwanza umpende (umuabudu) ili yeye apate nini? Halafu usipompende ati akuchome, wewe kosa lako lipo hapo? Yaani moyo wako haumpendi Mungu aliyekuumba, unapenda jambo jingine nini kosa lako, iko wapi haki hapo?

Mungu mwenye Upendo na muweza wa yote, anataka mtu apende anachokipenda! Kwanza yeye ndio aliyekufanya uwe hivyo ulivyo, upende unayoyapenda, achana na yale unayoyatamani na kuyachukia.

Huwezi lazimisha kupendwa bhana, na kamwe Mungu hawezi kukulazimisha umpende. Kukulazimisha haibadilishi ukweli kuwa haumpendi. Kumbuka Mungu ni Haki na Kweli.

Mchongo ukoje? Ipo hivi;

Jinsi uonavyo Ulimwengu wa nje (huu unaoonekana) ndivyo katika Ulimwengu wa ndani usioonekana, Ulimwengu wa Nafsi.

Itazame Dunia, Dunia ni moja lakini inamazingira tofauti tofauti, kuna sehemu zenye baridi kali mpaka barafu, kuna sehemu za jangwa, kuna sehemu za hali ya hewa ya kati, kuna sehemu zenye mvua nyingi, na zipo zenye mvua za Waarabu.

Kuna milimani na mabondeni, sehemu zenye maziwa, mito na bahati, sehemu yenye misitu mine, nyasi na vichaka, sehemu yenye wanyama wa aina hii sehemu nyingine hakuna.

Sasa ni uchaguzi wa mtu kutumia kile akipendacho, ukitaka kuishi kwenye baridi ni wewe, Mungu hawezi kukulazimisha uishi sehemu isiyo ya baridi wakati wewe unapenda. Haipo hiyo. Ukitaka kula chakula au wanyama fulani ni wewe mwenyewe.

Ila elewa kuwa vipo vitu ni sumu na cool vitu sio sumu. Ni wewe mwenyewe unachagua ule sumu au usile. Nasema ni wewe mwenyewe, ni kutokana na upendo wako.

Kama unavyoishi hapa Duniani kulingana na umri wako, jinsia yako, kipato na hadhi yako, mtazamo wako ndivyo nafsi yako itakavyoishi baada ya mwili wako kuondoka.

Mfano huwezi ishi Masaki, Mikocheni, Upanga wakati kipato chako na daraja lako ni kuishi kwa walalahoi huko.

Kunguru na njiwa hawawezi kaa pamoja, wanasema ndege wafananao huruka pamoja. Nenda hata wodini huko mahospitalini utaona kabisa kuwa mgonjwa wa akili hawezi lazwa wodi ya wazazi au mgonjwa aliyemahututi hawezi lazwa wodi ya wagonjwa wa meno.

Maisha ni uchaguzi wa mtu mwenyewe. Mungu kamwe hana huo muda wa kukuamulia nini chakupenda. Kuku hawezi zaa bata, kila mmoja atakaa sehemu yake. Vivyohivyo hata ukifa roho yako itaenda mahali inapopapenda, na wala hautachomwa moto.

Kama unapenda uzinzi na kuchukua wake za watu na kuua watu basi nafsi yako itaishi katika Ulimwengu wa watu wa aina yako ili mchukuliane wake na waume zenu kwa jinsi mpendavyo, ili muone utamu wa kile mnachokipenda.

Sheria siku zote sio upendo, Sheria hizi za nchi zipo kwaajili ya kudhibiti matendo ha mwili na sio nafsi. Upendo upo kwenye nafsi ya mtu wakati sheria ipo katika mwili wa mtu. Mtu anapoua akahukumiwa jela kinachoadhibiwa ni mwili wake lakini nafsi yake haiadhibiwi.

Utalipwa sawasawa na matendo ya nafsi yako, Dhamiri na utapelekwa kwenye Ulimwengu unaofanana na nafsi yako. Hiyo ndio tafsiri ya moto wa Jehanum na sio kuchomwa kama wengi walivyotafsiri au wanavyojua.

Mungu Mkuu hukupa na anatoa kitu kulingana na mtu au kiumbe husika, Ulimwengu wa wapenda haki, wapenda dhulma, wenye upendo, wenye chuki, wasema uongo na wauaji, ulimwengu wa wasema kweli na watoa uzima.

Ni wewe tuu unachagua wapi unapenda na hayo ndio yatakuwa maisha yako mpaka Mungu Mkuu atakapoona imetosha. Ukitaka kubadili vitu upendavyo ni wewe, lakini mpaka Mungu atakapoona inatosha, uende katika Ulimwengu mwingine.

Ni kama hapa Duniani, vile unavyoishi ndivyo ulivyoamua kuishi au wazazi wako walivyotaka uishi (kumbuka ulikuwa katika mwili wa wazazi wako). Hakuna kulaumiana wala hakuna wakumlaumu. Hayo ndio maisha!

Acha nipumzike sasa,
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Jifariji.
 
MUNGU Yehova, Baba yetu wa mbinguni hamchukii mtu, Bali huichukia dhambi. Dhambi ni uasi dhidi ya MUNGU. MUNGU Huwa na uwezo wa kughadhabika kutokana na dhambi. Kuna mifano dhahiri ya madhihirisho ya ghadhabu ya MUNGU kushukia wanadamu.

Yehova YWHW Aliwahi kuiangamiza dunia yote kwa gharika ya maji. walipona watu wanane tu. Nuhu na familia yake.

Mwenyezi MUNGU, Yehova YWHW Aliwahi kuiteketeza miji miwili mikubwa ya Sodoma na Gomora kwa moto. wakaokoka watu watatu tu. Lutu na mabinti zake wawili.

hivyo endeleeni KUJIDANGANYA!


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Uliona wapi upendo unatafutwa Kwa nguvu au kulazimishwa na Kwa vitisho?

unalazimishwa na nani mzee wa fasihi???

umeumbwa na uhuru wa kuchagua uende wapi unasema unalazimishwa unatishwa.

ukishikwa na traffic polisi akakwambia wewe kenge vaa kofia ngumu na uendeshe piki piki kwa umakini laa sivyo utapasuka,unasema anakutisha.
 
unalazimishwa na nani mzee wa fasihi???

umeumbwa na uhuru wa kuchagua uende wapi unasema unalazimishwa unatishwa.

ukishikwa na traffic polisi akakwambia wewe kenge vaa kofia ngumu na uendeshe piki piki kwa umakini laa sivyo utapasuka,unasema anakutisha.
Kwani mungu aliumba pikipiki ...ukitembea Kwa miguu hilo kofia gumu la kazi Gani ????
 
MUNGU Yehova, Baba yetu wa mbinguni hamchukii mtu, Bali huichukia dhambi. Dhambi ni uasi dhidi ya MUNGU. MUNGU Huwa na uwezo wa kughadhabika kutokana na dhambi. Kuna mifano dhahiri ya madhihirisho ya ghadhabu ya MUNGU kushukia wanadamu.

Yohova YWHW Aliwahi kuiangamiza dunia yote kwa gharika ya maji. walipona watu wanane tu. Nuhu na familia yake.

Mwenyezi MUNGU, Yohova YWHW Aliwahi kuiteketeza miji miwili mikubwa ya Sodoma na Gomora kwa moto. wakaokoka watu watatu tu. Lutu na mabinti zake wawili.

hivyo endeleeni KUJIDANGANYA!


JESUS IS LORD&SAVIOR
Mungu angefuta kitu kinachoitwa dhambi....mbona simple tu kwake .anaona ugum gan Sasa kufuta dhambi watu tuishi
 
Kwani mungu aliumba pikipiki ...ukitembea Kwa miguu hilo kofia gumu la kazi Gani ????

Mungu kaumba vitu vya maana kuliko piki piki.

ukitembea kwa miguu huhitaji piki piki,ila unahitaji umakini ndio maana ktk ubongo kuna sehem ya tahadhali.
 
Mungu kaumba vitu vya maana kuliko piki piki.

ukitembea kwa miguu huhitaji piki piki,ila unahitaji umakini ndio maana ktk ubongo kuna sehem ya tahadhali.

Mungu kaumba vitu vya maana kuliko piki piki.

ukitembea kwa miguu huhitaji piki piki,ila unahitaji umakini ndio maana ktk ubongo kuna sehem ya tahadhali.
Ungepewa nafas ya kumshauri mungu ..ungemshauri aendelee kumwacha shetani msumbufu anatufanya sisi tunakua wadhambi....
 
Huo ndiyo ukweli. Huwezi fanya dhambi miaka 70 halafu ukachomwa moto milele. Yaani miaka elfu, laki, milioni, bilioni, trilioni wewe unaungua tu. Hii ni hadithi iliyotungwa na shetani.
 
Ungepewa nafas ya kumshauri mungu ..ungemshauri aendelee kumwacha shetani msumbufu anatufanya sisi tunakua wadhambi....

siwezi kumshauri Mungu.

ushawishi na usumbufu ni wa shetani,ila dhambi ni za kwako.

faida utakayopata ni kuchomwa pamoja nayeye kama ulivyokuwa naye hapa mnapeana michongo.
 
Back
Top Bottom