Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Mungu mwenye Upendo hawezi kuchoma watu kwa moto. Huo ni Ushetani

Vitabu vyote vya kidini ni stori za kusadikika, Fiction stories. Ndio maana hutofautiana maelezo kwenye kuelezea uwepo wa Mungu

Biblia ni reference kwa imani yako tu, Na si reference ya watu wote, Maana hata mwislamu atakwambia reference yake ni Quran.

Nimechagua kuiamini biblia as my reference kama wewe ulivyochagua kuviamini vyanzo unavyovitumia ingawa hujanieleza ni reference zipi ulizotumia mpaka kusema biblia ni fiction stories
 
Anaandika Robert Heriel,
Mtibeli.

Kuna Mungu Muumba wa mbingu na nchi halafu kuna miungu. Mungu Mkuu ambaye hajawahi kuonekana na kamwe hatokuja kuonekana Daima milele, hawezi kufanya wala kuwaza huo upuuzi wa kuchoma watu, hilo haliwezekaniki!

Miungu hii inayoabudiwa ndio inaweza kufanya hivyo, lakini yule Mungu wa miungu huo muda hana, na hawezi kufanya hivyo.

Mungu Mkuu ni Upendo, na kamwe upendo haulazimishwi. Yaani, ati Mungu aliyekuumba akulazimishe umpende (umuabudu) wakati alikuwa na uwezo wa kukuumba automatic ukawa unampenda!

Kwanza umpende (umuabudu) ili yeye apate nini? Halafu usipompende ati akuchome, wewe kosa lako lipo hapo? Yaani moyo wako haumpendi Mungu aliyekuumba, unapenda jambo jingine nini kosa lako, iko wapi haki hapo?

Mungu mwenye Upendo na muweza wa yote, anataka mtu apende anachokipenda! Kwanza yeye ndio aliyekufanya uwe hivyo ulivyo, upende unayoyapenda, achana na yale unayoyatamani na kuyachukia.

Huwezi lazimisha kupendwa bhana, na kamwe Mungu hawezi kukulazimisha umpende. Kukulazimisha haibadilishi ukweli kuwa haumpendi. Kumbuka Mungu ni Haki na Kweli.

Mchongo ukoje? Ipo hivi;

Jinsi uonavyo Ulimwengu wa nje (huu unaoonekana) ndivyo katika Ulimwengu wa ndani usioonekana, Ulimwengu wa Nafsi.

Itazame Dunia, Dunia ni moja lakini inamazingira tofauti tofauti, kuna sehemu zenye baridi kali mpaka barafu, kuna sehemu za jangwa, kuna sehemu za hali ya hewa ya kati, kuna sehemu zenye mvua nyingi, na zipo zenye mvua za Waarabu.

Kuna milimani na mabondeni, sehemu zenye maziwa, mito na bahati, sehemu yenye misitu mine, nyasi na vichaka, sehemu yenye wanyama wa aina hii sehemu nyingine hakuna.

Sasa ni uchaguzi wa mtu kutumia kile akipendacho, ukitaka kuishi kwenye baridi ni wewe, Mungu hawezi kukulazimisha uishi sehemu isiyo ya baridi wakati wewe unapenda. Haipo hiyo. Ukitaka kula chakula au wanyama fulani ni wewe mwenyewe.

Ila elewa kuwa vipo vitu ni sumu na cool vitu sio sumu. Ni wewe mwenyewe unachagua ule sumu au usile. Nasema ni wewe mwenyewe, ni kutokana na upendo wako.

Kama unavyoishi hapa Duniani kulingana na umri wako, jinsia yako, kipato na hadhi yako, mtazamo wako ndivyo nafsi yako itakavyoishi baada ya mwili wako kuondoka.

Mfano huwezi ishi Masaki, Mikocheni, Upanga wakati kipato chako na daraja lako ni kuishi kwa walalahoi huko.

Kunguru na njiwa hawawezi kaa pamoja, wanasema ndege wafananao huruka pamoja. Nenda hata wodini huko mahospitalini utaona kabisa kuwa mgonjwa wa akili hawezi lazwa wodi ya wazazi au mgonjwa aliyemahututi hawezi lazwa wodi ya wagonjwa wa meno.

Maisha ni uchaguzi wa mtu mwenyewe. Mungu kamwe hana huo muda wa kukuamulia nini chakupenda. Kuku hawezi zaa bata, kila mmoja atakaa sehemu yake. Vivyohivyo hata ukifa roho yako itaenda mahali inapopapenda, na wala hautachomwa moto.

Kama unapenda uzinzi na kuchukua wake za watu na kuua watu basi nafsi yako itaishi katika Ulimwengu wa watu wa aina yako ili mchukuliane wake na waume zenu kwa jinsi mpendavyo, ili muone utamu wa kile mnachokipenda.

Sheria siku zote sio upendo, Sheria hizi za nchi zipo kwaajili ya kudhibiti matendo ha mwili na sio nafsi. Upendo upo kwenye nafsi ya mtu wakati sheria ipo katika mwili wa mtu. Mtu anapoua akahukumiwa jela kinachoadhibiwa ni mwili wake lakini nafsi yake haiadhibiwi.

Utalipwa sawasawa na matendo ya nafsi yako, Dhamiri na utapelekwa kwenye Ulimwengu unaofanana na nafsi yako. Hiyo ndio tafsiri ya moto wa Jehanum na sio kuchomwa kama wengi walivyotafsiri au wanavyojua.

Mungu Mkuu hukupa na anatoa kitu kulingana na mtu au kiumbe husika, Ulimwengu wa wapenda haki, wapenda dhulma, wenye upendo, wenye chuki, wasema uongo na wauaji, ulimwengu wa wasema kweli na watoa uzima.

Ni wewe tuu unachagua wapi unapenda na hayo ndio yatakuwa maisha yako mpaka Mungu Mkuu atakapoona imetosha. Ukitaka kubadili vitu upendavyo ni wewe, lakini mpaka Mungu atakapoona inatosha, uende katika Ulimwengu mwingine.

Ni kama hapa Duniani, vile unavyoishi ndivyo ulivyoamua kuishi au wazazi wako walivyotaka uishi (kumbuka ulikuwa katika mwili wa wazazi wako). Hakuna kulaumiana wala hakuna wakumlaumu. Hayo ndio maisha!

Acha nipumzike sasa,
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Kuna tukio zito linakwenda kuukumba mji wa BANDARI salama,

Tetemeko kuu litatikisa Bahari na kupasua ardhi ya mji huo, madhara yatakuwa mji nzima,

Hakutakuwa na nyumba ilosimama juu ya ardhi.

TAREHE : (1-20).

Mwezi: April - May.

Mwaka: 2024.

SAFETY ZONE: Kuanzia KIBAHA Banda la ndege na kuendelea.

Huo Si mwisho wa Dunia, Bali ni mwanzo tu wa Mungu kuwakumbusha WANADAMU kuwa Yupo na hapendi dhambi na UOVU.

NB: Wajinga watachukua hatua, bt Werevu/wasomi watapuuza kama enzi za Safina na NUHU Ili wasubiri yatokee ndo wapige Mbizi.

ANGALIZO: Tembelea U-Tube, UNYAKUO TV. Kwa taarifa zaidi.

Amen
 
Hata kama sio moto bali ni hali tu iweje iwe ya mateso? Yaani kwanini atutese?
Yeye achukue watu wake wanaomwamini na wasiotenda dhambi, hao wengine aachane nao , iweje iwe lazima kufata anavyotaka yeye?

Hapo hapo katumwaga humu duniani tumejikuta tunatofautiana kiimani tunapigana vita wenyewe kwa wenyewe, ili iweje sasa?
Alishindwaje kufanya tuwe na imani moja anayoitaka yeye?
Anatuchanganya haeleweki
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Kwa akili ya kawaida kuna vitu havimake sense, basi tu mmeamua kujitoa ufahamu kwasababu mnamuogopa Mungu, lkn mkiulizwa maswali mnashindwa kutoa ufafanuzi
🤓🤓🤓🤓🙌🙌🙌😂😂😂
Hayo mambo yapo Demi
Ni vile kuna situation ujakutana nazo tu
 
Mimi ni Deist.

Deists hatupingi uwepo wa muumbaji (creator) lakini hatukubaliani na dini yoyote ile.

Uzi mzuri sana kwa open-minded people. Wenzetu (wazungu) huwa wanafanya debates "Theist vs Atheist" na huwa wanajadili kwa points za msingi sana.

Nitaacha hapa quote ya Atheist mmoja maarufu.
20230728_192907.jpg
 
Inawezekana ni kweli Mungu yupo. Ila jinsi mnavyomtafsiri na kuwalisha watu matango pori ndo tatizo.
Ila wale viongozi wa mchongo ndio ulisha watu matango poli..

Pia ishu zingine zote sijui moto.
Ni vitisho na nazani unajua why kuna vitisho kama hivo
 
MPAKA SASA UPO NEUTRAL

kaka robert kadri unavyozidi kusoma naona unafunguka kuwa tu mkweli kama sisi mungu mwenye upendo wote, ujuzi wote na nguvu zote hayupo.
Muanzisha uzi ni Agnostic Atheist. Bado ana maswali mengi ambayo yanafanya anashindwa kuelewa asimame wapi kwasababu tokea akiwa mdogo ameshakuwa brainwashed na dini.
 
Back
Top Bottom