Mungu na Allah mbona wana itikadi tofauti? Je, ni wamoja au pande mbili zinazokinzana?

Mungu na Allah mbona wana itikadi tofauti? Je, ni wamoja au pande mbili zinazokinzana?

Unataarifa kwamba Wote wamehidi vitu sawa??

Je Mungu wa Biblia Hajaahidi Pombe??
Unaamini Mungu wa Biblia Hajafundisha kisasi?
Unaamini Kwamba Mitume wa Biblia (Yahudi) ni sawa na Mitume wa Ukristo na ni sawa na mitume wa Uislam?
Nipe mfano wao. Usiniulize maswali .
 
Mambo ya dini ni changamoto sana
Vipi wahindu
Vipi kuhusu wabudha
Na dini nyinginezo
na mimi nilitaka kusema hivyo umeniwahi
Ila wazo langu ni kuwa mungu ana majina mengi waarabu wansema Alah,kiswahili tunasema MUNGU kingereza tunasema GOD kiitaliano tunasema Dio,Ugiriki ya kale Sol yaani Jua wengine wasema Yehova wengine wanasema Yahwe hata kilugha changu kuna jina lake

Mambo ya dini yanachanganya sana ya kaizari mpe kaizari ya mungu mpe mungu

Wahindu nao huyu mungu wetu tunayemuabudu wanamtambua kivingine kabisa ukiingiza habari za kina Ibrahim,Yakoo,Ismail,Daudi,Selemani,YESU hawawezi kukuelewa

BUDHA Ndio kabisaa hawaamini uwepo wa mungu yeyote wanasema na supreme being kila kitu kinakwenda kiasili ila ukitenda ubaya ukifa unaweza kuwa simba au mti na roho ya mtu inatoka duniani inakuwa form nyingine
 
Hawa ni wawili tofauti kabisa.. Mmoja ni Gangster tena muongo tena ni mwizi wa maandiko ya mwenzake na mwingine ni Ukweli na Uzima
 
Nipe mfano wao. Usiniulize maswali .
Ok sawa..
Kwanza kabisa Kuna Majina Ya Mungu zaidi ya 50 kwenye Biblia labda kama hufahamu Hilo..

Umezungumzia kuhusu Pombe wote wameahidi pombe..

Japo Nikukumbushe Kuwa Katika agano la kale Hakukuwa na Ahadi ya Kwenda Mbinguni wala Unyakulio Hilo jambo limeanza kipindi cha agano jipya..

Ila Usisahau Yesu aliahidi Wanafunzi kwamba watapata Kilaji siku ile Mpya..
So nadhani kuhusu Hilo wako sawa..

Marko 14:25

Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.

Verily I say unto you, I will drink no more of the fruit of the wine, until that day that I drink it new in the kingdom of God.

Andiko la pili limeeleza Nitakapokunywa na nyinyi..

Mathayo 26:29

Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

But I say unto you, I will not drink henceforth of this fruit of the wine, until that day when I drink it new with you in my Father's kingdom.

Tuendelee na Kuhusu Pombe..

Zaburi 75:8

Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe,

Na mvinyo yake inatoka povu;
Kumejaa machanganyiko;
Naye huyamimina.
Na sira zake wasio haki wa dunia

Watazifyonza na kuzinywa.

For in the hand of the LORD there is a cup, and the wine is red; it is full of mixture; and he poureth out of the same: but the dregs thereof, all the wicked of the earth shall wring them out, and drink them

so Huo ni.mfanano wa kwanza mfanano wa Pili ni kuwa Wote wameahidi Kuna Siku ya qiyama kitu ambacho kwa wayahudi hakuna Hiyo siku..

So nakukaribisha Mkuu Tuendelee na Mjadala ila wote ni sawa na hata Muhamedi na Yesu wote ni sawa tu
 
Wataalamu wa dini mje hapa?

Je, kuna andiko lolote linaonesha kuwa Mungu ni Allah au Allah ni Mungu?

Mungu alijifunua kwa mara ya kwanza kwene uzao wa Israel (mlolongo uliowaleta Israel yaan Abraham—Isack —-Yakobo (Israel)——Yesu)

Wakati ALLAH alijifunua kwa waarabu uzao wa mtoto wa nje ya ndoa Ishmael.

Yaan mlolongo ulioleta Waarabu
(Abraham——Ishmael (arabs)——Mtume Muhammad).

Mungu alijifunua miaka mingi kabla ya kuja kwa Yesu kuja kwamba miaka mingi kabla (2000+ nyuma).

Allah miaka 600 baadaa ya kuja Yesu au alikuja miaka zaidi ya mingi baada ya kujifunua Mungu wa kwanza.

Kwanini hawa wawili wawe ni wamoja?

NB: Ni suali la uelewa tu sina maana mbaya ndugu zangu.
Swali gumu sana
 
Siyo kweli allah maana yake ni mungu hata wakristo waarabu wanatumia neno allah kanisani kumaanisha mungu
Kwanini hairuhusiwo kwa waislamu kutaja jina Mungu lugha zao hadi warejee jina alaah
 
Kabla ya uislamu waarabu wengi walikuwa wakristo, na wengine wayahudi, wamajusi na waabudu masanamu, ko hawa waliokuwa wakristo kutokana na kuisoma sana injili(kitabu halisi cha yesu na sio biblia human version) ko walisubiri ujio wa mtume aliyetabiriwa kwenye injili naye ni muhammad, then Mungu yuleyule aliyetabiriwa kwenye ukristo wa before Islamic era ndiye yuleyule aliyeabudiwa within muhammad era.

Jamaa ameuliza kistaarabu, ila kutokana na ujinga wako na chuki ukaandika usiyoyajua ili waislamu waumie,,,,,!!!!

Kumbe binadamu mimi nimekuja kujufunza usiyoyajua ikiwamo adabu na heshima.
Madrasut gani walikudanganya huu upupu Mwamba?
😁😁
 
Inaruhusiwa mkuu ni kukosa elimu tu na kutofahamu
Hairuhusiwi na nimeshuhudia shahada kibao watu wakishahadia kwa lugha zote mwisho hutaja alaah na sio Mungu kwa lugha husika

Kwa mfano waSwahili wasiokuwa kiarabu hushuhudia hivi " Hapana Mungu anayepaswa kuabudiwa isipokuwa "Allah" na Muhammad mtume wake"

Kingereza hushuhudia hivi
I bear witness that there is no God but Allah – i.e. there is none worthy of worship but Allah), and Muhammad is the Messenger of Allah.

Unaona hapo? Lugha mbili zimetumika kushuhudia ila neno Allah limetokea ilhali lugha zote hizo Zina tafsiri ya Mungu katika lugha husika
 
Kwaiyo ulimwengu nani kaumba bro..Tungependa kujua.
Kwa nini unadhani ulimwengu Lazima uwe umeumbwa?

Kwa nini hudhani kwamba ulimwengu upo wenyewe tu pasipo kuumbwa?

Kama umeweza kuamini Mungu usiyemjua wala hujawahi kumuona hana muumbaji, Unashindwaje kuamini pia kwamba ulimwengu haujaumbwa?

Kama haiwezekani ulimwengu kujiumba wenyewe, Pia hata huyo Mungu haiwezekani ajiumbe mwenyewe.

Na kama huyo Mungu haitaji muumbaji, Basi hata ulimwengu hauhitaji muumbaji.

You cannot exclude that God from this logic.
 
Hairuhusiwi na nimeshuhudia shahada kibao watu wakishahadia kwa lugha zote mwisho hutaja alaah na sio Mungu kwa lugha husika

Kwa mfano waSwahili wasiokuwa kiarabu hushuhudia hivi " Hapana Mungu anayepaswa kuabudiwa isipokuwa "Allah" na Muhammad mtume wake"

Kingereza hushuhudia hivi
I bear witness that there is no God but Allah – i.e. there is none worthy of worship but Allah), and Muhammad is the Messenger of Allah.

Unaona hapo? Lugha mbili zimetumika kushuhudia ila neno Allah limetokea ilhali lugha zote hizo Zina tafsiri ya Mungu katika lugha husika
Ndio nasema ni makosa ya lugha yanafanyika ila allah maana yake ni mungu kwa kiarabu na hata wakristo wa nchi za kiarabu makanisani mwao wanatumia allah na huyu mkristo mwenzako hapo chini kaelezea vizuri sana kuhusu swala hilo mkuu
 
Attachments

  • Screenshot_20240614-134612_Chrome.jpg
    Screenshot_20240614-134612_Chrome.jpg
    357.4 KB · Views: 4
  • Screenshot_20240614-154127_Chrome.jpg
    Screenshot_20240614-154127_Chrome.jpg
    219.8 KB · Views: 4

Sijui kuhusu wakristu waarabu ila basi kama ni hivyo waislamu waache hili kosa la kummiliki Mungu na kumpa jina Allah kama ujumuishi wa uungu katika lugha zote
 
Sijui kuhusu wakristu waarabu ila basi kama ni hivyo waislamu waache hili kosa la kummiliki Mungu na kumpa jina Allah kama ujumuishi wa uungu katika lugha zote
Yes hilo ni kosa allah maana yake ni mungu hata waarabu wakristo hata leo ukienda palestina wakristo wanamwita allah, simply maana yake ni mungu
Na kwa kihebrew mungu ni yahweh na sio jina lake yahweh kama wakristo wengi wanavyojua ,yahweh maana yake ni mungu
 
Wataalamu wa dini mje hapa?

Je, kuna andiko lolote linaonesha kuwa Mungu ni Allah au Allah ni Mungu?

Mungu alijifunua kwa mara ya kwanza kwene uzao wa Israel (mlolongo uliowaleta Israel yaan Abraham—Isack —-Yakobo (Israel)——Yesu)

Wakati ALLAH alijifunua kwa waarabu uzao wa mtoto wa nje ya ndoa Ishmael.

Yaan mlolongo ulioleta Waarabu
(Abraham——Ishmael (arabs)——Mtume Muhammad).

Mungu alijifunua miaka mingi kabla ya kuja kwa Yesu kuja kwamba miaka mingi kabla (2000+ nyuma).

Allah miaka 600 baadaa ya kuja Yesu au alikuja miaka zaidi ya mingi baada ya kujifunua Mungu wa kwanza.

Kwanini hawa wawili wawe ni wamoja?

NB: Ni suali la uelewa tu sina maana mbaya ndugu zangu.

Kwa kukusaidia; Ungeanza kwa kuandika maana ya neno Mungu kwa kadri ya Uelewa wako kwani Miungu wapo wengi hivyo sijui kama unaongelea Mungu yupi. Ukisha tupa definition (Maana yake) ndio tutajua kama unaongelea Allah au Mungu mwingine....
 
Yes hilo ni kosa allah maana yake ni mungu hata waarabu wakristo hata leo ukienda palestina wakristo wanamwita allah, simply maana yake ni mungu
Na kwa kihebrew mungu ni yahweh na sio jina lake yahweh kama wakristo wengi wanavyojua ,yahweh maana yake ni mungu
Yahweh ni jina katika utambulisho yenye maana "Mimi ndiye" au "Mimi ninayekuwepo" inayowakilisha ukuu wa Mungu lakini hakuna muislamu atakayekubali kumuita Mungu Yahweh au Yehova
 
Yahweh ni jina katika utambulisho yenye maana "Mimi ndiye" au "Mimi ninayekuwepo" inayowakilisha ukuu wa Mungu lakini hakuna muislamu atakayekubali kumuita Mungu Yahweh au Yehova
Yahweh ni kihebrew maana yake ni mungu ndio maana nasema tatizo la waafrika ni elimu, sasa wewe mtu mweusi unatakiwa useme mungu ,yahweh sio jina la mungu
Pata elimu hapo chini mkristo mwenzako aliyezunguka dunia na akaelimika amekuelezea vizuri
 
Attachments

  • Screenshot_20240614-154127_Chrome.jpg
    Screenshot_20240614-154127_Chrome.jpg
    219.8 KB · Views: 4
  • Screenshot_20240614-134612_Chrome.jpg
    Screenshot_20240614-134612_Chrome.jpg
    357.4 KB · Views: 4
na mimi nilitaka kusema hivyo umeniwahi
Ila wazo langu ni kuwa mungu ana majina mengi waarabu wansema Alah,kiswahili tunasema MUNGU kingereza tunasema GOD kiitaliano tunasema Dio,Ugiriki ya kale Sol yaani Jua wengine wasema Yehova wengine wanasema Yahwe hata kilugha changu kuna jina lake

Mambo ya dini yanachanganya sana ya kaizari mpe kaizari ya mungu mpe mungu

Wahindu nao huyu mungu wetu tunayemuabudu wanamtambua kivingine kabisa ukiingiza habari za kina Ibrahim,Yakoo,Ismail,Daudi,Selemani,YESU hawawezi kukuelewa

BUDHA Ndio kabisaa hawaamini uwepo wa mungu yeyote wanasema na supreme being kila kitu kinakwenda kiasili ila ukitenda ubaya ukifa unaweza kuwa simba au mti na roho ya mtu inatoka duniani inakuwa form nyingine
Msingi wa dini ni kuwa na jamii ya kutenda mema hata babu zetu katika matambiko yao tabia njema ilisisitizwa sana.

Ni vile tu kwetu ukristo umevamiwa na matapeli na uislam umevamiwa na magaidi ni machafuko kila kona.
 
Kabla ya uislamu waarabu wengi walikuwa wakristo, na wengine wayahudi, wamajusi na waabudu masanamu, ko hawa waliokuwa wakristo kutokana na kuisoma sana injili(kitabu halisi cha yesu na sio biblia human version) ko walisubiri ujio wa mtume aliyetabiriwa kwenye injili naye ni muhammad, then Mungu yuleyule aliyetabiriwa kwenye ukristo wa before Islamic era ndiye yuleyule aliyeabudiwa within muhammad era.

Jamaa ameuliza kistaarabu, ila kutokana na ujinga wako na chuki ukaandika usiyoyajua ili waislamu waumie,,,,,!!!!

Kumbe binadamu mimi nimekuja kujufunza usiyoyajua ikiwamo adabu na heshima.
Kuna ujinga umeandikwa hapa.
 
Back
Top Bottom