Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Nashukuru Sana kwa mchango wako ulionyeshaa ukomavu wako wa kifikra, umechagia hoja kiungwana Sana. Napenda nikuhakikishie kuwa Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati katika kutumia mamlaka take kuwatumikia watanzania, amefanya hivyo pasipo ubaguzi wa aina yoyote Ile, ndio sababu unaona hata namna alivyoweza kutoa nafasi ya kuweza kuonana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya upinzani

Ni kiongozi aliye msikivu,mwenye masikio ya kusikia sauti zote na macho ya kumtazama kila mtu, Ni kiongozi anayethamini mchango wa kila mtanzania katika ujenzi wa Taifa letu, Ni kiongozi anayeamini kuwa pamoja na tofauti zetu za kisiasa tunaweza tukaijenga nchi yetu na tukafaidi kwa pamoja matunda ya kazi za mikono yetu Kama Taifa.

Ndio maana ya kuona namna Taifa lilivyoungana kwa Sasa na kushikamana vizuri
 
Hayati Magufuli mlimpa SIFA Kama hizi matokeo yake mpaka Mkamkufuru MUNGU na MATOKEO yake mnayajua kilichompata ENDELEENI kumdhihaki MUNGU
Katiba ndio iliyompa MAMA yetu URAIS
 
Mama hawezi kazi,ingekuwa wananchi serious alitakiwa kufukuzwa ikulu hata leo saa 8 mchana
Kama Ofisi zenu tu hapo ufipa zinewashinda kuzipaka rangi tu zipendeze kwa matumizi mabaya ya Fedha, Naamini huwezi ukaelewa kazi kubwa anayoifanya mh Rais iliyoiheshimisha nchi yetu Ndani na nje ya Tanzania, huwezi ukaona kazi iliyofanyika katika kilimo,afya, Elimu, N.k kwa kuwa umejipa ukipofu wa akili na mawazo
 
Wewe ni Samia Samia Samia hadi kero hebu katafute hela zako maana yeye hakuji na anatafuta zake
Mimi Ni mkulima na naishi kwa kilimo ,jembe ndio kalamu yangu na shamba ndio daftari langu na mabega yangu ndio begi langu
 
Mimi Ni mkulima na naishi kwa kilimo ,jembe ndio kalamu yangu na shamba ndio daftari langu na mabega yangu ndio begi langu
Acha kiherehere Cha mama Samia tafuta hela yeye Hana mpango nawewe maana Huna dili unachosha mama Samia tafuta hela ndio inshu mzima
 
Ndo maana nasema hapo Lumumba hamna mkakati mzuri wa kuhakikisha CCM inaendelea kushika DOLA.

Ktk wakati mgumu kama huu mnawezaje mtuma mtu aje amsifie kiongozi sifa za ajabu ajabu na anaweka namba ya simu kutafuta uteuzi?

Mnamuharibia KIONGOZI wetu Badala ya kumsaidia, tunaosema Kweli ndo TUNAMPENDA.

Ameeeen.
 
Acha kiherehere Cha mama Samia tafuta hela yeye Hana mpango nawewe maana Huna dili unachosha mama Samia tafuta hela ndio inshu mzima
Naendelea na kazi zangu na naendelea kumshukuru mh Rais kwa namna alivyotusaidia wakulima msimu huu kwa kutupatia mbolea za Ruzuku zenye Bei nafuu ukilinganisha na msimu uliopita.

Mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa elfu 70 tu
 
Ndo maana nasema hapo Lumumba hamna mkakati mzuri wa kuhakikisha CCM inaendelea kushika DOLA...
Kwani Kuna shida kumsifia Kiongozi?

Afu mtoa mada anasema Raia kawekwa na Mungu wewe unasema anasifiwa.

Mbona wengine wameaeka matamasha ya kumuombea Mbeya na Mwanza?
 
Ukame haujaanza leo kilichopo ni kutokuwajibika huu utani mngefanya kipindi cha Mwendazake raia hawataki mikakati wanataka matokeo sio blah blah miaka 61 ya uhuru bila maji na umeme
Matokeo ndio yanakuja baada ya mikakati Kama ambavyo ulishuhudia namna mh Rais akizindua mradi mkubwa wa maji pamoja na mitambo mikubwa ya kuchimbia visima virefu vya maji vitakavyo saidia kuondoa tatizo la maji
 

Usimchanganye Mungu na majizi ya kura.
 
Haya mambo ya kusifia viongozi dhalimu yalikuwepo hata wakati wa fashisti Adolf Hitler, so wakina nyinyi kumsifia mlinzi mkuu wa mafisadi haliwezi kuwa jambo jipya sana, ni mwendelezo wa Mambo yale yale ya kiwendawazimu kwa nyakati tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…