Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Ccm ni chama cha ki freemasonry, jinsi raia wanavyotaabika kwa shida ndipo na chenyewe kinapopata nguvu.
CCM ndio chama pekee barani Afrika na Dunia nzima kwa ujumla kilichobaki kinaheshimika miongoni mwa vyama vichache vilivyopo vya umri wake, hii Ni kutokana na namna kinachogusa maisha ya watu na kuwa karibu zaidi na watu kwa kuwasikiliza na kuwatatulia kero wananchi
 
Haya mambo ya kusifia viongozi dhalimu yalikuwepo hata wakati wa fashisti Adolf Hitler, so wakina nyinyi kumsifia mlinzi mkuu wa mafisadi haliwezi kuwa jambo jipya sana, ni mwendelezo wa Mambo yale yale ya kiwendawazimu kwa nyakati tofauti.
Rais mama Samia Ni Mzalendo wa dhati na mwenye dhamira ya dhati katika kuijenga nchi yetu, uzalendo wake ndio umewafanya watanzania Kuendelea kumwamini na kumuunga mkono
 
Ccm ni chama cha ki freemasonry, jinsi raia wanavyotaabika kwa shida ndipo na chenyewe kinapopata nguvu.
Hapana. CCM inapata nguvu kwasababu ya kujimilikishia Vyombo vyote vya Usalama. Na wananchi tunataabika kwasababu ya upumbavu wetu wenyewe.

Siku tukijitambua tabu zetu zitatoweka na hapo ndipo patakuwa mwisho wa CCM.
 
Rais Samia kawekwa na mungu kwa kusudi kuu moja.

Mungu anataka kuifuta ccm tanzania kwa sababu ya kukufuru.
Mwenyezi Mungu anaipenda Sana Tanzania ndio sababu huwa anatuvusha katika nyakati zote ngumu tunazopitia Kama Taifa, Na siku zote watanzania tumekuwa tukiliombea Taifa letu na kuliweka mikononi mwake kimaombi, Rais wetu Ni mcha Mungu Ndio sababu hata uongozi wake unapendwa na watanzania kwa kuwa Ni uongozi unaomthamini kila mtu na kusikiliza sauti zote
 
Unaweza kuthibitisha pasipo na shaka haya unayosema?
Lucas mwashambwa

1. Ni kweli kabisa mamlaka ya U - rais aliyonayo Bi. Samia Suluhu Hassan imetoka kwa Mungu na ni yake Mungu...

2. Ni kweli pia, mwanadamu yeyote kwa njia za kubinadamu hawezi kumnyang'anya hiyo mamlaka yake...

3. Lakini ni UKWELI WA KIBIBLIA USIOPINGIKA kuwa Mungu mwenyewe aweza kumshusha na kumwondolea mamlaka yake ya u - Rais wakati wowote akitaka na kukiwa na sababu tena akiwatumia wanadamu hawahawa unaosema hawawezi kumwondoa/kumshusha...!

4. Na sababu zinazoweza kumfanya Mungu aruhusu wanadamu kumwondoa mamlakani Rais Samia ni iwapo atashindwa kutumia mamlaka yake kuhudumia watu wa Mungu kwa kadiri ya mapenzi yake Mungu..

5. Na hii huja iwapo watu WATALALAMIKA NA KUSEMA KWA MUNGU WAO kuwa, huyu uliyempa mamlaka yako ya u - Rais hatutendei haki yako na kwa hiyo mchukue, tupe mtu mwingine...!

It's just simple like that..
 
Hapana. CCM inapata nguvu kwasababu ya kujimilikishia Vyombo vyote vya Usalama. Na wananchi tunataabika kwasababu ya upumbavu wetu wenyewe. Siku tukijitambua tabu zetu zitatoweka na hapo ndipo patakuwa mwisho wa CCM.
Watanzania wanatambua kuwa CCM ndio chama pekee chenye uchungu na maisha yao na kilicho na Dira na muelekeo unaoeleweka,ndio sababu ya Kuendelea kuaminika kwa watanzania wote
 
Mwenyezi Mungu anasemaje kuhusu Katiba mpya?
Mwenyezi Mungu hutoa maaraifa kwetu wanadamu, katika maarifa aliyotupatia na kutupatia kiongozi mcha Mungu na mzalendo aliamua kuimarisha Demokrasia na umoja wa kitaifa ambapo Kuna kikosi kazi kiliiundwa na kuja na mapendekezo 18 ambayo yalikabidhiwa kwa serikali, serikali itayachakata kuyatathimini na kuyafanyia maboresho kwa maslahi mapana ya Taifa letu
 
MAMA kapata URais kwasababu ya Katiba yetu, aendelee kumshukuru. MUNGU kwa kuteuliwa hapo mwanzo kua makamu wa Rais bila hivo ingetuchukua labda karne kupata Rais mwanamke. Vilevile sio kila jambo linatokea limefanywa na MUNGU hata shetani anakazi zake pia.
Taifa letu siku zote lipo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na siku zote huyo ndio Ngao yetu Kama Taifa
 
Mara nyingi wajinga wanakuwaga wengi, na ndio hao mamilioni
Watanzania siyo wajinga, watanzania wanafahamu Ni chama kipi na kiongozi yupi mwenye upendo nao na anayeweza kuwatumikia kizalendo. Watanzania kwa umoja wao walishatambua kuwa CCM ndio chama pekee chenye uwezo wa kuwatumikia kwa uzalendo.

Watanzania wanaendelea kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kwa kutambua dhamira yake ya dhati katika kuwatumikia kiuzalendo na kwa utumishi uliotukuka na siyo kujitukuza na kujiinua
 
Wewe kichwa chako kinafanya kazi vizuri?
Unafahamu ni wafanyabiashara na wafanyakazi wangapi wanategemea umeme kama huduma ya msingi kwenye kazi zao na hasara wanayopata kuukosa?
Umeme ni vitu vidogo hivyo mvua zikitengamaa hutosikia Tena
 
Tatizo kuu la Rais Samia siyo urais wake Mama yetu mpendwa bali ni uthubutu wa kiuongozi wa kushindwa kuwajibika na kuwashisha. Yaani huku mitaani Rais Samia anatukanwa sana tena angekuwa na uwezo wa kusikia hayo matusi na machungu ya watu wanavyomuwazia nadhani asingeweza kulala usingizi. Chuki juu yake siyo ya kubumba kama ya enzi za vyuma za Dkt Magufuli, ya Rais Samia inasindikizwa na vitu vya kawaida sana kama kuteua watu wasio waadilifu, kukubali mgao wa maji na umeme, kuruhusu gharama za maisha kupanda etc. Yeye kosa lake ktk ni kuache ili mradi liende. Sisi wana CCM ndiyo tunaonja chungu ya kushindwa kumtetea. Kama upo Tanzania hebu jitokeze kitaa umsifie ila usiende msikitini
Mimi nipo mtaani nako kutana na watanzania wenzangu wa ainaa zote, ambapo kiukweli Ni kuwa Rais Samia anakubalika Sana huku mitaani , hata hili suala la umeme ameeleweka vizuri maana hata wananchi nao wanaona ukame uliopo ambapo hata maeneo yanayokuwag na maji mpaka muda huu kila mmoja anaona namna yalivyokauka,hivyo watanzania bado Wana Subira na kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali yetu ambayo imekuwa ikifanya mambo kwa uwazi na kuwaeleza watanzania kila kinachokuwa kinaendelea na hatua zinazokuwa zimechukuliwa katika kila kero
 
Hana tofauti na wale wanaosema Putin ni mteule wa Mwenyezi Mungu.
Mungu haipendi Tanzania kiasi hiki mpaka atuletee kiongozi dhaifu kiasi hiki?au mambo gani yanamfanya awe dhaifu?
 
Mungu haipendi Tanzania kiasi hiki mpaka atuletee kiongozi dhaifu kiasi hiki?au mambo gani yanamfanya awe dhaifu?
Rais Samia Ni kiongozi shupavu na madhubuti Sana, ndio maana unaona nchi ikiwa Tulivu na Amani, Ndio sababu unaona kila kero Inayojitokeza mbele yetu ikikabiliwa kishupavu na serikali yetu, ndio sababu unaona namna tulivyo fanikiwa katika secta nyingi ndani ya muda mfupi wa uongozi wake mama Samia
 
Back
Top Bottom