Mungu ndiye aliyempa Urais Mama Samia. Hawezi kushushwa na Mwanadamu mwenye chuki binafsi

Rais Samia Ni kiongozi Mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu Ndio sababu unaona namna anavyoungwa mkono na mamillion ya watanzania,huyo Hitler Nadhani unafahamu hatima yake kule ujerumani na historia yake katika Taifa lake mpaka leo
Mara nyingi wajinga wanakuwaga wengi, na ndio hao mamilioni
 
Tatizo kuu la Rais Samia siyo urais wake Mama yetu mpendwa bali ni uthubutu wa kiuongozi wa kushindwa kuwajibika na kuwashisha. Yaani huku mitaani Rais Samia anatukanwa sana tena angekuwa na uwezo wa kusikia hayo matusi na machungu ya watu wanavyomuwazia nadhani asingeweza kulala usingizi.

Chuki juu yake siyo ya kubumba kama ya enzi za vyuma za Dkt Magufuli, ya Rais Samia inasindikizwa na vitu vya kawaida sana kama kuteua watu wasio waadilifu, kukubali mgao wa maji na umeme, kuruhusu gharama za maisha kupanda etc. Yeye kosa lake ktk ni kuache ili mradi liende. Sisi wana CCM ndiyo tunaonja chungu ya kushindwa kumtetea. Kama upo Tanzania hebu jitokeze kitaa umsifie ila usiende msikitini
 
Samia angekuwa dhalimu Mbowe angekuwa ananyea debe saizi
Alternatively Mbowe yupo nje lakini wananchi walio wengi ambao hawaelewi hata nchi inaendeshwa vip ndio wanaopata taabu na hili wimbi jipya la walamba asali lililopata teuzi za kulindana baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki.
 
Hizo mbolea za ruzuku zipo wapi!!??
Mbona huku Kusini hazipo? Nimetoka Dodoma na Moro sijaziona,wakulima wanalalamika!!???


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alternatively Mbowe yupo nje lakini wananchi walio wengi ambao hawaelewi hata nchi inaendeshwa vip ndio wanaopata taabu na hili wimbi jipya la walamba asali lililopata teuzi za kulindani baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki.
Kama kupata ruzuku ya mbolea Ni tabu Bora iwe,

Kama kupata soko la uhakika la Mazao Yao Ni tabu Bora iwe,

Kama kueomeshewa watoto wao bure kuanzia chekechea Hadi University Ni tabu Bora iwe,

Kama kupata Huduma za jamii kila Kara Bora iwe,

Kama kupata ajira kila siku ni tabu Bora iwe,

Kama kupata miradi ya maji nk Ni tabu Bora iwe πŸ‘‡
 
Mungu haipendi Tanzania kiasi hiki mpaka atuletee kiongozi dhaifu kiasi hiki?au mambo gani yanamfanya awe dhaifu?
 
Kuona hivo ulivyotaja unabonyesha nyota ngapi ngapi
 
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu. Hizi nguvu bora ungewekeza kumsifia mama au baba yako mzazi kwa kukuleta duniani na kukupa malezi mazuri (kama kweli ulipewa) kuliko kutumia muda mwingi kumsifia mlinzi wa mafisadi.
 
 
Hitler alipewa na nani ?

Na wale wakoloni waliokuja na kutuibia nani aliwaonyesha njia...

Ya Kaisari mwachie Kaisari..., apart from wizi wa hapa na pale wananchi ndio wanamuweka mtu pale..., ndio maana hata wachawi wanaweza kuongoza (no divine power involved)
 
Mtoa mada. Vipi kuhusu wale wanamkubali na wanaompinga hii pia ni mipango ya nani.
 
MAMA kapata URais kwasababu ya Katiba yetu, aendelee kumshukuru. MUNGU kwa kuteuliwa hapo mwanzo kua makamu wa Rais bila hivo ingetuchukua labda karne kupata Rais mwanamke.

Vilevile sio kila jambo linatokea limefanywa na MUNGU hata shetani anakazi zake pia.
 
Rais Samia kawekwa na mungu kwa kusudi kuu moja.

Mungu anataka kuifuta ccm tanzania kwa sababu ya kukufuru.
 
Rais Samia kawekwa na mungu kwa kusudi kuu moja.

Mungu anataka kuifuta ccm tanzania kwa sababu ya kukufuru.
Ccm ni chama cha ki freemasonry, jinsi raia wanavyotaabika kwa shida ndipo na chenyewe kinapopata nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…