Mungu Ndiye Anayejua Atakayempokea Urais Rais Samia 2030

Mungu Ndiye Anayejua Atakayempokea Urais Rais Samia 2030

Mbona Trump alisema marekani imepata rais shetani Biden na mashetani wenzake!
 
Usimuhusishe Mungu na majizi ya kura, hakuna Mungu anayeendesha wizi wa kura. Nyie bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi hamuwezi kuelewa.

Usiombee machafuko au mapinduzi . Au wewe ulishajiripua ulaya kama mrundi hujali ?? Zanzibar toka 1964 haijakaa sawa tena , imekuwa ghost county hakuna kinachokwenda zaidi ya dhuluma na ubabe.

Nchi mwisho wake imekuwa ni ngawira ya Tanganyika.

Hayo ni matunda ya mapinduzi na vurugu. Likianza Tanganyika hakuna pa kukimbilia nchi zote jirani haziko sawa labda Zambia kidogo afadhali . Maji utaita mma
 
2025 nchi apewe Mwabukusi amejifafanua vizuri Kama mtetezi wa rasilimali za Tanganyika.
 
Baada ya Mama 2030
Kuna watu kama Simbachawene ,Lukuvi wanafaa kuwa next president.
 
Ndugu zangu watanzania,

Uongozi unatoka kwa Mungu,huyo ndiye awezaye kumuinua mtu na kumpa madaraka,huyo ndiye humpa kibali mtu akakubalika ,kuungwa mkono na kupendwa na watu,huyo ndiye humpitisha mtu katika njia ambayo wengine hawapitishwi,huyo ndiye humlinda na kumshindia vita vyote viwavyo mbele yake,huyo ndiye humpa mtu njia na maarifa,humuandalia mazingira na watu wa kumvusha na kumshika mkono, Humficha dhidi ya maadui na kuwapumbaza wabaya ili wasiweze kumfikiria wala kumtupia mishale ya kumjeruhi.

wakati mwingine hawa wateule walioandaliwa na Mungu huwa hata hawaelewi kama wanajukumu zito mbele yao juu ya Taifa letu,huwa siyo watu wenye uchu wala uroho wa madaraka na huwezi ukawakuta wakitumia mafedha mengi kununua au kuutafuta uongozi, bali watu hawa hupiganiwa sana na watu wazalendo ndani ya chama kuanzia wazee hadi wastaafu, hupiganiwa sana na watu nyeti na muhimu ndani ya vyombo vyote vya ulinzi na usalama,kuanzia usalama wa Taifa,JWTZ na polisi kwa ujumla.

Nawaambieni watanzania ya kuwa Mungu wetu ambaye amekuwa akilipigania Taifa letu Tayari ameshamuandaa Rais wetu ajaye baada ya mama Samia kumaliza muda wake 2030,Tayari ameshamuweka sawa katika ulimwengu wa kiroho,Tayari ameshayaelekeza macho,masikio na hisia ya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa mtu huyo ili waendelee kumlinda dhidi ya waroho na mafia wa kimadaraka.Tayari ameshaweka mkono wake juu ya mtu huyo, Tayari ameshatoa kibali kwake na kumpatia,ujio wake utapokelewa kwa shangwe , nderemo na vifijo katika kuendeleza kazi njema na ya kutukuka anayoendelea kuifaya Rais samia mpaka 2030.

Mungu ndiye anajuwa kwanini Amemuandaa huyo, kwanini kwa wakati huo ,Hivyo ndivyo alivyomuinua katika ulimwengu wa kiroho hayati Baba wa Taifa mwalimu nyerere ,mh Mzee Alli Hassan mwinyi ,Hayati Benjamini William mkapa ,Mh Dr Jakaya mrisho Kikwete,Hayati Dr John Pombe Joseph magufuli na Hatimaye mama wa Shoka kipenzi cha watanzania nuru ya wanyonge na Taa ya Taifa mh mama samia suluhu Hasssan.

Jiulizeni wakati wa kuinuliwa kwa mh All Hassan mwinyi kuliongoza Taifa letu kulikuwa na watu wangapi waliokuwa wakitupiwa macho kumrithi mwalimu nyerere nje ya mwinyi mwenyewe? Vipi wakati wa kuinuliwa kwa Hayati Benjamin mkapa ambaye wakati huo hakuwa maarufu sana ndani ya chama na hata kwa watanzania na wagombea wenzake? Vipi wakati wa mh Dr Jakaya mrisho Kikwete kulikuwa na wagombea wangapi? Vipi wakati wa hayati Dr Magufuli? Nani alitegemea kuwa ndiye angepewa ridhaa yakupeperusha Bendera ya chama mbele ya akina marehemu Benard kamilliusi Membe Au mh Edward lowassa aliyejiandaa kwa vita ya kuutaka Urais Tangia miaka ya Tisini?

Wenyeviti wangapi wa mikoa, wabunge, makatibu wa wa CCM wa mikoa walikuwa wakimuunga mkono mh lowassa? Mnakumbuka wimbo ulioimbwa wakati mh Kikwete akiingia ukumbini juu ya lowassa? Mnafikiri kwa nini aliinuliwa hayati Dr magufuli na kuwaacha wote na majina yao makubwa na ya kihistoria ndani ya chama na ndani ya serikali?

Jibu ni kuwa uongozi unatoka kwa Mungu na kila mtu huinuliwa Na Mungu kwa makusudi maalumu na kwa wakati wake na Mungu akikupitisha katika ulimwengu wa kiroho hakuna mwanadamu yeyote wa cheo chochote awezaye kukuzuia ,kila mtu huja kwa sababu ya kutimiza kusudi fulani alilolipanga mwenyezi Mungu kulingana na makusudi yake katika ulimwengu wa kiroho. Watu hawa wakati mwingine wanaweza pata vikwazo mbalimbali au kukataliwa na wenye kupitisha au kuamua .

lakini kwa kuwa Mungu huwa ameamua juu ya watu hao, basi huishia kushinda kwa kuwekewa watu ambao watazungumza na sauti zao zikasikika au kwa kupitia vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo huweka kauli zao juu ya nani ambaye wangependa kufanya naye kazi kwa wakati huo na kwasababu zipi na kwa Taarifa zipi za kiusalama juu ya mhusika.

watu hao siyo wale ambao huwa wanatajwa tajwa hadharani,huja tu kama mshangao kwa wengi au kwa lazima au kwa kuhitajika na watu walio wengi kutegemeana namna Mungu alivyoamua kuwapitisha na kuwafikisha mbele za watu,wengine anaweza waleta kwa kukubalika kwao kuanzia mwanzo hadi mwisho kiutendaji, kiuchapa kazi pamoja na misimamo yao katika historia zao au safari zao za kiutumishi .na wengine akawaleta mwishoni na kuwainua ghafla na kuwapa kibali mkononi mwao.

Ukiona mtu amekuwa mkuu wa nchi yaani Rais na Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa Taifa letu ,basi ujue kuna vita iliyopiganwa na Mwenyezi Mungu katika kumuinua mhusika.kuna kinga ya kiroho aliyopewa mhusika kuwashinda wengine .

Ndio maana asiyejuwa haya mambo anaweza kuhangaika kutafuta na kuiba mahela serikalini ili kuja kununua wapiga kula lakini akaishia kuanguka kwa laana ya kuwaibia watanzania wanyonge fedha ambazo zingenunua dawa mahospitalini au vifaa tiba na kuokoa vifo vya baadhi ya watu waliotangulia mbele za haki kwa kukosa madawa au vifaa tiba ambavyo wakati huo havifanyi kazi kwa sababu fedha za kutengenezea hazipo, na huku mwingine amejirundikia kwa ufisadi ili aje awanunue wajumbe.

Tuendelee kumuomba Mungu wetu aendelee kumbaliki na kumlinda Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan ili aendelee kututumikia watanzania kwa moyo wa upendo na huruma. Aendelee kumtia nguvu na kumpatia njia na maarifa ya kuliongoza Taifa, maana pekee yake kwa akili za kibinadamu hawezi pasipo msaada wake Mungu, Aendelee kumpa ujasiri wa kuyakabili yote yajayo mbele yake pasipo kuyumba wala kuyumbishwa, maana Mamilioni ya Watanzania wengi Tupo nyuma yake na upande wake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
UMEMSAHAU ROSTAMU
 
Mkuu hivi hujagundua watu hatusomi huu ujinga unaoandika unatujazia seva tu
 
Mkuu jicheki kwanza kama hujaingia oeriod maana naona kama unachoandika hukielewi
 
Mleta uzi ana jaziba hana uvumilivu katika hoja na hajui theory of elasticity of demand, mambo sasa hivi ni magumu sana kuliko wakati wowote wa uongozi wa Taifa letu, Samia hana shida kabisa lakini wanaomzunguka hawamshauri vizuri kiasi ambacho Watanzania walio wengi hawaoni nuru ya tuendako tukiwa pamoja naye.
kwa hekima yake natamani Mungu amfunulie kukiachia kiti kwa salama 2025 akiwa bado hajapoteza mvuto. anaweza kuendelea kuwania lakini atapata ugumu sana kipindi cha pili kwa maana bunge litakuwa na nyuso mpya nyingi zisizo muunga mkono ndani ya chama na upande wa upinzani pia.
kuna mabadiliko makubwa sana tutakayoanza kuyashuhudia ktk uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.
 
Back
Top Bottom