Mungu Ndiye Anayejua Atakayempokea Urais Rais Samia 2030

Utakuwa umekosea ni wa kumpokea 2025, watanzania wamepanga kuachana na haya mauzauza ifikapo 2025.
 
Mkuu Lucas mwashambwa kwanza niendelee kukupongeza kwa kipaji cha kuandika, ila leo pia ndio nimejua pia una upako wa kuhubiri.

Ni kweli naunga mkono hoja, viongozi wote ni chaguo la Mungu, hata JPM ni chaguo la Mungu ni Mungu alimleta, ni Mungu alimtwaa na kutuletea Samia Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
Ni kweli
Nawaambieni Watanzania ya kuwa Mungu wetu ambaye amekuwa akilipigania Taifa letu Tayari ameshamuandaa Rais wetu ajaye baada ya Mama Samia kumaliza muda wake 2030,
Jee una uhakika ni Samia ndie ameandaliwa na Mungu kwa 2025?. Mimi nilitoa wito huu Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! na baadae nikaisikia sauti hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Nashauri tusibiri ya
2025 itimie ndipo tumzungumzie wa 2030!.
Naunga mkono hoja
Naunga mkono hoja
Vipi wakati wa Hayati Dr Magufuli? Nani alitegemea kuwa ndiye angepewa ridhaa yakupeperusha Bendera ya chama mbele ya akina marehemu Benard Camilliusi Membe Au Mh Edward Lowassa aliyejiandaa kwa vita ya kuutaka Urais Tangia miaka ya Tisini?
Naunga mkono hoja, hii ya kuinuliwa kwa JPM, mimi nilikutangaza humu mwaka mmoja kabla Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli by that time hata JPM mwenyewe alikuwa hajui!.
Naunga mkono hoja
Naunga mkono hoja
Naunga mkono hoja
Ukiona mtu amekuwa Mkuu wa Nchi yaani Rais na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama kwa Taifa letu ,basi ujue kuna vita iliyopiganwa na Mwenyezi Mungu katika kumuinua mhusika.kuna kinga ya kiroho aliyopewa mhusika kuwashinda wengine .
Naunga mkono hoja
Ndio maana asiyejuwa haya mambo anaweza kuhangaika kutafuta na kuiba mahela serikalini ili kuja kununua wapiga kula lakini akaishia kuanguka kwa laana
Hili la laana ni kweli, na sio tuu laana ya kuiba fedha na kununua kura, hata kushinda uchaguzi kwa hila, kuwafanyia wapinzani figisu, mhusika unapata laana!, hili nililizungumza humu Elections 2015 - Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali Yetu ni Serikali Dhalimu?, Haramu?. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!
Naunga mkono hoja
Aendelee kumpa ujasiri wa kuyakabili yote yajayo mbele yake pasipo kuyumba wala kuyumbishwa, maana Mamilioni ya Watanzania wengi Tupo nyuma yake na upande wake.
Naunga mkono hoja, na katika kuyakubali yote pia ampe ujasiri wa kujiandaa kisaikojia endapo atashauriwa vinginevyo kuhusu 2025
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda Nchi yangu.

0742-676627.
Naunga mkono hoja
P
 
Umeenda mbali sana. Kuna 2025. Kama Mungu ndiye anayejua ni nani tampokea Samia 2030, je wewe unajua ni nani atakayempokea samia 2025?
Mazeri sijui kama atafikai 2025
 
Utakuwa umekosea ni wa kumpokea 2025, watanzania wamepanga kuachana na haya mauzauza ifikapo 2025.
Njoo mitaani uwaambie hivyo watanzania uone namna watakavyokufurusha kwa hasira kali.maana watanzania wanamkubali sana Rais Samia na ndio maana wameamua kumpa tena muhula wa pili ili awaongoze Tena.
 
Mazeri sijui kama atafikai 2025
Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ambaye amekuwa akimpigania ,kumlinda na kumtetea ataendelea kusimama naye na kuendelea kumpatia uzima na afya njema ya kuendelea kututumikia watanzania. Watanzania kwa mamilioni wameamua kwenda na Rais samia uchaguzi ujao ili atuongoze mpaka 2030
 
MIE NADHANI WEWE ULIFAA SANA UMPOKEE
 
Nashukuru sana Mkuu na Nimepokea na Kujitahidi kufanya hayo Marekebisho japo naweza nikawa Sijafanikiwa kuyamaliza.
 

Magufuli watu kama wewe aliwaita vichaa ambao mnaweza kukubali nchi kuuzwa,Masai wakifukuzwa kama mbwa kwenye nchi Yao,misitu inauzwa na Bado wewe ukasema Hadi 2030. Wewe ni chizi,kichaa,tapeli,mpumbavu na juha wa kiwango cha juu Sana. Mungu chukua hili lishetani na lipumbavu haraka
 
Siyo 2030 ni 2035.

Awamu hii siyo ya mama Samia, hii ni ya mwendazake.
Kama ni ya mwendazake mbona mnaiita awamu ya sita badala ya awamu ya tano?

Acheni kuwa vigeugeu kwa maslahi binafsi!
 
Sawa Nashukuru na naheshimu mawazo yako juu yangu.Lakini mimi siwezi kukushambulia kwa lugha kama ulizotumia wewe ,maana naheshimu utu wa Mtu na ubinadamu na huwa siwezi kumdhalilisha mtu pale tunapotofautiana mitizamo. Lakini pia napenda kukwambia kuwa Rasilimali zetu zipo katika mikono salama ya Mh Mama Samia Suluhu Hasssan Mzalendo wa Kweli. Mali zote na Rasilimali zote zitaendelea kulindwa kwa nguvu zetu zote na kwa uchungu mkubwa ili siku zinufaishe na vizazi vijavyo
 
Kama 2030 Mungu ndiye anayejua basi ata 2025 Mungu ndiye anayejua pia sio wewe kujipangia.Acha kuweweseka.
 
W
Wakupe tu hata ukuu wa Wilaya maana sio kwa uchawa huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…