Habari zenu
Husika na kichwa cha habari
Sina shaka juu ya muumbaji wa huu ulimwengu na vitu na limwengu zingine zote tunazozijua na tusizozifahamu; kwamba M/Mungu aliyeumba wakristo na waislamu na watu wa dini zingine zote na wasiokuwa na dini pia ni yule yule tu M/Mungu mmoja;
Aliyeumba bahari,mito, aliyeumba binaadamu, majini kwa wanaoamini aliyeumba dunia na sayari zingine zote zinazotambulika na zisizotambulika na viumbe vilivyoko huko pia ..
Na msioamini uwepo wa M/Mungu sitaki kuwakera katika hili najua mtauliza M/Mungu mwenyewe ndio nani? Sitawajibu hilo swali nawajuza mapema..
Nimekaa nimeangalia sana waislam na waikristo naona hawana tofauti yeyote kimaumbile na kitabia pia yaani bila shaka ni wapo sawa tu wazi kuwa tumeumbwa na M/Mungu mmoja.. sasa kinachoshangaza hizi tofauti zetu kuchukiana, kugombana kupelekea mpaka kuuana na mambo mengine ya hovyo kufanyiana.. kama tumeumbwa na M/Mungu tofauti ...haipendezi..
Na bora nchi yetu chuki juu ya imani/dini tofauti haipo sana haijashika kasi sana mataifa mengine ni hatari zaidi walimu wadini wanapaswa kutoa elimu nzuri kwa waumini wao na kutohubiri au kutotoa mawaidha ya chuki kwa waumini wao..
Asante