"Kumbukumbu la Torati 30:19"
Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
Tafsiri!
Ndani ya Mungu wa Biblia hakuna kitu kinaitwa mauti (kuua/kifo). Ndani ya Mungu kuna uzima.
Mungu alitoa neno lake katika Biblia ambalo kwalo binadamu anachagua aende upande hupi na aache upande hupi. Kila uchaguzi binadamu anaouchagua unaendana na matokeo! Anayetekeleza matokeo ya neno la Mungu kutegemea na maamuzi ya binadamu ni (wa kwanza) ni shetani katika kuhakikisha adhabu inatolewa. Wa pili anayehakikisha neno linatekelezwa ni binadamu.
Kwahiyo mauaji yoyoye yaliyowahi kutokea na yanayotokea, na yatakayotokea ni kwa mujibu wa neno la Mungu na anayehakikisha haki inatendeka kwa anayetii neno na yule anayehasi neno ni shetani na binadamu. Ndani ya Mungu hakuna mauti, dhiki, magonjwa, hofu, wasiwasi, mashaka, njaa, n.k.