Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Aisee yukoje Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo?
Mimi kumuamini inatosha sitaki kumuona Kwa macho yangu, nitamkimbia.
Sio lazima kumuona ila kama inawezekana share tufahamu zaidi.
Je ana rangi kwenye ngozi yake?
Maana aisee Kuna mafunuo sikuhizi eti Yesu ni black man , mi huwa nashangaa tu.
 
Walokole waanatumia biblia moja...ila katika mapokeo yao ya neno yamewekwa ndani ya mioyo yao na wanayaishi

Labda nikupe mfano hapo kwa Lutheran...

Mimi ni mlutheran hadi kipaimara nimesoma ila sasa nimeokoka ni mlokole...ishu sio dhehebu...

Siwezi kuzungumzia suala la hao Manabii na mafuta wanayotumia maana ni wapakwa mafuta ya Bwana...

Ila ninaouwezo wa kupima Roho zao nikajua huyu ni wa Bwana na huyu sio...
 
Kimsingi, yeye anajifunua kulingana na nini anataka kukufundisha/kusema nawe. Binafsi nakiri leo nikiwa na akili timamu kuwa nimemuona si chini ya mara 4 toka nikiwa mdogo na anajifunua kwa namna tofauti tofauti. Katika mara zote sijawahi iona sura tokana na mwanga mkali uliopo usoni mwake so sio "mzungu wala black " huwezi muangalia/uona uso wake lakini nywele za kichwa chake ni nyeupe na zinang'ara kama theluji ila zimelala kama za mzungu.(Ufunuo 1:14, Daniel 7:10)
Nimemwona kama Nuru kali(Matendo 9:3) nimemwona kama hiyo mzee wa siku, nimemwona kama mtu mrefu na mkubwa yaani Mbingu ni kiti chake na duniani ni sehemu ya kuweka miguu yake(Isaya 66:1) nimemuona akija na mawingu akiwa na malaika wengi, nimemuona akiwa amepanda farasi mweupe(Ufunuo 19:11-14)

Kuhusu Yesu kuwamweusi wakati akiwa jinsi ya mwili au lah, Nakumbuka mwaka 2016 au 17 huku JF kulikuwa na mada kuhusu Yesu kuwa black. Nami niliiamini ile na ilinikaa moyoni. Nikamuuliza, bwana kwa jinsi ya mwili ulikuwa mweupe au mweusi? Akaniambia kuwa mweupe au mweusi haitakusaidia kitu ila kuna siku nikalala nikaona "Mkutano mkubwa wa watu wamekusanyika na Kijana mmoja mweupe/mwekundu na mwenye nywele nyeusi fupi zilizonyolewa na kuwa chini chini/ndogo zisizolala kama za wazungu ila zimesimama kama za Waafrika akiwa amesimama katikati ya kusanyiko hilo akiwa kwenye mimbari/jukwaa akihutubia. Akashuka toka kule jukwaani na kuja karibu nami na kuniita jina langu na akaniuliza, wewe una kanisa gani? Kabla ya kumjibu akaondoka ila wakati akiwa kule jukwaani/mimbari nilijua bila kuambiwa kuwa huu ndio muonekano wake alipokuwa duniani kwa jinsi ya mwili." Kwani katika ulimwengunwa Rohonkila kitu ni wazi na unaoata majibu ya moja kwa moja kwa yale uyawazayo. Kimsingi, hakuwa mnene wala mwembamba, hakuwa mrefu sana wala mfupi ni wa kati kati. Alivaa kanzu nyeupe na kujifunika kikoi/shuka cha khakhi huku amevaa sendors miguuni kwake.
 
Umeelezea vyema
 
Umeeleza vyema
 
Anhaa so Yesu rangi Iko ka ya wale Middle East hivi?
 
Ni kweli ila ukiwawekea kwenye kitabu utawasaidia walioko nje ya hapa jf maana huu ni moja ya utafiti bora Duniani ambao utafungua akili za wanadamu

Kitabu kitauzika sana hiki
Habari za mmliki wa wamiliki na mkuu wa wakuu na mungu wa walokole haziuziki kama unavyofikiria.Lakini upo sawa ndugu yangu sababu imefikiri kama ambavyo mti mwingine yoyote angefikiri.
 
Mi nadhani aliyefanya walokole kuwa wengi ni YESU tu! Yesu peke yake!! Mwana wa Mmiliki peke yake! Yeye tu! Hakuna cha kanisa hata moja lililomfia mtu hapa duniani!

Watu wanaokolewa kwa neno la uzima! Yesu ndiye huyo neno! Hakuna cha mchungaji, nabii, mwinjiristi, mtume, mwalimu wala nani NI YESU TU! SIFA NA UTUKUFU KWA MWANAKONDOO!

Katika hili, ulokole siyo dhehebu!
 
Sijajua wapoje ila naweza sema ni kama red indian hivi. Sizijui sana hizi races mkuu ila alikuwa mweupe but sio mzungu pure kama wazungu wa sasa pia nywele hazikuwa za wazungu i.e zimelala ila zilikuwa zimesimama na fupi.
Kuhusu rangi ya ngozi yake naona inaendana na Maandiko , maana iliandikwa lazima Kristo atoke kwenye ukoo wa Daudi na rangi ya Daudi ilikuwa nyekundu

1 Samweli 16:12-13
[12]Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema, Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
And he sent, and brought him in. Now he was ruddy, and withal of a beautiful countenance, and goodly to look to. And the LORD said, Arise, anoint him: for this is he.
[13]Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya BWANA ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.
Then Samuel took the horn of oil, and anointed him in the midst of his brethren: and the Spirit of the LORD came upon David from that day forward. So Samuel rose up, and went to Ramah.
 
Sijajua wapoje ila naweza sema ni kama red indian hivi. Sizijui sana hizi races mkuu ila alikuwa mweupe but sio mzungu pure kama wazungu wa sasa pia nywele hazikuwa za wazungu i.e zimelala ila zilikuwa zimesimama na fupi.
Watu wa Middle East ni waarabu mkuu ndo nilimaanisha, achana na Wayahudi wa Sasa walioko Israeli mi nawaona kama wazungu vile.
 
Mkuu uzi huu umenipa hamasa Sana ya kusoma neno, wakati nafuatilia Habari za muonekano wa Malaika aka watu wa refu wanaoakisi mwanga Nika kutana na neno hili ambalo kiasi kikubwa linathibitisha usemayo, waebrania 1:7..na kwa Habari ya Malaika kasema, a fanya Malaika wake kuwa pepo na watumishi wake kuwa miali ya moto.. Pia Waebrania 1:13-14,je hao wote si roho watumikao, wa kitumwa kuwa huduma wale watakaourithi wokovu?
Kama unaesoma hujaokoka nakusihi kimbilia Neema hii ya wokovu Kuishi kama mwana wa mfalme... Tunapendwa sie.. Tunalidwa balaa... YESU nakushukuru kunifungua Macho ya Rohoni nikaona thamani ya Wokuvu Mkuu namna hii🙏🙏
 
Nilikuwa natafuta hii comment ili nikujibu.
Ni hivi hakuna Mungu katili wa namna huyo. Leo aniumbe Kinengenengu na kunileta duniani ili aniangamize. Biblia inasema kuhusu shetani na chanzo cha dhambi ni uasi wake mwenyewe.
Ezekieli 28:13-19 In summary inasema "Mungu alimuumba Lucifer akiwa mkamilifu na mwenye kupendeza. Alimuumba maalumu kwa ajili ya sifa ila tokana na uzuri wake, kiburi kikainuka ndani yake iliyopelekea kumuasi Mungu na hivyo kuhukumiwa.
Pia Isaya 14:12-15 utaona inasema "Namna kiburi, kutamani utukufu wa Mungu na kutaka kufanana au kuwa zaidi ya Mungu ndio chanzo cha kuanguka kwa Ibilisi"
Kwa hiyo mkuu, Mungu hakuwa na mpango wa kumuumba ibilisi na mapepo(Malaika waasi) ili kuwaangamiza ila kiburi na majivuno ya shetani ndio chanzo cha hayo yote.

Kuhusu mwanadamu, Mungu hawezi kuumba mwanadamu tena kiumbe dhaifu na kukiangamiza. Biblia inasema wazi, Mungu alimuumba mwanadamu ili awe mtawala katika hii dunia. Akampa dunia ikiwa kamili apate kuishi na kutawala humo. Mungu aliumba kiumbe kinachofanana naye na kukipa mamlaka, kumuabudu, kishirikiane naye, kimuheshimu naye amuheshimu, kuwe kitoto chake naye awe Baba yake. Mungu kamwe hakumuumba mwanadamu ili amuhukumu na kumuangamiza. Huyo atakuwa Mungu wa hovyo na katili sana.

Adam alikaa bustanini katika mazingira mazuri ila alishindwa kutii. Anguko lake ndio lilileta dhambi na hukumu ya mauti. Ila tokana na upendo wake, Mungu mwenyewe akavaa mwili ili aje mkomboa Mwana wa Adam. Kwa hiyo, Mungu anatuwazi mema ila dhambi zetu ndio zimetutenga na uso wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…