Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Unataka kujua na kusaidika, au unaweka msimamo wako. Kama lengo lako ni kujua, unaweza kuelezwa hatua kwa hatua kimaandiko juu ya hoja zako zote. Kama ni kuweka msimamo, itakuwa vigumu hata kama malaika ashuke akueleze.
 
kazi ya Mungu lazima isonge mbele kwa gharama yoyote.
Unakubaliana nami kuwa Hata kama hakuna wakuchangia, Mungu anaweza kuamuru uuze mawe ukapata pesa za kuendeleza huduma. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mwamposa.
 
kazi ya Mungu lazima isonge mbele kwa gharama yoyote.
Unakubaliana nami kuwa Hata kama hakuna wakuchangia, Mungu anaweza kuamuru uuze mawe ukapata pesa za kuendeleza huduma. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Mwamposa.
Kwamba Mungu amemuagiza Mwamposa auze maji na mafuta Kwa ajili ya uponyaji Ili KAZI yake iendelee?

Au nimekuelewa vibaya!!!
 
Kwamba Mungu amemuagiza Mwamposa auze maji na mafuta?
Utajuaje hilo? Mungu akikupa majukumu ya kuenza Injili lazima akupe vyanzo vya pesa. Ukiona mtu anaeneza Injili ilio hai, mwache usije ukajitwisha hukumu. Labda iwe injili ya kupeleka wstu iwe shetani
 
Utajuaje hilo? Mungu akikupa majukumu ya kuenza Injili lazima akupe vyanzo vya pesa. Ukiona mtu anaeneza Injili ilio hai, mwache usije ukajitwisha hukumu. Labda iwe injili ya kupeleka wstu iwe shetani
Kwahiyo vyanzo vya pesa ni kuuza uponyaji kupitia mafuta chumvi na maji?

Unalo andiko?

Hivi unajua kuwa hata wachawi Wana mungu wao anaitwa Ibilisi na shetani?
 
Kwahiyo vyanzo vya pesa ni kuuza uponyaji kupitia mafuta chumvi na maji?

Unalo andiko?

Hivi unajua kuwa hata wachawi Wana mungu wao anaitwa Ibilisi na shetano
Mwamposa anakuambia hauwezi kununua uponyaji wa Mungu. Gharama yake hakuna mtu ataweza. sasa sijui hiyo kauli ya kuuza uponyaji umeitoa wapi?
Kama Mwamposa mungu wake ni shetani basi atawapeleka wafuasi wake huko, ila mimi bado sijaliona hilo, labda utufafanulie.
 

Nafikiri Mleta uzi yuko sahihi Mkuu. Kumbuka Mungu Hana ugomvi na Shatani, kwa sababu Shetani alishahukumiwa kitambo na anasubiri tu ukamilifu wa hukumu yake. Ila utofauti unakuja pale ambapo Mungu na Shetani wote wanapoihitaji nafsi ya Mwanadamu kuimiliki hapo sasa ndipo tofauti yao inajitokeza. Kumbuka kwenye kitabu cha Ayubu, Mungu na Shatani wanaongea juu ya Ayubu. Je wangekua na ugomvi wangeongea? Hapana wasingeongea. Ila unaona Mungu anasema Ayubu ni Mtumishi wake muaminifu na Shetani anasema Hapana ni muaminifu kwa sababu umempa mali!. Nini kinatafutwa Nafsi ya Ayubu. Mwisho Mungu anamwambia fanya yooote ila tu usimuue Mtumishi wangu Ayubu.

Na Kumbuka mleta uzi anasema kabisa kibali Kimeombwa ila tu hicho kibali kisiwe na madhara kwa wana wa Mungu. Ulimwengu wa Roho unawasiliana vizuri sana sana tu. Maana kama Mwanadamu huna Mungu una Shetani na kama huna Shetani una Mungu. Na Mungu Ametupa nafasi ya kuchagua ama lah tumtumainie yeye au shetani. Hivyo mawasiliano yapo ingawa Shetani anajua hukumu yake Iko palepale hivyo anatafuta wafuasi tu wa kwenda nao.

Kwa Hivyo Mungu Hana shida tena na Shetani ila ina shida na Nafsi yako na hivyo hivyo kwa Shetani anajua ukuu wa Mungu na yeye anashida na Nafsi ya Mwanadamu. Ila Mungu na Shetani hawana Ugomvi. Najua ni ngumu kuelewa ila ni hivyo
 
HUNA HOJA SI HAPA Wewe Umetaja hiyo miungu sasa Uongo Upi Tena MKUU HAUPO SAWA MPOKEE YESU

MAANA MASUALA YA ROHONI WEWE NI MTUPU unamjua huyo zyeusi wako

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
Twende taratibu bro, nini hasa logic yako au unataka uthibitisho wa namna gani kuhusu uwepo wa Mungu? Naomba uniambie, nitakujibu.
No
Mpaka sasa japan aliyetihibitsha zaidi ya kunielezea stori ushaamua kua kondoo sikulazimishi
 
Unajua kifo cha taji wewe? watakatifu wengi wameuwawa kwa njia hiyo
Wengine walikatwa na misumeno, wengine walikaangwa kwenye mafuta na wangine walipigwa mawe
 
 
Mzeebaba sijasoma yote ila uchawi au ushirikina haupo ni story za kusadikika zinazoshamiri sana kwenye jamii za watu wajinga na maskini ndo maana ni rahisi mtu wa Chitipa kuamini karogwa kuliko mtu wa Masaki achilia mbali Ulaya na bongo.
hayajakukuta mzee baba shukuru kwa hilo.
 
hayajakukuta mzee baba shukuru kwa hilo.

Hamna mtu yamewahi kumkuta zaidi ya kulishana matango pori tu na kuamini without questioning. Story zote ushirikina ni hearsay na unapaswa kuamini tu kama nyumbu bila kutumia akili.
 
NINAENDELEA............
Mnajua kwanini baadhi ya watu mnabishana?????
Ni kwa sababu kuna upinzani wa kiroho kati yenu.Na sio rahisi kuelezea mambo ya kiroho bila kupata upinzani.LAKINI LAITI MNGEFUNGULIWA MACHO YENU YA KIROHO MNGEELEWA NACHOELEZEA KUHUSU MUNGU WA WALOKOLE....NINAOMBA TU MNIVUMILIE MAANA HATA KUANDIKA TU HUMU KUNA UPINZANI WA KIROHO NA KIMWILI NDIO MAANA NAENDA TARARIBU.Na tunaweza kuandika na kusoma haya sababu kuna mahali walokole wanatuombea ili tupate neema ya Mwana wa mmliki.
Sio lazima kwa watu kuamini na kama hawaamini basi wawaulize wanajimu au waganga kuhusu Mungu wa walokole.
Kubalini au mkatae ila mungu wa walokole hana upinzani.Hakuna miungu inayoweza kutembea na farasi wa moto,magari ya deraya ya moto na kuwalinda wafuasi wake kwa pumzi za moto.
Unaweza ukabisha ila kama unabisha basi jaribu kuwadhuru walokole kiroho afu utaona nguvu za mungu wao.
Kila kitu cha mlokole kinalindwa na wale watu warefu wenye haki,kuanzia familia na mali na roho zao pia.
Unaweza kuona nyumba ya kawaida tu ya mlokole inalindwa na wale watu warefu wenye haki zaidi ya mia.Wanajimu wanajua chimbuko la kila dini ila hawaelewi kwanini chimbuko la dini ya walokole ni fumbo wasiloweza kulifumbua sababu kwenye chimbuko la dini ya walokole kuna alama mnaita""Msalaba""kiroho hiyo ni nembo ya chimbuko la imani ya walokole.
Unaweza kumuona mlokole anahubiri barabarani ukachukulia kawaida ila kiroho kuna watu wamemzunguka wanamsikiliza hata kama binadamu hawataki kumsikiliza au wanampuuzia au wanamsikiliza kwa uchache.Namaanisha walokole wakiwa wanahubiri mitaani wanasikilizwa na binadamu wachache ila watu warefu wenye haki pia wanawasikiliza mahubiri yao.
Kitabu cha kusalia cha walokole,kiroho ni kitabu chenye siri zoote,kina mafumbo ambayo kinajimu hayafumbuliki.Mfano mmoja ni asili ya Alfa na Omega na mfano mwingine ni ile wa mtu mmoja mwebrania wa kale anaitwa""Musa""alienda wapi baada ya kupanda mlimani na kuongea na """Nguvu ya ukuu""" je alifariki au alipotea maana hakurudi chini mlimani kuungana tena na watu wake na mwili wake haukuonekana kwa wanajimu waliokua wanaifuatilia ile safari ya waebrania katika ulimwengu wa nyota.Na pia yule mwebrania mjuzi wa elimu kuu wanamwita ""Eliya""kama alikua binadamu au roho ya kiungu.Hayo ni baadhi ya mafumbo yanawasumbua wanajimu kutoka katika kitabu wanachotumia walokole.
Mimi sio mtafiti wa kwanza kuchunguza mambo ya kiroho,wapo watu wengi tu wanaamua kuchunguza mambo ya kiroho.Wengine wanaamua kuchunguza uchawi na wengine wanaamua kuchunguza unajimu au uganga na wengine kama mimi tukaamua kuchunguza ulokole baada ya kuvutiwa nao.
Miungu wapo wengi kwenye huu ulimwengu wa kimwili kimapokeo kama alivyo mungu wa walokole.Lakini tofauti ya mungu wa walokole na miungu mingine ni uwezo wake na makazi yake katika mwanga wa nje ya mfumo huu wa sayari za ulimwengu na ni ishara tosha kua anatamalaki mfumo woote wa anga nje ya anga la mfumo wa sayari.Pia mfumo wake wa kujibu maombi au sala za walokole kwa njia ya radi na moto ni sayansi tata ya kiroho inayoonyesha ukuu wake kuliko miungu mingine.
WANAJIMU NA WAGANGA WANAWAOGOPA WALOKOLE SABABU HIYO TU MUNGU WAO ANAJIBU MAOMBI YAO KWA MFUMO WA MOTO NA RADI.Dunia hii lazima binadamu uchague upande kiroho na kila imani ya mwanadamu ina upande wake.Sijui kuhusu imani zingine sikuzifanyia utafiti ila kwa upande wa walokole,imani yao ipo upande wa yule anaeitwa Mwana wa mmliki ambae ni mlinzi wa walokole.
NITAENDELEA..........!!!!!
Wachawi waga wanakaa vikao vya jinsi ya kupunguza idadi ya walokole duniani sababu hao walokole ndio mabingwa wa kuwaharibia kazi zao kiroho.Ndio maana katika ulimwengu wa kawaida wanapigwa vita sana,ila angalia hao watu wanaowapiga vita sana hao walokole utakuta asilia yao ni wanajimu au waganga (WACHAWI).
Mzee matata alisema kua washirika wa majini au vibwengo hawana usharika na walokole na ni maadui na ukiona imani yoyote ile ya kinajimu au kiganga ina usharika na majini basi ujue ina uadui na walokole.
 
Yaani nimeamka cha kwanza Hapa, nione kama umeendelea.... 😁 😁 Mungu akulinde zaidi mwamba... Unazidi kuthibitisha uweza wa Yesu Kristo, aka Mwana wa Mmiliki... Na sisitiza kama una fuatilia uzi huu na hujaokoka, omba Mungu akupe Neema ya kuokoka, ujue uweza huu mkubwa Wa Mungu baba kwako... Maana siri hii imefuchwa kwa wenye hekima ya dunia hii, na kufunuliwa kwa watoto wadogo.. Yaani wanyeyekevu wa moyo wasiotukuza elimu au utajiri wao zaidi ya Mungu... Maana mambo ya Mungu haya make sense kisayansi... Ukitaka logic utakesha na usiambulie kitu... Mitihani wako ni Imani tu... πŸ™
 
Amen. Mungu anatutumia sisi wanadamu kuudhihirisha ukuu wake kwa namna mbalimbali.
 
Kuna kitu nimegundua katika tafakari.
Sii rahisi kumkuta mchawi, mnajimu au mganga akimkufuru mwana wa mmiliki. Wao kazi yao kubwa ni kuwashawishi wanadamu wa kawaida au wakidini wamkufuru ili iwe fursa(mlango) kwao kuwaadabisha kwa dhiki, adha na magonjwa na hatinae kifo cha mauti.
Watu wote wanakufa ila kuna tofauti kati yake. Kuna wanaolala mauti na kuna wanaokufa kifo cha mauti.
Kama ilivyo katika mwili mtu akifa anazikwa katika kaburi lile shimo la udongo tunalochimba physically lakini aliyekufa kifo cha mauti huyu ni ile mauti ya pili. Hii ni lile kaburi la kiroho ambalo linaitwa lisilo na ukomo au ziwa la moto.
Wakuu wa kidini waliwahi mtukana mwana wa mmiliki kuwa yeye ni "belzebuli" alipokuwa katika ule mwili wa udongo. Kauli ile ya kukufuru ilipelekea yule mwana wa mmiliki kuwaambia kuwa kufuru yao kwake katika mwili ule wa udongo ina msamaha wakitubu lakini atakapokuwa ameondoka katika ile flesh na kurudi kwa walikole(kanisa) kwa ule wa roho, kumkufuru hautasamehewa kamwe katika ulimwengu huu wala ule ujao.
Kwa hiyo wachawi, wanajimu na waganga wao ni pepo wanaoweza kuunganishwa katika ulimwengu wa roho ya uchawi na wana uelewa kwa matukio(experience) ya kuzifahamu nguvu zisizomilikika za mwana wa mmiliki zilivyo kuu mara matrilion kuwashinda. Hivyo wanachofanya wao ni kugeuka pepo kwa kuwapagaa wapagani na watu wa kidini wakufuru kwa kuzikana nguvu za roho wa mungu au kuzidhihaki ili wapotee mazina katika ulimwengu huu na ule ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…