Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

INAENDELEA........
Basi udadisi wangu ulianzia kwa dadangu wa kuzaliwa tumbo moja,ilikua kila jioni wakati nipo mdogo miaka ya shule ya msingi,kila ikifika jioni mamangu ambae alikua mlokole alikua anawaita wamama majirani zake kusali jioni baada ya kula na wanasalia uani kwenye nyumba.Wakiwa wanasali na sisi kama watoto tunaenda kukaa chini pale tunasali nao ila sio serious,basi dadangu ananiambia angalia ukutani kuna "Malaika"wamekuja.Mimi natoa macho sioni na kumbe kuna baadhi ya wale walokole wanawaona pia ila hawasemi.Dada baadae anaenda kumsimulia mamangu na mamangu anaenda kuwasimulia waumini wenzake kua mwanangu jana kaona malaika.Basi wale wamama wakiongozwa na mama mmoja hivi anaitwa "Mama Samueli"ndio kama wamemwagiwa maji ya moto maana kesho wakija ni maombi pale uani masaa saba au sita kila jioni na kila siku nachungulia nitawaona hao malaika au sitowaona,nikaambulia patupu ila dadangu siku moja moja anawaona na kunielezea.Ndipo udadisi wangu ukaanzia hapo kutaka kujua viumbe hawa wa kiroho na jinsi walivyo na utararibu wao wa maisha na wanakaa wapi na madhumuni yao kushuka duniani kuja kukaa na walokole wanapokua wanasali.
Miaka ikaenda na nikasahau hayo mambo ila kuna vitu vikawa.Kuna siku nilikua msibani nikajiuliza sana kwanini binadamu wanakufa na wakifa wanaenda wapi,nikaanza upya udadisi wangu kuhusu ulimwengu usioonekana.Kuna wakati nilisafiri mkoani kigoma nikakutana na mzee mmoja nikamuelezea kuhusu udadisi wangu wa haya mambo ya ulimwengu usionekana.
Mosi:Akaniambia nje ya ulimwengu huu wa kawaida kuna ulimwengu mwengine na kuna jamii mbili ambazo ni jamii za watu wanaofanana na binadamu na wanaakisi mwanga wa jua na makazi yao ni anga za mbali nje kabisa na mfumo kani wa ulimwengu karibia maili trion zisizohesabika kwa hesabu za kibinadamu.Na pia jamii ya watu wanaofanana na binadamu ambao wanakaa katikati ya dunia ila wanazurura kwenye sayari zote za mfumo wa jua ila hawawezi kwenda nje ya mfumo kani wa ulimwengu sababu sio eneo lao la kiutawala.
Pili:Hizo jamii zote zina imani zao na zimeleta imani hizo kwa binadamu na kuwafundisha na nikitaka anaweza kunifundisha pia,lakini ni imani kinzani.
Tatu:Nikitaka kujua haya mambo nichague upande mmoja wa jamii zile mbili niwe mfuasi wake lakini kuna miiko na utaratibu wake wa kuzingatia katika hilo.
Akaniuliza yule mzee ""Wewe unataka kujua nini""nikamjibu kua mimi nataka kujua na kuwaona wale viumbe waliokua wanamtokea dadangu utotoni ikiwezekana niwahoji baadhi ya vitu kuhusu wao.Nakumbuka yule mzee akachekaa akaniita kwa kucheka""Mulashani""nani alikupa jina hilo na mimi nikamjibu ni babu yangu mzaa baba,akacheka akasema unajua maana yake hilo jina.Nikamjibu sijui,akasema maana yake ni mtu mpiganaji na wapiganaji waga wadadisi na wadadisi hupatwa na majanga sababu ya udadisi wao.Lakini akaniambia nitakupa njia rahisi ya wewe kuwaona hao viumbe,ila akauliza ni nani aliyekuelekeza kwangu..Nikamjibu kua wewe mzee............ ni mnajimu na una elimu ya anga nilielekezwa kwako na flani........nikamtajia jina la mtu aliyenielekeza kwake.
Akasema wewe shida yako tu ni kuwaona hao viumbe wanaokwenda kwa walokole kila mara??????Nikamjibu ndio,akaniuliza ukiwaona hautoweza kuzungumza nao sababu haujapitia njia yao kwenye ulimwengu wa ndani,kwanini usiende kwa walokole wakufundishe jinsi ya kuwaona.Nikamjibu kua shida yangu ni kuwaona na kuamini kama wapo hao viumbe.Akaniuliza tena unajua wanaitwaje,nikamjibu kwa kusema wanaitwa"Malaika au makerubi""akaniambia wanaitwa watu wa jamii ya jua na mkuu wao hana upinzani katika ulimwengu zoote saba.Nikaanza udadisi na maswali kwanini wanajihusisha na walokole.
Mzee akanijibu wanajihusisha na walokole sababu walokole wana usharika nao kupitia""Mwana wa mmliki""ambae walokole wanamwita Mungu wao na wanatumia jina lake ila hawezi kulitaja hapo sio mahali pake.Akasema wao hao watu wa jamii zenye kuakisi mwanga wa jua wana makazi yao nje kabisa ya mfumo wa sayari za ulimwengu na wana miaka sawa na mwanga wa mfumo wa sayari za ulimwengu mara trioni.Akimaanisha kua walikuepo miaka trioni kabla ya mfumo wa sayari za ulimwengu kuwepo.
Nikamuuliza vipi kuhuusu ile jamii nyingine ya wale watu alioniambia wanakaa katikati ya dunia kupitia chini ya maji,akanijibu shida yangu ni kuwajua viumbe marafiki wa walokole basi hayo mengine niachane nayo kwanza.Akaniambia tayari washajua nia yangu ya kutaka kuwaona hivyo nikwaona nijue ni kwamba wao wameamua niwaone na nisipowaona nijue ni wao wameamua nisiwaone.
Akaniuliza nia yako ni kuwaona tu hakuna jingine lolote,nikamjibu ndio.Basi akasema atanielekeza nimuone mkuu wao ambae ni nyota ya mashariki wao wanajimu wanamuita hivyo.Akasema ikifika jioni twende karibia na kanisa lolote la kilokole au mkusanyiko wowote wa kilokole hasa wakiwa katika maombi yao.Yeye hawezi kusogea ila mimi naweza kuwasogelea wale walokole na wakianza kusali nifumbe macho pia ni ishara ya heshima kwa mkuu wao(Mungu wao)..Afu nitakachokiona iwe siri yangu ili nisiwashitue wale walokole wanaosali pale
Basi ile wilaya niliyokuwepo kuna makanisa mengi ya walokole hasa pale mjini,nikaona ndio kitovu cha utafiti wangu kuwatafiti walokole kisayansi nijiridhishe dukuduku zangu kuhusu matukio ya utotoni.Basi kufikia jioni tukaenda kwenye kanisa alilonielekeza tukawadadisi walokole tuwapeleleze.Mimi na akili zangu za kisayansi afu mzee wangu mnajimu na akili zake za uganga na utaalamu wa nyota na anga wanaita unajimu.Tulipokua njiani akawa ananiambia wewe kijana mdadisi ila na mimi udadisi wako umenivutia na mimi ngoja nikupeleke afu mimi nakaa mbali maana walokole nawajua na imani zao nazijua na kwa mbali tunasikia miziki ya vyombo inatoa sauti watu wanaimba kwaya maana kanisa halikua mbali sana ni kilimani tu unapandisha,mimi mbele na mzee wangu nyuma tunapandisha kilima.Cha ajabu sasa nipo njiani yule mzee wangu mnajimu tunapiga story mara nahisi ukimya ile kugeuka eeeh kanikimbia kimiujiza nimebaki peke yangu njiani.Nageuka kushoto simuoni nageuka nyuma simuoni,nageuka kulia simuoni.Lakini nilipoangalia mbele tena"""Eeeeh"""Nakutana na mtu mrefu kama wale wachezaji wa mpira wa kikapu ananitazama,na anaakisi mwanga wa jua,amevaa kanzu bwanga na miguu yake haifiki chini ila imefunikwa na ile kanzu.Uso wake ulikua wa kirafiki sababu alikua anatabasamu ila hauonekani vizuri hata nywele sababu ya kuakisi mwanga wa jua na ngozi yake kama rangi za sarafu ya mia mbili au sarafu za shilingi hamsini,kwa haraka haraka ni kama mtu wa shaba ila mrefu kuliko binadamu wa kawaida.Lakini sasa anatembea kuja barabarani nilipo,na sio kwa kutembea kule bali kuelea wimawima hewani.Hayo yote ni ndani ya nusu dakika,na mzee kashakimbia simuoni.Ile nataka nianguke kwa hofu yule mtu akapotea ila sasa mimi nipo nimeganda kama sanamu hofu yoote imetoweka limebaki bumbuwazi natoa macho tu.
Baadae kidogo ndio akili inarudi ila cha ajabu hofu sina naona kawaida tu,yule mzee wangu simuoni sijui alipoteaje bila kunitaarifu.Safari ya kwenda kanisani kwa wale walokole ikaishia hapo nikaanza kurudi chini kilimani kumtafuta mzee wangu na nilipomkosa nikarudi mpaka nyumbani kwake namkuta kakaa ananisubiri huku kanuna ila mimi nikaanza kucheka.Akaniuliza unacheka nini afu yeye akaanza kucheka ila ananicheka mimi""Wewe si mdadisi mbona ulikimbia mjukuu wangu"""nikamwambia sikukimbia ila niliganda kwa hofu na yule kiumbe alitokea na kupotea ndani ya nusu dakika.Akaniambia yule sio kiumbe bali ni wale watu wa jamii ya jua walinzi wa walokole.Akasema mpango wa kuwadadisi wale walokole tutaufanyia tukiwa mbali ila sio karibu na makanisa yao na akanitaka ninuie kua mimi shida yangu ni udadisi tu na sio kitu kingine chochote.Nikanuia pale na akaniapiza na tukapanga tutaendelea na udadisi wetu siku nyingine kwa siku ile nilichokiona kinatosha,ila sasa nikitaks kuendelea na udadisi lazima niwe msiri nisitangaze kwa watu,afu niwe nakariri maombi ya walokole maana waga wanaongea moja kwa moja na mkuu wao ambae anaitwa""Mwana wa mmliki"'ikiwezekana niombe kibali cha kufanya udadisi wangu sababu sina nia mbaya na walokole bali nachofanya ni udadisi wa kujiridhisha utafiti wangu.Cha ajabu japo yule kiumbe alikua ametokea ghafla ila sikua na uoga kabisa moyoni baada ya yeye kutoweka.Akili yangu na hamu ya udadisi kwenye ubongo wangu ikaendelea kuongezeka wakati ule nipo mkoani kigoma kwenye wilaya moja inayopakana na nchi jirani.Mzee wangu akaniambia kila alhamisi ndio siku atakazokua na nafasi kunifundisha kidogo kidogo na kunielezea kwa undani hao walokole ni watu wa aina gani na hiyo alhamisi atanieleza kwanini alinikimbia siku ile pale kilimani wakati tunaenda kuwapeleleza walokole kwenye kanisa lao
ITAENDELEA............!!!!!
 
Maswali mazuri,nitakujibu yote mkuu ucjali
 
Napata shaka kama ulimuona huyo MUNGU wa walokole...

Mbona umetumia Mnajimu? Maana Mnajimu huyo ni Mkuu wa giza...

Kumuona Mungu sio kwa kutumia mtu na nguvu za kibinadamu.

Bali ni kwa kumpokea Bwana kuwa mwokozi wa maisha yako, kuomba, kufunga, kusali...

Na hii ndio maana wapo ambao wanaenda kanisani kila siku ila hawaoni mambo ya Rohoni...

Wanajiita wakristo lakini YESU hawajui...
 
Mungu wa walokole au mkuu wa walokole haonekani mpaka uwe kwenye njia yake kiroho,wanajimu wenyewe hawawezi kufika alipo huko nje ya kani za ulimwengu wa mfumo wa jua,ila kwa utafiti wao wanajimu wanasema yeye ni moto ndani ya roho ya moto na hakuna binadamu aliyemuona akabaki hai au kurudi duniani.Bali ule moto wa viduara unaowazunguka walokole ndio wanajimu wanaita ni pumzi za Mungu wa walokole.Na kuna nyota ya mashariki wanajimu wanamuita ""Mwana wa mmliki"""inaangaza usiku angani,wanajimu wanasema ndie kiungo kati ya walokole na mungu wao,na huyo mwana wa mmliki ndie anaodhi anga lote la mfumo wa jua na nje ya mfumo wa jua.Ndio maana wanamwita Nyota ya mashariki.Ni kiumbe wa kiroho na kiongozi wa wale watu warefu wanaoakisi mwanga wa jua.
 
Uliposema hawawezi kumsogelea ni kweli kwakuwa yeye ni moto na huwa unawaunguza...

Pia hao wakuu wa giza wanamjua YESU/MUNGU kuwa anauwezo mkubwa kuliko wao...
 
usipoteze muda, ukitaka kujua Mungu wa walokole, kawaulize wachawi. wanatujua vizuri sana na nyumba zetu huwa wanaruka hawakanyagi ng'oo. hii ni kwasababu Mungu wetu tunamwabudu katika Roho na kweli, na anakaa mioyoni mwetu, hakati kanisani au kwenye masanamu au eneo fulani kwenye nchi fulani tu.
 
Nimekuelewa Sana!

Barikiwa Sana
 
Hivi mlokole ni mtu gani?
 
Uliposema hawawezi kumsogelea ni kweli kwakuwa yeye ni moto na huwa unawaunguza...

Pia hao wakuu wa giza wanamjua YESU/MUNGU kuwa anauwezo mkubwa kuliko wao...
Wanajimu wanajua uwezo wa miungu wote nje ya ubinadamu lakini mungu wa walokole""Haelezeki"ni roho yenye nguvu na kumsogelea lazima uwe katika njia yake kiroho kama wafuasi wake walokole.Wao walokole wanaita""Utakatifu""
 
Hivi mlokole ni mtu gani?
Kivipi katika ubinadamu wa nje au wa ndani???? Maana walokole wengine kwa ubinadamu wa nje ni masikini wa kutupwa au wanaishi kawaida ila kwa ubinadamu wa ndani wana tunu za moto kama mataji ya kunga'aa hv vichwani mwao na hawasogeleki ukiwa na nia mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…