Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

INAENDELEA:
Basi alhamisi ikafika na kama kawaida mimi na mzee Matata tukaendelea na utafiti wetu.Mzee matata akaniambia kijana wangu unajua siku ile pale kilimani sikukimbia,bali kile kilikua kivuli changu tu.Mimi nilikaa nyumbani na kukuacha wewe uende kwenye utafiti hatua ya kwanza.Ulipotoka tu hapa wale watu warefu walikua pembeni yako wanayasoma mawazo yako na wakaamua kukusindikiza ila wewe ulikua huwaoni mpaka pale mmoja wao alipoamua kujionyesha kwako kwa sekunde chache mbele yako.Na mimi nisingeweza kuja kuongozana na wewe sababu mimi ni mganga na mnajimu,vitu ambavyo kwa wale watu warefu ni makufuru.Na huu unajimu sikuutoa kwao bali nilipata hii elimu kwa wapinzani wao.Sasa mimi pamoja na unajimu wangu kuna vitu siwezi kama kusoma mawazo yote ya binadamu"""Elimu yetu ya unajimu na uganga ina kikomo""sababu kumjua tu binadamu ni elimu pana sana na tumefundishwa tu kiduchu na viumbe wasio binadamu wa kawaida ola hilo sio la muhimu sana wewe kujua,wewe shida yako ni kuwadadisi walokole na wale watu warefu ili kuwajua.Lakini kuwajua wale watu warefu wenye miili ya shaba na wanaoakisi mwanga wa jua ni ngumu zaidi,sababu maarifa yao ni mara trion elfu za maarifa ya unajimu.Historia yao kwa elimu ya kibinadamu ya uganga na unajimu inasema kua hawa watu warefu wanaoakisi mwanga na wenye mabawa kama ya ndege,na wengine hawana mabawa ni jamii moja na wale watu warefu wasioakisi mwanga wa jua ambao hawana mabawa na wanakaa katikati ya dunia kupitia chini ya zuio lolote la maji juu ya dunia,kama bahari au ziwa au mto au maporomoko ya maji.
Walipokua jamii moja miaka trion elfu za nyota kwa hesabu ya kinajimu.Waligombana na sababu kuu ya kugombana haijulikani ila inaonyesha ilikua ni kugombea madaraka na udhibiti wa anga lote la juu nje ya mfumo kani wa ulimwengu wa sayari.Jamii moja ikaja duniani na jamii nyingine ikabaki angani,na kila jamii ina kiongozi wake mkuu.Tokea hapo hizo jamii mbili hazijawahi kupatana na ile jamii ya angani ina nguvu kubwa kuliko ile jamii ya baharini.Jamii ya angani ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani na jamii ya baharini ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani,namaanisha wafuasi ambao ni binadamu.Hakuna binadamu au jamii yoyote ya wale watu warefu wa baharini ambayo inaweza kuvuka mpaka uliowekwa na mkuu wa wale watu wa angani kuelekea kwenye makao yao ya mwanga wa jua.Nchi yao inaitwa"Mwanga wa jua""sababu hakuna usiku huko ni mchana tu,na kwa hesabu za unajimu huwezi kufika huko ila unaweza kukadiria uwepo wake kupitia wale watu wa angani wakiwa wanakuja na kuondoka duniani kuwatembelea walokole unaotaka kuwadadisi.
Mzee matata akaniambia hakuna kitu kizuri duniani kama udadisi wenye manufaa.Nikamuuliza sasa wewe mzee wangu hizi habari zote umezipataje????? Akanijibu kwa kusema na mimi nilikua mdadisi kama wewe ila kwa kupitia uganga na unajimu.Akaniambia kuna vitu hatonieleza sababu mimi sio mnajimu na kuna vitu atanieleza kuhusu udadisi wangu.Hiyo ilikua alhamisi mchana na ilipofika jioni akaniambia nenda kwa jirani zako wale walokole ukae nao na uwaambie wakufundishe kuhusu imani yao na dini yao na jinsi wanavyosali kwa mkuu wao.Wakishakujibu na kukufundisha imani yao basi utakuja hapa alhamisi inayofuatia tuendelee na utafiti wetu taratibu wala hatuna haraka
.Nikaondoka pale nyumbani kwa mzee Matata moja kwa moja mpaka nyumbani,nikapanga jumamosi nitaenda kwa jirani yangu mzee Karugala anifundishe kuhusu dini yake ya kilokole na anijuze zaidi imani yao na utaratibu wao wa maisha na nitamuuliza pia kuhusu wale watu warefu wa angani wanaoakisi mwanga wa jua na kuelea angani kama manyoya ya kuku au ndege.
Kichwani ile picha ya mtu mrefu anayeelea angani kama unyoya haikunitoka na jinsi alivyovaa na uangavu wake na sura yake ya shaba za kumetemeta haikua rahisi kuisahau japo ilikua ni kwa sekunde thelathini tu.Nikajipa moyo nitaendelea na utafiti wangi hata ipite miaka kumi taratibu bila haraka yoyote ile.
Basi jumamosi ikafika nikaenda nyumbani kwa mzee Karugala na nikamkuta,baada ya salaamu nikamueleza yafuatayo.
MIMI:Mzee wangu leo nimekuja kusali nyumbani kwako na unihubirie kidogo
MZEE KARUGALA:Akichekaa"""umekuja mwanangu kunisalimia na kusali pamoja na mimi?????
MIMI:Ndio mzee wangu na ninataka unifundishe kuhusu nguvu ya imani yako ya kuokoka na unifundishe kuhusu Yesu na roho mtakatifu.Na unifundishe kuomba kama nyinyi walokole mnavyoomba.
MZEE KARUGALA:Inabidi baada ya mafundisho nikuongoze sala ya toba kijana wangu.
MIMI:Sawa mzee wangu
MZEE KARUGALA:Simama tuombe kwanza ulinzi wa roho ya Mungu kabla ya yote maana naamini ni roho wa Mungu wangu kakuleta hapa.
Tuliposimama tu ile mzee anaanza kusali tukiwa tumefumba macho,nikahisi uwepo wa wale watu warefu,kuwaona siwaoni ila nahisi wapo pembeni yetu kama wananigusa begani.Mzee karugala akamaliza kuomba huku mimi begani kuna mkono wa moto umenigusa maana nilikua nahisi vidole kabisa ila cha ajabu lile joto haliniunguzi.Mzee Karugala akaanza mahubiri yake huku mimi simuelewi hata neno moja akili yangu yoote ipo kwenye ule mkono ulionigusa begani.Nilikua nimekaa kwenye kiti sebuleni kwa mzee Karugala na pembeni yake alikuja kukaa mkewe na binti zao wawili kuendelea na ile ibada.Mzee ananihubiria ila mimi nachokumbuka ni maneno ya ""Ameen""tu basi.Akili yote ipo kwenye ule mkono ulionishika kirafiki begani.Nikahesabu kimoyomoyo mpaka tatu,afu nikageuka ghafla nimuone yule mtu alienishika mkono.
Si nikakutana uso kwa uso na yule mtu wa siku ile ila safari hii amesimama pembeni yangu kwa nyuma huku akitabasamu kunielekea na sura yake ile ile ya rangi ya shaba,nikajikuta naropoka"""Wewe tena"".Kumbe ile sauti yangu hakuna aliyeisikia wao wanaendelea tu na ibada kiongozi akiwa mzee wa familia Karugala na hawaoni kama nimegeuka bali wanaona nimetulia nawasikiliza""Hayo maelezo walinipa baadae"".
Yule mtu mrefu akaniambia kwa kiswahili ila kwa mtindo wa kuniuliza swali""UNATUPENDA KAMA TUNAVYOKUPENDA??? akacheka na kupotea tena.Yote hayo yalifanyika ndani ya sekunde ishirini hivi pale kwa mzee wangu Karugala.Basi tukaendelea na ibada iliyotuchukua masaa mawili na alipomaliza maombi ya kufunga ibada akaniambia nipige magoti anisalie toba.Ile napiga magoti ule mkono ukanishika tena begani ila safari hii sikufumbua macho nikatulia tuli.Mzee Karugala akasali maneno yake akaniambia nimfuatishe kusema na alipomaliza akaniambia nisimame.Ule mkono ukaacha kunishika bega pia niliposimama.Nikala chakula cha jioni pale kwa Mzee wangu Karugala afu nikaaga kurudi nyumbani na baiskeli yangu.Sikumwambia chochote mzee Karugala wala Babu Matata nikagonja mpaka alhamisi tukiendelea na utafiti wetu ndio nitamwambia tukio lile.
Lakini cha ajabu sikua na uoga bali moyo wa udadisi ndio ukaongezeka na nikaamua mengine nitakua simuambii Mzee Matata bali nitakua nayaweka moyoni ili yanisaidie kwenye utafiti wangu wa viumbe wale warefu wasiokua wa kawaida ila ni marafiki wa walokole.Nikarudi nyumbani kuendelea na maisha mengine nikisubiria Alhamisi inayokuja niendelee na utafiti wangu wa kiudadisi na kisomi kuhusu walokole nikiwa na Mzee Matata mganga bingwa na mnajimu wa nyota na mambo ya Anga.
ITAENDELEA.................
 
Uzi unatakiwa uchanje mbuga kwa michango pia ya wachangiani. Hata hivyo hakuna sababu ya kupoteza nguvu nyingi kujibizana na wale wanaosema hakuna Mungu.
Mfanya research katika huu uzi unajitosheleza kuna jamii mbili katika research yake kama alivyo ainisha. Na nguvu zao zina source mbili tofauti zinazowa- back.
Katika uumbaji kuna hatua nyingi kuweza kufikia dhumuni la ukamilifu wa kile unachitaka kukiumba. Unaogopa kufa kifo cha mwili? Wala haina haja kuogopa hicho kwani madhumuni ya aliyekuumba ni kukuleta katika state ya juu zaidi ya hiyo uliyo nayo.
Umeshaona wale wanaochakata dhahabu au almasi? Inasagwa na kupondwa ikiishapitiswa kwenye moto mkali sana na halafu kisha material nyingine zote zilizokuwa zimegandamana nayo zinateketea kwa moto. Likichukuliwa sasa lile jiwe la thamani lililostahimili tanuru kali ya moto ndiyo linachongwa shape ya anachotaka muumbaji. Likiisha chongwa utaliona likiakisi rangi saba za upinde.
Mungu yeye hakutuhurumia kwa namna ile sisi tunavyoitafsiri huruma bali katika namna yake yeye mwenyewe.
Alimwingiza mwana wake Yesu katika miili hii tuliyo nayo na akapitia katika mateso yale yaliyo kawaida ya kibinadamu bila kutenda dhambi. Na aliposhinda na kufufuka ndio katoka anang'aa kama dhahabu iliyopitishwa kwenye moto wa tanuru na kutoka safi.
Sasa anamiliki juu ya uumbaji wote katika ulimwengu huu wa material na ule wa roho.
Mwanafunzi anapofundishwa na mwalimu kwani mwalimu hajui uwezo wa kila mwanafunzi hata awape mtihani?
Mtihani ni tendo la ku-justify hukumu kwa haki.
Mkuu umedadavua vyema sana
 
Bufa unataka nikuunganishe na mtu aje chumbani kwako usiku saa sita kamili umuulize maswali kuhusu uchawi??? Lakini kuna masharti na viapo utavifanya.Yeye atatokea afrika ya kati ila hapo america itamchukua nusu dakika.Sema sasa ukíshakula viapo utaacha kutuadithia ndio tatizo la haya mambo.
Niunganishe nae mimi
 
Nataka kukua hao watu huwa wanawatokea walokole Tu,

Je umeshachunguza kwenye haya makanisa yetu kama Roma na KKKT je hao watu wa kuakisi Mwanga wanatokea?

Je Kwa misikitini hawa watu wanatokea?

Na kama hawatokei Je Kwa uchunguzi wako haya madhehebu mengine wakiwa ibadani nini huwa kinatokea?

Je hawa wapani wasioamini kitu chochote Je hawana ulinzi wowote ule katika ulimwengu wa nje ya mwili?

Nijibu Kwanza haya nikitulia bado nina maswali mengi,

Na ninaomba uendele kuna mengi ya kujifunza
nakujiu.Kuna kitu Kinaiwa fellowship ya mchanganyiko ya makanisa hayo yote .Kawida watu wote waliokoka toka Lutheran,Moravian ama Baptist hukutana pamoja baada ya kutoks makanisani kwako kwa maombi.

Au Roman kuna kalsmatic catolic
 
Mzeebaba sijasoma yote ila uchawi au ushirikina haupo ni story za kusadikika zinazoshamiri sana kwenye jamii za watu wajinga na maskini ndo maana ni rahisi mtu wa Chitipa kuamini karogwa kuliko mtu wa Masaki achilia mbali Ulaya na bongo.
Vipi unaamini mungu yupo?
 
Mungu hachunguziki kwa akili za kibinadamu,ila ukitaka kuwa karibu naye atakuwa karibu na wewe,ulipokosea ni kusema kuwa Mungu huyu ni wa walokole,hapo ndio umeondoa maana ya hadithi yako,kwa hiyo unataka kusema kuwa waislamu hawana Mungu...?
 
Nilikua kwenye utafiti wa mungu wa walokole na nilipata majibu ya utafiti wangu kupitia unajimu wa nyota na uganga wa anga..Sikuwahi kufanya utafiti wa mungu wa waislamu aitwaye Allah au mungu wa wahindu katika koo zake zote...!!!!Ukisoma vizuri utanielewa kwanini niliamua kuwadadisi walokole wale wanaolialia nyie mnaita(Kusali au kunena kwa lugha)
 
Wewe ni mlokole dada? Unajua hapo una watu warefu wenye kuakisi mwanga na miale yao ya blue kama radi wamekuzunguka? Ukicheka wanacheka na ukilia wanalia na ukiwaamrisha wanatenda vile vile unavyosema..Ila walokole hamjui kua mkuu wenu(Mungu wenu)ana nguvu kiroho kuliko jamii yoyote ile ya ulimwengu wa kiroho na washirika wake ni hao watu warefu weupe wengine wana mabawa na wengine hawana ila wanakuja duniani kujishugulisha na walokole tu,huko mbele nitaadithia kwanini.

Mungu mwenye utatu Mtakaifu na Jeshi lake la mbinguni (Maserafi,makerubi n.k)

Mwanadamu (yule aliyetoka katika uzao wa Adam, tena aliyefinyangwa kwa udongo na kutiwa pumzi ya uhai na Mungu mwenyewe)

Malaika (Ndio hao unaita watu warefu wenye nguo nyeupe na wapo makundi na vyeo tofauti)

Viumbe wengine
 
Ule mtindo ulioanza nao ulikua mzuri kuliko huu wa simulizi, simulizi hazikosagi chai, na sio rahisi kukumbuka convo zote so chai ni unkwepable.
Mtindo upi mzee ebu nikumbushe niendelee nao???Maana mimi naelezea kwa kifupi kifupi matokeo ya utafiti wangu na mkufunzi wangu Mzee Matata.Ilituchukua miaka mingi na ukumbuke nilikua ninahama hama mikoa kutokana na utafutaji...Lakini tulihitimisha utafiti wetu 2019 kwa kusema kwa pamoja""Huyu mungu wa walokole hagawanyiki kwa hesabu za angani kwa kutumia uganga wa kinajimu kumchunguza tuachane nae la sivyo tutakua vichaa maana jinsi mnavyochunguza ndio mnavyoibua vitu visivyotafsirika kwa akili ya kiubinadamu""""Mzee Matata yeye aliamua kua mlokole kabisa akaacha uganga na unajimu.
 
Mungu mwenye utatu Mtakaifu na Jeshi lake la mbinguni (Maserafi,
Mwanadamu
Malaika (Ndio hao unaita watu warefu wenye nguo nyeupe na wapo makundi na vyeo tofauti)
Viumbe wengine
Kuna watu warefu wana mabawa wanapenda kuongea na watoto na kuna wale wasio na mabawa wanawasindikiza walokole njiani.Na kuna wale wanaozurura hewani hawagusi chini kama wanaelea hivi na panga zao mikononi.Na kuna wale wa kutoka baharini hawaakisi mwanga wa jua wana ugomvi siku zote na hawa wanaoelea angani sijui wanagombania nini""Ugomvi wao ni kama radi zinagongana""""...Hawa wa baharini hawana urafiki na walokole,bali wana urafiki na wanajimu na waganga..Mimi utafiti wangu ulikua kuhusu wale watu warefu wanaoakisi mwanga wa jua na wenye urafiki na walokole.
 
INAENDELEA:
Basi alhamisi ikafika na kama kawaida mimi na mzee Matata tukaendelea na utafiti wetu.Mzee matata akaniambia kijana wangu unajua siku ile pale kilimani sikukimbia,bali kile kilikua kivuli changu tu.Mimi nilikaa nyumbani na kukuacha wewe uende kwenye utafiti hatua ya kwanza.Ulipotoka tu hapa wale watu warefu walikua pembeni yako wanayasoma mawazo yako na wakaamua kukusindikiza ila wewe ulikua huwaoni mpaka pale mmoja wao alipoamua kujionyesha kwako kwa sekunde chache mbele yako.Na mimi nisingeweza kuja kuongozana na wewe sababu mimi ni mganga na mnajimu,vitu ambavyo kwa wale watu warefu ni makufuru.Na huu unajimu sikuutoa kwao bali nilipata hii elimu kwa wapinzani wao.Sasa mimi pamoja na unajimu wangu kuna vitu siwezi kama kusoma mawazo yote ya binadamu"""Elimu yetu ya unajimu na uganga ina kikomo""sababu kumjua tu binadamu ni elimu pana sana na tumefundishwa tu kiduchu na viumbe wasio binadamu wa kawaida ola hilo sio la muhimu sana wewe kujua,wewe shida yako ni kuwadadisi walokole na wale watu warefu ili kuwajua.Lakini kuwajua wale watu warefu wenye miili ya shaba na wanaoakisi mwanga wa jua ni ngumu zaidi,sababu maarifa yao ni mara trion elfu za maarifa ya unajimu.Historia yao kwa elimu ya kibinadamu ya uganga na unajimu inasema kua hawa watu warefu wanaoakisi mwanga na wenye mabawa kama ya ndege,na wengine hawana mabawa ni jamii moja na wale watu warefu wasioakisi mwanga wa jua ambao hawana mabawa na wanakaa katikati ya dunia kupitia chini ya zuio lolote la maji juu ya dunia,kama bahari au ziwa au mto au maporomoko ya maji.
Walipokua jamii moja miaka trion elfu za nyota kwa hesabu ya kinajimu.Waligombana na sababu kuu ya kugombana haijulikani ila inaonyesha ilikua ni kugombea madaraka na udhibiti wa anga lote la juu nje ya mfumo kani wa ulimwengu wa sayari.Jamii moja ikaja duniani na jamii nyingine ikabaki angani,na kila jamii ina kiongozi wake mkuu.Tokea hapo hizo jamii mbili hazijawahi kupatana na ile jamii ya angani ina nguvu kubwa kuliko ile jamii ya baharini.Jamii ya angani ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani na jamii ya baharini ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani,namaanisha wafuasi ambao ni binadamu.Hakuna binadamu au jamii yoyote ya wale watu warefu wa baharini ambayo inaweza kuvuka mpaka uliowekwa na mkuu wa wale watu wa angani kuelekea kwenye makao yao ya mwanga wa jua.Nchi yao inaitwa"Mwanga wa jua""sababu hakuna usiku huko ni mchana tu,na kwa hesabu za unajimu huwezi kufika huko ila unaweza kukadiria uwepo wake kupitia wale watu wa angani wakiwa wanakuja na kuondoka duniani kuwatembelea walokole unaotaka kuwadadisi.
Mzee matata akaniambia hakuna kitu kizuri duniani kama udadisi wenye manufaa.Nikamuuliza sasa wewe mzer wangu hizi habari zote umezipataje????? Akanijibu kwa kusema na mimi nilikua mdadisi kama wewe ila kwa kupitia uganga na unajimu.Akaniambia kuna vitu hatonieleza sababu mimi sio mnajimu na kuna vitu atanieleza kuhusu udadisi wangu.Hiyo ilikua alhamisi mchana na ilipofika jioni akaniambia nenda kwa jirani zako wale walokole ukae nao na uwaambie wakufundishe kuhusu imani yao na dini yao na jinsi wanavyosali kwa mkuu wao.Wakishakujibu na kukufundisha imani yao basi utakuja hapa alhamisi inayofuatia tuendelee na utafiti wetu taratibu wala hatuna haraka
.Nikaondoka pale nyumbani kwa mzee Matata moja kwa moja mpaka nyumbani,nikapanga jumamosi nitaenda kwa jirani yangu mzee Karugala anifundishe kuhusu dini yake ya kilokole na anijuze zaidi imani yao na utaratibu wao wa maisha na nitamuuliza pia kuhusu wale watu warefu wa angani wanaoakisi mwanga wa jua na kuelea angani kama manyoya ya kuku au ndege.
Kichwani ile picha ya mtu mrefu anayeelea angani kama unyoya haikunitoka na jinsi alivyovaa na uangavu wake na sura yake ya shaba za kumetemeta haikua rahisi kuisahau japo ilikua ni kwa sekunde thelathini tu.Nikajipa moyo nitaendelea na utafiti wangi hata ipite miaka kumi taratibu bila haraka yoyote ile.
Basi jumamosi ikafika nikaenda nyumbani kwa mzee Karugala na nikamkuta,baada ya salaamu nikamueleza yafuatayo.
MIMI:Mzee wangu leo nimekuja kusali nyumbani kwako na unihubirie kidogo
MZEE KARUGALA:Akichekaa"""umekuja mwanangu kunisalimia na kusali pamoja na mimi?????
MIMI:Ndio mzee wangu na ninataka unifundishe kuhusu nguvu ya imani yako ya kuokoka na unifundishe kuhusu Yesu na roho mtakatifu.Na unifundishe kuomba kama nyinyi walokole mnavyoomba.
MZEE KARUGALA:Inabidi baada ya mafundisho nikuongoze sala ya toba kijana wangu.
MIMI:Sawa mzee wangu
MZEE KARUGALA:Simama tuombe kwanza ulinzi wa roho ya Mungu kabla ya yote maana naamini ni roho wa Mungu wangu kakuleta hapa.
Tuliposimama tu ile mzee anaanza kusali tukiwa tumefumba macho,nikahisi uwepo wa wale watu warefu,kuwaona siwaoni ila nahisi wapo pembeni yetu kama wananigusa begani.Mzee karugala akamaliza kuomba huku mimi begani kuna mkono wa moto umenigusa maana nilikua nahisi vidole kabisa ila cha ajabu lile joto haliniunguzi.Mzee Karugala akaanza mahubiri yake huku mimi simuelewi hata neno moja akili yangu yoote ipo kwenye ule mkono ulionigusa begani.Nilikua nimekaa kwenye kiti sebuleni kwa mzee Karugala na pembeni yake alikuja kukaa mkewe na binti zao wawili kuendelea na ile ibada.Mzee ananihubiria ila mimi nachokumbuka ni maneno ya ""Ameen""tu basi.Akili yote ipo kwenye ule mkono ulionishika kirafiki begani.Nikahesabu kimoyomoyo mpaka tatu,afu nikageuka ghafla nimuone yule mtu alienishika mkono.
Si nikakutana uso kwa uso na yule mtu wa siku ile ila safari hii amesimama pembeni yangu kwa nyuma huku akitabasamu kunielekea na sura yake ile ile ya rangi ya shaba,nikajikuta naropoka"""Wewe tena"".Kumbe ile sauti yangu hakuna aliyeisikia wao wanaendelea tu na ibada kiongozi akiwa mzee wa familia Karugala na hawaoni kama nimegeuka bali wanaona nimetulia nawasikiliza""Hayo maelezo walinipa baadae"".
Yule mtu mrefu akaniambia kwa kiswahili ila kwa mtindo wa kuniuliza swali""UNATUPENDA KAMA TUNAVYOKUPENDA??? akacheka na kupotea tena.Yote hayo yalifanyika ndani ya sekunde ishirini hivi pale kwa mzee wangu Karugala.Basi tukaendelea na ibada iliyotuchukua masaa mawili na alipomaliza maombi ya kufunga ibada akaniambia nipige magoti anisalie toba.Ile napiga magoti ule mkono ukanishika tena begani ila safari hii sikufumbua macho nikatulia tuli.Mzee Karugala akasali maneno yake akaniambia nimfuatishe kusema na alipomaliza akaniambia nisimame.Ule mkono ukaacha kunishika bega pia niliposimama.Nikala chakula cha jioni pale kwa Mzee wangu Karugala afu nikaaga kurudi nyumbani na baiskeli yangu.Sikumwambia chochote mzee Karugala wala Babu Matata nikagonja mpaka alhamisi tukiendelea na utafiti wetu ndio nitamwambia tukio lile.
Lakini cha ajabu sikua na uoga bali moyo wa udadisi ndio ukaongezeka na nikaamua mengine nitakua simuambii Mzee Matata bali nitakua nayaweka moyoni ili yanisaidie kwenye utafiti wangu wa viumbe wale warefu wasiokua wa kawaida ila ni marafiki wa walokole.Nikarudi nyumbani kuendelea na maisha mengine nikisubiria Alhamisi inayokuja niendelee na utafiti wangu wa kiudadisi na kisomi kuhusu walokole nikiwa na Mzee Matata mganga bingwa na mnajimu wa nyota na mambo ya Anga.
ITAENDELEA.................
Umenikumbusha jambo moja kuu kuhusu waamini katika Mungu wa mbingu na nchi ambao wanaomwamini hupitia jina lake la utambulisho la wakati yaani Yesu Kristo hata wakaitwa wakristo kwa maana ya ufuasi wao kwa Kristo. Miongoni mwao ni hao walipachikwa jina walokole au wa kulialia.
Jambo lenyewe ni hili kuna siri kuu katika mambo ya ulimwengu wa roho ambayo wanajimu, waganga na wachawi wanayafahamu kumhusu Mungu mara mia elfu zaidi ya wakristo. Hata hivyo kwa kuyafahamu hakuwafanyi kujisalimisha maisha yao kwake kwa sababu ya maslahi binafsi.
Adamu kabla ya kuwekwa katika mwili ule wa udongo kwa kazi ya kuilima nchi na kuitiisha, aliishi ulimwengu zote mbili yaani wa kiroho na kimwili hata alipoanguka na kupoteza haki ya umiliki.
Maana yake kumbe uwezo wa kumiliki ya kiroho na kimwili haitoshi tu kuwa sababu pekee ya ushindi dhidi ya kumuasi Mungu.
Mama jusi ambao ni wanajimu ndio walioiona na kuitambua nyota ya Yesu na kufunga safari ya miaka kadhaa kutoka huko kwa wakaldayo(mashariki ya mbali) kuifuata hata ilipowafikisha mahali mtoto alizaliwa ambaye walimsujudia maana walinjua kuwa mfalme tena juu ya wafalme wote maana nyota yake ilizidi zote.
Daniel alipokuwa utumwani huko babeli miaka kama miatano kabla ya Yesu kuzaliwa aliwahi kuwekwa kuwa kiongozi juu ya hawa wanajimu, wenye hekima, waganga na wachawi wa huko. Na ni baada ya kumshuhudia na kuhakiki kuwa yeye alikuwa mshiriki wa miungu mitakatifu isiyo na ushirika na wanadamu yenye uwezo wa juu mara mamilioni kuwazi.
Hawa wanajimu waliotoka huko mashariki ya mbali pamoja na magombo yao lakini walihitaji muongozo wa magombo ya manabii kama kina Danieli kufikia ufanisi wa kuzisoma nyota na kuelewa maana yake.
Kingine cha ajabu Yesu alijulikana na wafuasi tena hohehahe wa wakati wao na sii wakuu wa kidini.
Mfano wa mtu aitwae simion na nabii mke kwa jina la Ana. Hawa walipo muona mtoto Yesu ameletwa hekaluni waliingiwa na roho na kutabiri juu yake.
Mapepo nayo yalimtambua kila aendako kabla ya wengine na mengi yalipiga kilele kwa kuomba rehema na kusihi asiyaangamize kabla ya wakati wao.
Wakati yakipaaza sauti kuwa wewe ndiye mtakatifu wa Mungu, hekaluni makuhani na wakuu wa dini walimwita Yesu belzebuli yaani mkuu wa pepo kwa kumdhihaki.
Yesu asingeweza kuwaangamiza wale mapepo kabla ya wakati. Aliyafukuzia baharini ambako Mungu ndiko alikompa Lewiathani kuwa makazi yake hata siku ya kuangamizwa.Zaburi 104:25-26
[25]Bahari iko kule, kubwa na upana,
Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,
Viumbe hai vidogo kwa vikubwa.
So is this great and wide sea, wherein are things creeping innumerable, both small and great beasts.
[26]Ndimo zipitamo merikebu,
Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo.
There go the ships: there is that leviathan, whom thou hast made to play therein.

Na maangamizi yake Isaya aliyanenea
Isaya 27:1
[1]Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.
In that day the LORD with his sore and great and strong sword shall punish leviathan the piercing serpent, even leviathan that crooked serpent; and he shall slay the dragon that is in the sea.

Natamani kuongelea wale mwenye uzi anawaita watu warefu.
Lakini ukweli wake ni walinzi wa kile kiti cha rehema cha Mungu ambacho kwa sasa kipo katika moyo wa mwamini halisi wa Yesu Kristo.
Zamani kilikuwa katika hekalu patakatifu pa patakatifu(utukufu wa shekina) kikilindwa na makerubi.
Sasa hivi ni zile injili nne yaani Matayo, Marko, Luka na Yohana zikilinda matendo ya roho mtakatifu ndani ya mitume ambapo waandishi waliyaita MATENDO YA MITUME .
 
Back
Top Bottom