Ulitaka tuumbwe maroboti kila ikifika saa Moja asubuhi tuseme " Eh Mungu tunakupenda sana"!!
Tuna uhuru wa kumchagua, na huo ndo UPENDO wa kweli, kumchagua mtu kwa utashi wako!
Mungu hajaribu mtu!
Yak 1:13 SUV
Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
Aliyetilia shaka utawala wa Mungu na utii wetu na anayejaribu watu:
Mwanzo 3:1
......Basi, nyoka akamwambia huyo mwanamke, “Ati Mungu alisema msile matunda ya mti wowote bustanini?”
Ayubu 1:12
Bwana akamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”
Ndipo Shetani akatoka mbele za Bwana
Ayubu 2:5-6
BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini tunza tu uhai wake.
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hadi utosi wa kichwa.
Luka 4:13 NEN
Ibilisi alipomaliza kila jaribu, akamwacha Yesu mpaka wakati mwingine ufaao.
Anachofanya Mungu:
Isaya 48:17-18
.....“Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ninayekufundisha kwa faida yako, ninayekuongoza katika njia unayotakiwa kwenda.
Laiti ungalizitii amri zangu!......
1 Wakorintho 10:13 BHN
Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
Methali 27:11 BHN
Uwe na hekima mwanangu upate kunifurahisha moyo,nami sitakosa la kumjibu yeyote anayenilaumu.
Kukataa uwepo wa Mungu ni kujitoa. ufahamu. Tena unatumia sheria za asili za Mungu, sheria zisizobadilika, sheria zinazosimama milele, sheria zipitazo ulimwengu wa mwili, yaani sheria za Mantiki!
Nafananisha na katoto kabishi kasumbufu hakataki kufuata muongozo halafu mwisho wa siku akimaliza ku poo anakuita ukasafishe!