INAENDELEA:
Basi alhamisi ikafika na kama kawaida mimi na mzee Matata tukaendelea na utafiti wetu.Mzee matata akaniambia kijana wangu unajua siku ile pale kilimani sikukimbia,bali kile kilikua kivuli changu tu.Mimi nilikaa nyumbani na kukuacha wewe uende kwenye utafiti hatua ya kwanza.Ulipotoka tu hapa wale watu warefu walikua pembeni yako wanayasoma mawazo yako na wakaamua kukusindikiza ila wewe ulikua huwaoni mpaka pale mmoja wao alipoamua kujionyesha kwako kwa sekunde chache mbele yako.Na mimi nisingeweza kuja kuongozana na wewe sababu mimi ni mganga na mnajimu,vitu ambavyo kwa wale watu warefu ni makufuru.Na huu unajimu sikuutoa kwao bali nilipata hii elimu kwa wapinzani wao.Sasa mimi pamoja na unajimu wangu kuna vitu siwezi kama kusoma mawazo yote ya binadamu"""Elimu yetu ya unajimu na uganga ina kikomo""sababu kumjua tu binadamu ni elimu pana sana na tumefundishwa tu kiduchu na viumbe wasio binadamu wa kawaida ola hilo sio la muhimu sana wewe kujua,wewe shida yako ni kuwadadisi walokole na wale watu warefu ili kuwajua.Lakini kuwajua wale watu warefu wenye miili ya shaba na wanaoakisi mwanga wa jua ni ngumu zaidi,sababu maarifa yao ni mara trion elfu za maarifa ya unajimu.Historia yao kwa elimu ya kibinadamu ya uganga na unajimu inasema kua hawa watu warefu wanaoakisi mwanga na wenye mabawa kama ya ndege,na wengine hawana mabawa ni jamii moja na wale watu warefu wasioakisi mwanga wa jua ambao hawana mabawa na wanakaa katikati ya dunia kupitia chini ya zuio lolote la maji juu ya dunia,kama bahari au ziwa au mto au maporomoko ya maji.
Walipokua jamii moja miaka trion elfu za nyota kwa hesabu ya kinajimu.Waligombana na sababu kuu ya kugombana haijulikani ila inaonyesha ilikua ni kugombea madaraka na udhibiti wa anga lote la juu nje ya mfumo kani wa ulimwengu wa sayari.Jamii moja ikaja duniani na jamii nyingine ikabaki angani,na kila jamii ina kiongozi wake mkuu.Tokea hapo hizo jamii mbili hazijawahi kupatana na ile jamii ya angani ina nguvu kubwa kuliko ile jamii ya baharini.Jamii ya angani ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani na jamii ya baharini ina imani yake (Dini) na ina wafuasi wake duniani,namaanisha wafuasi ambao ni binadamu.Hakuna binadamu au jamii yoyote ya wale watu warefu wa baharini ambayo inaweza kuvuka mpaka uliowekwa na mkuu wa wale watu wa angani kuelekea kwenye makao yao ya mwanga wa jua.Nchi yao inaitwa"Mwanga wa jua""sababu hakuna usiku huko ni mchana tu,na kwa hesabu za unajimu huwezi kufika huko ila unaweza kukadiria uwepo wake kupitia wale watu wa angani wakiwa wanakuja na kuondoka duniani kuwatembelea walokole unaotaka kuwadadisi.
Mzee matata akaniambia hakuna kitu kizuri duniani kama udadisi wenye manufaa.Nikamuuliza sasa wewe mzee wangu hizi habari zote umezipataje????? Akanijibu kwa kusema na mimi nilikua mdadisi kama wewe ila kwa kupitia uganga na unajimu.Akaniambia kuna vitu hatonieleza sababu mimi sio mnajimu na kuna vitu atanieleza kuhusu udadisi wangu.Hiyo ilikua alhamisi mchana na ilipofika jioni akaniambia nenda kwa jirani zako wale walokole ukae nao na uwaambie wakufundishe kuhusu imani yao na dini yao na jinsi wanavyosali kwa mkuu wao.Wakishakujibu na kukufundisha imani yao basi utakuja hapa alhamisi inayofuatia tuendelee na utafiti wetu taratibu wala hatuna haraka
.Nikaondoka pale nyumbani kwa mzee Matata moja kwa moja mpaka nyumbani,nikapanga jumamosi nitaenda kwa jirani yangu mzee Karugala anifundishe kuhusu dini yake ya kilokole na anijuze zaidi imani yao na utaratibu wao wa maisha na nitamuuliza pia kuhusu wale watu warefu wa angani wanaoakisi mwanga wa jua na kuelea angani kama manyoya ya kuku au ndege.
Kichwani ile picha ya mtu mrefu anayeelea angani kama unyoya haikunitoka na jinsi alivyovaa na uangavu wake na sura yake ya shaba za kumetemeta haikua rahisi kuisahau japo ilikua ni kwa sekunde thelathini tu.Nikajipa moyo nitaendelea na utafiti wangi hata ipite miaka kumi taratibu bila haraka yoyote ile.
Basi jumamosi ikafika nikaenda nyumbani kwa mzee Karugala na nikamkuta,baada ya salaamu nikamueleza yafuatayo.
MIMI:Mzee wangu leo nimekuja kusali nyumbani kwako na unihubirie kidogo
MZEE KARUGALA:Akichekaa"""umekuja mwanangu kunisalimia na kusali pamoja na mimi?????
MIMI:Ndio mzee wangu na ninataka unifundishe kuhusu nguvu ya imani yako ya kuokoka na unifundishe kuhusu Yesu na roho mtakatifu.Na unifundishe kuomba kama nyinyi walokole mnavyoomba.
MZEE KARUGALA:Inabidi baada ya mafundisho nikuongoze sala ya toba kijana wangu.
MIMI:Sawa mzee wangu
MZEE KARUGALA:Simama tuombe kwanza ulinzi wa roho ya Mungu kabla ya yote maana naamini ni roho wa Mungu wangu kakuleta hapa.
Tuliposimama tu ile mzee anaanza kusali tukiwa tumefumba macho,nikahisi uwepo wa wale watu warefu,kuwaona siwaoni ila nahisi wapo pembeni yetu kama wananigusa begani.Mzee karugala akamaliza kuomba huku mimi begani kuna mkono wa moto umenigusa maana nilikua nahisi vidole kabisa ila cha ajabu lile joto haliniunguzi.Mzee Karugala akaanza mahubiri yake huku mimi simuelewi hata neno moja akili yangu yoote ipo kwenye ule mkono ulionigusa begani.Nilikua nimekaa kwenye kiti sebuleni kwa mzee Karugala na pembeni yake alikuja kukaa mkewe na binti zao wawili kuendelea na ile ibada.Mzee ananihubiria ila mimi nachokumbuka ni maneno ya ""Ameen""tu basi.Akili yote ipo kwenye ule mkono ulionishika kirafiki begani.Nikahesabu kimoyomoyo mpaka tatu,afu nikageuka ghafla nimuone yule mtu alienishika mkono.
Si nikakutana uso kwa uso na yule mtu wa siku ile ila safari hii amesimama pembeni yangu kwa nyuma huku akitabasamu kunielekea na sura yake ile ile ya rangi ya shaba,nikajikuta naropoka"""Wewe tena"".Kumbe ile sauti yangu hakuna aliyeisikia wao wanaendelea tu na ibada kiongozi akiwa mzee wa familia Karugala na hawaoni kama nimegeuka bali wanaona nimetulia nawasikiliza""Hayo maelezo walinipa baadae"".
Yule mtu mrefu akaniambia kwa kiswahili ila kwa mtindo wa kuniuliza swali""UNATUPENDA KAMA TUNAVYOKUPENDA??? akacheka na kupotea tena.Yote hayo yalifanyika ndani ya sekunde ishirini hivi pale kwa mzee wangu Karugala.Basi tukaendelea na ibada iliyotuchukua masaa mawili na alipomaliza maombi ya kufunga ibada akaniambia nipige magoti anisalie toba.Ile napiga magoti ule mkono ukanishika tena begani ila safari hii sikufumbua macho nikatulia tuli.Mzee Karugala akasali maneno yake akaniambia nimfuatishe kusema na alipomaliza akaniambia nisimame.Ule mkono ukaacha kunishika bega pia niliposimama.Nikala chakula cha jioni pale kwa Mzee wangu Karugala afu nikaaga kurudi nyumbani na baiskeli yangu.Sikumwambia chochote mzee Karugala wala Babu Matata nikagonja mpaka alhamisi tukiendelea na utafiti wetu ndio nitamwambia tukio lile.
Lakini cha ajabu sikua na uoga bali moyo wa udadisi ndio ukaongezeka na nikaamua mengine nitakua simuambii Mzee Matata bali nitakua nayaweka moyoni ili yanisaidie kwenye utafiti wangu wa viumbe wale warefu wasiokua wa kawaida ila ni marafiki wa walokole.Nikarudi nyumbani kuendelea na maisha mengine nikisubiria Alhamisi inayokuja niendelee na utafiti wangu wa kiudadisi na kisomi kuhusu walokole nikiwa na Mzee Matata mganga bingwa na mnajimu wa nyota na mambo ya Anga.
ITAENDELEA.................