Mungu wetu ni Mungu wa rehema

Mungu wetu ni Mungu wa rehema

Unajua ama kuelewa kilichokuwa kinasemwa hapa?

Kwahiyo Mimi ya milango ndo jf ya Sasa?
Kumbukumbu la Torati 6:7-9

[7]nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

[8]Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.

[9]Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Zingatia mstari wa 9
 
Tuombe,
Eeeh Mungu Mwenyezi Muumba Mbingu na ardhi pamoja vyote tunavyoviona na tusivyoviona, Tunakushukuru kwa zawadi ya uzima na afya njema, Tunakusifu na kukuabudu wewe kwa kuwa hakuna mungu kama wewe,

Baba tunakuomba ubariki kazi za mikono yetu, tusipungukiwe na chochote,
-Utusamehe makosa yetu
-Utuepushe na kila aina za hatari na bahati mbaya
-Uwasaidie wale wote wanaopitia changamoto mbalimbali za kimaisha, wagonjwa, waliofungwa kwa kesi za kusingiziwa , wasio na ajira na wote wanaopita changamoto za kiuchumi.
-Uwaepushe na ajali wale wote waliopo safarini.
-Ulilinde taifa letu, Uwape viongozi wetu hekima ya kuongoza nchi vema na kuwa na hofu juu yako.

Ninaomba kwa ajili ya wote wanaokumbuka na wasiokumbuka kuomba, tazama sisi sote ni watoto wako,
Katika Jina la YESU KRISTO, jina lipitalo majina yote ninaomba nikiamini AMEN.
kwa mamlaka gani unatuombea mkuu
 
Wagalatia 6:1-5
Wagalatia6:1 Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. 2 Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. 3 Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. 4 Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5 Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. 6 Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.

hiyo hapo au nyingine.
mimi nimeuliza tu nielewe mkuu. haya maombi unayotufanyia kwa aya yoyote kwenye biblia ambayo inatoa mamlaka kwa mtu mmoja kumuombea mwingine? mimi ni mwanafunzi wa biblia
Aya ninayoijua ni ile inayotuagiza tuombe kwa jina la Yesu naye atatusikia
sasa hili la kumuombea mtu mwingine ,naomba aya
 
Una Uhakika na Kuamini Ya Kwamba,,Yesu Kristo Yu Hai??
 
Yakobo 5:13-14

[13]Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

Is any among you afflicted? let him pray. Is any merry? let him sing psalms.

[14]Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

Is any sick among you? let him call for the elders of the church; and let them pray over him, anointing him with oil in the name of the Lord:
 
aliyetuombea, huyo mleta mada ni mzee wa kanisa lipi, sisi ni waumini wa hilo kanisa la mleta mada
Is any sick among you? let him call for the elders of the church; and let them pray over him, anointing him with oil in the name of the Lord:
aliye tuombea ni mzee wa kanisa letu?
 
kama anakaa ndani yetu sasa, why mtu mtu atuombeee
Una uhakika wewe ni mwana wa Mungu?

Yapo mazingira ambayo yatakuhitaj uombewe, unaumwa huwezi basi utahitaji kuombewa, unapita kwenye changamoto ambayo akili yako imefika mwisho utahitaji kuombewa, huna nguvu ndani yako(mahusiano yako na Mungu ni hayapo au hafifu) utahitaji kuombewa
 
Ushasema ni Mungu wa Rehema, sasa anakuwaje wetu?

Au we ndio Rehema mwenyewe umeamua kujimilikisha?
 
aliye tuombea ni mzee wa kanisa letu?
Waefeso 6:18

[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

Praying always with all prayer and supplication in the Spirit, and watching thereunto with all perseverance and supplication for all saints;

Sio lazima awe mzee wa kanisa mkuu, soma na hapo
 
Ushasema ni Mungu wa Rehema, sasa anakuwaje wetu?

Au we ndio Rehema mwenyewe umeamua kujimilikisha?
unaelewa maana ya Rehema au umekalili kwakuwa umewazoea akina Rehema
 
Back
Top Bottom