Mungu wetu ni Mungu wa rehema

Unajua ama kuelewa kilichokuwa kinasemwa hapa?

Kwahiyo Mimi ya milango ndo jf ya Sasa?
 
kwa mamlaka gani unatuombea mkuu
 
Wagalatia 6:1-5
Wagalatia6:1 Ndugu zangu, mkimwona mtu amenaswa katika dhambi fulani, basi ninyi mnaoongozwa na Roho, mrejesheni mtu huyo kwa upole. Lakini mjihadhari, ili na ninyi msije mkajaribiwa. 2 Chukulianeni mizigo yenu; na kwa njia hiyo mtaweza kutimiza sheria ya Kristo. 3 Mtu akijiona kuwa yeye ni bora na kumbe siyo, basi mtu huyo anajidanganya mwenyewe. 4 Lakini, kila mtu apime mwenendo wake, ndipo anaweza kuwa na sababu ya kujisifu bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine. 5 Kwa maana, kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe. 6 Basi, mwanafunzi na amshirikishe mwalimu wake vitu vyote vilivyo vyema.

hiyo hapo au nyingine.
mimi nimeuliza tu nielewe mkuu. haya maombi unayotufanyia kwa aya yoyote kwenye biblia ambayo inatoa mamlaka kwa mtu mmoja kumuombea mwingine? mimi ni mwanafunzi wa biblia
Aya ninayoijua ni ile inayotuagiza tuombe kwa jina la Yesu naye atatusikia
sasa hili la kumuombea mtu mwingine ,naomba aya
 
Una Uhakika na Kuamini Ya Kwamba,,Yesu Kristo Yu Hai??
 
Yakobo 5:13-14

[13]Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

Is any among you afflicted? let him pray. Is any merry? let him sing psalms.

[14]Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.

Is any sick among you? let him call for the elders of the church; and let them pray over him, anointing him with oil in the name of the Lord:
 
aliye tuombea ni mzee wa kanisa letu?
 
kama anakaa ndani yetu sasa, why mtu mtu atuombeee
Una uhakika wewe ni mwana wa Mungu?

Yapo mazingira ambayo yatakuhitaj uombewe, unaumwa huwezi basi utahitaji kuombewa, unapita kwenye changamoto ambayo akili yako imefika mwisho utahitaji kuombewa, huna nguvu ndani yako(mahusiano yako na Mungu ni hayapo au hafifu) utahitaji kuombewa
 
Ushasema ni Mungu wa Rehema, sasa anakuwaje wetu?

Au we ndio Rehema mwenyewe umeamua kujimilikisha?
 
aliye tuombea ni mzee wa kanisa letu?
Waefeso 6:18

[18]kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

Praying always with all prayer and supplication in the Spirit, and watching thereunto with all perseverance and supplication for all saints;

Sio lazima awe mzee wa kanisa mkuu, soma na hapo
 
Ushasema ni Mungu wa Rehema, sasa anakuwaje wetu?

Au we ndio Rehema mwenyewe umeamua kujimilikisha?
unaelewa maana ya Rehema au umekalili kwakuwa umewazoea akina Rehema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…