Mungu Yuko wapi?

Unatumia simu ambayo ni wireless, lakini unaamini unaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali nawe.

Unamfahamu mtu wa kwanza kugundua simu ya wireless? Alipotangaza kile alichokigindua, marafiki zake walimkamata na kumpelekea hospitalini kwa kuamini kuwa kachanganyikiwa. Si ajabu na wewe kutokuamini kuwa kuna ulimwengu zaidi ya huo unaouona. Unaweza usiamini, lakini si rahisi kukwepa athari zake kwako.

Hapo ulipo, kuna sauti nyingi japo huzioni: ITV, RADIO ONE, ALJAZEERA, BBC NEWS, etc. Zote hizo zipo karibu nawe lakini hutambui. Lakini ukiwa na receiver sahihi, unaweza kuzisikia.

Hapo ulipo, kuna nguvu za ulimwengu wa roho, ama mapepo au Malaika, nguvu za Mungu au za Shetani. Either of the two anaweza akawa na ushawishi kwako kulingana na upande unaouamini.

Kutokuona ambacho wengine wanakiona si uthibitisho kuwa havipo, bali ni ama wewe au hao wengine wasioviona hawapo katika tune ya kuweza kuona.

Unafikiri vitu vingine ni uoga? Utakuwa hujui, pengine! Kuna mambo yanayoendelea, hata hapo ulipo, lakini wewe huyaoni. Kama kweli hujui kuwa vitu kama hivyo vipo, labda, ipo siku utakuja kufahamu, ila sijui ni lini!
 
Kwa tafsiri ya kawaida Mungu ni uwezo mkuu usiyowezwa.
Ikiwa akili yako na imani yako haiwezi kuelewa au kujua uwepo wa Mungu ni tatizo lako binafsi. Kuleta mjadala wa Mungu pasina elimu ni sawa na kukanusha, hivyo basi ni bora ufanye juhudi ya makusudi na nia thabiti kuwaendea wale wabobezi katika masuala ya kiroho huwenda ukapata majibu ya maswali yako. Kama upo serious. Ikiwa unataka kufurahisha barza kwa kweli mada hiyo ibadilishe tafuta mada nyingine.
 
Ndio...coz ukisema una Imani ya Mungu wa Biblia unakuwa hujajibu swali la kwa Nini umechagua Imani hio na sio vitu kibao vingine ambavyo umeacha kuamini, why Mungu umempa special treatment
 
Ukijiamini wewe tayari ushaamini wanachokiita Mungu ,ili ujue sasa inabdi ujijue wewe ni nani ? Umetoka wap na utaenda wap.
Sasa Kama haya majibu Sina ndo nitunge story au niamini story? Mi ndo naamua Mimi ni nani na ninaenda wapi, na nimetoka tumboni kwa mama angu
 
Ushahidi wa wireless communication tunaona from telephones, television na internet, haya ushahidi wa roho na mapepo uko wapi
 
Nimefanya tafiti nimeona Mungu anayeaminiwa hawezi kuwepo coz Hana logical consistency kwenye sifa zake
 

Na Mungu akikuchoma anafaidi nini.
 
 
Kabisaa! Marekani ni Taifa lililoendelea, lakini masuala ya Imani ya Kimungu na ya kishirikina zingalipo.

Katika ushirikina wapo juu sana, mpaka kuna mahekalu ya waabudu Shetani, tena yaliyosajiliwa Kisheria.

Wanaomwamini Mungu wapo wengi sana.

Na katika uchumi na teknolojia, karibia kila mtu mwenye ufahamu anajua Marekani imeshapiga hatua sana.

Uchawi upo kila eneo, na imani ya kumwamini Mungu pia imetapakaa kila mahali.
 
Asante sana mkuu ubarikiwe sana,hizi mada kuhusu mungu inapaswa kuzipuuzwa,maana isije ikawa ni njama za shetani kutupeleka kwenye majaribu,maana wanga na wachawi wanatabia za kuleta mada kama hizi ili uteleze ujalibiwe wakuloge vizuri(kama freemason tunao waita wabudu shetani wanaa kipo kitu kinachoitwa supreme being) yeye ni nani asietambua uwepo wake,tuipuuze hii mada
 
Na ndio maana nakwambia sasa wapo madaktari kabisa ambao wanaamini Mungu na kuamini story zilizoelezwa kwenye vitabu vya dini.
Dr. Norman Vincent Peale, ameelezea kwenye Moja ya Vitabu vyake jinsi mtu mmoja alivyoshangaa kukuta Biblia kwenye ofisi y Daktari wa magonjwa ya akili.

Katika hali ya mshangaoy, na kwa nia ya kutaka kujiridhisha, alimwuliza huyo daktari kama na wao wanasoma Biblia!

Daktari alimjibu: "Kama watu wote wataisoma Biblia na kufuata maelekezo yake, madaktari wote tutaenda kufanya kazi ya kuvua samaki. Hatutakuwa na wagonjwa wa kuwatibu"
 
Nimefanya tafiti nimeona Mungu anayeaminiwa hawezi kuwepo coz Hana logical consistency kwenye sifa zake
Unaweza ukawa sahihi kutokana watu tofauti wana amini miungu tofauti, lakini Mungu ambaye ni Uwezo mkuu usiyowezwa huwezi kumjadili kwa kuwa yupo kinyume kabisa na sisi wanadamu tunavyomfikiria.
 
mpuuzieni huyo mtoa mada atakuwa mwanga au mchawi atawakufurisha bule, anadai hatambui uchawi,hajui majini,hatambui mungu, wakati daily watu wanapandisha mashetan,wana logwa, baasi naomba wachawi na wanga mliomo humu mumuloge ili kesho ajue uwepo wenu humu duniani kupitia nyinyi atatambua uwepo wa mungu alie hai.
 
utakuwa mwanga na mchawi tu usinikufurishe na mungu wangu hujui nimepitia mangapi, we mwenye elimu ya kukalilishwa ubaon imekusaidia nini mpaka hapo ulipo,wenzako kupitia uchawi wamevumbua ndege lakin we usiku unapaa na ungo wa buku jelo
 
Hakuna nilichotenganisha katika hivyo vitu viwili kwa sababu sizungumzii habari za kwanini afrika hakuna maendeleo, nimeonyesha hayo ambayo wewe unayaaeleza.
Huelewi kwamba kukosa elimu ni moja ya sababu kubwa ya Africa kutokuwa na maendeleo?
 
1. Basi ninalolifahamu ni lile nililolipanda. Elezea na wewe uzuri wa ulilolipanda ili nivutiwe kulipanda.

2. Wewe hujawahi kuwa Mkristo. Unajua maana ya kuwa Mkristo? Wewe hujawahi kuwa Mkristo.

Kuzaliwa kwenye familia ya Kikristo hakukufanyi kuwa Mkristo. Mkristo ni yule mwenye uhusiano binafsi na Kristo, na huwezi kuwa na uhusiano na usiyeamini kuwa Yupo. Kwa kuwa huamini kuwa Yupo, ni jibu dhahiri kuwa hujawahi kuwa Mkristo.

Kuimba Kwaya hakukufanyi kuwa Mkristo. Mtu yeyote anaweza kuigiza kuwa ni Mkristo na kumbe siyo. Mtu yeyote anaweza kuigiza ni mganga wa Kienyeji na kumbe siyo. Inawezekana na wewe uliigiza na ukafanikiwa.

Kuhudhuria Kanisani hakukufanyi kuwa Mkristo. Hata Mpagani, Mchawi, n.k. anaweza kuhudhuria Kanisani, na hata kuwa Mwanachama wa Kanisa husika, lakini hilo kamwe halimfanyi kuwa Mkristo.

Nifahamuvyo, nyumba za Ibada zipo wazi kwa kila anayetaka kuhudhuria. Au wewe kuna mahali popote ulikokuta zuio la watu wasio washirika wa dini fulani kuhudhuria ibada kwenye nyumba ya ibada isiyo ya dini yao?

Ninakosali kwa mfano, wanakaribishwa watu wa kila aina: wanaomwamini Mungu, wasiomwamini Mungu, wachawi, walevi, wazinzi, n.k. Tena, huwa ni furaha pale wasiomwamini Mungu wanapofika ibadani kwa sababu tunajua huenda wataisikia KWELI itakayowaweka huru.

Na wewe ninakukaribisha, siyo kujiunga, bali kusikiliza mahubiri. Ukivutiwa kumwamini Yesu ili nawe uwe Mkristo, unakaribishwa. Kama utataka kujiunga, milango iko wazi.

Labda uliowasikia wakimwelezea Mungu hawakukuelezea kwa ufasaha. Karibu! Huenda kiu yako itatoshelezwa.

3. Mimi sijasoma dini yoyote. Sijasoma Theolojia, wala Bible Knowledge au Divinity. Nilipokuwa A Level, nilijiandikisha kwenye darasa la Divinity, lakini nilipogundua kuwa somo lenyewe halinisaidii kumjua Mungu zaidi, niliachana nalo.

Nilizaliwa kwenye familia ya kipagani. Niliamua mwenyewe kuwa Mkristo baada ya kuona utofauti wa maisha ya Mkristo na ya wasiokuwa Wakristo. Nolivutowa na maisha ya Wakristo.

Tokea niwe Mkristo, nimejiridhisha pasipo shaka , kuwa Mungu Yupo, ananijua kwa jina langu, ananipenda, anao uwezo usiopimika, n.k. Nimejihakikishia mwenyewe. Sukuambiwa na mtu.

Kwanza, niliisoma kwenye Biblia. Pili, nikaamini. Nilipochukua hatua sawasawa na Imani, matokeo yakadhihirika.

Zaidi ya hayo, Mungu hana upendeleo. Ukiamua, atajidhihirisha na kwako pia.
 
Nani kalinganisha elimu? Unaanza kunichosha mkuu,we kuwa na amani wala mimi sitaki kuwashusha utukufu unaouona kwa wazungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…