Mungu Yuko wapi?

Mungu Yuko wapi?

Why matukio ya hivi hayawezi kuwa video recorded, ni coz ni illusion na hallucinations za akili, mi Nikisema nimeona tembo anapaa usiku haitamaanisha kuwa kweli hata tukiwa ishirini, Fatima Portugal watu 3000 waliona jua linacheza cheza sijui malaika wanaimba Ila ni kweli Hilo tukio lilitokea, hujiulizi why kitu muone watu wachache katika mazingira fulani halafu wengine wa mazingira mengine yasitokee kabisa. Kuona sio kila kitu, camera Ina accuracy kubwa kuliko macho, recorder Ina accuracy kubwa kuliko maskio coz haviwi affected na psychology mazingira uoga aibu hasira ujinga na pia utamaduni. Ndo maana utaskia story sijui huyu kaona Nini, wazungu Wana camera mpaka barabarani mbona vitu vya ajabu havirekodiwi
Unatumia simu ambayo ni wireless, lakini unaamini unaweza kuwasiliana na mtu aliye mbali nawe.

Unamfahamu mtu wa kwanza kugundua simu ya wireless? Alipotangaza kile alichokigindua, marafiki zake walimkamata na kumpelekea hospitalini kwa kuamini kuwa kachanganyikiwa. Si ajabu na wewe kutokuamini kuwa kuna ulimwengu zaidi ya huo unaouona. Unaweza usiamini, lakini si rahisi kukwepa athari zake kwako.

Hapo ulipo, kuna sauti nyingi japo huzioni: ITV, RADIO ONE, ALJAZEERA, BBC NEWS, etc. Zote hizo zipo karibu nawe lakini hutambui. Lakini ukiwa na receiver sahihi, unaweza kuzisikia.

Hapo ulipo, kuna nguvu za ulimwengu wa roho, ama mapepo au Malaika, nguvu za Mungu au za Shetani. Either of the two anaweza akawa na ushawishi kwako kulingana na upande unaouamini.

Kutokuona ambacho wengine wanakiona si uthibitisho kuwa havipo, bali ni ama wewe au hao wengine wasioviona hawapo katika tune ya kuweza kuona.

Unafikiri vitu vingine ni uoga? Utakuwa hujui, pengine! Kuna mambo yanayoendelea, hata hapo ulipo, lakini wewe huyaoni. Kama kweli hujui kuwa vitu kama hivyo vipo, labda, ipo siku utakuja kufahamu, ila sijui ni lini!
 
Mi najiuliza maswali mengi. Mungu Ni Nini, anataka Nini na Yuko wapi.

Ukifuatilia historia ya binadamu tokea tukiwa wawindaji maporini miungu ilikuwepo. Wazee walikuwa wanaongoza vijana kwa kuwaambia kuwa Mungu anataka mfanye hivi, na hio miungu ilikuwepo pangoni ambapo wazee tu wanaingia, baadae vijana wakajitoa akili kwenda wakaona wazee ni waongo na hamna kitu mule. Wagiriki wakaja na miungu yao wakasema ipo ya milima ya Olympus, Leo hii watu wamepanda milima yote ugiriki hawajaona miungu hio.

Wakaja wayahudi, wakasema Mungu yupo mawinguni. Ukifuatilia hata Yesu alipaa mawinguni, Mungu alifungua madirisha ya mbinguni kuleta mafuriko, alichungulia kutoka mawinguni kwenye mnara wa babel, etc. Waislamu nao wakaja na mbingu Saba sijui. Anyways wazungu wametengeneza ndege na rocket zimeenda mawinguni, nje ya dunia, mpaka mwezini. Sasa hivi watu wa dini wanasema yupo nje ya ulimwengu.

So nikagundua trend, wanamficha, wanamweka mbali ili watu wasiweze kumfikia, why? Kwa sababu hayupo? Kwa sababu hajasema hizo sheria? Why wanamficha. Afu wanakuambia anataka uamini yupo ndo utapona usipoamini unaunguzwa. Ukiuliza nikimwona afu nikamwamini, anasema no, lazma usimwone ndo uamini. Na wanaweka kifo mwisho wa kumuani ili waweze kuendelea kutunga sheria kwa jina lake na kuweza kuendelea kutawala watu kwa sababu hamna mtu Ashawahi kurudi akasema baada ya kifo kipo hivi.

Mwanasayansi mi nauliza Mbinguni Kuna Nini. Hamna njaa hamna maumivu hamna ndoa hamna chochote zaidi ya kumuabudu Mungu. Watu kanisani na msikitini hawapendi kwenda unategemea watapenda milele ya Ibada. So wakaamua kuanzisha motoni kutishia watu kwamba wataunguzwa milele. Sasa, ukifa unaacha mwili wako hapa, wanasema una roho, roho ni Nini, hoo mawazo sijui pumzi, ukiuliza unajua kazi ya ubongo ni Nini mtu hajui, haya tufanye roho ni ka upepo kanaenda motoni ehe kanaunguaje, hakana nyama, hakana nervous system hakana ngozi, hakana pain receptors, hakana ubongo au spinal cord, maumivu unayasikiaje, na bado hatujauliza huu Moto upo wapi, walisemaga chini kisa mavolcano lakini now hawasemi Tena coz of elimu.

Tukienda kwenye sheria zenyewe sijui usivae nguo tofauti, usile shellfish, usichanganye mazao, usimwage nje, usiabudu sanamu lakini abudu kitu Cha kufikiriwa na myahudi, hivi kwa Nini mtu atengeneze nyota billion 60 na sayari trillion afu aje kujali binadamu wewe ambae ni Kama vumbi kwa huu ulimwengu unamwaga wapi. Na kwa Nini sheria hizi zinaonekana Kama sheria za kabila ya la zamani huko kwenye majangwa na haziendani na sheria za binadamu kuishi na watu vizuri. Na Wanavyosema tumuabudu siku ya Saba.

Siku zimekuja kutengenezewa baadae Sana na zimebadilika badilika Mara kwa Mara katika historia ya Mayans na Romans. Na wamechagua sun day coz ni siku ya pagans kuabudu jua. Ila yote haya tuyaache, why Mungu muweza yote anataka hela, mwisho wa siku wote mnabidi mgundue kuwa binadamu walitengeneza miungu ili kujibu maswali magumu yasiyojibika kipindi kile na ku
Kwa tafsiri ya kawaida Mungu ni uwezo mkuu usiyowezwa.
Ikiwa akili yako na imani yako haiwezi kuelewa au kujua uwepo wa Mungu ni tatizo lako binafsi. Kuleta mjadala wa Mungu pasina elimu ni sawa na kukanusha, hivyo basi ni bora ufanye juhudi ya makusudi na nia thabiti kuwaendea wale wabobezi katika masuala ya kiroho huwenda ukapata majibu ya maswali yako. Kama upo serious. Ikiwa unataka kufurahisha barza kwa kweli mada hiyo ibadilishe tafuta mada nyingine.
 
Imani hailazimishwi pia nilisema kuna sababu za kuamini, ila wewe unakimbilia uthibitisho kama silaha na kinga kwa dhana ya kwamba huyu nikimwambia uthibitisho hawezi kutoa hivyo inakuwa nachokisema mimi ndio sahihi na yeye hata atoe hoja gani siikubali kwa sababu hawezi kuthibitisha inakuwa ni uongo.
Ndio...coz ukisema una Imani ya Mungu wa Biblia unakuwa hujajibu swali la kwa Nini umechagua Imani hio na sio vitu kibao vingine ambavyo umeacha kuamini, why Mungu umempa special treatment
 
Ukijiamini wewe tayari ushaamini wanachokiita Mungu ,ili ujue sasa inabdi ujijue wewe ni nani ? Umetoka wap na utaenda wap.
Sasa Kama haya majibu Sina ndo nitunge story au niamini story? Mi ndo naamua Mimi ni nani na ninaenda wapi, na nimetoka tumboni kwa mama angu
 
Ushahidi wa wireless communication tunaona from telephones, television na internet, haya ushahidi wa roho na mapepo uko wapi
 
Kwa tafsiri ya kawaida Mungu ni uwezo mkuu usiyowezwa.
Ikiwa akili yako na imani yako haiwezi kuelewa au kujua uwepo wa Mungu ni tatizo lako binafsi. Kuleta mjadala wa Mungu pasina elimu ni sawa na kukanusha, hivyo basi ni bora ufanye juhudi ya makusudi na nia thabiti kuwaendea wale wabobezi katika masuala ya kiroho huwenda ukapata majibu ya maswali yako. Kama upo serious. Ikiwa unataka kufurahisha barza kwa kweli mada hiyo ibadilishe tafuta mada nyingine.
Nimefanya tafiti nimeona Mungu anayeaminiwa hawezi kuwepo coz Hana logical consistency kwenye sifa zake
 
Kuna mtu alisema ubongo ni receiver tu, kuna master brain ipo ambayo inatunza kumbukumbu zako na ikifika siku ya mwisho ndo tutajua hatujui pale utakaposhangaa una mwili mpya na ubongo mpya usioungua ukaisha ila maumivu hayazoeleki.

INASIKITISHA MNO.

Na Mungu akikuchoma anafaidi nini.
 
Hayo mambo yapo. Shetani yupo, na Mungu Yupo, lakini Mungu anao uweza wote.

Wanaobisha ni kwa sababu ama hawajahusishwa kukutana na hayo mazingits au wanakusudia kufanya hivyo kwa lengo la kuwapotosha wasio na ufahamu sahihi.

Matukio ya kishirikina na ya Mungu pia yanafahamika kote duniani, kuanzia Afrika, Ulaya, Amerika na Asia, n.k.

Kipindi Magufuli akiwa Rais, alisimulia tukio lililotokea alipokuwa Waziri wa Ujenzi. Kulikuwa na ujenzi wa daraja pande za Sumbawanga ambapo kila daraja liliposetiwa, setting ilibadilika tofauti na ilivyosetiwa. Tukio hilo liliwafanya maingeneer kuogopa kuendelea na kazi maeneo hayo, ikabidi Magufuli na baadhi ya viongozi kwenda kuonana na wazee wa huo ukanda, na baada ya kufuata masharti yao, ndipo zoezi lilipoweza kuendelea.

Ushirikina upo, na Mungu yupo. Ni wazi kuwa kilichokuwa kikiwakwamisha hao mainjinia ni nguvu za giza, na tatizo likatatuliwa kwa nguvu za giza vile vile.


Mwaka fulani, tulienda Singi
 
Ndio hata huko kwa wazungu wenye elimu na maendeleo pia wapo wenye kuamini Miujiza,uchawi,malaika na majini.

Wapo ambao kazi zao zenye kuingiza kipato ndio zinahusu mambo hayo kwa huku tunaweza kuita waganga, kuna mavitabu kibao yenye kuzungumzia hayo mambo.
Kabisaa! Marekani ni Taifa lililoendelea, lakini masuala ya Imani ya Kimungu na ya kishirikina zingalipo.

Katika ushirikina wapo juu sana, mpaka kuna mahekalu ya waabudu Shetani, tena yaliyosajiliwa Kisheria.

Wanaomwamini Mungu wapo wengi sana.

Na katika uchumi na teknolojia, karibia kila mtu mwenye ufahamu anajua Marekani imeshapiga hatua sana.

Uchawi upo kila eneo, na imani ya kumwamini Mungu pia imetapakaa kila mahali.
 
Asante sana mkuu ubarikiwe sana,hizi mada kuhusu mungu inapaswa kuzipuuzwa,maana isije ikawa ni njama za shetani kutupeleka kwenye majaribu,maana wanga na wachawi wanatabia za kuleta mada kama hizi ili uteleze ujalibiwe wakuloge vizuri(kama freemason tunao waita wabudu shetani wanaa kipo kitu kinachoitwa supreme being) yeye ni nani asietambua uwepo wake,tuipuuze hii mada
 
Na ndio maana nakwambia sasa wapo madaktari kabisa ambao wanaamini Mungu na kuamini story zilizoelezwa kwenye vitabu vya dini.
Dr. Norman Vincent Peale, ameelezea kwenye Moja ya Vitabu vyake jinsi mtu mmoja alivyoshangaa kukuta Biblia kwenye ofisi y Daktari wa magonjwa ya akili.

Katika hali ya mshangaoy, na kwa nia ya kutaka kujiridhisha, alimwuliza huyo daktari kama na wao wanasoma Biblia!

Daktari alimjibu: "Kama watu wote wataisoma Biblia na kufuata maelekezo yake, madaktari wote tutaenda kufanya kazi ya kuvua samaki. Hatutakuwa na wagonjwa wa kuwatibu"
 
Nimefanya tafiti nimeona Mungu anayeaminiwa hawezi kuwepo coz Hana logical consistency kwenye sifa zake
Unaweza ukawa sahihi kutokana watu tofauti wana amini miungu tofauti, lakini Mungu ambaye ni Uwezo mkuu usiyowezwa huwezi kumjadili kwa kuwa yupo kinyume kabisa na sisi wanadamu tunavyomfikiria.
 
mpuuzieni huyo mtoa mada atakuwa mwanga au mchawi atawakufurisha bule, anadai hatambui uchawi,hajui majini,hatambui mungu, wakati daily watu wanapandisha mashetan,wana logwa, baasi naomba wachawi na wanga mliomo humu mumuloge ili kesho ajue uwepo wenu humu duniani kupitia nyinyi atatambua uwepo wa mungu alie hai.
 
Hujiulizi why vinatokea kigoma a place ambao Ina watu wenye low level of economic status na low level of education. Why not Moshi, dar, Arusha na bukoba. Why places za tanga, sumbawanga, shinyanga na kigoma places zenye watu wenye maisha duni na wasio na elimu
utakuwa mwanga na mchawi tu usinikufurishe na mungu wangu hujui nimepitia mangapi, we mwenye elimu ya kukalilishwa ubaon imekusaidia nini mpaka hapo ulipo,wenzako kupitia uchawi wamevumbua ndege lakin we usiku unapaa na ungo wa buku jelo
 
Hakuna nilichotenganisha katika hivyo vitu viwili kwa sababu sizungumzii habari za kwanini afrika hakuna maendeleo, nimeonyesha hayo ambayo wewe unayaaeleza.
Huelewi kwamba kukosa elimu ni moja ya sababu kubwa ya Africa kutokuwa na maendeleo?
 
1. Hujawahi panda basi lingine huwezi sema lako tu ndo zuri wakati wengine wamepanda mengine na wamefika.
2.vipi kuhusu Mimi ambae nishawahi kuwa mkristo mwana kanisa na mwana kwaya Ila baada ya kuisoma Biblia vizuri nikaona ni uwongo nikaacha
3. Hujajibu why hujasoma dini zingine Ila dini ya wazazi wako tu, wazazi wako wangekuwa waislamu ungesema hivyo hivyo kuhusu Quran
1. Basi ninalolifahamu ni lile nililolipanda. Elezea na wewe uzuri wa ulilolipanda ili nivutiwe kulipanda.

2. Wewe hujawahi kuwa Mkristo. Unajua maana ya kuwa Mkristo? Wewe hujawahi kuwa Mkristo.

Kuzaliwa kwenye familia ya Kikristo hakukufanyi kuwa Mkristo. Mkristo ni yule mwenye uhusiano binafsi na Kristo, na huwezi kuwa na uhusiano na usiyeamini kuwa Yupo. Kwa kuwa huamini kuwa Yupo, ni jibu dhahiri kuwa hujawahi kuwa Mkristo.

Kuimba Kwaya hakukufanyi kuwa Mkristo. Mtu yeyote anaweza kuigiza kuwa ni Mkristo na kumbe siyo. Mtu yeyote anaweza kuigiza ni mganga wa Kienyeji na kumbe siyo. Inawezekana na wewe uliigiza na ukafanikiwa.

Kuhudhuria Kanisani hakukufanyi kuwa Mkristo. Hata Mpagani, Mchawi, n.k. anaweza kuhudhuria Kanisani, na hata kuwa Mwanachama wa Kanisa husika, lakini hilo kamwe halimfanyi kuwa Mkristo.

Nifahamuvyo, nyumba za Ibada zipo wazi kwa kila anayetaka kuhudhuria. Au wewe kuna mahali popote ulikokuta zuio la watu wasio washirika wa dini fulani kuhudhuria ibada kwenye nyumba ya ibada isiyo ya dini yao?

Ninakosali kwa mfano, wanakaribishwa watu wa kila aina: wanaomwamini Mungu, wasiomwamini Mungu, wachawi, walevi, wazinzi, n.k. Tena, huwa ni furaha pale wasiomwamini Mungu wanapofika ibadani kwa sababu tunajua huenda wataisikia KWELI itakayowaweka huru.

Na wewe ninakukaribisha, siyo kujiunga, bali kusikiliza mahubiri. Ukivutiwa kumwamini Yesu ili nawe uwe Mkristo, unakaribishwa. Kama utataka kujiunga, milango iko wazi.

Labda uliowasikia wakimwelezea Mungu hawakukuelezea kwa ufasaha. Karibu! Huenda kiu yako itatoshelezwa.

3. Mimi sijasoma dini yoyote. Sijasoma Theolojia, wala Bible Knowledge au Divinity. Nilipokuwa A Level, nilijiandikisha kwenye darasa la Divinity, lakini nilipogundua kuwa somo lenyewe halinisaidii kumjua Mungu zaidi, niliachana nalo.

Nilizaliwa kwenye familia ya kipagani. Niliamua mwenyewe kuwa Mkristo baada ya kuona utofauti wa maisha ya Mkristo na ya wasiokuwa Wakristo. Nolivutowa na maisha ya Wakristo.

Tokea niwe Mkristo, nimejiridhisha pasipo shaka , kuwa Mungu Yupo, ananijua kwa jina langu, ananipenda, anao uwezo usiopimika, n.k. Nimejihakikishia mwenyewe. Sukuambiwa na mtu.

Kwanza, niliisoma kwenye Biblia. Pili, nikaamini. Nilipochukua hatua sawasawa na Imani, matokeo yakadhihirika.

Zaidi ya hayo, Mungu hana upendeleo. Ukiamua, atajidhihirisha na kwako pia.
 
Sio elimu ya darasani ya kujua mitochondria is the powerhouse of the cell, elimu ya kureason na logic na kugenerate ideas, hamna scientific discoveries au philosophical ideas za mtanzania, si kazi yetu ni kusoma kilichogunduliwa na wenzetu so huwezi linganisha elimu yetu na ya kwao
Nani kalinganisha elimu? Unaanza kunichosha mkuu,we kuwa na amani wala mimi sitaki kuwashusha utukufu unaouona kwa wazungu.
 
Back
Top Bottom