GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Mungu aliiumba dunia safi isiyo na dhambi, akamkabidhi mwanadamu aitawale kwa niaba Yake. Kwa maneno mengine, Mungu alimfanya mwanadamu kuwa mungu wa dunia hii. Kila kitu alikiweka chini yake. Alimpa mwanadamu mamlaka kamili juu ya ulimwengu wote. Zaburi 115:16.Hivyo ni visingizio ili usikosoe dini, Mara hoo Mungu hachunguzwi, 🤣ujinga mtupu...kiumbe chenye nguvu kuliko kingetengeneza dunia isiyo na dhambi na shida, na Kama anatujali na anajua yote hamna haja ya kuumba watu afu awachome baadae, Mungu wa hivi ni wa kutungwa ili watu waogope watoe sadaka na kufata sheria za waliotunga, Mungu anajali unamwaga wapi kweli
Shetani alipofanikiwa kumdanganya mwanadamu, alimpindua Adamu kwenye nafasi yake ya kuwa mungu wa dunia hii, badala yake, yeye Shetani ndiyo akawa mungu wa dunia hii. 2Wakorintho 4:4.
Jehanamu haijaandaliwa kwa ajili ya mwanadamu. Ni kwa ajili ya Shetani. Ikiwa mwanadamu ataenda motoni, si kwa sababu Mungu kampeleka huko, ila kachagu yeye mwenyewe kwa kuamua kutokumwamini Mungu.
Kukataa kumwamini Mungu ni kuchagua kumfuata Shetani kwa hiari.
Mungu anawapenda watu wote, hata wanaokataa kumwamini. Japo kumkataa Mungu kutampelekea mtu kuishia Jehanamu ya milele, hakumfanyi Mungu kumchukia.
Mungu anayaheshimu maamuzi ya kila mtu. Ndiyo maana amemjulisha mwanadamu faida ya kumwamini Yeye na hasara ya kutokumwamini. Hampangii mtu, anachofanya ni kukujulisha faida na hasara na kukuacha uchague mwenyewe kumfuata kwa faida yako au kumkataa kwa hasara yako. Kumbukumbu la Torati 30:19-20.
Mungu hachomi watu. Mungu hapeleki watu motoni. Mtu akienda motoni ni kwa sababu kachagua yeye mwenyewe kwa kukataa kumwamini Mungu.