Mungu Yuko wapi?

Mungu aliiumba dunia safi isiyo na dhambi, akamkabidhi mwanadamu aitawale kwa niaba Yake. Kwa maneno mengine, Mungu alimfanya mwanadamu kuwa mungu wa dunia hii. Kila kitu alikiweka chini yake. Alimpa mwanadamu mamlaka kamili juu ya ulimwengu wote. Zaburi 115:16.

Shetani alipofanikiwa kumdanganya mwanadamu, alimpindua Adamu kwenye nafasi yake ya kuwa mungu wa dunia hii, badala yake, yeye Shetani ndiyo akawa mungu wa dunia hii. 2Wakorintho 4:4.

Jehanamu haijaandaliwa kwa ajili ya mwanadamu. Ni kwa ajili ya Shetani. Ikiwa mwanadamu ataenda motoni, si kwa sababu Mungu kampeleka huko, ila kachagu yeye mwenyewe kwa kuamua kutokumwamini Mungu.

Kukataa kumwamini Mungu ni kuchagua kumfuata Shetani kwa hiari.

Mungu anawapenda watu wote, hata wanaokataa kumwamini. Japo kumkataa Mungu kutampelekea mtu kuishia Jehanamu ya milele, hakumfanyi Mungu kumchukia.

Mungu anayaheshimu maamuzi ya kila mtu. Ndiyo maana amemjulisha mwanadamu faida ya kumwamini Yeye na hasara ya kutokumwamini. Hampangii mtu, anachofanya ni kukujulisha faida na hasara na kukuacha uchague mwenyewe kumfuata kwa faida yako au kumkataa kwa hasara yako. Kumbukumbu la Torati 30:19-20.

Mungu hachomi watu. Mungu hapeleki watu motoni. Mtu akienda motoni ni kwa sababu kachagua yeye mwenyewe kwa kukataa kumwamini Mungu.
 
Why we ndo unaamua nani mkristo wa kweli na sio wa kweli, we Kama nani, ni sawa na kusema Kama we hufaulu shule we sio mwanafunzi wa kweli, unalazimisha hoja yako iwe juu, we onja utamu hata watoto wadogo wamaenjoy kuambiwa wameokotwa baharini na wamenunuliwa dukani Ila wakikuwa wanajua ukweli wametoka wapi. Assume Mimi ndo nimekuwa kifikra nimeachana na story za kuambiwa na mababu
 
Ni viwango tu ndiyo vinatofautiana. Hata Dar , Arusha, Bukoba, Moshi n.k. kuna ushirikina na kuna wanaoamini katika Mungu.
 
Nimeteuliws na nani na lini kuwaainisha Wakristo wa Kweli na wasio wa Kweli?

Ni wapi nilikosema mimi ndiye ninayeamua nani Mkristo wa Kweli na kinyume chake?

Sijawahi kupewa hilo jukumu na wala sijawahi kusema nina hayo mamlaka.
 
1. Magonjwa hayatoki kwa Mungu? Ye anajua yote anaweza yote na anatupenda, why Kuna magonjwa? Kwa Nini hayazui?
2. Hiyo story ya Adam na Eve imetungwa kuelezea mambo yameanzaje na pia imeibwa ideas from epic of Gilgamesh ya mesapotemia na Pandora's box ya ugiriki na pia haina ushahidi wa kihistoria.
3. Madaktari mpaka wanalipwa mamillion kufanya upasuaji ni kwa sababu wagonjwa wanamshukuru Mungu badala ya kuwashukuru wao ambao wamesoma miaka 7 na kufanya upasuaji masaa 20 ili we upone, so ni Kama hasira coz anafanya kazi kubwa bila kupewa shukrani.
4. Mungu ni kama group partner ambae kazi unafanya wewe ukikosea anakulaumu ukipatia sifa anachukua yeye ni kama mpenzi ambae anakuonea(abusive husband)
 
Hiyo imeitofautishaje na Tanzania? What's the difference?
Marekani Kuna atheists wengi kuliko Tanzania. So kusema kwamba ni watu wa dini Sana it's not realistic coz kule mpaka wanakuwa na public debates kuhusu atheism na religion na atheists wanapewa freedom kutoa views zao.
 
Acha uwongo marekani sio taifa ka kidini na sheria zake hazifavour dini yoyote ndo maana ya 1st amendment kwenye katiba Yao. Ndo maana Wana ruhusu abortion, ushoga, pornography, etc coz wanavalue individual freedom na sio religion. Tanzania ni nchi ya kidini kuliko marekani in terms of sheria, ila tunatumia mwamvuli wa "utamaduni wetu" ili tusiseme tu tunafata dini. Marekani hawaruhusu kusali kwa lazima shuleni, na kuanzisha vipindi vya dini katika shule za serikali. Wazungu ambao wanafanya uvumbuzi katika Karne ya 21 ni wanasayansi ambao wengi hawana dini kwa sababu wametumia logic na reason kugundua kua dini zote ni story tu za kale za mababu wa jamii fulani na hamna moja special kuliko wenzako so wanazitreat Kama tamaduni tu na kuzipa heshima.
 
Mtafute daktari yeyote mwenye akili umwulize kuhusu Mungu. Naamini atakusaidia pa kubwa sana.
 
"Siyo kila anayemuamini Mungu yupo, anamwamini Mungu", Rudi la kwanza ujifunze kuandika ukimaliza ndo uje ueleweke naona unatype shit tu hapa
 
Wazinzi, walevi, wasengenyaji, Sehemu yao ni ziwa la moto. Haya ni maneno yangu?
Ni maneno ya Mungu? Una uhakika ni maneno ya Mungu na si maneno ya wayahudi wa kale waliosema hivyo ili kutishia na kutawala watu wafate sheria zao? Una uhakika Hilo ziwa la moto lipo?
 
Sijamtafiti Mungu coz hayupo, we umemtafiti Babu Christmas? Unajuaje hayupo? Nimetafiti story ambazo wanaziita ni za Mungu za dini tofauti tofauti. Angalia movie inaitwa religulous utaelewa.
 
According to ur story
1. Why Mungu ameumba Malaika ambae alijua beforehand atakuja kuwa shetani na atakuja kutesa watu, Kama kweli ni muweza yote mjua yote na mpenda wote asingeruhusu Hilo.
2. Kulikuwa na haja Gani ya kuweka matunda ambao angewakataza kula na anajua watakula afu awaadhibu wao na uzao wao. Ni sawa na mwalimu ampe mtoto mtihani mgumu ambao anajua atafeli afu ampe adhabu Kali
3. Shetani alikuwa anafanya Nini katika bustani Ile, Mungu mweza yote na mjua yote asingeruhusu Hilo ni either alikuwa Hana Nia njema na binadamu au alikuwa Hana uwezo wa kumzidi shetani.
4. Why Mungu awaadhibu uzao mzima kwa kosa la watu wawili. Je Ni haki Kama baba kaua na wewe ukizaliwa unyogwe pia?
5. No matter how u look at it hii story haimake sense kwa akili ya kawaida ndo maana wakristo wengine hukimbilia kusema ni mafumbo
 
Nimeteuliws na nani na lini kuwaainisha Wakristo wa Kweli na wasio wa Kweli?

Ni wapi nilikosema mimi ndiye ninayeamua nani Mkristo wa Kweli na kinyume chake?

Sijawahi kupewa hilo jukumu na wala sijawahi kusema nina hayo mamlaka.
Basi usiseme kwamba huyu mkristo wa kweli huyu sio ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…