Mungu Yuko wapi?

Nani kakupa wewe cheo cha kuamua point ni ipi?

Hujathibitisha Mungu yupo.

Hujaondoa contradictions zilizopo katika dhana ya kuwapo Mungu.

Kwa sababu Mungu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo na ondoa contradictions hizo.
Mimi ndio niliyoleta hiyo hoja ya kuhusu hao waarabu na utajiri na point yangu ni huko kuwa matajiri na wanaamini Mungu, sasa wewe unaleta habari za sijui utajiri wao ni kwa sababu ya mafuta mara sijui ni utajiri wa bahati. Point haikuwa jinsi walivyoupata utajiri bali ni huo utajiri wenyewe.

Kama ushahitimisha kwa kusema kwa uhakika kabisa kuwa hakuna Mungu, sasa kuondoa contradictions ndio kutafanya Mungu awepo?
 
Usihame hame nje ya hoja. Narudia, inaanza imani ya uwepo wa MUNGU kisha inafuata dini. Hakuna unafiki wala uongo hapo zaidi ya akili yako kuona kiini cha hoja "Imani ya uwepo wa MUNGU" dini na aina za dini zinafuata baada ya hiyo imani.

Unaweza futa dini kwa kuibadili na dini nyingine ila huwezi futa imani ya uwepo wa MUNGU kwa udhaifu wa dini. Imani ya uwepo wa MUNGU itafutwa kwa kujibu maswali yaliyosababisha uwepo wa hiyo imani.

Ulimwengu ni nini?

Chanzo chake ni nini?

Hatma yake ni nini?

Kifo ni nini?

Kama huna majibu yasiyo na shaka kuhusu hayo maswali watu hawawezi fata porojo zako wakaachana na imani ya uwepo wa MUNGU just sababu unadhani una maarifa kuliko mababu walioturithisha hiyo imani.

Suala la wahindi na ng'ombe ni mfano bila kujali uhalisia wake halisi, ni jambo ambalo ulipaswa kuliona kiwepesi tu, nia haikuwa kutoa elimu sahihi ya mungu wa wahindi.
 
Mungu yuko Ulaya.
 
Acha bangi mkuu.
 
Of course Biblia itasema Kuna watu hawataamini story zake, coz walioandika walijua story zao haziaminiki. Ni sawa nitengeneze thread afu niseme watu wataniponda, afu watu waniponde kweli nijiite mtabiri na mkweli. Nipe hoja sio hekaya
Ni wachache sana tunao kuelewa.
Wana mistari yao ya vitisho,utasikia ;
OLE
OLE
OLE
OLE.
 
Kwamba Musa na Zumaridi lao moja 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Unamuabudu kakuambia umuabudu au mwarabu/myahudi/mrumi kakuambia umuabudu ili achukue hela zako na aendeshe maisha yako na anatumia story za Mungu Kama kivuli na kukuambia usiulize maswali utaunguzwa na we unakubali ka mtoto muoga
Myunani,Mrumi,Myahudi na Mwarabu, hawa watu wana tutumia sana kutangaza vivutio vyao vya utalii huku tukilipia fedha ili tuvitangaze ndani ya majengo (kanisani na misikitini) wanaita sadaka na zaka. Ni unyonyaji wa viwango vya juu sana.
 
Aliyejibu hayo maswali ni nani na majibu aliyatoa wapi? Mnatishwa sana na mnatishika sana.
 
Sasa kama kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na matajiri wakubwa sana na masikini wa kutupwa, by mere chance of geography?

Huoni hiyo tu kuwa ni contradiction inayoonesha Mungu huyo hayupo?
 
Aliyejibu hayo maswali ni nani na majibu aliyatoa wapi? Mnatishwa sana na mnatishika sana.
Anatishwa nani na nini? Ni uchaguzi wa njia tu hakuna matisho. Aliyechagua kuamini uwepo wa MUNGU sababu hajui majibu ya hayo maswali anafanana na wewe unayejiamini kwa elimu unayosoma soma ya wazungu ambayo haijakupa majibu ya hayo maswali.

Tofauti yenu ni moja tu, wewe unajiamini kupita kiasi au ni muoga kupita kiasi.
 
Na Astaghfirullah, Mussa ni Nabii wa Allah kua na heshima.

Chunga maneno yako,
 
Unamuamini mzungu ktk jina lingine eti Mungu lkn unaponda elimu aliyokupa ili ujikwamue.
Ama kweli nyani haoni kundule.
 
Unamuamini mzungu ktk jina lingine eti Mungu lkn unaponda elimu aliyokupa ili ujikwamue.
Ama kweli nyani haoni kundule.
Imani ya uwepo wa MUNGU haijaletwa na mzungu. Elimu ya hiyo imani ilikuwepo kabla mzungu hajafika Tanganyika. Dini ya biblia ndiyo iliyoletwa na mzungu.

Hakuna sehemu nimeponda elimu inayotolewa na mzungu. Mtu akisema elimu unayosoma soma ya wazungu maana yake ni kaiponda elimu ya wazungu? Kuna tatizo la kutafsiri hoja.
 
Unamuamini mzungu ktk jina lingine eti Mungu lkn unaponda elimu aliyokupa ili ujikwamue.
Ama kweli nyani haoni kundule.
 
Wewe unamzungumzia Mungu wa kabla ya ujio wa dini ya biblia au wa baada ya ujio wa dini ya biblia?
 
Hizo akili zenu siwezi ziita za kijasiri kwa kumhoji Uwepo wa Mungu bali ni mawazo ya waliyokata tamaa.
Nani aliyekwambia kwamba Mungu ni kiumbe?
Nani aliyekwambia Mungu ameumba dunia isiyo na dhambi wala shida?
Kwenye utafiti wako umeshindwa hata kusoma Mathayo 13:24?
Je unajua nini maana na kusudio la sadaka?
Tatizo tunashindwa kutofautisha kati ya ukweli na uongo, haki na batili katika dini zetu, kwani kuna watu wengi wanaotumia imani za dini kwa kujinufaisha kiuchumi.
Critical thinker huwa hapingi uwepo wa Mungu bali anapinga aina ya miungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…