Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Nazungumzia uwepo wa imani ya MUNGU bila kujali matokeo yake ikiwemo kuzaliwa kwa dini. Dini zote zinatokana na imani ya uwepo wa MUNGU. Ukishasema yupo MUNGU, swali linalokuja ni ana sifa zipi?. Hili swali ndilo linalozaa dini.Wewe unamzungumzia Mungu wa kabla ya ujio wa dini ya biblia au wa baada ya ujio wa dini ya biblia?
Sasa kamwe udhaifu wa dini hauwezi futa imani ya uwepo wa MUNGU. Wewe hujiulizi? Kwanini dunia nzima binadamu wamerithishwa imani ya uwepo wa MUNGU ila tofauti ni sifa zake tu? Wanakubaliana yupo MUNGU halafu linapokuja swali la ana sifa zipi ndipo kutokukubaliana kunapokuja na ndipo dini zinapozaliwa.
Sasa ukisema MUNGU wa wakristo hayupo ila kuna konokono mawinguni ndiye mungu sababu anateleza na kuna siku aliteleza ndo akasababisha dunia iwepo hizo ni hoja za dini ambazo sitaki kujikita huko, mimi hoja yangu ni kiini cha imani ya UWEPO WA MUNGU, ukisema hakuna MUNGU swali litakalofata ni kuna nini? Maana umeamua kufuta urithi wa imani ya uwepo wake tangu enzi na enzi za mababu zetu. Sasa huwezi futa hiyo historia ya imani kwa bla bla tu. Lazima uwe na sababu zenye uhalisia na maana kushinda imani ya uwepo wake iliyoishi karne na karne.
Huwezi chukua udhaifu wa dini katika kueleza sifa za MUNGU ukautumia kufuta imani ya uwepo wake. Imani ya uwepo wake itafutwa na sababu za msingi zilizosababisha uwepo wa imani kuwa yupo iwepo. Jambo ambalo hakuna aliyeweza kulifanikisha mpaka sasa.