Mungu Yuko wapi?

Mungu Yuko wapi?

Wewe unamzungumzia Mungu wa kabla ya ujio wa dini ya biblia au wa baada ya ujio wa dini ya biblia?
Nazungumzia uwepo wa imani ya MUNGU bila kujali matokeo yake ikiwemo kuzaliwa kwa dini. Dini zote zinatokana na imani ya uwepo wa MUNGU. Ukishasema yupo MUNGU, swali linalokuja ni ana sifa zipi?. Hili swali ndilo linalozaa dini.

Sasa kamwe udhaifu wa dini hauwezi futa imani ya uwepo wa MUNGU. Wewe hujiulizi? Kwanini dunia nzima binadamu wamerithishwa imani ya uwepo wa MUNGU ila tofauti ni sifa zake tu? Wanakubaliana yupo MUNGU halafu linapokuja swali la ana sifa zipi ndipo kutokukubaliana kunapokuja na ndipo dini zinapozaliwa.

Sasa ukisema MUNGU wa wakristo hayupo ila kuna konokono mawinguni ndiye mungu sababu anateleza na kuna siku aliteleza ndo akasababisha dunia iwepo hizo ni hoja za dini ambazo sitaki kujikita huko, mimi hoja yangu ni kiini cha imani ya UWEPO WA MUNGU, ukisema hakuna MUNGU swali litakalofata ni kuna nini? Maana umeamua kufuta urithi wa imani ya uwepo wake tangu enzi na enzi za mababu zetu. Sasa huwezi futa hiyo historia ya imani kwa bla bla tu. Lazima uwe na sababu zenye uhalisia na maana kushinda imani ya uwepo wake iliyoishi karne na karne.

Huwezi chukua udhaifu wa dini katika kueleza sifa za MUNGU ukautumia kufuta imani ya uwepo wake. Imani ya uwepo wake itafutwa na sababu za msingi zilizosababisha uwepo wa imani kuwa yupo iwepo. Jambo ambalo hakuna aliyeweza kulifanikisha mpaka sasa.
 
Usihame hame nje ya hoja. Narudia, inaanza imani ya uwepo wa MUNGU kisha inafuata dini. Hakuna unafiki wala uongo hapo zaidi ya akili yako kuona kiini cha hoja "Imani ya uwepo wa MUNGU" dini na aina za dini zinafuata baada ya hiyo imani.

Unaweza futa dini kwa kuibadili na dini nyingine ila huwezi futa imani ya uwepo wa MUNGU kwa udhaifu wa dini. Imani ya uwepo wa MUNGU itafutwa kwa kujibu maswali yaliyosababisha uwepo wa hiyo imani.

Ulimwengu ni nini?

Chanzo chake ni nini?

Hatma yake ni nini?

Kifo ni nini?

Kama huna majibu yasiyo na shaka kuhusu hayo maswali watu hawawezi fata porojo zako wakaachana na imani ya uwepo wa MUNGU just sababu unadhani una maarifa kuliko mababu walioturithisha hiyo imani.

Suala la wahindi na ng'ombe ni mfano bila kujali uhalisia wake halisi, ni jambo ambalo ulipaswa kuliona kiwepesi tu, nia haikuwa kutoa elimu sahihi ya mungu wa wahindi.
Okay so why uamini Mungu yupo, Kuna umuhimu gani, na kwa vigezo vipi alivyokupa? Naomba ujibu haya maswali bila kutumia dini
 
Hizo akili zenu siwezi ziita za kijasiri kwa kumhoji Uwepo wa Mungu bali ni mawazo ya waliyokata tamaa.
Nani aliyekwambia kwamba Mungu ni kiumbe?
Nani aliyekwambia Mungu ameumba dunia isiyo na dhambi wala shida?
Kwenye utafiti wako umeshindwa hata kusoma Mathayo 13:24?
Je unajua nini maana na kusudio la sadaka?
Tatizo tunashindwa kutofautisha kati ya ukweli na uongo, haki na batili katika dini zetu, kwani kuna watu wengi wanaotumia imani za dini kwa kujinufaisha kiuchumi.
Critical thinker huwa hapingi uwepo wa Mungu bali anapinga aina ya miungu.
Sasa why unaniletea mathayo badala kuniletea Aya za Quran? Why umechagua Mungu wa Biblia na sio wa Quran au wa kihindi au kipersia
 
Nazungumzia uwepo wa imani ya MUNGU bila kujali matokeo yake ikiwemo kuzaliwa kwa dini. Dini zote zinatokana na imani ya uwepo wa MUNGU. Ukishasema yupo MUNGU, swali linalokuja ni ana sifa zipi?. Hili swali ndilo linalozaa dini.

Sasa kamwe udhaifu wa dini hauwezi futa imani ya uwepo wa MUNGU. Wewe hujiulizi? Kwanini dunia nzima binadamu wamerithishwa imani ya uwepo wa MUNGU ila tofauti ni sifa zake tu? Wanakubaliana yupo MUNGU halafu linapokuja swali la ana sifa zipi ndipo kutokukubaliana kunapokuja na ndipo dini zinapozaliwa.

Sasa ukisema MUNGU wa wakristo hayupo ila kuna konokono mawinguni ndiye mungu sababu anateleza na kuna siku aliteleza ndo akasababisha dunia iwepo hizo ni hoja za dini ambazo sitaki kujikita huko, mimi hoja yangu ni kiini cha imani ya UWEPO WA MUNGU, ukisema hakuna MUNGU swali litakalofata ni kuna nini? Maana umeamua kufuta urithi wa imani ya uwepo wake tangu enzi na enzi za mababu zetu. Sasa huwezi futa hiyo historia ya imani kwa bla bla tu. Lazima uwe na sababu zenye uhalisia na maana kushinda imani ya uwepo wake iliyoishi karne na karne.

Huwezi chukua udhaifu wa dini katika kueleza sifa za MUNGU ukautumia kufuta imani ya uwepo wake. Imani ya uwepo wake itafutwa na sababu za msingi zilizosababisha uwepo wa imani kuwa yupo iwepo. Jambo ambalo hakuna aliyeweza kulifanikisha mpaka sasa.
Okay Kuna uthibitisho gani kuwa Kuna Mungu. Mababu zetu wakiamini dunia ni flat na jua linazunguka dunia lakini wanasayansi wakagundua tofauti. Je tungeamua kushika tu vya Babu zetu Leo hii tungekuwa wapi. Ndo maana wazungu wanaendelea kifikra na kiuchumi kwa sababu wanataka mabadiliko, we unalazimisha uwe Kama Babu yake Babu yako ndo maana hutagundua kitu unataka tu upewe vya watu usifikirie vya kwako ndo tofauti. We Kama Mungu yupo mlete, mi sijui Kama yupo au hayupo, jibu langu ni sijui, we unayesema yupo na unajua yupo, mlete.
 
Myunani,Mrumi,Myahudi na Mwarabu, hawa watu wana tutumia sana kutangaza vivutio vyao vya utalii huku tukilipia fedha ili tuvitangaze ndani ya majengo (kanisani na misikitini) wanaita sadaka na zaka. Ni unyonyaji wa viwango vya juu sana.
Yaani Mungu atengeneze sayari nyingi nyota billions afu aumbe mtu ili aende jangwani kupata haraka(mecca) afu na watu wanaamini
 
Anatishwa nani na nini? Ni uchaguzi wa njia tu hakuna matisho. Aliyechagua kuamini uwepo wa MUNGU sababu hajui majibu ya hayo maswali anafanana na wewe unayejiamini kwa elimu unayosoma soma ya wazungu ambayo haijakupa majibu ya hayo maswali.

Tofauti yenu ni moja tu, wewe unajiamini kupita kiasi au ni muoga kupita kiasi.
We ndo unajiamini kusema Mungu yupo bila ushahidi. Leo hii Nikisema wewe ni shoga, afu watu wote wakasema wewe ni shoga, wakaandika vitabu kuwa wewe ni shoga, wakachora mabango kwamba we ni shoga, je utakuwa shoga ghafla coz ya vyote hivyo, No. Reality doesn't care wat u believe, watu wanaweza amini mtu ni mchawi, mtu ni mwizi, lakini Kama sio haitobadilisha chochote, so we kuamini Mungu yupo haimaanishi yupo, mi naweza amini Babu Christmas yupo na nikasoma vitabu kuhusu yeye na kuhadithia story zake lakini haimaanishi Kama yupo even though hamna ushahidi wa kusema yupo au hayupo
 
Na
Astaghfirullah, Mussa ni Nabii wa Allah kua na heshima.

Chunga maneno yako,
Musa mwenyewe historia inasema hajawahi kuishi, archaeology iliyofanyika Egypt na Israel inasema story yote ya Exodus haina uthibitisho wa kihistoria
 
Sasa why unaniletea mathayo badala kuniletea Aya za Quran? Why umechagua Mungu wa Biblia na sio wa Quran au wa kihindi au kipersia
I assumed you read Bible and not Quran, ndiyo maana nikakuletea mfano ndani ya kitabu kilicho familiar na wewe, kwani hata kwenye Quran kuna maandiko mengi yenye mfano huo.
 
Okay so why uamini Mungu yupo, Kuna umuhimu gani, na kwa vigezo vipi alivyokupa? Naomba ujibu haya maswali bila kutumia dini
Swali: Why uamini MUNGU yupo?

Jibu: Naamini MUNGU yupo sababu hakuna logical explanation yoyote yenye matumaini inayotoa majibu ya maswali haya.

Ulimwengu ni nini/Chanzo chake ni nini, hatma yake ni nini? Maisha ni nini? Kifo ni nini?

Swali: Kuna umuhimu gani?

Jibu: Tukiachana na faida za kiimani kuna faida muhimu nyingi, mfano Sheria za nchi hazitoshi kumpa binadamu sababu ya kuwa mwema, lazima yawepo matumaini nje ya sheria tunazojiwekea. Matumaini kwamba kuna sababu ya kuishi maisha mema zaidi ya sababu tulizozikuta hapa duniani yamesaidia serikali nyingi za binadamu na kuyafanya maisha yawe kama ulivyoyakuta. Jaribu kujenga picha ya jamii isiyo na hofu ya uwepo wa MUNGU halafu utaelewa ni kwanini historia ya imani ya uwepo wa MUNGU haikupuuzwa na mababu zako na ikarithishwa mpaka kizazi cha leo.

Swali: Kwa vigezo vipi alivyokupa?

Jibu: Hapa unataka kumfahamu MUNGU wangu, huu mjadala utakusababisha uingie kwenye kuihoji dini yangu. Kama hutaki kuhusisha dini,uliza maswali yasiyohusisha dini.
 
Okay Kuna uthibitisho gani kuwa Kuna Mungu. Mababu zetu wakiamini dunia ni flat na jua linazunguka dunia lakini wanasayansi wakagundua tofauti. Je tungeamua kushika tu vya Babu zetu Leo hii tungekuwa wapi. Ndo maana wazungu wanaendelea kifikra na kiuchumi kwa sababu wanataka mabadiliko, we unalazimisha uwe Kama Babu yake Babu yako ndo maana hutagundua kitu unataka tu upewe vya watu usifikirie vya kwako ndo tofauti. We Kama Mungu yupo mlete, mi sijui Kama yupo au hayupo, jibu langu ni sijui, we unayesema yupo na unajua yupo, mlete.
Mzungu kaendelea sababu anaamini hakuna MUNGU?

Unataka nikuletee MUNGU wa sifa zipi?

Unashindwa kutenganisha sababu za imani ya uwepo wa MUNGU na mungu wa dini fulani.
 
We ndo unajiamini kusema Mungu yupo bila ushahidi. Leo hii Nikisema wewe ni shoga, afu watu wote wakasema wewe ni shoga, wakaandika vitabu kuwa wewe ni shoga, wakachora mabango kwamba we ni shoga, je utakuwa shoga ghafla coz ya vyote hivyo, No. Reality doesn't care wat u believe, watu wanaweza amini mtu ni mchawi, mtu ni mwizi, lakini Kama sio haitobadilisha chochote, so we kuamini Mungu yupo haimaanishi yupo, mi naweza amini Babu Christmas yupo na nikasoma vitabu kuhusu yeye na kuhadithia story zake lakini haimaanishi Kama yupo even though hamna ushahidi wa kusema yupo au hayupo
Unaanza kupuyanga.
 
I assumed you read Bible and not Quran, ndiyo maana nikakuletea mfano ndani ya kitabu kilicho familiar na wewe, kwani hata kwenye Quran kuna maandiko mengi yenye mfano huo.
Nimesoma zote, so don't make assumptions, na pia uje na mifano ya kitabu Cha wahindi na story za kigiriki pia ndio nitakuelewa
 
Swali: Why uamini MUNGU yupo?

Jibu: Naamini MUNGU yupo sababu hakuna logical explanation yoyote yenye matumaini inayotoa majibu ya maswali haya.

Ulimwengu ni nini/Chanzo chake ni nini, hatma yake ni nini? Maisha ni nini? Kifo ni nini?

Swali: Kuna umuhimu gani?

Jibu: Tukiachana na faida za kiimani kuna faida muhimu nyingi, mfano Sheria za nchi hazitoshi kumpa binadamu sababu ya kuwa mwema, lazima yawepo matumaini nje ya sheria tunazojiwekea. Matumaini kwamba kuna sababu ya kuishi maisha mema zaidi ya sababu tulizozikuta hapa duniani yamesaidia serikali nyingi za binadamu na kuyafanya maisha yawe kama ulivyoyakuta. Jaribu kujenga picha ya jamii isiyo na hofu ya uwepo wa MUNGU halafu utaelewa ni kwanini historia ya imani ya uwepo wa MUNGU haikupuuzwa na mababu zako na ikarithishwa mpaka kizazi cha leo.

Swali: Kwa vigezo vipi alivyokupa?

Jibu: Hapa unataka kumfahamu MUNGU wangu, huu mjadala utakusababisha uingie kwenye kuihoji dini yangu. Kama hutaki kuhusisha dini,uliza maswali yasiyohusisha dini.
1. So kama hujui jibu la rais wa Nicaragua jibu lake atakuwa Mungu mpaka utakapopata jibu?
2. So wewe bila kuwa na dini ambayo inakuambia sheria za Mungu wa dini hiyo, kusingekuwa na sababu ya kutoua na kutoiba? So katiba za nchi zimeweka sheria ili kumfurahisha Mungu na sio kufaidisha watu? Sawa Kama we unahitaji wayahudi wakuambie usiuwe sawa, usiongee na Mimi kwa sababu umenionyesha kuwa we sio mtu mwema, unafanya mema kwa hope ya kupata kitu, huo ni unafki na Kama unaamini Mungu anajua yote na muweza yote, ataona hio nafsi yako na hatapendezwa na Hilo, so in the end of the day it's a lose lose
 
Mzungu kaendelea sababu anaamini hakuna MUNGU?

Unataka nikuletee MUNGU wa sifa zipi?

Unashindwa kutenganisha sababu za imani ya uwepo wa MUNGU na mungu wa dini fulani.
Huwezi sema Imani na dini ni vitu tofauti kitendo Cha kuamini Mungu yupo ni kutokana na dini kukuambia yupo, ndo maana wewe una dini Fulani, huwezi tenganisha dini na Mungu. Soma general studies form 5 kwenye topic ya philosophy uone religion Ina comprise vitu gani, yaani tatizo elimu tunayo lakini tunasoma tujibu mtihani. Mtu anaelimu Yake ya biology history physics chemistry GS Ila anaamini mapepo na mauchawi wenzetu wanasoma na wanavumbua magari machanjo ndege smartphone internet sisi tunasoma ili tufaulu mtihani tuwe na cheti tuajiriwe ofisini
 
Sasa kama kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na matajiri wakubwa sana na masikini wa kutupwa, by mere chance of geography?

Huoni hiyo tu kuwa ni contradiction inayoonesha Mungu huyo hayupo?
Nimekuuliza kama ushahitimisha kwa kusema kuwa hakuna Mungu sasa kuondoa hizo contradictions kutafanya Mungu awepo?
 
Back
Top Bottom