Mungu Yuko wapi?

Mungu Yuko wapi?

Sio mada nayojadili hapa.
Huu nao ni ujinga.

Huwezi kuona mstari unaounganisha umasikini na kukosa elimu, ambao unakwenda moja kwa moja pia kutoka kukosa elimu mpaka imani ya Mungu.

Imani ya Mungu => Kukosa elimu => Umasikini.

Huoni uhusiano huu?
 
Ndio...coz ukisema una Imani ya Mungu wa Biblia unakuwa hujajibu swali la kwa Nini umechagua Imani hio na sio vitu kibao vingine ambavyo umeacha kuamini, why Mungu umempa special treatment
Umekuta kuna mgawo wa vitu mbali mbali, tena vinatolewa bure! Halafu unapewa uhuru wa kuchagua, ungechagua kipi?

Umeruhusiwa kuchagua kimojawapo kati ya hivi:

1. Chumvi kilo mia mbili

2. Pamba kilo mia

3. Sukari kilo themanini

4. Dhahabu safi kilo hamsini

5. Baiskeli mpya

Wewe ungechagua kipi?

Mimi nitachukua kilo hamsini za dhahabu. Kwa kilo hizo hamsini, naweza kuvipata na hivyo vyote vilivyoorodheshwa, na vingine vingi, ikiwa nitahitaji.

Ikiwa mtu amejiridhisha kuwa Mungu anayemwamini ni kila kitu, na ni zaidi ya Miungu mingine yote,ya nini kuhangaika tena na tumiungu tudogo?

Aliye na MUNGU MKUBWA hahitaji tumiungu. Mwenyezi Mungu ni kila kitu!
 
Kabisaa! Marekani ni Taifa lililoendelea, lakini masuala ya Imani ya Kimungu na ya kishirikina zingalipo.

Katika ushirikina wapo juu sana, mpaka kuna mahekalu ya waabudu Shetani, tena yaliyosajiliwa Kisheria.

Wanaomwamini Mungu wapo wengi sana.

Na katika uchumi na teknolojia, karibia kila mtu mwenye ufahamu anajua Marekani imeshapiga hatua sana.

Uchawi upo kila eneo, na imani ya kumwamini Mungu pia imetapakaa kila mahali.
Population ya watu wasio na dini Tanzania ni less than 1% wakati marekani wapo Kama 12% ya population na kumbuka population Yao ni kubwa Mara nne ya kwetu
 
Asante sana mkuu ubarikiwe sana,hizi mada kuhusu mungu inapaswa kuzipuuzwa,maana isije ikawa ni njama za shetani kutupeleka kwenye majaribu,maana wanga na wachawi wanatabia za kuleta mada kama hizi ili uteleze ujalibiwe wakuloge vizuri(kama freemason tunao waita wabudu shetani wanaa kipo kitu kinachoitwa supreme being) yeye ni nani asietambua uwepo wake,tuipuuze hii mada
Shetani Ashawahi kusema Mungu hayupo?, freemason Ashawahi kusema Mungu hayupo ? Shetani mwenyewe anataka watu wamjue Mungu ili wampinge. Shetani na Mungu ni story tu Kama movie zilivyokuwa na sterling na jambazi acha uwoga wa maisha Kama Mungu anapenda watu kwa Nini awachome, we unaweza mchoma mtoto wako moto, mmetishwa na makanisa ili muendelee kufata sheria zao na mtoe sadaka mwatajirishe
 
Dr. Norman Vincent Peale, ameelezea kwenye Moja ya Vitabu vyake jinsi mtu mmoja alivyoshangaa kukuta Biblia kwenye ofisi y Daktari wa magonjwa ya akili.

Katika hali ya mshangaoy, na kwa nia ya kutaka kujiridhisha, alimwuliza huyo daktari kama na wao wanasoma Biblia!

Daktari alimjibu: "Kama watu wote wataisoma Biblia na kufuata maelekezo yake, madaktari wote tutaenda kufanya kazi ya kuvua samaki. Hatutakuwa na wagonjwa wa kuwatibu"
Nielezee mtu kuzaliwa na cancer anakosa gani mpaka kaumwa🤣au mama ake hakuelewa biblia
 
Unaweza ukawa sahihi kutokana watu tofauti wana amini miungu tofauti, lakini Mungu ambaye ni Uwezo mkuu usiyowezwa huwezi kumjadili kwa kuwa yupo kinyume kabisa na sisi wanadamu tunavyomfikiria.
Hivyo ni visingizio ili usikosoe dini, Mara hoo Mungu hachunguzwi, 🤣ujinga mtupu...kiumbe chenye nguvu kuliko kingetengeneza dunia isiyo na dhambi na shida, na Kama anatujali na anajua yote hamna haja ya kuumba watu afu awachome baadae, Mungu wa hivi ni wa kutungwa ili watu waogope watoe sadaka na kufata sheria za waliotunga, Mungu anajali unamwaga wapi kweli
 
mpuuzieni huyo mtoa mada atakuwa mwanga au mchawi atawakufurisha bule, anadai hatambui uchawi,hajui majini,hatambui mungu, wakati daily watu wanapandisha mashetan,wana logwa, baasi naomba wachawi na wanga mliomo humu mumuloge ili kesho ajue uwepo wenu humu duniani kupitia nyinyi atatambua uwepo wa mungu alie hai.
Nilogeni hamna uchawi hamna majini hao wanasema mapepo sijui ni ukichaa tu waende milembe watibiwe🤣🤣🤣
 
utakuwa mwanga na mchawi tu usinikufurishe na mungu wangu hujui nimepitia mangapi, we mwenye elimu ya kukalilishwa ubaon imekusaidia nini mpaka hapo ulipo,wenzako kupitia uchawi wamevumbua ndege lakin we usiku unapaa na ungo wa buku jelo
🤣 Nitajie Sayansi aliyogundua mchawi.. wazungu wamegundua ndege marocket ya mwezini Ila Biblia zinatuambia Mungu yupo mawinguni, haya mbona tukipanda air tanzania tunavuka mawinguni hatumwoni au kajificha nje ya ulimwengu tusimpate
 
1. Basi ninalolifahamu ni lile nililolipanda. Elezea na wewe uzuri wa ulilolipanda ili nivutiwe kulipanda.

2. Wewe hujawahi kuwa Mkristo. Unajua maana ya kuwa Mkristo? Wewe hujawahi kuwa Mkristo.

Kuzaliwa kwenye familia ya Kikristo hakukufanyi kuwa Mkristo. Mkristo ni yule mwenye uhusiano binafsi na Kristo, na huwezi kuwa na uhusiano na usiyeamini kuwa Yupo. Kwa kuwa huamini kuwa Yupo, ni jibu dhahiri kuwa hujawahi kuwa Mkristo.

Kuimba Kwaya hakukufanyi kuwa Mkristo. Mtu yeyote anaweza kuigiza kuwa ni Mkristo na kumbe siyo. Mtu yeyote anaweza kuigiza ni mganga wa Kienyeji na kumbe siyo. Inawezekana na wewe uliigiza na ukafanikiwa.

Kuhudhuria Kanisani hakukufanyi kuwa Mkristo. Hata Mpagani, Mchawi, n.k. anaweza kuhudhuria Kanisani, na hata kuwa Mwanachama wa Kanisa husika, lakini hilo kamwe halimfanyi kuwa Mkristo.

Nifahamuvyo, nyumba za Ibada zipo wazi kwa kila anayetaka kuhudhuria. Au wewe kuna mahali popote ulikokuta zuio la watu wasio washirika wa dini fulani kuhudhuria ibada kwenye nyumba ya ibada isiyo ya dini yao?

Ninakosali kwa mfano, wanakaribishwa watu wa kila aina: wanaomwamini Mungu, wasiomwamini Mungu, wachawi, walevi, wazinzi, n.k. Tena, huwa ni furaha pale wasiomwamini Mungu wanapofika ibadani kwa sababu tunajua huenda wataisikia KWELI itakayowaweka huru.

Na wewe ninakukaribisha, siyo kujiunga, bali kusikiliza mahubiri. Ukivutiwa kumwamini Yesu ili nawe uwe Mkristo, unakaribishwa. Kama utataka kujiunga, milango iko wazi.

Labda uliowasikia wakimwelezea Mungu hawakukuelezea kwa ufasaha. Karibu! Huenda kiu yako itatoshelezwa.

3. Mimi sijasoma dini yoyote. Sijasoma Theolojia, wala Bible Knowledge au Divinity. Nilipokuwa A Level, nilijiandikisha kwenye darasa la Divinity, lakini nilipogundua kuwa somo lenyewe halinisaidii kumjua Mungu zaidi, niliachana nalo.

Nilizaliwa kwenye familia ya kipagani. Niliamua mwenyewe kuwa Mkristo baada ya kuona utofauti wa maisha ya Mkristo na ya wasiokuwa Wakristo. Nolivutowa na maisha ya Wakristo.

Tokea niwe Mkristo, nimejiridhisha pasipo shaka , kuwa Mungu Yupo, ananijua kwa jina langu, ananipenda, anao uwezo usiopimika, n.k. Nimejihakikishia mwenyewe. Sukuambiwa na mtu.

Kwanza, niliisoma kwenye Biblia. Pili, nikaamini. Nilipochukua hatua sawasawa na Imani, matokeo yakadhihirika.

Zaidi ya hayo, Mungu hana upendeleo. Ukiamua, atajidhihirisha na kwako pia.
1. Pagan means mtu ambaye ana dini tofauti na zinazojulikana, sio mtu asiye na dini
2. True Scotsman fallacy, unasema kitu ambacho mtu hawezi fanya afu mtu akianza kufanya unasema hakuwa mtu fulani. Hata kanisa lenyewe halijui mkristo wa ukweli ndo maana Kuna madhehebu elfu kumi kila mtu anakuja na ukristo wake so mkristo wa ukweli hajulikani. Ni sawa na kusema wachaga wote wanapenda hela afu akitokea mchaga asiyependa hela unasema ye sio mchaga ili kusupport theory yako. Atheists wengi walikuwa wanadini wakaamua kuifatilia kusoma Biblia zaidi kuuliza maswali kuhusu historia na logic kuhusu dini Yao wakagundua ni uwongo, ndo maana hoja za atheists Zina make sense Ila watu wanaogopa kukufuru coz wametishiwa moto ambao haupo, kusingekuwa na moto na mbingu hamna mtu angeamini story za Mungu wa Biblia
 
Population ya watu wasio na dini Tanzania ni less than 1% wakati marekani wapo Kama 12% ya population na kumbuka population Yao ni kubwa Mara nne ya kwetu
Hiyo umeitoa wapi kiongozi? Nimejaribu kucheki mtandaoni, ikasomankuwa kwa Marekani, atheist ni asilimia 4, kwa Tanzania, by 2020, takwimu zinazoonesha kuwa Christian ni asilimia 63.2, Islam asilimia 34.1, No Religion asilimia 1.5 na Traditional Religion ni asilimia 1.2.

Hata hivyo sijajua hoja yako hapo hasa ni ipi mkuu!

Kwamba Marekani imeendelea sana kwa sababu ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaomwamini Mungu?

Kunatofatianaje na Tanzania kwenye suala zima la Imani za kidini?
 
Nani kalinganisha elimu? Unaanza kunichosha mkuu,we kuwa na amani wala mimi sitaki kuwashusha utukufu unaouona kwa wazungu.
Mzungu katengeneza chanjo ya corona huku mnauombea uondoke mnadanganyana Mungu kaikoa nchi kwa corona kisa Ina dini kumbe watu kibao wanakufa na kuzikwa afu unasema we na mzungu mpo sawa kimaarifa, kamtawale basi
 
Hiyo umeitoa wapi kiongozi? Nimejaribu kucheki mtandaoni, ikasomankuwa kwa Marekani, atheist ni asilimia 4, kwa Tanzania, by 2020, takwimu zinazoonesha kuwa Christian ni asilimia 63.2, Islam asilimia 34.1, No Religion asilimia 1.5 na Traditional Religion ni asilimia 1.2.

Hata hivyo sijajua hoja yako hapo hasa ni ipi mkuu!

Kwamba Marekani imeendelea sana kwa sababu ya kuwa na idadi kubwa ya watu wanaomwamini Mungu?

Kunatofatianaje na Tanzania kwenye suala zima la Imani za kidini?
Asilimia kumi na mbili ya marekani hawana dini yoyote sijasema atheists elewa sawa
 
Back
Top Bottom