1. Pagan means mtu ambaye ana dini tofauti na zinazojulikana, sio mtu asiye na dini
2. True Scotsman fallacy, unasema kitu ambacho mtu hawezi fanya afu mtu akianza kufanya unasema hakuwa mtu fulani. Hata kanisa lenyewe halijui mkristo wa ukweli ndo maana Kuna madhehebu elfu kumi kila mtu anakuja na ukristo wake so mkristo wa ukweli hajulikani. Ni sawa na kusema wachaga wote wanapenda hela afu akitokea mchaga asiyependa hela unasema ye sio mchaga ili kusupport theory yako. Atheists wengi walikuwa wanadini wakaamua kuifatilia kusoma Biblia zaidi kuuliza maswali kuhusu historia na logic kuhusu dini Yao wakagundua ni uwongo, ndo maana hoja za atheists Zina make sense Ila watu wanaogopa kukufuru coz wametishiwa moto ambao haupo, kusingekuwa na moto na mbingu hamna mtu angeamini story za Mungu wa Biblia
Ni kweli, Mpagani si mtu asiye na dini, hata kuiabudu mizimu ni dini.
Ndiko nilikoanzia, kwenye dini ya asili. Kabla ya kuwa Mkristo, nilikuwa nikishiriki hata ibada za kipagani. Nakumbuka, nilishawahi kuhudhuria tukio ambalo kabla ya jambo lolote kufanyika, kulifanyika maombi kwanza. Maombi yalielekezwa kwa mti. Kwamba, mti ndiyo uliokuwa kama mungu.
Lakini baadaye nilikuja kugundua kuwa kuna Mungu MKUBWA kuliko mizimu ya mababu zetu. Nilipogundua hilo, niliamua kuachana na kamungu kadogoe na kumfuata MUNGU MKUU!!!
Kuwepo kwa madhehebu mengi si tatizo, muhimu tu wawe wanamwamini Kristo. Hata kukiwepo na madhehebu bilioni kumi, kama wanamwamini Kristo, wote watakuwa ni Wakristo.
Wakristo wa Kweli wanajulikana. Hata humu jukwaani, bila shaka, kuna nyuzi ambazo kwa kuzisoma tu, unajua huyo ni Mkristo au la.
Kwani wewe unashindwa kumfahamu Mkristo wa Kweli? Mbona ni rahisi tu! Hata Shetani hasumbuki kumtofautisha Mkristo wa Kweli na anayeuigiza Ukristo. Mkristo wa Kweli anafahamika, si makanisani tu, hata katika maeneo mengine. Imeandikwa, "Mtawatambua kwa matendo yao"
Hao waliogeka atheist mimi siwafahamu! Ukweli ni kuwa mtu akishaouonja utamu wa Kristo, hatatamani tena kitu kingine.
Kama kuna waliokuwa wakienda , labda makanisani lakini baadaye wakaamua kugeukia uatheist, ni kwa sababu hawajawahi kukutana na Mungu Halisi mioyoni mwao. Waliingia kwenye dini kwa kufuata mkumbo. Hawakumwamini Mungu!