Huwa siwaelewi mnapomkana Mungu na kuleta "problem of evil". hili swali nimelijibu katika uzi huu na kama hujaelewa nitarudia.
Kiranga , unaposema "problem of evil" huoni unafanya "assumption" zinazodai/zinazolazimu uwepo wa Mungu?
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" maishani mwako?
Soma zaidi hapa
Immanent critique - Wikipedia, the free encyclopedia
Kifupi, mimi kama sikubali kuna mungu, na wewe kama unasema kuna mungu, tukibishana wote kwa kusimamia pande zetu, hatutapata hata pa kuanzia.
Sasa kinachofanyika hapo, mimi naachana na position yangu ya kutokubali kwamba mungu yupo, kwa muda tu, ili kuangalia upande wako na mjadala uendelee.
Nasema, OK, tuseme mungu yupo, na ni mwenye ujuzi wote, na uwezo wote, na upendo wote. Tukubaliane kwamba hili ni kweli.
Swali linakuja tukishakubaliana hivyo.
Kama mungu yupo, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye upendo wote.
Kwa nini karuhusu iwezekane kuzaliwa watoto vilema?
Hii ni hesabu ya ku solve for x, ambapo katika ku solve for x, unafanya let x be y, halafu jibu utakalopata la x unaweza kuli verify.
Naona somo zima la "immanent critique" limekupitia mbali.
Mtu anaposema "let's say god exists, for the sake of carrying the ergument and analysis forward" hamaanishi kusema kwamba kakubali kwamba mungu yupo.
Unatofautishaje mema na mabaya katika ulimwengu ambao hakuna Mungu?
Kuna njia nyingi tu. Unaweza kuanza kwa kusema kwamba yale yote ambayo sipendi kutendewa ni mabaya, na yale yote ambayo napenda kutendewa ni mazuri.
Hapo hujamhitaji mungu.
Kwa mfano, mimi sipendi kuuawa, kwa hiyo hili ni baya kwangu, sipendi kufanyiwa, na sitaki kumfanyia mwingine.
Pia mimi napenda zawadi za Swiss watches, kwa hiyo hili ni jema, mtu akinifanyia nitapenda na mimi nitapenda kumpa mwingine.
Hapo tayari tushaona mema na mabaya ambayo hayamtegemei mungu.
Hebu ona hapa wanajadili "secular morality" ambayo haimuhitaji mungu
Secular morality - Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa hiyo kufikiri hakuna wema na ubaya nje ya mungu ni makosa, ni kama samaki kufikiria hakuna dunia isiyo na maji. Just because wewe umegubikwa katika bahari ya dini inayomtegemea mungu kwa kila kitu hilo halimaanishi hakuna watu wenye moral standards bila kumtegemea mungu
Msome Albert Einstein hapa
"A man's ethical behavior should be based effectually on sympathy, education, and social ties and needs; no religious basis is necessary. Man would indeed be in a poor way if he had to be restrained by fear of punishment and hopes of reward after death."
Albert Einstein, "Religion and Science," New York Times Magazine, 1930
Maana kusema tu "evil" una "imply" aina fulani ya sheria ya maadili (Moral Law) na hivyo Mtoa/Mtunga sheria hiyo (Mungu). Sasa kama wewe huamini kuwa Kuna Mungu, unatofautishaje kati ya zuri na baya? utuambie hili kwanza kabla hata hujauliza kuhusu "problem of evil". maana kama huwezi kutuambia tofauti ya jema na baya, then kwanini tuendelee zaidi ya hapo?
Einstein kakusaidia hapo jinsi ya kupata moral code ambayo haimtegemei mungu.
Wewe ulitaka afanyeje? atengeneze watu ambao hawana uhuru wa kuchagua? Kama angefanya unavyotaka unafikiri angekuwa ameumba watu kwa mfano wake? Unafikiri kuna upendo bila kuchagua?
Huu uongo wa "mungu ameacha mabaya kwa kuwa anapenda uhuru wa kuchagua" nilisha u debunk.
Kama mungu anapenda kuchagua mbona hajanipa uchaguzi wa kuamua nizaliwe katika dunia ya namna gani, nchi gani, kwa wazazi gani, niwe na genes gani etc? Mbona nimejikuta nimezaliwa tu? Huyu ni mungu anayependa tuwe na uhuru wa kuchagua kweli?
Imagine mke wako ukitaka akubusu anakubusu hata kama yeye hataki. Utakwenda mtaani kifua mbele kuwa kuna upendo kati yenu?
Kama anapenda sana uchaguzi, mbona hakunipa mimi uchaguzi wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe?
Mungu yuko sahihi kabisa kuumba ulimwengu wa namna hii na ndio maana Yesu ni mwanakondoo aliyechinjwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa. Hii ni kwa sababu Mungu aliamua (in his Sovereign choice) kuumba ulimwengu ambao si tu kwamba alijua maovu yanawezekana bali alijua pia Mwaadamu huyu ataasi. Na akaamua kuonyesha ni wa Upendo zaidi kwa kufanya njia ya kumwokoa toka katika uovu wake: Mpango ambao wewe
Kiranga unaukana leo hii.
Sasa mungu kaumba ulimwengu ambao anajua una maasi, na anajua kaumba wanadamu na udhaifu, makusudi, na kawawekea majaribu, na kajua kabisa wataasi, na kwa sababu kajua wataasi, na hawezi kukosea, hawawezi kuepuka kuasi.
Kwa maneno mengine kashawapangia kuasi.
Wakiasi atawalaumu?
Atawachoma moto kama wafanya dhambi? Wakati yeye mwenyewe ndiye aliyefanya kila jitihada kuhakikisha wanaasi?
Kaumba ulimwengu ambao uasi unawezekana, isitoshe kaweka vishawishi, isitoshe kawaumba binadamu dhaifu.
Binadamu wakiasi kosa ni la nani? Binadamu au mungu?
Kwa kuumba ulimwengu wa namna hii Mungu amedhihirisha upendo mkuu sana (Yohana 3)
Hapana.
Ukiwa software designer tu, halafu una uwezo wa kutengeneza software ya computer isiyo crash, lakini ukaamua tu kutengeneza software inferior inayocrash, unaweza kufukuzwa kazi. Hii ni standard ya kibinadamu tu.
Kwa nini mungu mwenye uwezo zaidi (mkuu) na ujuzi zaidi (mkuu) na upendo zaidi (mkuu) tumuwekee lower standards?
Simple! Kuna Magonjwa kwa sababu kuna dhambi. Kuna dhambi kwa sababu Mwanadamu aliamua kumwasi Mungu.
Uwezo wa mwanadamu kumuasi mungu mwanadamu aliutoa wapi? Mungu alipoumba ulimwengu kwa nini aliruhusu uasi uwezekanike?
Kama mungu kaumba ulimwengu na kuweka parameters zote, kwa nini aliruhusu parameters za ubaya kuwezekana?
Usiniambie kwa sababu alitaka mwanadamu awe na chaguo, kwa sababu mimi hakunipa chaguo nizaliwe au nisizaliwe, na nizaliwe wapi, vipi, niishije etc. Huyu si mungu anayependa viumbe wake wawe na chaguo
Mwanadamu alimwasi Mungu kwa sababu ya kutumia vibaya utashi wake.
Uwezo wa mwanadamu kutumia vibaya utashi wake umeumbwa na nani? Na kwa nini uliumbwa?
Mwanadamu alikuwa na utashi kwa sababu Mungu alimuumba na uwezo wa kuchagua.
Mimi mbona sikupewa uweza wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe? Katika tendo moja la kujamiiana kuna viini kama milioni mia mbili na nusu vinakufa ili kimoja tu kifanikiwe, kama mungu anapenda uchaguzi sana, mbona hivi vingine hajavipa uchaguzi wa kuishi?
Mungu alimuumba na uwezo wa kuchagua kwa sababu Mungu nu pendo.
Mbona mimi sijapewa uchaguzi kuamua nizaliwe au nisizaliwe? Na nizaliwe vipi? sehemu gani etc? Kama mungu kutoa uchaguzi ni upendo, sisi ambao hatujapata option kuchagua hatupendi.
Kwa hiyo "ultimately" kuna magonjwa kwa sababu kuna Mungu!
Alishindwa kuyazuia?
Unadhani kuna mahali popote ambapo ni sahihi kwa mtu kumbaka mtoto mchanga na kumkatakata vipande kisha kula nyama yake? Jibu lako lina maana gani (what does your answer imply)?
Kama si sahihi kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao hili linawezekana?
Hili tatizo lingine la wasioamini Mungu! Kama unaamini katika naturalism (kama ambavyo nimekusoma katika nyuzi kadhaa) kwa nini utumie "compassion, logic, ethics," vitu ambavyo havionekaniki wala kushikika?
All of those are perfectly understandable and logical memes. Einstein kakusaidia pale juu.
Compassion inaonekana pale mama anapolea mtoto na kumkuza, it is a practical concept, logic gates give you electicity and computing, unaposema logic haionekani sijui kama unajua kwamba unapotumia computer yako inatumia logic gates ambazo ziko katika circuitry za electronics ndani ya motherboard ya computer yako. Ethics ni somo la ubinadamu tu, kutumia akili ili kuwa mtu mwema.Halihitaji mungu. Einstein kakusaidia hapo juu, kwa nini unaona ni lazima kuwa na mungu ili kuwa na ethics wakati kuna watu mamilioni Asia huko hawaamini mungu lakini wana a very good ethical system?
Na pia hapa unajaribu kusema kuwa "God is morally wrong" na mimi nauliza "Under which Moral Law is God wrong?". Unapimaje ethics za Mungu na kuzithibitisha kuwa ziko chini? What are the scales?
Let's see.
If at all he exists, holding him to account.
God would violates the Hippocratic oath (he has the ability to eradicate disease but he does not).
God violates the International Criminal Court laws (he has the ability to stop all wars but chooses not to).
God violates The Universal Declaration of Human Rights (he has the ability to make all humans truly equal but he bestow on some fortunes and on some blindness from birth)
God violates The Code of Hammurabi (if a builder builds a house and the house collapses the builder is responsible, god created the earth but it is constantly crumbling down with earthquakes killing thousands)
The list goes on and on.
Apparently god violates his own laws. he forbids us to kill but he kills inordinately.
Katika ulimwengu/Dini unayoiamini ya "random and chance" kuna tatizo gani mtoto kuzaliwa kipofu?
Nani kakwambia naamini dini ya random and chance?
Katika dini yako ya "Hakuna Mungu" na hivyo hakuna "Ultimate Law" kuna tofauti gani kati ya mema na mabaya?
Ushaoneshwa hapo juu kwamba huhitaji mungu kuwa na mema na mabaya. Wewe hujaweza kutuambia kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote kauumba ulimwengu huu, mbona ulimwengu una maovu mengi sana?
Hitler aliona ni jambo Jema kuua wayahudi Mil 6+ na Stallin akaona ni jambo zuri tu kuua mamilioni ya Warusi.
Kwa nini mungu alimuumba Hitler na kuruhusu haya mauaji? Ina maana alishindwa kuyazuia? Kama hakushindwa kwa nini hakuyazuia? Alipendezwa nayo?
Kuna watu wanaona ni vyema wakibaka au kuua. Katika dini yenu ya hakuna Mungu, unawahukumu wana kosa? Kwa sheria ipi?
Apparently mungu naye anaona vyema, kama angeona si vyema, uwezo wa kuzuia alikuwa nao, ujuzi wa kuzuia alikuwa nao. Kwa nini hakuzuia?
Baba A akiona ni vyema kuwapa watoto chakula na Baba B akaona ni vyema watoto wake wakafa na njaa, na wote hawa ni binadamu, nani atakuwa amekosea? Kwa sheria ipi hiyo ya ubinadamu maana hawa wote ni wanadamu!
Mungu ndiye atakuwa amekosea kwa sababu yeye ndiye anayeruhusu yote, mpaka fikra za hawa watu.
Au mungu si muweza vyote?
Hujatuambia pa sheria hiyo mtunzi wake ni nani na kwa mamlaka gani aliitunga sheria hii!
Msome Einstein hapo juu.
Hujajibu kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote kachia watoto wa kijerumani wachomwe moto na Hitler? Ina maana alikuwa hana uwezo wa kuwaokoa? Au alikuwa na uwezo wa kuwaokoa hakutaka tu?
Kama hakutaka tu, kweli ana upendo mkuu?
You are right na ndivyo alivyo!
Sasa imekuwaje mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote achinjechinje watoto na kuachia wazaliwe na vilema? Mwanadamu angefanya hivyo tungemuita monster, mbona mungu mnamuabudu baada ya uovu wote huu?
Una maana hata pale viumbe hawa wanapochagua mauti badala ya uzima Mungu awalazimishe? Mfano, wewe Kiranga leo umemkataa Mungu mbele yetu sote, halafu unatarajia kwa sababu ya upendo wake akuachie tu uende, are you kidding?
Mungu kama kaumba kila kitu kaumba mpaka uwezo wangu wa kuelewa, sasa nisipomuelewa kwa sababu yeye hajanipa uwezo wa kumuelewa atanilaumu mimi vipi?
Mimi ndiye wa kumlaumu yeye.
Suppose mungu yupo, mimi sijamwelewa, kwa sababu hajanipa uwezo wa kumuelewa, na wewe umemuelewa, kwa sababu kakupa uwezo wa kumuelewa (after all tunaokoka kwa neema tu wameimba)
Unafikiri hiyo ni just and fair?
Kwa nini mungu awape neema wengine na wengine awanyime?
Kama huyu angekuwa bosi mwanaadamu tungesema ana favoritism.
Mungu ngani huyu kila standards za kibinadamu anashindwa kuzifikia?
Hakimu anapotoa hukumu huitoa kwa upendo kwa kuwa ni haki stahili.
Mfano wako mbovu.
Hakimu hakuumba ulimwengu, ana deal na ulimwengu iliokwishaumbwa kwa mujibu wenu.
Mungu kaumba ulimwengu from scratch.
Kwa nini hakufanya mabaya yasiwezekane tangu mwanzo?
Haya Magonjwa ni haki stahili ya Mwanadamu kwa sababu ya kuukaribisha uasi (dhambi).
Na mtoto mdogo anayezaliwa leo na kufa leo kwa ugonjwa kakaribisha dhambi gani?
Huwezi kukaribisha adui halafu ukalalamikia madhara yake. Each choice have its consequence!
Mtoto mdogo anayekufa mara baada ya kuzaliwa amefanya choice gani mpaka apate consequence hiyo? Kama makosa ya wazazi wake kwa nini mungu amuue mtoto? Kwa nini asiue wazazi na kumbakisha mtoto?
Bill hajawahi kumsaidia Mungu kazi hata siku moja. kupeleka chanjo Afrika haijawahi kuwa kazi ya Mungu. Umelipata wapi hili?
Mungu kawaumba watu bila chanjo. Bill kaona mungu kachemsha, kaumba watu bila chanjo, ngoja nimsaidie kuwapa hawa watu chanjo. Anawapa.
Watu wanapata chanjo wanaishi kwa afya bora zaidi.
Utasemaje Bill Gates hajamsaidia mungu hapo?
Jibu la swali hili nimeshalijibu hapo juu...madhara ya kukaribisha adui si kazi ya Mungu kuyabeba. Ukweli hata kama unauma ndio ukweli wenyewe!
Hujajibu, umebabaisha, na kubabaisha kwako kumezaa maswali zaidi. Kama mungu kaleta mabaya kutupa choice, kwa sababu anapenda sana choice, kwa nini hakunipa choice mimi niamue nizaliwe au nisizaliwe? Nizaliwe wapi, lini etc?
[/QUOTE]
Check the answer above! Huna haki ya kudai habari ya mabaya wakati unasema hakuna Mungu![/QUOTE]
Check the explanation above, including Einstein's. Huhitaji mungu kuwa na mfumo wa mabay na mazuri.
Swali hili unabadili tu namna ya kuliuliza na nimeshalijibu hapo juu!
Umebabaisha kwamba mungu anapenda choice, mbona katuleta duniani bila kutuuliza kama tunataka? Tumezaliwa bila hata kuulizwa tuchague wazazi, nchi, mwaka etc?
Huyu mungu anapenda choice kweli au mnatumia hilo conveniently tu?
Anyway hujaweka ushahidi wowote kuwa hakuna Mungu
You can't prove a negative.Kitu ambacho hakipo hakina ushahidi kwamba hakipo, kwa sababu hakipo.
Unaweza kunipa ushahidi kwamba hakuna Mchagga mwenye macho matatu anayekaa juu ya mlima Kilimanjaro?
Ukinipa ushahidi kwamba huyu hayupo na mimi nitakupa ushahidi kwamba mungu hayupo.
zaidi ya kuhoji kwa nini Mungu kama yupo alifanya A B C.
Swali ambalo hujalijibu.
Hakuna mahali umefuta point zangu na kwa ukweli umehakikisha nilichokisema kuwa ni dini yako tu inayokataa uwepo wa Mungu inakulazimisha kufika uliko.
Hakuna pahali ulipoelezea ukaeleweka kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kaumba ulimwengu unaoruhusu watoto kuzaliwa na vilema vya maisha.
Si kwa sababu hakuna Mungu bali kwa sababu hutaki kukubali uwepo wake ambao pia wajua ni halisi
Sasa umekuwa kigagula unajua ninachojua just like that?
Jibu swali, kwa nini mungu hajazuia watoto kuuawa na Hitler? Alishindwa au hakutaka tu?
Kama alishindwa, je anaweza kila kitu kweli?
Kama hakutaka, je ana upendo wa juu kabisa?
Umeruka na kukimbia point zangu badala ya kuzijibu moja baada ya nyingine.
Points gani? Za kukimbia kujibu "the problem of evil"? Do not flatter yourself.
Mungu yupo, alikuweko na ataendelea kuwepo!
Kama yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao uovu unawezekana wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?
Ukweli mchungu ni kwamba hujajibu swali jepesi tu la "the problem of evil".