Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Status
Not open for further replies.
Kwani kila swali lazima liulizwe ktk uzi huu? Na aliyekwaambia nina majibu yote nani?

kumbe hujiamni,mbona umeanza kwa risala ndefu kisha unasema huna majibu??,mbona unaweka mipaka kazika kujadili jambo hili??ama umeikariri biblia na ushakuwa mtumwa ??
 
Free ideas ,
Ni vema ukasoma na kuelewa malengo ya andiko husika. Sikuandika generally bali specifically. Pia hayo maswali ya kwa nini Mungu alifanya A B C wanapaswa kuuliza wanoamini uwepo wake. Vinginevyo ni maswali yasiyo na Maana.

Kifupi ni kuwa hujaelewa lengo la bandiko hili, acha nikusaidie. Hatujadili ktk uzi huu kuhusu biblia specifically, wala claims za imani zote duniani juu ya Mungu!

we si mmojawapo wa wanao amini/?niwaulize akina nani tena??,kama haujadili kuhusu biblia specifically uliikuwa na maana gan kusema mungu wa biblia??,mbona unajichanganya kijana
 
Last edited by a moderator:
Umesoma mada ukaielewa wewe?

Mbona unaulizamaswali ambayo mtoa mada ametoa angalizo kuyahusu?

Wewe ni free ideas kweli?

nimeelewa sana ye ndok ajichanganya,mbona anaikana bible tena kwamba haijadili yenyewe nakat mwanzo kasema ,anamuongelea mungu wa biblia?
 
Zorrander, na kaburungu:
Kiukweli watu wengi hawana ufahamu huu lakini uko wazi katika Biblia.
Argument zote hizi ziko wazi na wala si mpya. Kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa biblia kumejaa utajiri wa Falsafa, sayansi, Mantiki na kila namna ya mawe ya thamani.

Ashukuriwe Mungu aliyetupa hakika kuwa Yupo na kwamba kuna siku tutakaa nae bila kutengana Milele.
Lazima tufanye juhudi kuwasaidia akina Kiranga, CYBERTEQ na wengineo waujue ukweli kama Neno linavyosema:

"And others save with fear, pulling them out of the fire; hating even the garment spotted by the flesh" - Jude 23

Kumbuka Biblia inatuonya:

"But sanctify the Lord God in your hearts: and be ready always to give an answer to every man that asketh you a reason of the hope that is in you with meekness and fear" - 2Peter 3:15

Mbarikiwe Nyote!

Watu hatutaki kuamini, biblia tumeitoa makosa.

Wewe unakuja kutupa mistari ya biblia!

Kuamini biblia kikondoo bila backing ndio wengine hatutaki. Biblia unavyoiona sacred wewe si kila mtu, wengine tunaweza kuiangalia na kuitoa makosa kibao tu. Kwa hiyo usitake kufanya kwamba kwa kuwa kwako wewe biblia ni sacred basi kila mtu ataiamini tu.

This is exactly why religion is so lame.

Mnapewa maneno yameandikwa na wayahudi maelfu ya miaka, wayahudi wanawapa sheria zao, mnayakumbatia kwamba ya mungu.

Watu wakitaka a scientific explanation rooted in logic, mnawaita wana kasumba za ukoloni.

Kati ya nyie mnaokariri vitabu vya wayahudi na sisi tunaouliza maswali nani ana kasumba ya ukoloni?
 
Mkuu inaonekana kama wameuogopa huu uzi
Mbona siwaoni hapa?

Do not flatter yourself.

Wewe ndiye uliyeopgopa kujibu the problem of evil.

Mpaka leo hujatoa jibu.
 
Huwa siwaelewi mnapomkana Mungu na kuleta "problem of evil". hili swali nimelijibu katika uzi huu na kama hujaelewa nitarudia. Kiranga , unaposema "problem of evil" huoni unafanya "assumption" zinazodai/zinazolazimu uwepo wa Mungu?

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" maishani mwako?

Soma zaidi hapa

Immanent critique - Wikipedia, the free encyclopedia

Kifupi, mimi kama sikubali kuna mungu, na wewe kama unasema kuna mungu, tukibishana wote kwa kusimamia pande zetu, hatutapata hata pa kuanzia.

Sasa kinachofanyika hapo, mimi naachana na position yangu ya kutokubali kwamba mungu yupo, kwa muda tu, ili kuangalia upande wako na mjadala uendelee.

Nasema, OK, tuseme mungu yupo, na ni mwenye ujuzi wote, na uwezo wote, na upendo wote. Tukubaliane kwamba hili ni kweli.

Swali linakuja tukishakubaliana hivyo.

Kama mungu yupo, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye upendo wote.

Kwa nini karuhusu iwezekane kuzaliwa watoto vilema?

Hii ni hesabu ya ku solve for x, ambapo katika ku solve for x, unafanya let x be y, halafu jibu utakalopata la x unaweza kuli verify.

Naona somo zima la "immanent critique" limekupitia mbali.

Mtu anaposema "let's say god exists, for the sake of carrying the ergument and analysis forward" hamaanishi kusema kwamba kakubali kwamba mungu yupo.

Unatofautishaje mema na mabaya katika ulimwengu ambao hakuna Mungu?

Kuna njia nyingi tu. Unaweza kuanza kwa kusema kwamba yale yote ambayo sipendi kutendewa ni mabaya, na yale yote ambayo napenda kutendewa ni mazuri.

Hapo hujamhitaji mungu.

Kwa mfano, mimi sipendi kuuawa, kwa hiyo hili ni baya kwangu, sipendi kufanyiwa, na sitaki kumfanyia mwingine.

Pia mimi napenda zawadi za Swiss watches, kwa hiyo hili ni jema, mtu akinifanyia nitapenda na mimi nitapenda kumpa mwingine.

Hapo tayari tushaona mema na mabaya ambayo hayamtegemei mungu.

Hebu ona hapa wanajadili "secular morality" ambayo haimuhitaji mungu

Secular morality - Wikipedia, the free encyclopedia

Kwa hiyo kufikiri hakuna wema na ubaya nje ya mungu ni makosa, ni kama samaki kufikiria hakuna dunia isiyo na maji. Just because wewe umegubikwa katika bahari ya dini inayomtegemea mungu kwa kila kitu hilo halimaanishi hakuna watu wenye moral standards bila kumtegemea mungu

Msome Albert Einstein hapa

"A man's ethical behavior should be based effectually on sympathy, education, and social ties and needs; no religious basis is necessary. Man would indeed be in a poor way if he had to be restrained by fear of punishment and hopes of reward after death."
— Albert Einstein, "Religion and Science," New York Times Magazine, 1930

Maana kusema tu "evil" una "imply" aina fulani ya sheria ya maadili (Moral Law) na hivyo Mtoa/Mtunga sheria hiyo (Mungu). Sasa kama wewe huamini kuwa Kuna Mungu, unatofautishaje kati ya zuri na baya? utuambie hili kwanza kabla hata hujauliza kuhusu "problem of evil". maana kama huwezi kutuambia tofauti ya jema na baya, then kwanini tuendelee zaidi ya hapo?

Einstein kakusaidia hapo jinsi ya kupata moral code ambayo haimtegemei mungu.

Wewe ulitaka afanyeje? atengeneze watu ambao hawana uhuru wa kuchagua? Kama angefanya unavyotaka unafikiri angekuwa ameumba watu kwa mfano wake? Unafikiri kuna upendo bila kuchagua?

Huu uongo wa "mungu ameacha mabaya kwa kuwa anapenda uhuru wa kuchagua" nilisha u debunk.

Kama mungu anapenda kuchagua mbona hajanipa uchaguzi wa kuamua nizaliwe katika dunia ya namna gani, nchi gani, kwa wazazi gani, niwe na genes gani etc? Mbona nimejikuta nimezaliwa tu? Huyu ni mungu anayependa tuwe na uhuru wa kuchagua kweli?

Imagine mke wako ukitaka akubusu anakubusu hata kama yeye hataki. Utakwenda mtaani kifua mbele kuwa kuna upendo kati yenu?

Kama anapenda sana uchaguzi, mbona hakunipa mimi uchaguzi wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe?

Mungu yuko sahihi kabisa kuumba ulimwengu wa namna hii na ndio maana Yesu ni mwanakondoo aliyechinjwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa. Hii ni kwa sababu Mungu aliamua (in his Sovereign choice) kuumba ulimwengu ambao si tu kwamba alijua maovu yanawezekana bali alijua pia Mwaadamu huyu ataasi. Na akaamua kuonyesha ni wa Upendo zaidi kwa kufanya njia ya kumwokoa toka katika uovu wake: Mpango ambao wewe Kiranga unaukana leo hii.

Sasa mungu kaumba ulimwengu ambao anajua una maasi, na anajua kaumba wanadamu na udhaifu, makusudi, na kawawekea majaribu, na kajua kabisa wataasi, na kwa sababu kajua wataasi, na hawezi kukosea, hawawezi kuepuka kuasi.

Kwa maneno mengine kashawapangia kuasi.

Wakiasi atawalaumu?

Atawachoma moto kama wafanya dhambi? Wakati yeye mwenyewe ndiye aliyefanya kila jitihada kuhakikisha wanaasi?

Kaumba ulimwengu ambao uasi unawezekana, isitoshe kaweka vishawishi, isitoshe kawaumba binadamu dhaifu.

Binadamu wakiasi kosa ni la nani? Binadamu au mungu?

Kwa kuumba ulimwengu wa namna hii Mungu amedhihirisha upendo mkuu sana (Yohana 3)

Hapana.

Ukiwa software designer tu, halafu una uwezo wa kutengeneza software ya computer isiyo crash, lakini ukaamua tu kutengeneza software inferior inayocrash, unaweza kufukuzwa kazi. Hii ni standard ya kibinadamu tu.

Kwa nini mungu mwenye uwezo zaidi (mkuu) na ujuzi zaidi (mkuu) na upendo zaidi (mkuu) tumuwekee lower standards?

Simple! Kuna Magonjwa kwa sababu kuna dhambi. Kuna dhambi kwa sababu Mwanadamu aliamua kumwasi Mungu.

Uwezo wa mwanadamu kumuasi mungu mwanadamu aliutoa wapi? Mungu alipoumba ulimwengu kwa nini aliruhusu uasi uwezekanike?

Kama mungu kaumba ulimwengu na kuweka parameters zote, kwa nini aliruhusu parameters za ubaya kuwezekana?

Usiniambie kwa sababu alitaka mwanadamu awe na chaguo, kwa sababu mimi hakunipa chaguo nizaliwe au nisizaliwe, na nizaliwe wapi, vipi, niishije etc. Huyu si mungu anayependa viumbe wake wawe na chaguo

Mwanadamu alimwasi Mungu kwa sababu ya kutumia vibaya utashi wake.

Uwezo wa mwanadamu kutumia vibaya utashi wake umeumbwa na nani? Na kwa nini uliumbwa?

Mwanadamu alikuwa na utashi kwa sababu Mungu alimuumba na uwezo wa kuchagua.

Mimi mbona sikupewa uweza wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe? Katika tendo moja la kujamiiana kuna viini kama milioni mia mbili na nusu vinakufa ili kimoja tu kifanikiwe, kama mungu anapenda uchaguzi sana, mbona hivi vingine hajavipa uchaguzi wa kuishi?

Mungu alimuumba na uwezo wa kuchagua kwa sababu Mungu nu pendo.

Mbona mimi sijapewa uchaguzi kuamua nizaliwe au nisizaliwe? Na nizaliwe vipi? sehemu gani etc? Kama mungu kutoa uchaguzi ni upendo, sisi ambao hatujapata option kuchagua hatupendi.

Kwa hiyo "ultimately" kuna magonjwa kwa sababu kuna Mungu!

Alishindwa kuyazuia?

Unadhani kuna mahali popote ambapo ni sahihi kwa mtu kumbaka mtoto mchanga na kumkatakata vipande kisha kula nyama yake? Jibu lako lina maana gani (what does your answer imply)?

Kama si sahihi kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao hili linawezekana?

Hili tatizo lingine la wasioamini Mungu! Kama unaamini katika naturalism (kama ambavyo nimekusoma katika nyuzi kadhaa) kwa nini utumie "compassion, logic, ethics," vitu ambavyo havionekaniki wala kushikika?

All of those are perfectly understandable and logical memes. Einstein kakusaidia pale juu.

Compassion inaonekana pale mama anapolea mtoto na kumkuza, it is a practical concept, logic gates give you electicity and computing, unaposema logic haionekani sijui kama unajua kwamba unapotumia computer yako inatumia logic gates ambazo ziko katika circuitry za electronics ndani ya motherboard ya computer yako. Ethics ni somo la ubinadamu tu, kutumia akili ili kuwa mtu mwema.Halihitaji mungu. Einstein kakusaidia hapo juu, kwa nini unaona ni lazima kuwa na mungu ili kuwa na ethics wakati kuna watu mamilioni Asia huko hawaamini mungu lakini wana a very good ethical system?

Na pia hapa unajaribu kusema kuwa "God is morally wrong" na mimi nauliza "Under which Moral Law is God wrong?". Unapimaje ethics za Mungu na kuzithibitisha kuwa ziko chini? What are the scales?

Let's see.

If at all he exists, holding him to account.

God would violates the Hippocratic oath (he has the ability to eradicate disease but he does not).
God violates the International Criminal Court laws (he has the ability to stop all wars but chooses not to).
God violates The Universal Declaration of Human Rights (he has the ability to make all humans truly equal but he bestow on some fortunes and on some blindness from birth)
God violates The Code of Hammurabi (if a builder builds a house and the house collapses the builder is responsible, god created the earth but it is constantly crumbling down with earthquakes killing thousands)

The list goes on and on.

Apparently god violates his own laws. he forbids us to kill but he kills inordinately.

Katika ulimwengu/Dini unayoiamini ya "random and chance" kuna tatizo gani mtoto kuzaliwa kipofu?

Nani kakwambia naamini dini ya random and chance?

Katika dini yako ya "Hakuna Mungu" na hivyo hakuna "Ultimate Law" kuna tofauti gani kati ya mema na mabaya?

Ushaoneshwa hapo juu kwamba huhitaji mungu kuwa na mema na mabaya. Wewe hujaweza kutuambia kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote kauumba ulimwengu huu, mbona ulimwengu una maovu mengi sana?

Hitler aliona ni jambo Jema kuua wayahudi Mil 6+ na Stallin akaona ni jambo zuri tu kuua mamilioni ya Warusi.

Kwa nini mungu alimuumba Hitler na kuruhusu haya mauaji? Ina maana alishindwa kuyazuia? Kama hakushindwa kwa nini hakuyazuia? Alipendezwa nayo?

Kuna watu wanaona ni vyema wakibaka au kuua. Katika dini yenu ya hakuna Mungu, unawahukumu wana kosa? Kwa sheria ipi?

Apparently mungu naye anaona vyema, kama angeona si vyema, uwezo wa kuzuia alikuwa nao, ujuzi wa kuzuia alikuwa nao. Kwa nini hakuzuia?

Baba A akiona ni vyema kuwapa watoto chakula na Baba B akaona ni vyema watoto wake wakafa na njaa, na wote hawa ni binadamu, nani atakuwa amekosea? Kwa sheria ipi hiyo ya ubinadamu maana hawa wote ni wanadamu!

Mungu ndiye atakuwa amekosea kwa sababu yeye ndiye anayeruhusu yote, mpaka fikra za hawa watu.

Au mungu si muweza vyote?

Hujatuambia pa sheria hiyo mtunzi wake ni nani na kwa mamlaka gani aliitunga sheria hii!

Msome Einstein hapo juu.

Hujajibu kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote kachia watoto wa kijerumani wachomwe moto na Hitler? Ina maana alikuwa hana uwezo wa kuwaokoa? Au alikuwa na uwezo wa kuwaokoa hakutaka tu?

Kama hakutaka tu, kweli ana upendo mkuu?

You are right na ndivyo alivyo!

Sasa imekuwaje mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote achinjechinje watoto na kuachia wazaliwe na vilema? Mwanadamu angefanya hivyo tungemuita monster, mbona mungu mnamuabudu baada ya uovu wote huu?

Una maana hata pale viumbe hawa wanapochagua mauti badala ya uzima Mungu awalazimishe? Mfano, wewe Kiranga leo umemkataa Mungu mbele yetu sote, halafu unatarajia kwa sababu ya upendo wake akuachie tu uende, are you kidding?

Mungu kama kaumba kila kitu kaumba mpaka uwezo wangu wa kuelewa, sasa nisipomuelewa kwa sababu yeye hajanipa uwezo wa kumuelewa atanilaumu mimi vipi?

Mimi ndiye wa kumlaumu yeye.

Suppose mungu yupo, mimi sijamwelewa, kwa sababu hajanipa uwezo wa kumuelewa, na wewe umemuelewa, kwa sababu kakupa uwezo wa kumuelewa (after all tunaokoka kwa neema tu wameimba)

Unafikiri hiyo ni just and fair?

Kwa nini mungu awape neema wengine na wengine awanyime?

Kama huyu angekuwa bosi mwanaadamu tungesema ana favoritism.

Mungu ngani huyu kila standards za kibinadamu anashindwa kuzifikia?

Hakimu anapotoa hukumu huitoa kwa upendo kwa kuwa ni haki stahili.

Mfano wako mbovu.

Hakimu hakuumba ulimwengu, ana deal na ulimwengu iliokwishaumbwa kwa mujibu wenu.

Mungu kaumba ulimwengu from scratch.

Kwa nini hakufanya mabaya yasiwezekane tangu mwanzo?

Haya Magonjwa ni haki stahili ya Mwanadamu kwa sababu ya kuukaribisha uasi (dhambi).

Na mtoto mdogo anayezaliwa leo na kufa leo kwa ugonjwa kakaribisha dhambi gani?

Huwezi kukaribisha adui halafu ukalalamikia madhara yake. Each choice have its consequence!

Mtoto mdogo anayekufa mara baada ya kuzaliwa amefanya choice gani mpaka apate consequence hiyo? Kama makosa ya wazazi wake kwa nini mungu amuue mtoto? Kwa nini asiue wazazi na kumbakisha mtoto?

Bill hajawahi kumsaidia Mungu kazi hata siku moja. kupeleka chanjo Afrika haijawahi kuwa kazi ya Mungu. Umelipata wapi hili?

Mungu kawaumba watu bila chanjo. Bill kaona mungu kachemsha, kaumba watu bila chanjo, ngoja nimsaidie kuwapa hawa watu chanjo. Anawapa.

Watu wanapata chanjo wanaishi kwa afya bora zaidi.

Utasemaje Bill Gates hajamsaidia mungu hapo?

Jibu la swali hili nimeshalijibu hapo juu...madhara ya kukaribisha adui si kazi ya Mungu kuyabeba. Ukweli hata kama unauma ndio ukweli wenyewe!

Hujajibu, umebabaisha, na kubabaisha kwako kumezaa maswali zaidi. Kama mungu kaleta mabaya kutupa choice, kwa sababu anapenda sana choice, kwa nini hakunipa choice mimi niamue nizaliwe au nisizaliwe? Nizaliwe wapi, lini etc?

[/QUOTE]
Check the answer above! Huna haki ya kudai habari ya mabaya wakati unasema hakuna Mungu![/QUOTE]

Check the explanation above, including Einstein's. Huhitaji mungu kuwa na mfumo wa mabay na mazuri.

Swali hili unabadili tu namna ya kuliuliza na nimeshalijibu hapo juu!

Umebabaisha kwamba mungu anapenda choice, mbona katuleta duniani bila kutuuliza kama tunataka? Tumezaliwa bila hata kuulizwa tuchague wazazi, nchi, mwaka etc?

Huyu mungu anapenda choice kweli au mnatumia hilo conveniently tu?

Anyway hujaweka ushahidi wowote kuwa hakuna Mungu

You can't prove a negative.Kitu ambacho hakipo hakina ushahidi kwamba hakipo, kwa sababu hakipo.

Unaweza kunipa ushahidi kwamba hakuna Mchagga mwenye macho matatu anayekaa juu ya mlima Kilimanjaro?

Ukinipa ushahidi kwamba huyu hayupo na mimi nitakupa ushahidi kwamba mungu hayupo.

zaidi ya kuhoji kwa nini Mungu kama yupo alifanya A B C.

Swali ambalo hujalijibu.

Hakuna mahali umefuta point zangu na kwa ukweli umehakikisha nilichokisema kuwa ni dini yako tu inayokataa uwepo wa Mungu inakulazimisha kufika uliko.

Hakuna pahali ulipoelezea ukaeleweka kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kaumba ulimwengu unaoruhusu watoto kuzaliwa na vilema vya maisha.

Si kwa sababu hakuna Mungu bali kwa sababu hutaki kukubali uwepo wake ambao pia wajua ni halisi

Sasa umekuwa kigagula unajua ninachojua just like that?

Jibu swali, kwa nini mungu hajazuia watoto kuuawa na Hitler? Alishindwa au hakutaka tu?

Kama alishindwa, je anaweza kila kitu kweli?

Kama hakutaka, je ana upendo wa juu kabisa?

Umeruka na kukimbia point zangu badala ya kuzijibu moja baada ya nyingine.

Points gani? Za kukimbia kujibu "the problem of evil"? Do not flatter yourself.

Mungu yupo, alikuweko na ataendelea kuwepo!

Kama yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao uovu unawezekana wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Huu ndio ukweli mchungu!

Ukweli mchungu ni kwamba hujajibu swali jepesi tu la "the problem of evil".
 
Owner always makes the rules. You own your home you make the rules there.
He owns all thing and makes the rules....So simple!
Bado unapiga blaa blaa tu hapa, wewe jibu swali, NI NANI ALIYEKUAMBIA (or rather, UNA UTHIBITISHO GANI) kuwa huyo mungu wako ndiye Owner wa hii dunia kiasi kwamba atukuzwe kwa kuacha a-set lolote atakalo?
 
Unaweza kuwa na mtindio wa ubongo
Mtu anakuambia kuwa hoja hapa ni Mungu na hoja zingine sio mahala pake
Wewe unakuja na kudai hutaki limitations unadhani utakuwa sawa?

Amesema ana majibu yote kuhusu X sawa [ngoja tuassume hivyo kwakuwa hata hujui alichokisema japokuwa umesoma mada]na amekuambia kuwa majibu yaishie c kwakuwa hapa tunajadili c na sio X,kwakuwa c ni sehemu ya x na hatujadili x kwa ujumla wake

Ni sawa na mtu akuambie tujadili kuhusu kiuno na sio mwili wote kwakuwa hapa sio mahala pa kuujadili mwili wewe unakuja na maswali eti kwanini anniwekea limitations nisiujadili mwili wote

Utakuwa na ufikiri ulio sawa kweli?

Halafu unajaribu kujenga ka hoja ka kutokumuamini kwakuwa amekuambia tusiujadili mwili wote!!!!!

Sasa si umeambiwa ufungue mada nyingine kuhusiana na hayo?

Tatizo lenu mnadhani huwezi kumjadili Mungu bila kulijadili Taifa la Israel na Biblia kwa ujumla,mmejiweka kwenye ka kivuli ambako hata hakawatoshi

Mnatia huruma!
The Bottom Line is: Absence ya Mungu ni imani kama uwepo wake,; kwa maneno mengine hakuna uthibitisho wa kutokuwepo Mungu kama ilivyo kwa uwepo wake! Eti Kaunga, hiki si ndicho ulichojifunza kutoka kwenye uzi huu, au?
 
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" maishani mwako?

Soma zaidi hapa

Immanent critique - Wikipedia, the free encyclopedia

Kifupi, mimi kama sikubali kuna mungu, na wewe kama unasema kuna mungu, tukibishana wote kwa kusimamia pande zetu, hatutapata hata pa kuanzia.

Sasa kinachofanyika hapo, mimi naachana na position yangu ya kutokubali kwamba mungu yupo, kwa muda tu, ili kuangalia upande wako na mjadala uendelee.

Nasema, OK, tuseme mungu yupo, na ni mwenye ujuzi wote, na uwezo wote, na upendo wote. Tukubaliane kwamba hili ni kweli.

Swali linakuja tukishakubaliana hivyo.

Kama mungu yupo, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye upendo wote.

Kwa nini karuhusu iwezekane kuzaliwa watoto vilema?

Hii ni hesabu ya ku solve for x, ambapo katika ku solve for x, unafanya let x be y, halafu jibu utakalopata la x unaweza kuli verify.

Naona somo zima la "immanent critique" limekupitia mbali.

Mtu anaposema "let's say god exists, for the sake of carrying the ergument and analysis forward" hamaanishi kusema kwamba kakubali kwamba mungu yupo.

Kuna njia nyingi tu. Unaweza kuanza kwa kusema kwamba yale yote ambayo sipendi kutendewa ni mabaya, na yale yote ambayo napenda kutendewa ni mazuri.

Hapo hujamhitaji mungu.

Kwa mfano, mimi sipendi kuuawa, kwa hiyo hili ni baya kwangu, sipendi kufanyiwa, na sitaki kumfanyia mwingine.

Pia mimi napenda zawadi za Swiss watches, kwa hiyo hili ni jema, mtu akinifanyia nitapenda na mimi nitapenda kumpa mwingine.

Hapo tayari tushaona mema na mabaya ambayo hayamtegemei mungu.

Hebu ona hapa wanajadili "secular morality" ambayo haimuhitaji mungu

Secular morality - Wikipedia, the free encyclopedia

Kwa hiyo kufikiri hakuna wema na ubaya nje ya mungu ni makosa, ni kama samaki kufikiria hakuna dunia isiyo na maji. Just because wewe umegubikwa katika bahari ya dini inayomtegemea mungu kwa kila kitu hilo halimaanishi hakuna watu wenye moral standards bila kumtegemea mungu

Msome Albert Einstein hapa

Einstein kakusaidia hapo jinsi ya kupata moral code ambayo haimtegemei mungu.

Huu uongo wa "mungu ameacha mabaya kwa kuwa anapenda uhuru wa kuchagua" nilisha u debunk.

Kama mungu anapenda kuchagua mbona hajanipa uchaguzi wa kuamua nizaliwe katika dunia ya namna gani, nchi gani, kwa wazazi gani, niwe na genes gani etc? Mbona nimejikuta nimezaliwa tu? Huyu ni mungu anayependa tuwe na uhuru wa kuchagua kweli?

Kama anapenda sana uchaguzi, mbona hakunipa mimi uchaguzi wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe?

Sasa mungu kaumba ulimwengu ambao anajua una maasi, na anajua kaumba wanadamu na udhaifu, makusudi, na kawawekea majaribu, na kajua kabisa wataasi, na kwa sababu kajua wataasi, na hawezi kukosea, hawawezi kuepuka kuasi.

Kwa maneno mengine kashawapangia kuasi.

Wakiasi atawalaumu?

Atawachoma moto kama wafanya dhambi? Wakati yeye mwenyewe ndiye aliyefanya kila jitihada kuhakikisha wanaasi?

Kaumba ulimwengu ambao uasi unawezekana, isitoshe kaweka vishawishi, isitoshe kawaumba binadamu dhaifu.

Binadamu wakiasi kosa ni la nani? Binadamu au mungu?

Hapana.

Ukiwa software designer tu, halafu una uwezo wa kutengeneza software ya computer isiyo crash, lakini ukaamua tu kutengeneza software inferior inayocrash, unaweza kufukuzwa kazi. Hii ni standard ya kibinadamu tu.

Kwa nini mungu mwenye uwezo zaidi (mkuu) na ujuzi zaidi (mkuu) na upendo zaidi (mkuu) tumuwekee lower standards?

Uwezo wa mwanadamu kumuasi mungu mwanadamu aliutoa wapi? Mungu alipoumba ulimwengu kwa nini aliruhusu uasi uwezekanike?

Kama mungu kaumba ulimwengu na kuweka parameters zote, kwa nini aliruhusu parameters za ubaya kuwezekana?

Usiniambie kwa sababu alitaka mwanadamu awe na chaguo, kwa sababu mimi hakunipa chaguo nizaliwe au nisizaliwe, na nizaliwe wapi, vipi, niishije etc. Huyu si mungu anayependa viumbe wake wawe na chaguo

Uwezo wa mwanadamu kutumia vibaya utashi wake umeumbwa na nani? Na kwa nini uliumbwa?

Mimi mbona sikupewa uweza wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe? Katika tendo moja la kujamiiana kuna viini kama milioni mia mbili na nusu vinakufa ili kimoja tu kifanikiwe, kama mungu anapenda uchaguzi sana, mbona hivi vingine hajavipa uchaguzi wa kuishi?

Mbona mimi sijapewa uchaguzi kuamua nizaliwe au nisizaliwe? Na nizaliwe vipi? sehemu gani etc? Kama mungu kutoa uchaguzi ni upendo, sisi ambao hatujapata option kuchagua hatupendi.

Alishindwa kuyazuia?

Kama si sahihi kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao hili linawezekana?

All of those are perfectly understandable and logical memes. Einstein kakusaidia pale juu.

Compassion inaonekana pale mama anapolea mtoto na kumkuza, it is a practical concept, logic gates give you electicity and computing, unaposema logic haionekani sijui kama unajua kwamba unapotumia computer yako inatumia logic gates ambazo ziko katika circuitry za electronics ndani ya motherboard ya computer yako. Ethics ni somo la ubinadamu tu, kutumia akili ili kuwa mtu mwema.Halihitaji mungu. Einstein kakusaidia hapo juu, kwa nini unaona ni lazima kuwa na mungu ili kuwa na ethics wakati kuna watu mamilioni Asia huko hawaamini mungu lakini wana a very good ethical system?

Let's see.

If at all he exists, holding him to account.

God would violates the Hippocratic oath (he has the ability to eradicate disease but he does not).
God violates the International Criminal Court laws (he has the ability to stop all wars but chooses not to).
God violates The Universal Declaration of Human Rights (he has the ability to make all humans truly equal but he bestow on some fortunes and on some blindness from birth)
God violates The Code of Hammurabi (if a builder builds a house and the house collapses the builder is responsible, god created the earth but it is constantly crumbling down with earthquakes killing thousands)

The list goes on and on.

Apparently god violates his own laws. he forbids us to kill but he kills inordinately.

Nani kakwambia naamini dini ya random and chance?

Ushaoneshwa hapo juu kwamba huhitaji mungu kuwa na mema na mabaya. Wewe hujaweza kutuambia kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote kauumba ulimwengu huu, mbona ulimwengu una maovu mengi sana?

Kwa nini mungu alimuumba Hitler na kuruhusu haya mauaji? Ina maana alishindwa kuyazuia? Kama hakushindwa kwa nini hakuyazuia? Alipendezwa nayo?

Apparently mungu naye anaona vyema, kama angeona si vyema, uwezo wa kuzuia alikuwa nao, ujuzi wa kuzuia alikuwa nao. Kwa nini hakuzuia?

Mungu ndiye atakuwa amekosea kwa sababu yeye ndiye anayeruhusu yote, mpaka fikra za hawa watu.

Au mungu si muweza vyote?

Msome Einstein hapo juu.

Hujajibu kwa nini mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote kachia watoto wa kijerumani wachomwe moto na Hitler? Ina maana alikuwa hana uwezo wa kuwaokoa? Au alikuwa na uwezo wa kuwaokoa hakutaka tu?

Kama hakutaka tu, kweli ana upendo mkuu?

Sasa imekuwaje mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote achinjechinje watoto na kuachia wazaliwe na vilema? Mwanadamu angefanya hivyo tungemuita monster, mbona mungu mnamuabudu baada ya uovu wote huu?

Mungu kama kaumba kila kitu kaumba mpaka uwezo wangu wa kuelewa, sasa nisipomuelewa kwa sababu yeye hajanipa uwezo wa kumuelewa atanilaumu mimi vipi?

Mimi ndiye wa kumlaumu yeye.

Suppose mungu yupo, mimi sijamwelewa, kwa sababu hajanipa uwezo wa kumuelewa, na wewe umemuelewa, kwa sababu kakupa uwezo wa kumuelewa (after all tunaokoka kwa neema tu wameimba)

Unafikiri hiyo ni just and fair?

Kwa nini mungu awape neema wengine na wengine awanyime?

Kama huyu angekuwa bosi mwanaadamu tungesema ana favoritism.

Mungu ngani huyu kila standards za kibinadamu anashindwa kuzifikia?

Mfano wako mbovu.

Hakimu hakuumba ulimwengu, ana deal na ulimwengu iliokwishaumbwa kwa mujibu wenu.

Mungu kaumba ulimwengu from scratch.

Kwa nini hakufanya mabaya yasiwezekane tangu mwanzo?

Na mtoto mdogo anayezaliwa leo na kufa leo kwa ugonjwa kakaribisha dhambi gani?

Mtoto mdogo anayekufa mara baada ya kuzaliwa amefanya choice gani mpaka apate consequence hiyo? Kama makosa ya wazazi wake kwa nini mungu amuue mtoto? Kwa nini asiue wazazi na kumbakisha mtoto?

Mungu kawaumba watu bila chanjo. Bill kaona mungu kachemsha, kaumba watu bila chanjo, ngoja nimsaidie kuwapa hawa watu chanjo. Anawapa.

Watu wanapata chanjo wanaishi kwa afya bora zaidi.

Utasemaje Bill Gates hajamsaidia mungu hapo?

Hujajibu, umebabaisha, na kubabaisha kwako kumezaa maswali zaidi. Kama mungu kaleta mabaya kutupa choice, kwa sababu anapenda sana choice, kwa nini hakunipa choice mimi niamue nizaliwe au nisizaliwe? Nizaliwe wapi, lini etc?
Check the answer above! Huna haki ya kudai habari ya mabaya wakati unasema hakuna Mungu![/QUOTE]

Check the explanation above, including Einstein's. Huhitaji mungu kuwa na mfumo wa mabay na mazuri.

Umebabaisha kwamba mungu anapenda choice, mbona katuleta duniani bila kutuuliza kama tunataka? Tumezaliwa bila hata kuulizwa tuchague wazazi, nchi, mwaka etc?

Huyu mungu anapenda choice kweli au mnatumia hilo conveniently tu?

You can't prove a negative.Kitu ambacho hakipo hakina ushahidi kwamba hakipo, kwa sababu hakipo.

Unaweza kunipa ushahidi kwamba hakuna Mchagga mwenye macho matatu anayekaa juu ya mlima Kilimanjaro?

Ukinipa ushahidi kwamba huyu hayupo na mimi nitakupa ushahidi kwamba mungu hayupo.

Swali ambalo hujalijibu.

Hakuna pahali ulipoelezea ukaeleweka kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote kaumba ulimwengu unaoruhusu watoto kuzaliwa na vilema vya maisha.

Sasa umekuwa kigagula unajua ninachojua just like that?

Jibu swali, kwa nini mungu hajazuia watoto kuuawa na Hitler? Alishindwa au hakutaka tu?

Kama alishindwa, je anaweza kila kitu kweli?

Kama hakutaka, je ana upendo wa juu kabisa?

Points gani? Za kukimbia kujibu "the problem of evil"? Do not flatter yourself.

Kama yupo, kwa nini kaumba ulimwengu ambao uovu unawezekana wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Ukweli mchungu ni kwamba hujajibu swali jepesi tu la "the problem of evil".[/QUOTE]

Dah, Kiranga umetisha. Yaani wakariri dini wote wameingia mitini na akitokea hata 1 wa kujibu hizi Arguments zako njoo unidai bia!
 
Do not flatter yourself.
Wewe ndiye uliyeopgopa kujibu the problem of evil.
Mpaka leo hujatoa jibu.
Hapa kuna tofauti kubwa

Kuna tofauti kubwa kati ya jibu na jibu unalolitaka wewe
Pia kuna tofauti kati ya jibu lisilo sahihi na jibu sahihi

Wewe umetaka jibu
Jibu umepewa lakini bado unasema hujajibiwa,hii inamaana hata jibu hulijui
Yaani hujui kama jibu ni jibu

Ni bora ungesema jibu ulilopewa sio sahihi
Hii ingemaanisha kuwa unajua jibu ni kitu gani
Tungeanza kukuhoji kama unajua kama jibu sahihi ni kitu gani
Ili tujue kama una uwezo wa kung'amua kuwa kuna jibu ambalo sio sahihi na sahihi

Lakini umeendelea kudai jibu tu
Kitendo cha wewe kupewa jibu halafu unadai hujapewa ni ishara ya kutokujua ulichouliza achilia mbali kujua kama umejibiwa

Pia inathibitisha kuwa kama huwezi kulijua jibu maana yake huwezi kujua kama ni sahihi ama la!

" Don't flatter yourself " !!!!!!
 
The Bottom Line is: Absence ya Mungu ni imani kama uwepo wake,; kwa maneno mengine hakuna uthibitisho wa kutokuwepo Mungu kama ilivyo kwa uwepo wake! Eti Kaunga, hiki si ndicho ulichojifunza kutoka kwenye uzi huu, au?

Unamuuliza Kaunga au?
Maana sikuelewi
Umeniquote mimi halafu swali umelielekeza kwingine!
 
Last edited by a moderator:
Watu hatutaki kuamini, biblia tumeitoa makosa.

Wewe unakuja kutupa mistari ya biblia!

Kuamini biblia kikondoo bila backing ndio wengine hatutaki. Biblia unavyoiona sacred wewe si kila mtu, wengine tunaweza kuiangalia na kuitoa makosa kibao tu. Kwa hiyo usitake kufanya kwamba kwa kuwa kwako wewe biblia ni sacred basi kila mtu ataiamini tu.

This is exactly why religion is so lame.

Mnapewa maneno yameandikwa na wayahudi maelfu ya miaka, wayahudi wanawapa sheria zao, mnayakumbatia kwamba ya mungu.

Watu wakitaka a scientific explanation rooted in logic, mnawaita wana kasumba za ukoloni.

Kati ya nyie mnaokariri vitabu vya wayahudi na sisi tunaouliza maswali nani ana kasumba ya ukoloni?

Natumia definition ya kitabu chenu. Amri kumi za mungu wenu. Anasema tusiue. Halafu yeye anafanya iwezekane mama apate mimba na mtoto afe tumboni.

Huyu mtu ni mzima kweli?

Anatuhumu kitu ambacho hata yeye mwenyewe anakitumia!
Huruma iliyoje?
 
kumbe hujiamni,mbona umeanza kwa risala ndefu kisha unasema huna majibu??,mbona unaweka mipaka kazika kujadili jambo hili??ama umeikariri biblia na ushakuwa mtumwa ??

Ni heri anayekuwa mtumwa wa biblia,kuliko mtumwa wa kutokujijua hata nafsi yake mwenyewe,kwa sababu kama
unakana uwepo wa Mungu ni sawa na kujikana uwepo wako mwenyewe,kwani hukujiumba wewe'
 
Stephano Mtangoo

Umenikumbusha Story ya mtoto wa Kimarekani ambaye Professor wao asiyeamini kuwa kuna Mungu aliwatia sumu wote kwa mafunzo yake kuwa hakuna Mungu with various supporting arguments anazozijua. Huyu Professor alikuwa na gari zuri sana.

Mwishoni huyu dogo akiwa na Professor kabla hajapanda gari yake yule dogo akamwambia: you know professor hii gari yako iko poa sana. Ila imejitengeneza yenyewe Tyres, Engines, Shape etc etc. Yule Professor akang'aka sana kuwa gari ilitengenezwa na Engineers makini sana aache ujinga wake.

Dogo naye akamjibu kuwa wewe ndo mjinga usiyejua kuwa Design & Engineering ya Binadamu imefanyika kwa umakini wa hali ya juu kuliko gari yako. Kama huamini kuwa gari ilijitengeneza why do u want me to believe kuwa Binadamu aliibuka tu? Professor akagwaya.

Hakika naamini Binadamu aliiumbwa na aliiumbwa na Mungu.

So, Mungu yupo!
 
Last edited by a moderator:
Kifupi, mimi kama sikubali kuna mungu, na wewe kama unasema kuna mungu, tukibishana wote kwa kusimamia pande zetu, hatutapata hata pa kuanzia.
Sasa kinachofanyika hapo, mimi naachana na position yangu ya kutokubali kwamba mungu yupo, kwa muda tu, ili kuangalia upande wako na mjadala uendelee.
Ni sawa na kusema kama wewe unabisha kuwa risasi haiui na mimi nasema inaua inabidi mimi niruhusu unirarue nayo ili tuone kama inaua ama la!
Funny,isn't it?

Kwanini utoke kwenye msimamo wako?
Unataka tufanye majadiliano kutokakwenye msimamo fake,kwanini?

Kama unasema Mungu hayupo halafu ukapose kama gnostic inamaana wewe ni kigeugeu na hujui kama hujui Mungu yupo ama la!
Nasema, OK, tuseme mungu yupo, na ni mwenye ujuzi wote, na uwezo wote, na upendo wote. Tukubaliane kwamba hili ni kweli.
Kwanini "tuseme Mungu yupo"?
Kwanini tufanye majadiliano kwa kutumia assumption?
Sisi hapa atu-assume bali tunaamini yupo kama wewe UNAVYOAMINI hayupo!

Kama mungu yupo, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye upendo wote.
Kwa nini karuhusu iwezekane kuzaliwa watoto vilema?
Haya ni maswali ambayo anatakiwa aulize mtu ambae anaamini Mungu yupo sio anae-assume Mungu yupo
Maswali yako hayana maana kwakuwa una-assume tu!
Hii ni hesabu ya ku solve for x, ambapo katika ku solve for x, unafanya let x be y, halafu jibu utakalopata la x unaweza kuli verify.
Sisi hatusemi let x be,sisi tunasema x ni ......
Wewe ndio unasema let x be ....
Huoni kuwa tuko nchi mbili tofauti?
Tutajadilije jambo ambalo hata uwepo wake hatujakubaliana?
Mtu anaposema "let's say god exists, for the sake of carrying the ergument and analysis forward" hamaanishi kusema kwamba kakubali kwamba mungu yupo.
Nimeshakujibu hii
Kuna njia nyingi tu. Unaweza kuanza kwa kusema kwamba yale yote ambayo sipendi kutendewa ni mabaya, na yale yote ambayo napenda kutendewa ni mazuri.
How do you "distinguish" bad from good?
Unatumia kipimo gani?
Hapo hujamhitaji mungu.
Sio kweli
Kwa mfano, mimi sipendi kuuawa, kwa hiyo hili ni baya kwangu, sipendi kufanyiwa, na sitaki kumfanyia mwingine.
Kwanini hupendi?
Pia mimi napenda zawadi za Swiss watches, kwa hiyo hili ni jema, mtu akinifanyia nitapenda na mimi nitapenda kumpa mwingine.
Kwanini unapenda?
Hapo tayari tushaona mema na mabaya ambayo hayamtegemei mungu.
Umekosa tafakuri wewe
Ukishasema jema tayari umeshamtaja Mungu
Au na hili hujui?
Hebu ona hapa wanajadili "secular morality" ambayo haimuhitaji mungu
Kwahiyo "wakijadili" tayari wanakuwa wamemfanya Mungu kutokuwepo?
Huoni hata hapa tunajadili?
AAu kwa mimi kujadili morality inayothibitisha kuwepo kwa Mungu nakuwa nimemthibitisha tayari,right?

Halafu Moral ni nini?
Imetoka wapi?
Kwanini tunayo?
Kwa hiyo kufikiri hakuna wema na ubaya nje ya mungu ni makosa, ni kama samaki kufikiria hakuna dunia isiyo na maji. Just because wewe umegubikwa katika bahari ya dini inayomtegemea mungu kwa kila kitu hilo halimaanishi hakuna watu wenye moral standards bila kumtegemea mungu
Hebu tuambie kwanza baya na jema ni nini ili tujadili kama tunaweza kujua kama Kuna ubaya na wema nje ya Mungu

Maana naona unarukia mambo tu!
 
Is Uniformity one of the key elements to justify God's existence, siyo? Good, sasa hapo mwanzo biblia yako inatuambia hakukuwa na dhambi. Mungu Aliumba viumbe vyake vyote akiwemo Malaika Mkuu wake Lusifa a.k.a. Shetani wa leo akiwa mkamilifu. Ila ghafla bin vuu bwana mkubwa huyu akaota kiburi na kutaka kujifananisha na Muumba wake! Is this what you refer to be uniformity, one of your poor proofs of God's existence? Okay, following the same trend, Mungu Alijua kuwa Ulimwengu aliouumba baadaye ungetumbukia dhambini, sasa akaandaa mpango mkubwa, mgumu, wa gharama kubwa na tena usiofikirika eti wa kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini! Sasa two issues to be addressed here:-

  1. Ikiwa ni kweli kuwa Mungu Alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua mema na mabaya (sawa na wewe Baba/Mama unavyoweza kumpa uhuru mwanao aende Mzumbe Secondary au Ikinabushu Secondary), iweje tena Baba/Mama huyu huyu aanze kumtishia mwanaye kuwa “ukichagua kwenda Ikinabushu Secondary nitakufukuza kwangu tena na kukuchoma moto”? Iweje mtu anapo-exercise uhuru wake uliompatia wewe mwenyewe aonekane adui yako kisa tu hakuchagua vile ulivyotaka wewe? Je, katika viwango vya kibinadamu, huo kweli ni uhuru au ni udikteta zaidi ya ule wa Idd Amin Dada? Halafu tena, iweje mtoto wako ambaye amechagua kwenda Ikinabushu Secondary wewe mzazi uanze “njama”(maana humshirikishi) za kuandaa mpango wa kumuhamisha mara tu atakapokuwa amejiunga na Ikinabushu Secondary? Sasa hapo ulimpa achague kweli alichokitaka yeye mwenyewe au ulikuwa unamfanyia usanii tu? Na hata kama ulitaka asiende Ikinabushu Secondary kwa madai kuwa ni Shule ya Kata tena isiyo na vifaa wala walimu wazuri, kwa nini usisubirie hadi atakapoona madhara/matokeo ya uchaguzi wake huo iwapo tu ulifanya kazi ya kumshauri lakini hakusikia? Badala yake wewe Mzazi unayependa Mzumbe Secondary ndiye unayetoka huko uliko na kukurupuka kwenda kumuadhibu mwanao aliyeko Ikinabushu Secondary tena kwa mapenzi na utashi wake mwenyewe? Kwa nini usingemuacha tu na wewe ukabaki na chaguo lako, na iwapo una watoto wawili na bahati "nzuri kwako” mmoja amekukubalia chaguo lako (la kwenda Mzumbe Secondary) basi uwashindanishe wote wawili tena kwa usawa (pasipo upendeleo) kuliko kumtishia yule wa Ikinabushu kuwa atafeli, utamnyima ada, hela ya matumizi na hutakwenda kumsalimia huko shuleni na wala asije akarudi tena nyumbani kwako wakati wa likizo????????

  1. Back to Uniformity: Kama mwanadamu naye alikuwa mkamilifu, baadaye akaasi na mpango wa kumuokoa kutoka dhambini ukasukwa, sasa tuna uhakika gani kuwa mwanadamu yule yule atakayekuwa ameokolewa dhambini hataasi tena ktk paradise/akhera/mbingu/dunia ijayo? Kwa nini hapa usione kuwa kuna Non-uniformity katika plans za huyo Mungu wako? Iweje Duniani pa likuwa Patakatifu, Kisha Dhambi na Tunaambiwa Baadaye tena patakuwa Patakatifu lakini hatuelezwi kuwa yawezekana ikaja kuwa tena Dhambi na kufanya iwe Loop inayoonyesha hiyo Uniformity yako? Sasa Utakatifu >>> Dhambi >>> Utakatifu ndio hiyo Uniformity unayoizungumzia hapa? Na ni nini mpango wa Mungu endapo tena mwanadamu atakuja kuasi akifika huko mbinguni? Maana hapo mwanzo Mungu Alijua kuwa kiumbe wake mkamilifu angeasi, akajiandaa, lakini this time tunaambiwa kuwa huko mbinguni hakutakuwa na dhambi wala kifo tena (just as it was in the beginning) lakini hatuambiwi nini kitatokea endapo hali ikigeuka kuwa ndivyo sivyo! Au wanadamu watakaokuwepo kule hawatakuwa tena na uchaguzi wa kuamua njia waitakayo kama wale wa awali walivyopewa fursa hiyo? If that is the case, ina maana huyo Mungu atakuwa amewafunga watu wake wasiwe na any other choice except him? Na kama hivi ndivyo basi huyo Mungu hajiamini, ni dikteta wa hali ya juu na hajali athari za mabavu yake kwa watoto wake mwenyewe maana kama angelikuwa na upendo basi asingewanyima uhuru wao kama ule aliowapa hapo mwanzo!

  1. By the way, wewe (Mungu) ni Mwalimu wa Sanaa (Arts), unafundisha wanafunzi, kutunga mitihani, kusahihisha na mwisho kutoa matokeo. Sasa iweje tena wewe huyo huyo ulazimishe kutoa matokeo ya wanafunzi waliofanya somo la Hisabati ilhali halikuhusu, hukusomea, hukuwafundisha na wala hukutunga mtihani huo? Maana yangu ni kwamba, kwanini Mungu asi-deal na wale wanaofuata sheria zake tu (yaani awalinde, awatunze, awahudumie na hatimaye siku atakayoona inafaa awapeleke anakotaka yeye basi) na badala yake ana-cross over na kuwafuata wale wasiomuamini na kujifanya ndiye Jaji wao? Kwanini wale wasiomuamini (kwa maana nyingine ni wafuasi wa Mzee Mzima Shetani) asiwaache nao walindwe, watunzwe, wahudumiwe na hatimaye wapelekwe kule ambako Master wao atataka wawe halafu mwishoni ndio atoe ushuhuda kuwa “Niliwaambia hamkusikia, oneni jinsi uchaguzi wenu ulivyowagharimu”? Hayo ya Ngoswe yanamhusu nini yeye huyo Mungu wenu? Mbona huyo Kiongozi wa hilo kundi lingine (Shetani) yuko kimya tu, hajatangaza adhabu kwa wale wasiomtii (kama wewe unayejidai ni mfuasi wa Mungu)? Iweje huyu muungwana (Shetani) asiwe na noma kwenu nyie mnaokesha na kumtukana mchana na usiku kucha lakini kinyume chake huyo Mungu wenu mnayempamba ni mwenye haki na upendo atangaze shari kwa wasiomfuata? Yaani ni sawa na Kikwete (Rais wa Nchi na Watz wote + M/Kiti wa Magamba) atangaze kiama na majanga kwa watu wote wasio wafuasi wa Magamba lakini Dr. Slaa/Mbowe/Lipumba/Cheyo/Mrema/Mbatia/Mtikila/et al wao wabaki kimya wala hawawalalamikii watu ambao hawawaungi mkono/ni wafuasi wa Magamba, sasa kati ya pande hizi mbili ni upi unaoonekana kutenda haki na uungwana kwa standards za kibinadamu? Sasa iwapo kwa stabdards za kibinadamu imekuwa hivyo, habari gani kwa standards za huyo Mungu? Kwanini isiwe hivyo?????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  1. Kwa hali ya kibinadamu, wanasema “wengi wape”. Ninyi licha ya Shetani kutolalamika wala kuomba kutukuzwa kama vile Mungu wenu anavyotaka atukuzwe mchana na usiku kucha, lakini hata hivyo watu wengi (naamini na wewe ukiwemo) mnaimba mko kwa Mungu lakini matendo yenu hayana tofauti na ya Mzee Mzima Shetani! Hata huyo Yesu wenu aliwahi kukiri, kuwa vinywa vyenu vinaimba Mungu lakini miondoko na midundo ya matendo yenu ni ya Mzee mzima ambaye mnakesha mchana kutwa mkimpiga vijembe! Hii ina maana gani?????? Maana yake ni kwamba huyo Mungu wenu kimantiki hayupo maana kaweka vigezo vigumu sana vya kumfikia, na hata yeye mwenyewe anakiri kuwa njia yake ni nyembamba na waionao ni wachache! Yohana aliona idadi ya watakaourithi ufalme wa mbinguni ni mia moja arobaini na nne elfu tu! Sasa kati ya Watu zaidi ya 2 billion tuliopo, wateule ni sawa na asilimia 0.0072 tu! Anyway, sasa kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa nini nisiamini kuwa kitendo cha Mungu kuamua kuja kuchoma moto dunia hii (na wakati wa Nuhu kugharikisha dunia nzima) ni wivu tu baada ya Sera zake kukataliwa na watoto wake wa kuumba yeye mwenyewe? Kwanini isiwe hivyo iwapo hata kule mbinguni alivyotaka kupima ubavu na Lusifa Mzee Mzima alijinyakulia theluthi 1 ya malaika wote tena kwa mkupuo pasipo kufanya kampeni? BY LOGIC: Iwapo hao malaika na hata Lusifa mwenyewe aliyekuwepo kule mbinguni na akawa karibu sana na huyo Mungu waliasi, habari gani wewe Mnyalukolo mwenzangu ambaye hukuwahi hata kwenda juu ya haya mawingu tunayoyaona ujiaminishe kiasi hicho kuwa Mungu wako unayemtumainia ni mwenye upendo, huruma na msamaha? Hivi mwanao akikaidi ushauri wako na akaamua kufanya maamuzi yake anayoona ni sahihi kwake utamwadhibu au utamsikitikia na kumuonea huruma kwa kitakachompata? Sasa iweje kwa standards za Mungu JEHANAMU ndio iwe kusudio kwa wale watakaomkataa badala ya kuwahurumia, kuwasikitikia na ikiwezekana kuwaepushia majanga hayo????? Hivi bado tu hujaona mantiki hapa, au unaendelea kuimba na kukariri tu kama ambavyo wajanja fulani waliwataka muendelee kuamini hivyo milele? Unachekesha aiseee!!!!!!!!!!!

  1. MWISHO: Eti kuna Mungu au Shetani ni nadharia tu zisizo na mantiki wala mashiko yoyote katika viwango viwavyo vyovyote vile, hata iwe ni kwa kutumia akili ndogo kabisa za kibinadamu maana hata yasemwayo kuhusu hao wawili hayawezi kuthibitishwa pasipo kuacha chembe ya shaka! So, what for? Leave this Topic alone, don't waste your precious time at all!

Nizungumzie Kuhusu Uasi tena.
Ukisoma biblia, inaeleza wazi kutokomeza Dhambi/Uasi na Dunia kufanywa mpya isiokua na Mawaa ata kidogo!
Rejea shughuli za Hema takatifu lililokuwepo Hapa duniani likikusudia kua Mfano wa Kafara hails Yesu kuja kutufia Kama Kafara!
Katika shugghuli zile palikua na shughuli za Kila Siku na Mara moja kwa Mwaka!
Katika ile shughuli ya Mara moja kwa Mwaka kulikua baada ya shughuli anaachiwa Mbuzi wa AZAZERI,
Huyu Mbuzi alikua anabeba dhambi/Uasi zote na kwenda kufia huko nyikani; hichi Kitendo kinajulikana km kutokomeza Dhambi/Uasi.
Kwa Maana hiyo basi hizi shughuli zilikua nakala ya Yesu kuja kua Kafara halisi! Tayari Yesu alishakufa msalabani kazi iliyobaki ni Shetani kuangamizwa na Dhambi/Uasi kutokomezwa na Dunia kutengenezwa mpya bila ya kuwepo dhambi na Uasi!
Sasa wewe Uasi unaosema wewe kua waweza kutokea unaujenga kwa misingi gani?

Biblia Iko wazi na mipango ya Mungu Iko wazi yote ni Imani yako tu ndio inayokufanya useme hivyo!
Kwa mujibu wa Biblia Hapo baada ya kufanya nchi mpya kutakua hakuna Dhambi/Uasi tena!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom