Muongozo wa kununua Spark Plug sahihi: Usibahatishe ! Fundi na Ai wanaweza kukosea, tumia katalogi hii ya DENSO.

Muongozo wa kununua Spark Plug sahihi: Usibahatishe ! Fundi na Ai wanaweza kukosea, tumia katalogi hii ya DENSO.

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Makampuni ya spark plugs yapo mengi, lakini kwa uchache wa resources nilizoweza kupata, nimefanikiwa kuipata DENSO Spark Plug Catalog PDF na nimeona niishirikishe hapa kwa manufaa ya wengine.

Katalogi ya DENSO ina columns mbalimbali zinazokusaidia kutambua spark plug sahihi kulingana na aina ya gari, ukubwa wa injini, mwaka wa kutengenezwa na engine code.

  • MODEL - jina au aina ya gari, kwa mfano Toyota Alphard au Mazda CX-5.
  • CC - ukubwa wa injini ya gari. Kwa mfano, 1800cc
  • VEHICLE CODE - toleo maalumu la gari
  • ENGINE - Inaonyesha code ya injini iliyofungwa kwenye gari.
  • FROM–TILL - kipindi gari lilitengenezwa mfano, 02.5–08.5 hadi Mei 2002 hadi Mei 2008.
  • DENSO – Spark plug ya kawaida inayopendekezwa inadumu km elf 30
  • GENUINE P/N – Namba ya spare part ya kiwandani.
  • QTY (Quantity) – Idadi ya spark plugs zinazohitajika kwenye injini ya gari.
  • (-) kwenye katalogi inaonyesha kwamba hakuna namba ya spark plug iliyoorodheshwa katika column hiyo.



DENSO – Spark plug ya kiwango cha kiwandani. Kwa aina za kawaida za nickel, inapendekeza kubadilisha baada ya takribani km 15,000–20,000. Bei ndogo zimejaa mtaani elf 40 hadi 60 kwa piece 4

TT (Twin Tip) – Spark plug yenye teknolojia ya ncha mbili inayosaidia uwakaji mzuri wa cheche. Kwa aina ya Nickel TT,. zina bei ya chini ya kati

IRIDIUM POWER – Spark plug yenye teknolojia ya iridium inayolenga utendaji mzuri wa injini. zina bei ya kati

IRIDIUM TOUGH – Spark plug yenye teknolojia ya iridium inayolenga uimara na matumizi ya muda mrefu. Inaweza kudumu hadi km 100,000. zina bei kubwa hadi laki 3 kwa piece 4


Ulaji wa mafuta unafanana, kukiwa na tofauti basi ni asilimia 2, hivyo haimaanishi spark yenye bei inakula mafuta kidogo kuzidi nyingine

Mfano​


Kwa Toyota Alphard 3000cc yenye injini 1MZ-FE, katalogi inaonyesha SK20R11 kama spark plug ya kiwango cha kawaida, IK20 kama chaguo la Iridium Power na VK20 kama chaguo la Iridium Tough.

Catalogi imegawanyika kulingana na nchi yanakotengenezwa magari, mfano kwa japan ni ukurasa wa 221–260

Australia 54–102
China 103–131
India 132–135
Indonesia 136–144
South Korea 145–149
Malaysia 150–159
Philippines 160–170
Saudi Arabia 171–173
Singapore 174–190
Taiwan 191–208
Thailand 209–216
Vietnam 217–220
Japan 221–260
Europe & USA 261–305
 

Attachments

Back
Top Bottom