Museveni anaeonekana kuifahamu sana Tanzania, hii sio hatari kwa usalama?

Hatari ipi? Hiyo?
Kama sasa hv kwa google map tu,unaweza ukazoom Ikulu na ukajua Kuna magari mangapi yamepaki,hiyo hatari ipi unayoizungumzia kwa mtu kuifahamu nchi nyingine kwa undani.
Kwenye kada ya intelijensia hata nchi marafiki hufanyiana ujasusi,unaweza kukuta Uganda,Kenya,Rwanda,SA Zina maspy kibao kwenye vyombo vyetu vya usalama.
Hata sie huwa tunao maspy,ni kitu Cha kawaida kwenye ujasusi.
 
  • Kasoma UDSM
  • Kafundisha MUCCOBS
  • Kajifunza Jeshi hapa TZ
  • Kijana wake kwanza Muhoozi (Next president wa UG 😂😂😂) Kazaliwa hapa Dar
  • Kapigana Mozambique upande wa Frelimo na JWTZ,
  • Kapigana na Iddi Amin upande wa JWTZ
  • Kawekwa madarakani na TZ baada ya Obote kuzingua....
 


Unaelimu gani Sheikhe?

Mtu anaweza kujua jiografia ya eneo Fulani Kwa kufika, kusoma, au kuangalia tamthilia.

Kuna rafiki yangu kaishia Kidato cha nne anaijua Nigeria Kama Buza na hajawahi kufika. Hii ni kutokana na kuangalia Fulani za kinaijeria.
 
Kasoma chuo kikuu Mlimani miaka ya 1960 kama walivyosoma wanaharakati wengi wa mataifa ya kusini mwa afrika miaka ya sabini kuelekea themanini mwanzoni.
Yoweri baada ya kuhitimu UDSM kafanya kazi ya kufundisha uchumu chuo cha Ushirika Moshi.

Kajana wake Lt. Gen. Kainerugaba lazaliwa Dar wakati Yoweri na Mkewe Jannet wanaishi Dar.

Katika sehemu ya hotuba zake enzi ya JPM amekuwa akieleza namna alivyofanya kazi (akiwa trainee) kwa ukaribu na Mzee Butiku akiwa Katibu wa Rais Mwl. NYERERE, kafanya kazi na Bhoke Munanka aliekuwa waziri wa Nchi ofisi ya Rais - Usalama.

Yeye mwenyewe amejinasibu mwl. JKN alimtuma kuwa sehemu ya wapiganaji wa Tanzania waliokuwa kusini wakikomaa kumwondoa Mreno.

Kimsingi, Mseveni ni kijana wetu na kapata all necessary support akiwa vijiji vya Kagera wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Uganda kati ya 1980-86.
 
Hopefully unajua Lt. Gen. Kainerugaba sio mtoto wa kumzaa wa Mama Janet M7.
 
hahahaha
 
Kabila mkubwa miaka ile tuko wadogo Kijitonyama jirani na yard ya mzee wa Ubwabwa alikuwa anakuja sana nyumba ya jirani tulikuwa tunamwita Uncle Kabila. Baada ya muda tunasikia kawa rais wa Congo dunia INA siri nyingi
hahahaha alikua akiitwa hivo?uncle kabila miaka hy? Safi sana
 
watoto wadogo hawajua haya
 
President museveni, Phillipe Nyusi na Joseph kabila wamesoma na kuishi Tanzania
 
Kwa hyo wakishaijua nchi ndo tayari tumeshavamiwa?
 
Kwani umeambiwa sisi hatuijui Uganda?
 
Kwa taarifa yako, hata kuanzisha vita vya kumwondoa Obotte madarakani Museveni alipata 'go ahead' ya Mwalimu. Museven ni kijana (sasa hivi mzee) wetu, siyo ajabu kuijua vizuri Tanzania.
 
DSM wadada wa kazi za ndani ni Wamalawi siku hizi.
 
Sio duka tuu, wengine unaweza kuta wako hata kwenye nafasi za uongozi (mtaa/kijiji/kata.....) katika maeneo husika.
 
Sasa huyu alisoma huku,alikaa miji mbalimbali na alikuwa kama kijana wa mwl nyerere

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Siku ukuambiwa M7 ni Mtz si ndio utadata kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…