Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Joyce joyce

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
457
Reaction score
1,973
Wakuu,

Tundu Lissu Siku ya Kuamkia leo alilala nyumbani kwa baba wa taifa Mwalimu Nyerere baada ya kuombwa na watoto wa Baba wa Taifa.

Watoto hao walijisikia furaha kubwa mno kupata ugeni mzito huo ambao wamesema hawajawahi kupata mgeni wa kulala kwao mkubwa kama Lissu na walijisikia kama wako na Baba yao Mzazi.,

Mmoja wa watoto hao Madaraka Nyerere amesema kuwa hawakuamini kama Lissu angewakubalia ombi lao hilo.

Kwenye Ukurasa wake wa Twitter, Tundu Lissu ameandika "In Mara we'd the honour of spending the night at Mwitongo, the birthplace & resting place of Mwl. J. K. Nyerere. We're privileged to be hosted by Madaraka, one of Mwalimu's sons, his sister Neema & her husband Carlo Giero both of whom treated us to a sumptuous dinner & breakfast."

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
 
Nakumbuka wakati muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya pili ya JK, KUB alikua Hamad Rashid Mohamed wa CUF. Siku ya Alhamisi ambayo ni siku ya maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, KUB alikua akipata kifungua kinywa nyumbani kwa PM na wakiondoka wote kwenda Bungeni.

Utamaduni huu umekomeshwa kikatili sana. Sasa hivi sio tu dhambi kumtembelea mtu mnae tofautiana itikadi za chama bali pia ni dhambi kumjulia hali mgonjwa hospitakini kama si wa chama chako! Na tunapoelekea hata kuzikana watu wa vyama tofauti itakua ni kosa la kimaadili la kuadhibiwa na chama. Nani katufikisha huku? Tusikubali.
 
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA, Tundu Lissu amekutana na familia ya Hayati Baba wa Taifa huko Mwitongo, sehemu ambayo alizaliwa na kuzikwa

Miongoni mwa wanafamilia waliowakaribisha ni pamoja na Mtoto wa Mwalimu Nyerere, Madaraka

1601201108915.png


1601201197094.png


1601201297876.png


Kupitia Mtandao wa Twitter Lissu ameandika:

 
Back
Top Bottom