Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Ni kweli kabisa walilala kwa watoto wa Baba wa Taifa, na Lissu aliwaomba apumzike pale ahani kwenye kaburi la baba wa taifa na aombe msamaha kwa kumtusi. Alifanya ibada hapo na maombi akisaidiwa na pasta wa kijijini.
 
Wakuu,

Tundu Lissu Siku ya Kuamkia leo alilala nyumbani kwa baba wa taifa Mwalimu Nyerere baada ya kuombwa na watoto wa Baba wa Taifa.

Watoto hao walijisikia furaha kubwa mno kupata ugeni mzito huo ambao wamesema hawajawahi kupata mgeni wa kulala kwao mkubwa kama Lissu na walijisikia kama wako na Baba yao Mzazi.,

Mmoja wa watoto hao Madaraka Nyerere amesema kuwa hawakuamini kama Lissu angewakubalia ombi lao hilo.

Kwenye Ukurasa wake wa Twitter, Tundu Lissu ameandika "In Mara we'd the honour of spending the night at Mwitongo, the birthplace & resting place of Mwl. J. K. Nyerere. We're privileged to be hosted by Madaraka, one of Mwalimu's sons, his sister Neema & her husband Carlo Giero both of whom treated us to a sumptuous dinner & breakfast."

View attachment 1582402View attachment 1582403View attachment 1582404View attachment 1582405
Mkuu umezidisha chumvi- punguza mahaba
 
Una fikra finyu sana comrade.
Mkuu ndo maana nikakuuliza wewe mwenye fikra pana kwamba ni kazi ipi mnataka kuendelea nayo,je ni ile ya kuteka na kuua watu? Je ni ile ya kuharibu masoko ya mazao yetu kama korosho,mbaazi,tumbaku,kahawa etc au ni ile ya kukandamiza haki za watanzania?na kuongeza unemployment rate?
 
Watoto wamekusamehe uliposema baba yao alikuwa na siasa ya uongo na kudanganya
 
Mkuu ndo maana nikakuuliza wewe mwenye fikra pana kwamba ni kazi ipi mnataka kuendelea nayo,je ni ile ya kuteka na kuua watu? Je ni ile ya kuharibu masoko ya mazao yetu kama korosho,mbaazi,tumbaku,kahawa etc au ni ile ya kukandamiza haki za watanzania?na kuongeza unemployment rate?
Comrade wewe tulia sindano iwaingie vizuri baada ya tar 28 October akili zitawarudi tu.
 
Mkuu nitajie mwanaccm mmoja ambaye akili haijamwingie vizuri 2015 to 2020.chagua magu at your own risk
 
Nikikutajia itakusaidia nini wewe? hatufanyi kazi kwa manufaa ya ccm bali tunafanya kazi kwa maendeleo ya watanzania kwa ujumla.

Magufuli ni chaguo la wengi na tutamchagua kwa kura nyingi sana.
 
Nakumbuka wakati muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya pili ya JK, KUB alikua Hamad Rashid Mohamed wa CUF. Siku ya Alhamisi ambayo ni siku ya maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, KUB alikua akipata kifungua kinywa nyumbani kwa PM na wakiondoka wote kwenda Bungeni.

Utamaduni huu umekomeshwa kikatili sana. Sasa hivi sio tu dhambi kumtembelea mtu mnae tofautiana itikadi za chama bali pia ni dhambi kumjulia hali mgonjwa hospitakini kama si wa chama chako! Na tunapoelekea hata kuzikana watu wa vyama tofauti itakua ni kosa la kimaadili la kuadhibiwa na chama. Nani katufikisha huku? Tusikubali.
Jiwe ndiye muasisi wa roho ya kutengana kwa watanzania kwa misingi ya kiitikadi.
 
Ni kweli kabisa walilala kwa watoto wa Baba wa Taifa, na Lissu aliwaomba apumzike pale ahani kwenye kaburi la baba wa taifa na aombe msamaha kwa kumtusi. Alifanya ibada hapo na maombi akisaidiwa na pasta wa kijijini.
RRwanda si mbali mfungasheeeeh
 
Nikikutajia itakusaidia nini wewe? hatufanyi kazi kwa manufaa ya ccm bali tunafanya kazi kwa maendeleo ya watanzania kwa ujumla.

Magufuli ni chaguo la wengi na tutamchagua kwa kura nyingi sana.
Wewe ndo mwakilishi au msemaji wa hao wengi au ni utopolo wako tu?
 
Nakumbuka wakati muhula wa kwanza wa serikali ya awamu ya pili ya JK, KUB alikua Hamad Rashid Mohamed wa CUF. Siku ya Alhamisi ambayo ni siku ya maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, KUB alikua akipata kifungua kinywa nyumbani kwa PM na wakiondoka wote kwenda Bungeni.

Utamaduni huu umekomeshwa kikatili sana. Sasa hivi sio tu dhambi kumtembelea mtu mnae tofautiana itikadi za chama bali pia ni dhambi kumjulia hali mgonjwa hospitakini kama si wa chama chako! Na tunapoelekea hata kuzikana watu wa vyama tofauti itakua ni kosa la kimaadili la kuadhibiwa na chama. Nani katufikisha huku? Tusikubali.

Tusikubali mtu mmoja atuharibie nchi yetu.

Hivi nikichagua chama pinzani ni uhaini!?..........Mitano inamtosha akapumzike.
 
Back
Top Bottom