Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Lisu si alimkashifu Baba wa Taifa kwenye Bunge maalum la Katiba,imekuaje leo?

JPM ANATOSHA
CCM USHINDI NI JADI
 
Hasira zao za kushindwa tu kura za maoni

Watoto wa Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro na Madaraka, wamepata kura chache katika kura za maoni Jimboni kwao Butiama, Mara.




Jimbo la Butiama lilikuwa na wagombea 59 na wajumbe waliopiga kura walikuwa 555 na matokeo yaliongozwa na Jumanne Sagini aliyepata kura 84, akifuatiwa na Frank Mahemba aliyepata kura 80, wa tatu akiwa Joseph Nyamboha kura 46.

Katika kura hizo za maoni Makongoro Nyerere alipata kura 5 na Madaraka Nyerere aliambulia kura 2. Makongoro Nyerere aliwahi kuwa Mbunge wa Arusha kupitia NCCR-Mageuzi.
Watoto wa nyerere waligoma kutoa rushwa kwa wajumbe, wajumbe wakatoa adhabu kali kwao.
 
Ni mimi nimesoma vibaya ama ni watu wamejitoa ufahamu? Au ni Watanzania wamekua wavivu kusoma? Tweet inasema kaspend a night Mwitongo Butiama haijasema kalala kwa Nyerere

Mbili inasema kawa hosted na Madaraka Nyerere haijasema kama ni nyumbani kwa Nyerere hivyo itakua nyumbani mwa Madaraka Nyerere.

also kuna impact gani kisayansi na kijamii kama akionekana na watoto wa Nyerere ambao wameshindwa hata kupita kura za maoni?
 
Waligombea kura za maoni watu wa jimbo hilo wakawanyima kura Makongoro alipata kura tano mwiingine huyo madaraka alipata kura tatu naona wana hasira

Kura wakose wao hasira wazioyesheee kwa kumlaza Lisu kwao!!!!!!
Uliwahi kuwanunulia hata shuka wewe kula kulala?
 
Kwa jinsi utawala huu wa washamba na malimbukeni wa awamu hii kama hawakumpigia simu Yesu wa ccm na kiongozi wa malaika mkuu kumuomba ruhusa ya Lissu kulala hapo , basi wajiandae kubambikia kesi , tra kuwafuata , kutekwa as usual .
 
Mara nyingi nimemsikia Tundu Lisu alimtukana na kumdhihaki Nyerere leo amethubutu kwenda kulala kwake labda anatafuta kiki ya kuomba kura lakini kesho utasikia tena akimtukana na Mbowe ajiandae naye lazima atatukanwa tu subirini.
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?


Hizi 'Hasira' za Madaraka Nyerere kwa Kukosa Kwake kuonekana mwenye uwezo wa kuwa Mbunge wa Butiama na 'Kumrithi' Mzee Nimrod Elirehema Mkono kupitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) si tu kwamba kinaweza 'Kumuathiri' Yeye bali wanaweza sasa kujikuta 'Wanamponza' hadi na Mama yao ( Mjane wa Hayati Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere )

Hivi kwa mfano tu ingetokea Madaraka Nyerere 'Kateuliwa' kuwa Mgombea 'Ubunge' wa Jimbo hilo la Butiama kwa Tiketi ya CCM bado tu angemuomba Tundu Lissu 'akatembelee' pale Kwao Mwintongo Butiama na hadi alale? Kitendo hiki 'Kimeshathibitisha' kuwa kumbe kuanzia Wajumbe 'waliommaliza' na hadi Chama cha CCM kutokuwa na Imani nae hawakukosea kwani ni Mnafiki na Mpinzani wa Awamu hii ya JPM.

Sisemi kwamba Madaraka Nyerere alitakiwa au anatakiwa auchukie Upinzani bali hiki Kitendo alichokifanya 'amekurupuka' nacho na Kitamgharimu.
 
Genta the Genius. Hamna mtu atakayeponzwa. Magufuli sio Raisi wa Tanzania 2020-2025. Visasi vyake anarudi navyo chato.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 ni Tundu Antiphas Lissu
 
Vp kuhusu Bwana Yule kumlipia Mh Msigwa fine Mahakamani, Haikuwa fedheha kwa ccm??
 
Genta the Genius. Hamna mtu atakayeponzwa. Magufuli sio Raisi wa Tanzania 2020-2025. Visa si vyake anarudi navyo chato.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 ni Tundu Antiphas Lissu

Kuna Swali nimeuliza katika hiyo 'post' yangu hujaliona au? Je, Madaraka 'angepitishwa Kugombea 'Ubunge' na CCM 'angemkaribisha' Tundu Lissu?
 
Kwa nafasi ya Familia ya Nyerere hawatakiwi kuwa na upande. Kwa sababu hata mfumo wa vyama vingi ulihasisiwa na Nyerere na hupo kisheria. Na Nyerere ni Baba wa Taifa.
Yaani CCM mnategemea mtuwekee mtu muuaji, fedhuli, mzandiki, mwenye chuki, roho mbaya na visa si visivyo vya kawaida alafu mnategemea familia ya Mwl Nyerere imuunge mkono????

Kweli CCM wajinga sana
 
Mara nyingi nimemsikia Tundu Lisu alimtukana na kumdhihaki Nyerere leo amethubutu kwenda kulala kwake labda anatafuta kiki ya kuomba kura lakini kesho utasikia tena akimtukana na Mbowe ajiandae naye lazima atatukanwa tu subirini.
Alimtukana tusi gani??? Kama wanafamilia hawajaliona hilo tusi wewe ni nani utushawishi???
 
Hayajitambui, mtu alimtukana baba yao hadharani kabisa
Ni kweli. Mbaya sana. Lakini alitukana zamani. Na si ajabu ameenda pale kuomba msamaha. Mwingine alimburuza mama yao hivi karibuni. Kisha akawakejeli vibaya wao wenyewe juzi tu. Hapo vipi?
 
Back
Top Bottom